Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

- think Mbowe (a man who would rather be a slave under the Brits because he hates being a "Freeman", an opposition leader speaking his mind freely. He hates being a businessman and entrepreneur under the Black rule).

As for the young crop of opposition politicians (Mnyika, Zitto, etc), it remains to be seen whether college agitation can turn into mature political posture. With Zitto's misjudgement (taking someone's wife who is infected with HIV/AIDS) and demagoguery, with Mnyika's ineptness - all resulting from lack of proper political grooming and guidance - I don't see hope.



The bottom line: with the current opposition leadership, CCM is not going anywhere, despite thievery and incompetence. If you read Jambo Forum, and have not visited Nkasi, or Ileje, or Kamachumu, you would think CCM is going down tomorrow. People like Mnyika, Kabwe and Mbowe and their army of supporters spend their days here - and smell State House as a result.

I
Miaka 15 vyama vingi nchini: Je, yapo matumaini ya upinzani?


We Mzee wa Twanga una matatizo sana! Umeshalezwa na kufafanuliwa Mbowe alisema nini na anamaanisha nini juu ya kufananisha CCM na ukoloni lakini we upo tu umekazania! Husikii, huelewi na hutaki kuamini vinginevyo. Unaamka asubui ukiwa umeweka msimamo mkali katika uongo, kisha unakuja hapa kujengnga hoja juu ya msingi wa uongo. Baada ya muda utapoteza uwezo wa asili wa mwanadamu wa kutambua uongo na ukweli, mema na mabaya! Nakuombea siha njema na afya ya akili.

Hoja yajo juu ya zito na Mnyika imeweka uchi mtazamo wako na makusudio yako kwao sina la kuongeza zaidi ya kumshukuru alie juu kwa namna ya kipekee anavyofunua malengo na mitazamo ya binadamu. Hii inatuweka salama wengine kujua njia za kupita. Ubarikiwe
 
Naweka hizi makala na mahojiano na viongozi wa CHADEMA,pia inaonyesha jinsi ambavyo walivyo waadilifu na sio walarushwa kama walivyo wa CCM.


Happiness Katabazi

MIAKA 15 sasa tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi, ambao wataalamu wa masuala ya kisiasa wanakiri kuwa umeleta changamoto kwa chama kilichopo madarakani mbali na wananchi kuwa huru kutoa maoni yao, lakini changamoto nyingine iliyotokana na mfumo huo ni uanzishwaji wa taasisi ambazo zimekuwa msaada kwa wananchi. Wakati imetimia miaka 15, ni utamaduni wetu kutafakari na kutathimini kule tulikotoka na hali ya sasa ikoje hususani kwa kuangalia mabadiliko na changamoto zilizoko. Katika mahojiana na Mwandishi Wetu HAPPINESS KATABAZI, Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, anaelezea hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini.

Swali: Je, ndani ya Bunge kuna mabadiliko gani tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe hapa nchini mwaka 1992?

Jibu: Kwanza lazima tukiri kwamba idadi ya wabunge wa upinzani ni ndogo.

Wabunge wa upinzani wapo 45 kati ya wabunge 320. Wabunge wa CHADEMA ni 11 kati ya hao 45 wa upinzani.

Lakini uchache si hoja japo maamuzi bungeni yanafanyika kwa kura na hivyo yote yanapitishwa kwa wingi wa wabunge wa CCM hata kama maamuzi hayo hayana maslahi kwa taifa.

Hasa suala la ongezeko la kodi na ushuru wa mafuta ambalo ni dhahiri kabisa halina maslahi kwa wananchi wa kawaida na kwa vyovyote ongezeko hilo litapandisha gharama ya maisha, hoja ambayo iliungwa mkono na wabunge wote wa CCM.

Pamoja na hali hiyo, kambi ya upinzani imetoa changamoto nyingi ndani ya Bunge.

Watanzania sasa wana nafasi ya kujua hali halisi ya mambo yalivyo katika uendeshaji wa nchi yao.

Hata wabunge wa chama tawala wakifungwa mdomo, wabunge wa kambi ya upinzani hakuna wa kuwafunga mdomo, watapasua mabomu tu.

