Nini kifanyike kufufua sekta ya umeme/nishati nchini?

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Ndugu zangu wana JF kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hivi kweli nchi kama Tanzania pamoja na resources tulizo nazo tunashindwa kuzalisha umeme wa kututosheleza na hata kuuza nje?

Tuna vyanzo vya maji vya miaka ya 70, lakini ni nini kinashindikana kuviboresha au kuanzisha vituo vipya? Tuna makaa ya mawe, je ni juhudi gani za makusudi kuhakikisha tunatumia makaa haya kuzalisha umeme wa uhakika?

Sijui sheria ya uwekezaji ktk sector ya umeme inasemaje na hapa nahitaji maelezo kutoka kwenu JF members, kwamba, hivi mtu akijitokeza anataka kuzalisha umeme na kuusambaza ktk wilaya labda moja au mbili au hata mkoa mzima na akakusanya mapato na kisha yeye akalipa kodi kwa serikali, je, hili linashindikana nini kwa Tanzania? Au sheria zinasemaje ktk hili??

Na kama sheria inaweka ukiritimba kwamba ni lazima TANESCO ndo isambaze umeme je, kubadili sheria inachukua miaka mingapi Tanzania??

Nasikia kiwanda cha TPC moshi wana uwezo wa kuzalisha megawati 10, je kwanini wasiruhusiwe wakasambaza wenyewe kwa wateja, wakakusanya mapato na kulipa kodi kwa serikali?? Kwani ni lazima waiuzie umeme TANESCO??

Ndugu wana JF hili mimi linanikera na kama nikiwa waziri wa nishati na madini (ipo siku) lazima ni hakikishe hata wilaya inakuwa na mwekezaji ambaye ana supply umeme kwenye wilaya na analipa kodi serikalini basi. Siyo kusumbuka na ukiritimba wa TANESCO ambayo inatumiwa na wanasiasa mafisadi.

Kwa mawazo haya naomba tuchangie na tuone tatizo liko wapi na ngeleja najua anatembelea JF aseme tatizo liko wapi???
 
Sheria iliyopo inawaruhusu Tanesco tu kufanya distribution. Unaweza kugenerate independently isipokuwa ni lazima uwauzie Tanesco. Hii inaleta matatizo kwasababu monopoly imewafanya wajanja kufanya deal nyingi through the firm kwa vigezo kuwa hakuna namna tunaweza kuwakwepa.
Ila way forward nafikiri independent power producers wangeruhusiwa pia kufanya mpaka distribution kupunguza matatizo yanayoletwa na monopoly ya Tanesco.
Halafu pia ili nchi iweze kuwa economic hub ya EA suala la power lazima liwe agenda ya juu maana bila power production itakuwa ni ya kusuasua na cost zitakuwa juu sana.
It is high time now tukaazimia kutengeneza umeme kwa kutumia na makaa ya mawe. South Africa na recently Mozambique, wamatumia makaa ya mawe kutengeneza umeme. Kiwira could be revived and contribute as it should in the power requirements of the country.
Ilivyosasa distribution network ya umeme kwenda Mwanza, Arusha na baadhi ya mikoa ambayo wako katika mgao ni kwasababu network imezidiwa. Matumizi/mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wa Tanesco wa kusambaza. Yaleyale tuliozoe..kudeal na athari za tatizo badala ya kuwa proactive
 
This thread is very constructive, but it is a shame Tanesco kushindwa kuweka uwazi wa how should people contribute in production ya electricity so that people can benefit and/or make money through such investments.

The conduit must be open to the public kama njia ya kuvutia au hamasisha watu.
 
This thread is very constructive, but it is a shame Tanesco kushindwa kuweka uwazi wa how should people contribute in production ya electricity so that people can benefit and/or make money through such investments.

The conduit must be open to the public kama njia ya kuvutia au hamasisha watu.

Mkuu nimekupata na kilicho nisukuma kuweka thread hii ni maumivu nayo yapata kutokana na utendaji usio na tija wa tanesco halafu serikali ipo tu kimya.

Mimi naumia sana kuona tunaendekeza siasa badala ya kujenga uchumi, uchumi haujengwi kwa maneno ya kijinga ya makamba na chiligati, uchumi unajengwa na kazi za wataalamu wa mambo mbalimabli ktk nchi.

Naomba watanzania hata kama tuko nje ya Tanzania tuamue sasa kuweka mikakati na tuwalazimishe mawaziri wanaoteuliwa ili wafanye kazi kama huku nje mambo yanavyo kwenda.

