Mjadala: Hoja za Wadau kuhusu namna ambavyo Mgawo wa Umeme umeathiri shughuli za Kijamii na Kiuchumi nchini

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1708456070633.jpeg

Kukatika kwa Umeme mara kwa mara katika maeneo mbalimbali Nchini kumeripotiwa kusababisha athari tofauti ikiwemo hasara kwa Wafanyabishara wanaotegemea Nishati hiyo ili kuendesha shughuli zao.

JamiiForums kwa kutambua hilo, itaendesha Mjadala kupitia XSpaces, utaogusia Kero zinazotokana na Mgawo wa Umeme, Alhamisi Februari 22, 2024 saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku. Usikose!

Link ya Mjadala https://jamii.app/MgawoUmeme

Pia unaweza kuweka maswali au maoni yako katika uzi huu. Yatasomwa siku ya mjadala

Karibuni
---

Jiunge nasi katika mjadala, muda huu unaoangazia Athari za Mgawo wa Umeme kwa Wananchi na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na changamoto hiyo kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala bofya https://jamii.app/MgawoUmeme

---
1708616148389.jpeg


Maoni yaliyotolewa na MARTIN MBWANA (Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo)

MARTIN MBWANA: Hasara ya kukatika kwa Umeme Kariakoo ni kubwa, mali nyingi za wafanyabiashara zinazohitaji Umeme zimeoza ikiwemo Samaki, Kuku na vitu vingine vya aina hiyo Shughuli nyingi zinafanyika kwa Mifumo ya Umeme ikiwemo malipo na ripoti, hivyo Umeme unavyokatika inakuwa shida na Mamlaka kama TRA zinakuwa hazielewi kuhusu hilo.

Tulikuwa katika mpango wa kufunga Kamera maeneo yote ya Kariakoo, lakini kukosekana kwa Umeme wa uhakika imekuwa tabu kubwa sio tu kwa Wafanyabiashara bali Watu wote wa Maeneo hayo.

Umeme umesababisha Watu wengi wawe na matumizi makubwa ya Mafuta lakini matumizi hayo hayatambuliki TRA katika mahesabu, hivyo Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipata hasara

Umeme umesababisha sehemu kama Kariakoo Shimoni kuwe na shidaKazi haziwezi kufanyika bila Umeme kule, lakini pia giza limesababisha matukio ya wizi kuongezeka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watambue kuwa suala la Umeme ni janga, wasiwe tu wanaishia kulalamika na kutupa lawama kwa WafanyabiasharaHii ‘system’ ya kata washa kata washa si rafiki, tunatakiwa kujua kabisa kuwa Umeme upo au haupo kwa muda gani ili tujipange.

Maoni ya BERNARD KIHIYO (Mkurugenzi wa Chama cha Walaji Tanzania)
BERNARD KIHIYO: Umeme kukatika mara kwa mara umesababisha bidhaa nyingi kupanda bei kwa kuwa uzalishaji umepungua na hali hiyo imekuwa changamoto kwa Wananchi wengi.

Serikali inakusanya takwimu za idadi ya Watu na kufanya makadirio kuwa hadi kufikia Mwaka fulani idadi ya Watu inaweza kuongezeka na kuwa kiasi fulani, hata upangaji wa bajeti na Maendeleo ya Kijamii unatakiwa kuakisi idadi ya Watu.

Maoni ya JOHN HECHE (Mbunge wa Zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA)
JOHN HECHE: Umeme unaathiri Uchumi wa Nchi na maisha ya watu moja kwa moja ndio maana kumekuwa na kelele nyingiSerikali imeshindwa kuwa na utatuzi wa changamoto ya Umeme kwa Miaka mingi, ukiangalia Kampuni za Mawasiliano zimeanza Miaka ya hivi karibuni lakini Huduma zao zimefika hadi ngazi ya Vijiji na katika sehemu nyingi.