Mfano, tuhuma za ubadhirifu ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambazo Gavana wa benki hiyo, Daudi Balali anauhusishwa, kwa mara ya kwanza sasa wananchi wa nchi hii wamejua kwamba ndani ya chombo kikubwa kama BoT kuna shutuma nzito kama hizo.

Aidha, Watanzania wamejua sasa kwamba kuna uwezekano wa kutengeneza bajeti mbadala kutoka kwenye rasilimali ya nchi yetu kama madini, misitu, uvuvi ambao kwa mara ya kwanza kambi ya upinzani imeonyesha kwamba taifa linaweza kupata sh trilioni 8 ikilinganishwa na sh trilioni 6 za serikali bila kuongeza mzigo wa ushuru na kodi kwa mwananchi wa kawaida.

Aidha, kutokana na rasilimali hizo, tungeweza kuwekeza zaidi kwenye huduma za jamii kama elimu ambayo tungeweza kuifanya kuwa bure hadi chuo kikuu, matibabu na yakalipiwa na serikali kikamilifu bila ya kumbughudhi mwananchi.

Swali: Unafikiri mchanganuo wa hoja za wabunge wa kambi ya upinzani zimeleta changamoto ndani ya Bunge?

Jibu: Siyo siri, tena mchanganuo wa hoja za kambi ya upinzani zimeleta changamoto ndani ya Bunge na zinaendelea kuleta changamoto wa utajiri wa mawazo, ambazo serikali ikizizingatia zitaleta unafuu kwa wananchi wa taifa hili kwa ujumla.

Kwa kuwa wapinzani hawawezi kufungwa midomo, serikali hivi sasa hailali tena, inajiandaa vizuri zaidi kwa maovu yanayoibuliwa na wapinzani ambayo wanayafanyia pamoja na uchache wao.

Naweza kusema ni sawa na mbwa mdogo ambaye kwa kupiga kelele tu, mwenye nyumba ataamka na kuchukua hatua za kulinda nyumba na mali zake.

Sasa kama wananchi hamtaamka baada ya kuamshwa na mbwa mdogo ili msaidiane naye kulinda rasilimali za nchi yenu, ipo siku mtajuta.

Swali: Manufaa na malengo ya mfumo wa vyama vingi nini?

Jibu: Lengo la msingi la vyama vingi vya siasa ni kushindanisha sera na ilani za vyama lengo likiwa ni kumnufaisha mwananchi apate kuchagua chama chenye sera bora.

Sura ya kwanza ya manufaa ya mfumo wa vyama vingi, ni kwamba umeleta utajirisho wa mawazo ambao huwezi kupata kwenye chama kimoja.

Hata kama vyama hivi havishiki madaraka kwa kuwa chama kimoja tu ndiyo kinatakiwa kiingie Ikulu, lakini kwa kuwa utajirisho huo si wa chama peke yake bali ni kwa wananchi wote, chama kina jukumu la kuchapisha na kutangaza sera zake, na mwisho wa hayo yote anayenufaika ni mwananchi.

Kwa hiyo, chama kinachotawala kinatakiwa kiwe na masikio ya kusikiliza sera za vyama vilivyoshindwa kutwaa madaraka na kisha izichukue na kuzifanyia kazi kwa maslahi ya wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

Kwa mfano mwaka 1992, ukiona sera ya kwanza kabisa ya CHADEMA ilisema jengo la Chimwaga lililopo Dodoma ligeuzwe kuwa Chuo Kikuu kwa kuwa mji huo kuwa makao makuu ya nchi ni ngumu na badala yake ugeuzwe na uwe mji wa kitaaluma.

Nchi zilizoendelea kama Uingereza, kuna mji mmoja umekuwa kwa sababu serikali ya nchi hiyo ilitenga mji huo kuwa wa kitaaluma na kujengwa maduka makubwa ya kuuza bidhaa mbalimbali.

Serikali yetu ilikalia kimya sera hiyo hadi hivi sasa ndiyo imekubali jengo la Chimwaga liwe chuo kikuu, kwa hiyo jambo hili ni la kihistoria na kama serikali ingetekeleza tangu mwanzo hiyo sera yetu, mkoa huo hivi sasa ungekuwa mbali kimaendeleo.