Nimemuomba Ngeleja kwa sababu huwa anatembelea JF basi atueleze ni nini kinasababisha ashindwe kupeleka mswada wa sheria ili wawekezaji binafsi waruhusiwe kugenerate na ku-distribute umeme wao wenyewe alafu walipe kodi kama wafanya biashara wengine.

Tafadhari Ngeleja ingia JF utupe majibu.
 
Mh. Zitto Kabwe naomba utupe mchango wako ktk hili kwamba ni nini kinashindikana kubadili sheria ili tupate wawekezaji binafsi ambao watakuwa na uwezo wa ku-generate na ku-distribute umeme wenyewe katika maeneo watakayo yapenda na walipe kodi kama wafanyabiashara wengine.

Je, Mh. Zitto na wabunge wengine kwa nini hamjaweza kufikiria hili au mna mawazo gani kuhusiana na kuboresha uzalishaji wa umeme?? Siyolazima tununue dowans, najua we can do without dowans!!
 
Last edited:
Mkuu nimekupata na kilicho nisukuma kuweka thread hii ni maumivu nayo yapata kutokana na utendaji usio na tija wa tanesco halafu serikali ipo tu kimya.

Mimi naumia sana kuona tunaendekeza siasa badala ya kujenga uchumi, uchumi haujengwi kwa maneno ya kijinga ya makamba na chiligati, uchumi unajengwa na kazi za wataalamu wa mambo mbalimabli ktk nchi.

Naomba watanzania hata kama tuko nje ya Tanzania tuamue sasa kuweka mikakati na tuwalazimishe mawaziri wanaoteuliwa ili wafanye kazi kama huku nje mambo yanavyo kwenda.

Nimemuomba Ngeleja kwa sababu huwa anatembelea JF basi atueleze ni nini kinasababisha ashindwe kupeleka mswada wa sheria ili wawekezaji binafsi waruhusiwe kugenerate na ku-distribute umeme wao wenyewe alafu walipe kodi kama wafanya biashara wengine.

Tafadhari Ngeleja ingia JF utupe majibu.

I think this month, kuna Wakenya wamefunga mtambo huko Kisumu wa kutengeneza umeme, na umeshakaguliwa na Rais Kibaki, nafikiri umeshaanza kazi, sasa cha ajabu, kwetu Tz, fikra zetu zinaendekeza siasa kuliko uchumi na kufikiria siasa itajenga nchi.

It is shame and sad hata hapa JF kitengo kinacho jaa watu na hoja ni cha siasa, wakati huo huo watu wanalalama kuhusu uchumi eti ni mbovu.

Mkuu Magezi you just don't know how you made my day nilipo ona thread yako, this is what we should be talking, kujenga nchi, kama utafanikiwa kupata conduit kama walivyo pata Richmond, itasaidia hata kikazi, kwani watu wengi wanaitaji kazi na kusambaza umeme at the same time. It is a dual help to the nation.

I am eager to hear from responsible parties ambazo zinahusika na shughuli hii ya umeme, yaani wakuu wa TANESCO.

 
Mkuu MaxShimba nimekusoma na nikiri kabisa kwamba wachangiaji wengi ktk JF utawakuta kwenye umbea wa mara CCM mara CHADEMA mara CUF lakini kwa kweli watanzania wenzangu hebu tujaribu kujadili mambo ambayo yanaweza kuikwamua nchi yetu iliyokwama kwenye tope la ujinga, wizi, ufisadi, magonjwa n.k.
Tuweke mikakati ambayo inaweza kuisaidia tanzania ikaondokana na matatizo iliyonayo kwa sasa.

Ni kweli akina Rostam wana tusumbua na mambo yao lakini nadhani kikwete kama ana akili tumesema sana aache uswahiba na hawa watu, asifikiri yeye ni rais basi hawezi kudhuriwa anapowakosea wananchi wake, no, uwezo wa kuthubutu tunao.
 
Nimesoma taarifa kwenye The Guardian Ngeleja anasema Tanzania inahitaji 700 billion (Tshs.) kumaliza matatizo ya umeme. Anasema kuna issue ya kujenga transmission lines kutoka mtwara hadi kidatu, lakini kitu cha ajabu serikali hii hii inatumia billion 221 kwenye vitambulisho vya uraia ambavyo siyo dharula.

Swali langu kwa kikwete ni je, kwa nini issue ya vitambulisho isi subiri na badala yake hiyo hela ikatumika angalau kuongeza 100MW kila mwaka??
 
Back
Top Bottom