Umeme unaathiri uchumi wa Wananchi
IMG_20240222_193607_117.jpg
Mbunge wa Zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, John Heche amesema Umeme unaathiri Uchumi wa nchi na maisha ya watu moja kwa moja ndio maana kumekuwa na kelele nyingi

Ameeleza kuwa Serikali imeshindwa kuwa na utatuzi wa changamoto ya umeme kwa miaka mingi, ukiangalia Kampuni za Simu zimeanza miaka ya hivi karibuni lakini huduma zao zimefika hadi ngazi ya Vijiji na katika sehemu nyingi

Amesema "Tanzania ni Nchi ambayo ina vyanzo vingi vya umeme, tuna umeme wa Megawati 1,500 hadi 1,700 lakini Geothermal ingeweza kuzalisha umeme hadi Megawati 7,000 lakini hilo halifanyiki"

Serikali iwe na vyanzo vingi vya umeme
Mbunge wa Zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA amesema ni lazima tufike hatua kama Nchi kuwe na vyanzo vingi vya kuzalisha Umeme, kuwe na Kampuni tofauti badala ya kutegemea Mamlaka moja, lazima kuwe na ushindani

Vile vile tutumie vyanzo vingine vya kuzalisha umeme ikiwemo makaa ya mawe, Upepo na umeme wa ‘Geothermal’

Amesema "Umeme wa Maji tunaambiwa hauaminiki, ikitokea kuna mabadiliko ya Tabianchi maji yakapungua ndivyo ambavyo changamoto ya umeme itakavyoendelea kama ilivyo sasa".

Serikali imeshindwa kutatua tatizo la umeme kwa muda mrefu
Mbunge wa Zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, John Heche amesema Umeme unaathiri Uchumi wa nchi na maisha ya watu moja kwa moja ndio maana kumekuwa na kelele nyingi

Ameeleza kuwa Serikali imeshindwa kuwa na utatuzi wa changamoto ya umeme kwa miaka mingi, ukiangalia Kampuni za Simu zimeanza miaka ya hivi karibuni lakini huduma zao zimefika hadi ngazi ya Vijiji na katika sehemu nyingi

Amesema "Tanzania ni Nchi ambayo ina vyanzo vingi vya umeme, tuna umeme wa Megawati 1,500 hadi 1,700 lakini Geothermal ingeweza kuzalisha umeme hadi Megawati 700 lakini hilo halifanyiki"

Maoni ya ISIHAKA RASHID MCHINJITA

BAJETI YA WIZARA YA NISHATI INAONESHA MAZINGIRA YA KUTAPANYA FEDHA

IMG_20240222_194623_653.jpg

Akishiriki katika Mjadala wa Athari za Kukatika kwa Umeme, Waziri Kivuli wa Nishati, Mjumbe wa Kamati Kuu ACT Wazalendo amesema Septemba hadi Januari 2024 kumekuwa na changamoto ya umeme, vyanzo vyetu vya uzalishaji umeme vinavyotumia maji vimekuwa vikipata upungufu wa maji na hivyo kusababisha uzalishaji kupungua

Ameongeza Bajeti ya Wizara ya Nishati inaonesha mambo mengi lakini utekelezaji wake umekuwa haukamiliki. Kumekuwa na mazingira ya kutapanya fedha za Serikali bila faida na wakati huo huo wamekuwa wakishindwa kutengeneza vipaumbele.

KUKOSEKANA KWA DHANA YA UWAJIBIKAJI NI MOJA YA CHANZO CHA TATIZO LA UMEME

Waziri Kivuli wa Nishati, Mjumbe wa Kamati Kuu ACT Wazalendo amesema kukosekana kwa dhana ya Uwajibikaji kwa Uongozi ni moja ya chanzo cha tatizo la umeme. Mfano; kuna utani ambao unafanywa na Viongozi wa Wizara ya Nishati wakati watu wengi wakiwemo Wafanyabiashara wanapata hasara kubwa

Amesema kuna ahadi nyingi ambazo hazitekelezi zinatolewa, wanaahidi changamoto itamalizika Januari, ikifika muda huo wanasema Februari, ikifika muda huo anakuja kiongozi mwingine anasema tofauti.

Maoni ya Hammy (Mdau wa X)
HATA TUKISEMA SGR INAANZA NI UONGO! HILO HALIWEZEKANI. KWA UMEME UPI?