Hivyo wananchi wanaweza kuangalia ushindani wa sera za vyama katika uchaguzi wa mwaka 2000, Serikali ya CCM ilikuwa inasema elimu ya msingi inalipiwa na wazazi, lakini vyama vya upinzani viliibuka na sera kwamba huwezi kumsomesha mtoto kwa kutegemea mchango wa wazazi ambao wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku na tulipendekeza elimu ya msingi itolewe bure.

Ilipotimu mwaka 2001, serikali ilipokea hayo mawazo na kuanza kutekeleza licha ya kuwa Ilani ya CCM ilikuwa haisemi kwamba watoto wasome bure na mara moja ikafuta UPE, ikapunguza ada na sasa taifa libeba mzigo wa gharama za wanafunzi.

Badala ya mzazi mmoja kuchangia, wanachangishwa wanajamii kwa kuchangia ujenzi wa madarasa.

Sasa huu ni utajirisho uliotokana na vyama vingi. Chama makini kinapaswa kuchukua sera za vyama vingine na si chama tawala tu ndiyo kichukue sera nzuri, la hasha, hata vyama ambavyo havijashika dola.

Asilimia 95 ya Watanzania wanaishi chini ya dola moja na hizi ni takwimu za serikali. Sasa taifa linapokuwa na idadi hiyo ya maskini kisha unawawekea kodi nyingi, hatuoni kwamba anakandamizwa mwananchi hapo?

Sasa kwa upande wa ilani za vyama vya upinzani, vilipunguza kodi za kichwa, kodi za usumbufu katika Jimbo la Hai, Karatu, Bariadi Mashariki na Kigoma, majimbo haya yanaongozwa na wabunge wa vyama vya upinzani.

Hata hivyo Julai 2002, serikali ilitangaza rasmi kufuta kodi zote za kichwa na usumbufu.

Hivyo hapa utabaini kwamba wapinzani baada ya kupunguza kodi hizo, serikali ikazifuta kabisa kwa hiyo, bila kuwepo ushindani katika hili la kodi serikali isingezifuta.

Hata hivyo, dhana ya vyama kuingia Ikulu katika utendaji, hili si muhimu kwa wananchi, mwananchi anachoangalia atapata faida gani. Na kitu kitakachomwondoa madarakani aliyepo madarakani, ni jinsi atakavyotekeleza yale aliyoyaahidi.

Sasa utekelezaji ni yale aliyobuni kiongozi anayeongoza na sera na ilani ya chama chake.

Sura ya pili ya mfumo huu, ukichukulia miaka 40 iliyopita iliyokuwa chini ya mfumo wa chama kimoja uhuru wa mawazo uliminywa kwa kiwango kikubwa.

Taifa lilitawaliwa na hofu kubwa hadi kwenye mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Leo hii Watanzania tunaweza kutembea kifua mbele kwamba kwa kiasi kikubwa hofu imeondoka.

Lakini kwanini imeondoka? Imeondoka kwa sababu sisi wanachama wa vyama vingi hatuogopi, tunawatangulia wananchi katika kuonyesha njia kuondoa hofu.

Na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamefunguliwa kesi nyingi za kubambikizwa.

Hadi vituo vya polisi, mahakama vimekuwa sebule za nyumba za viongozi wa vyama vya upinzani.

Watanzania watakumbuka Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo katika kampeni yeye na wafuasi wake walipigwa mabomu na marungu na kisha kuangukia kwenye mitaro kwa ajili ya kufanya maandamano na mkutano wa amani.

Sasa leo hii hayo yote yatabaki kuwa ni historia kwa kuwa hivi sasa tupo huru kufanya mikutano ya hadhara kwa kutoa taarifa tu kwa polisi, si kuomba tena kibali kwa Mkuu wa Wilaya yeyote na polisi anawajibika kutoa ulinzi kwa sababu wapinzani na wafuasi wa vyama vyao hivyo ni sehemu ya jamii.

Hakika ni mabadiliko makubwa sana na mtu atakayebeza vyama vya upinzani havijaleta mabadiliko tangu vianzishwe, basi mtu huyo atakuwa ni hayawani.

