Ndugu zangu wana JF kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hivi kweli nchi kama Tanzania pamoja na resources tulizo nazo tunashindwa kuzalisha umeme wa kututosheleza na hata kuuza nje?
Tuna vyanzo vya maji vya miaka ya 70, lakini ni nini kinashindikana kuviboresha au kuanzisha vituo vipya? Tuna makaa ya mawe, je ni juhudi gani za makusudi kuhakikisha tunatumia makaa haya kuzalisha umeme wa uhakika?
Sijui sheria ya uwekezaji ktk sector ya umeme inasemaje na hapa nahitaji maelezo kutoka kwenu JF members, kwamba, hivi mtu akijitokeza anataka kuzalisha umeme na kuusambaza ktk wilaya labda moja au mbili au hata mkoa mzima na akakusanya mapato na kisha yeye akalipa kodi kwa serikali, je, hili linashindikana nini kwa Tanzania? Au sheria zinasemaje ktk hili??
Na kama sheria inaweka ukiritimba kwamba ni lazima TANESCO ndo isambaze umeme je, kubadili sheria inachukua miaka mingapi Tanzania??
Nasikia kiwanda cha TPC moshi wana uwezo wa kuzalisha megawati 10, je kwanini wasiruhusiwe wakasambaza wenyewe kwa wateja, wakakusanya mapato na kulipa kodi kwa serikali?? Kwani ni lazima waiuzie umeme TANESCO??
Ndugu wana JF hili mimi linanikera na kama nikiwa waziri wa nishati na madini (ipo siku) lazima ni hakikishe hata wilaya inakuwa na mwekezaji ambaye ana supply umeme kwenye wilaya na analipa kodi serikalini basi. Siyo kusumbuka na ukiritimba wa TANESCO ambayo inatumiwa na wanasiasa mafisadi.
Kwa mawazo haya naomba tuchangie na tuone tatizo liko wapi na ngeleja najua anatembelea JF aseme tatizo liko wapi???