Akichangia Mjadala wa athari za Mgawo wa Umeme Kiuchumi, Mdau amesema ukikosa umeme gharama za maisha zinapanda kwa kuwa uzalishaji unapungua, hivyo tutakuwa tunajidanganya kusema Uchumi wetu unakua wakati Wananchi tuna maisha magumu

Amesema inatakiwa kuweka vipaumbele, tunaweza kuamua labda kufikia Mwaka 2025 kuwe na umeme wa uhakika, mfano mwingine sasa hivi hata tukisema Huduma ya Treni ya SGR itaanza, ni uongo, hilo haliwezekani, kwa umeme upi?
 
Nalaza kazi za ofisi katika matumizi ya computer, nalazimika kusafiri km 15 kufuata mafuta sheli ili generator liwake.

Wakati mwingine umeme urudipo usiku kama hivi leo nalazimika kwenda ofisini nikafanye kazi kwa kuwa sina uhakika kama kesho asubuhi umeme utakuwepo, tabu tupu ni mgogoro tu na wife kunihisi nipo mchepuko wakati napiga kazi muda huu.
 

Kukatika kwa Umeme mara kwa mara katika maeneo mbalimbali Nchini kumeripotiwa kusababisha athari tofauti ikiwemo hasara kwa Wafanyabishara wanaotegemea Nishati hiyo ili kuendesha shughuli zao.

JamiiForums kwa kutambua hilo, itaendesha Mjadala kupitia XSpaces, utaogusia Kero zinazotokana na Mgawo wa Umeme, Alhamisi Februari 22, 2024 saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku. Usikose!

Link ya Mjadala https://jamii.app/MgawoUmeme

Pia unaweza kuweka maswali au maoni yako katika uzi huu. Yatasomwa siku ya mjadala

Karibuni
Mimi kazi zangu nafanyia nyumbani (working from home), kwa sababu nafanya kazi remotely, ninaofanya nao kazi makao makuu yao yako Marekani.

Hivyo, umeme na internet ni muhimu sana kwangu. Umeme uliwahi nifanya nikakosa meeting muhimu sana, ambayo mimi ndo nilitakiwa kufanya presentation.

Tangu hapo, nikaingia gharama kubwa kuweka solar back up nyumbani, hivyo kwa sasa hata umeme ukatike masaa 24, sina shida.
 
Tumpongeze tu mama kwa kweli maana bila yeye umeme ungepotea jumla kabisa maana yeye ndo kafanya uwepo na kua wa mgao, maana huku mtaana shughuli zinaenda kama kawa hata vinyozi wanafurahia maana wameongeza ujuzi hata kwa kunyoa kwa nyembe za mkono
 
Umeathiri kila kitu.

Wajasiliamali wadogo kama vinyozi, mafundi wa kuchomelea hela sasa hivi wanazishika kwa manati, huduma za kijamii zimekuwa hovyo mfano kuna maeneo utokaji wa maji unategemea uwepo wa umeme kama umeme hakuna maji inakuwa msamiati mwingine.

TANESCO na waziri wa hii wizara ajitafakali sana kwanini enzi za jiwe umeme ulikuwa hauna shida wao wanashindwa nini, kuna biashara gani wanafanya kwenye huu mgao wa umeme?
 
Changamoto sana aisee.

Umeme kama hamna inabidi utulie tu home.

Au kama kuna magazine mengi inabidi uingie restaurant yenye jenerator ukombize
 
Nilikuwa natotoresha vifaranga kwa kutumia incubator. Nilikuwa natotoresha vifaranga 1000 vya kuku, Bata na Kanga. Niliacha toka mwezi wa 10 tokana na changamoto ya umeme nikajua baada ya muda utastablelize.

Tokana na pressure ya wateja, ikabidi nitafute generator na kuanza kupiga kazi mwezi 12. Gharama zimekuwa juu kwani inabidi nitumie ⛽️ ⛽️ kuendesha mtambo. Sasa sipati faida kwani nafanya kuridhisha wateja tu.
 
Nauza vifaa vya kuchomelea kama Square pipe, shiti nk tangu kuwe na mgao wa umeme biashara imeshuka sana kinachoumiza zaidi kodi TRA ipo palepale
 
Back
Top Bottom