Nenda kwenye utawala bora, watendaji wa vijiji na wa kata enzi hizo waligeuka miungu watu, wananchi walipigwa kwa kukosa fedha za kuchangia mbio za Mwenge, wakaporwa mali zao na viongozi hao.

Hivi ninavyosema, manyanyaso hayo yamepungua, hasa jimbo ninaloliongoza la Karatu, na sehemu nyingine kama Bariadi Mashariki, Tarime na Kigoma.

Katika miaka hiyo ya nyuma, watendaji wa vijiji walikuwa wanakwenda kwa wanavijiji wanataka ng’ombe kinguvu na mwanakijiji akikataa kutoa anabambikiwa kesi za mauaji ambazo hazina dhamana. Kwa sababu upinzani umeimarisha utawala bora, watu hawanyamazi wanaongea yanayowakera, kwa hiyo haya nayo ni mabadiliko ya msingi.

Uhuru wa magazeti baada ya mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanzishwa umepanuka, leo magazeti, redio na televisheni ni nyingi sana.

Zamani tulikuwa tunasikiliza habari zinazohusu nchi yetu kupitia BBC ya Uingereza na Deutschewelle ya Ujerumani.

Sisi kama CHADEMA tupo mstari wa mbele tangu kuanzishwa mfumo huu, hasa uchaguzi wa mwaka 1995, baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, chama chetu kiliingia bungeni na kutumia nafasi yetu nje ya Bunge.

Kazi tuliyoifanya, matokeo yake CHADEMA ilikubalika kwa wananchi na hatimaye kupata halmashauri tatu za Hai, Karatu na Kigoma. Na katika maeneo hayo, kulifanya CCM kuwa chama cha upinzani jambo ambalo ni mabadiliko kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita ya enzi ya mfumo wa chama kimoja.

Kazi ya maendeleo iliyofanyika Karatu, wananchi walikichagua tena CHADEMA kwa sababu kilileta maendeleo.

Mwaka 2000 Karatu ilikuwa na sekondari moja iliyokuwa imejengwa kwa nguvu za wananchi.

“Leo Karatu inakamilisha sekondari 22… wakati Serikali ya CCM inazungumzia ujenzi wa sekondari katika kata, chama chetu Karatu kimeishamaliza ujenzi wa sekondari katika kila kata,” anasema.

Wakati leo serikali inazungumzia ujenzi wa zahanati kwenye kata, mpango ambao haujaanza, Karatu mwaka 2001 imetekeleza ujenzi wa zahanati katika vijiiji kwa mujibu wa sera ya chama chetu.

Kimsingi serikali tumeionyesha njia katika mambo mengi na inatufuata. Ndiyo manufaa ya ushindani na mfumo wa vyama vingi.

Vivyo hivyo vjiiji vya Karatu karibu vyote vinapata mradi wa maji na kimsingi si kwa mkono wa serikali na isipokuwa vijiji 10 kati ya 45 ndani ya jimbo hilo vinapata maji toka mradi wa Benki ya Dunia (WB).

Nasisitiza haya ni matokeo ya kushindanisha, Karatu haisubiri serikali, tunatafuta kwa njia zetu na ndiyo maana tangu nimeingia bungeni sijawai kuiomba serikali inijengee zahanati wala shule, ila serikali kuu inaposaidia pale ni jukumu lake.

Leo hii mbunge anasimama analialia na kuomba serikali imjengee shule, anapewa jibu na wizara husika arudi kwenye halmashauri yake jambo ambalo ni tusi, kana kwamba mbunge amekurupuka kutoa ombi hilo bila kupitia au kuwasiliana na halmashauri yake.

Sasa kulialia huko hakuwezi kutokea kwa mbunge toka kambi ya upinzani, kwa sababu anajua kabisa anachokitaka kwa serikali.

Ni wajibu wa Serikali Kuu kutekeleza mahitaji ya wananchi wa jimbo husika kwa kuwa wananchi hao ni sehemu ya walipa kodi wa nchi hii.

Na hali ya kulialia ufanywa na wabunge wengi wa CCM kutokana na mfumo wa chama chao ulivyo.

0755 312 859
katabazihappy@yahoo.com
www.katabazihappy.blogspot.com
 
Mzee,Mtei amenifurahisha hebu soma hapa.

Pia anajibu maswali mengi amabyo yameulizwa hapa na wakina mgongo na wenzake.

Edwin Mtei

KUTOKANA na kusambaratika kwa iliyokuwa Jamhuri ya Muungano wa Sovieti (Union of Soviet Socialist Republics) na kukoma kwa Malumbano ya Vita Baridi (Cold War) baina ya mataifa ya Magharibi na ya Mashariki miaka ya mwisho ya 1980, serikali nyingi za kimla na mitindo ya utawala wa chama kimoja ilianza kuporomoka.

Wimbi la kuwa na tawala za kidemokrasia liliIkumba Afrika. Hapa kwetu Tanzania, Rais Ali Hassan Mwinyi aliteua Tume ya Jaji Francis Nyalali ili ishauri jinsi mfumo na utaratibu wa vyama vingi vya siasa ungeweza kuingizwa katika siasa na utawala wa nchi yetu.

Ikumbukwe kwamba wakati wa uhuru mwaka wa 1961, katiba ya nchi yetu ilikuwa inaruhusu vyama vingi vya siasa, lakini kutokana na sababu mbalimbali, baada ya 1965, ni TANU na ASP tu vilitawala na katiba ilirekebeshwa rasmi 1977 na kutamka bayana kwamba CCM pekee ndiyo chama cha siasa Tanzania.

Mimi binafsi nilifurahia sana uteuzi wa Tume ya Nyalali ambayo ingeturejesha katika mfumo wa vyama vingi. Wakati Ripoti ya Nyalali ikijadiliwa bungeni, nilikuwa nakaa muda mwingi Dar es Salaam kwa vile nilikuwa nakamilisha ripoti ya Tume ya Rais iliyokuwa ikitathmini kodi, mapato na matumizi ya serikali, ambayo nilikuwa mwenyekiti wake.

Watanzania wengi waliokuwa wanajua misimamo yangu kisiasa na kiuchumi, walinishawishi na nikakubali tuanze chama cha siasa mara tu katiba itakaporuhusu. Tulianza majadiliano, na hawa jamaa wakanitaka niwe mwenyekiti wao.

Kwa kweli nahisi hata niliharakisha kukamilisha ile ripoti ya tume yangu ili niwe huru kushughulikia suala la kuunda chama kipya cha siasa.

Ilipojulikana kwamba Mtei anashiriki katika kuanzisha chama, viongozi wengi wa CCM na serikalini walinijia kuzungumza, na kwa vile tulijua tutafanya mambo kihalali, nilikuwa wazi kwao na wakati mwingine nilijaribu hata kuwataka wafikirie kutuunga mkono.

Itakumbukwa kwamba, hatimaye Edward Barongo ambaye alikuwa kada wa TANU/CCM na alishika nyadhifa nyingi zikiwemo Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa, alituunga mkono na Kamati ya Maandalizi ilimteua tukaungana kutia saini katika fomu za maombi ya CHADEMA kusajiliwa kwa awali.

Hata hivyo, wakati huo ndipo hasa Usalama wa Taifa walikuwa wakifuatilia napata wageni gani nyumbani au ofisini; nakula na nani chakula cha mchana n.k. Waliweka hata gari nje ya geti la shamba langu Arusha, wakisimamisha na kuuliza majina ya kila mtu aliyenitembelea.

Hii ilinilazimu kuonya wakati tukizindua CHADEMA na kampeni za kupata wanachama kwamba ni hatari kwa Idara ya Usalama wa Taifa kudhani na kufanya kazi kana kwamba ni Idara ya Usalama wa Chama Tawala badala ya usalama wa Tanzania yote kama taifa. Ni jambo la kusikitisha kwamba hadi leo, miaka 15 baadaye, idara hii ingali inaendelea na kasumba hii.

Fursa ya kuunda chama mbadala kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na hasa kutokana na uzoefu wa wengi walioshiriki, ilitulazimu tubuni falsafa na sera ambazo kutekelezwa kwake kungeepusha taifa letu kurudia makosa ya zama za ujamaa, zenye sera ambazo hazikuwa na tija na zilisimika uendeshaji wa kiimla.

Tulisisitiza katika sera zetu kwamba, wananchi ni lazima kuamua kwa uhuru kamilifu na kwa ujasiri mambo yahusuyo maendeleo ya taifa lao na kuepukana na utawala wa kiimla.

Rasilimali za nchi ni lazima zitumike kunufaisha wananchi na mazingira ya uendeshaji wa uchumi hayana budi kuwezesha wazawa kupiga hatua zitakazorekebisha ufinyu wa maendeleo kwao, uliotokana na historia ya ubaguzi wa kikoloni.

Hata hivyo, sera zetu zilitamka kwamba serikali ina wajibu wa kuweka mazingira yanayowezesha mitaji na teknolojia kuingia nchini. Uhuru wa soko ndiyo njia endelevu ya kuvutia mitaji ya ndani na nje kuharakisha kutumika kwa rasilimali za nchi yetu.

Mazingira ni lazima yawekwe kuhakikisha wananchi wanajituma kwa kadiri iwezekanavyo kupata kipato chao wenyewe. Papo hapo, wasiojiweza na wale ambao hawatapata ajira watadhaminiwa na umma. Miundombinu ya kiuchumi na ya kijamii itamilikiwa na umma au kwa ubia pale inapolazimu, na itaendeshwa kwa utaalamu na kisayansi. Miradi ya umma iliyobuniwa kwa pupa na kisiasa na ambayo inagharimu taifa bila tija, kwa mfano, kuhamishia makao makuu Dodoma, itatathminiwa upya.

Katika kuanzisha CHADEMA, hatua za makusudi zilichukuliwa kuhakikisha chama kinasambaa nchi nzima. Tulihakikisha kwamba kila kiongozi anayechaguliwa au kuteuliwa ana historia ya kiuadilifu, ni mzalendo wa kweli kweli mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake.

Makamu Mwenyekiti Bara alikuwa Brown Ngwilulupi toka Mkoa wa Mbeya aliyebobea katika fani ya ushirika. Katibu Mkuu, Bob Makani alitoka Shinyanga, mwanasheria mashuhuri aliyepata pia kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu.

Makamu wake Bara, Eric Mchatta alikuwa mzaliwa wa Mkoa wa Mtwara, mwanasheria machachari. Nimekwisha mtaja Barongo kutoka Kagera ambaye alikuwa Katibu Mwenezi. Mwenyekiti wa wanawake alikuwa Mary Kabigi, mzaliwa wa Mbeya, ambaye hapo awali alikuwa kada shupavu wa CCM na Mkuu wa UWT, Dar es Salaam. Vijana wa CHADEMA walimchagua Freeman Mbowe kuwa mwenyekiti wao.

Tulihakikisha kwamba Kamati Kuu ya Taifa ilikuwa na wajumbe kutoka kila mkoa. Ninaokumbuka majina yao ni George Wassira (Mara), Bujimu (Mwanza), Kivuyo (Arusha), Alphonce Maskini Dar es Salaam, Mama Costa (Morogoro), Kabugimila (Kagera), Philemon Ndesamburo (Kilimanjaro), Medard Mutungi (Dar es Salaam), Kasisiko (Kigoma), Victor Kimesera wa Kiteto (Manyara), aliyebobea katika fani ya menejimenti ya kibiashara na Mziray (Tabora).

Mweka Hazina alichaguliwa Kanali mstaafu Geoffrey Marealle, mfanyabiashara aliyekuwa na mawasiliano mazuri sana na wafadhili waliotuwezesha kupata vifaa na fedha, hasa za ndani, muhimu sana pale mwanzoni.

Sikuwataja wawakilishi toka Zanzibar na Pemba kwa vile lawama zilizolenga CHADEMA zilihusu ukanda na ukabila. Narudia tena kwamba kiongozi yeyote makini hawezi kubagua na kuwazuia watu wenye uwezo kuchaguliwa eti kwa vile wana uhusiano wa karibu naye.

Kukua kwa CHADEMA

Baada ya uzinduzi rasmi Agosti 1992, ambapo falsafa, misimamo na sera za CHADEMA zilifafanuliwa kwa uwazi na ujasiri wa aina yake, Watanzania wengi sana walijitokeza na kujiunga na chama.

Tulilazimika tu kwenda Unguja na Pemba ili kupata ile idadi ya wanachama 250 katika kila mkoa ili tupate usajili wa kudumu. Hata Unguja na Pemba nilifanya mikutano minne tu na kukamilisha idadi ya kutosheleza kwa usajili wa kudumu.

CHADEMA tuliweza kupeleka maombi ya kupata usajili wa kudumu mwisho wa Septemba 1992, tukiambatanisha orodha za majina ya wanachama na anwani zao kwa mikoa iliyohitajika kisheria. Nahisi vyama vya NCCR na UMD navyo viliwasilisha maombi hayo mapema.

Kwa vile Msajili wa Vyama vya Siasa alihitaji muda kuhakiki katika mikoa yote, CHADEMA hatukupata cheti cha usajili wa kudumu hadi Januari, 1993, wakati NCCR na UMD pia nao walipewa.

Licha ya kwamba kukua kwa CHADEMA kulikuwa kunaridhisha, msimamo wetu tangu mwanzo ulikuwa kwamba ni lazima vyama vya upinzani vyenye mwelekeo usiotofautiana sana, viungane ili kuweza kuiondoa CCM madarakani.

Kama hilo haliwezekani hapo mwanzo, basi ni lazima kupata wabunge wa kutosha kuikosoa serikali kikamilifu kwa nia ya kuimarisha utendaji wake. Kwa hiyo tuliwakaribisha kwa dhati wale viongozi wa vyama vilivyoshindwa kupata usajili wa kudumu na kuwapa nafasi za kuteuliwa kitaifa na kimkoa. Wengine walichaguliwa na kushika nyadhifa mbalimbali.

Juhudi za kuunganisha wapinzani zilitupeleka hata kwa Oscar Kambona aliporudi Tanzania, lakini aliamua kuunda TADEA. Hata hivyo iliwezekana kuwa na mkutano wa vyama Zanzibar ambapo vitano vilikubaliana kwa pamoja kuunda chama kimoja ambacho kingeweza kukabiliana kikamilifu na CCM.

Ili kuepuka mbinu za Serikali ya CCM kutucheleweshea usajili wa kudumu, iliamuliwa chama kimojawapo kiombe kubadili jina rasmi, na baada ya hapo vyama vingine vijiunge nacho na kuacha kujiendesha kama chama pekee. CHADEMA kilichaguliwa kibadilishe jina, kijiite Umoja wa Demokrasia Tanzania (UDETA), na tulianza majadiliano na msajili mara moja, ambaye alikiri hakukuwa na pingamizi lolote kisheria kubadilisha jina.

Kabla ya Kamati Kuu ya CHADEMA kukamilisha maandalizi ya kubadilisha jina, kulikuwa na mlipuko wa kisiasa katika vyama vyote vilivyokubaliana kuunda UDETA.

Hasa katika NCCR, hata Katibu Mkuu wake alijiuzulu pamoja na viongozi wengine mahiri na kuunda chama kingine, Mageuzi Asilia, wakidai viongozi wao waliokubali UDETA hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo. Pingamizi nyingine zilijikita katika dhana kwamba CHADEMA ilitaka “kumeza” vyama vingine, viongozi wa CHADEMA walikuwa na uroho wa madaraka n.k.

Hata katika CHADEMA kuliibuka upinzani, lakini iliwezekana kuepusha mgawanyiko mkubwa. Kikao cha Baraza Kuu ambacho kilikasimiwa mamlaka ya kubadilisha jina na kuunganisha nguvu na vyama vyenye misimamo inayofanana na yetu, kiliamua kwamba tuombe tu kibali cha kubadilisha jina pale tutakaporidhika kwamba kuna chama kingine kinachodhamiria kuungana nasi.

Nahisi kwamba kushindwa kwa juhudi hizi za kuungana kulikuwa na mkono wa mbali wa wenye madaraka na wanaotaka kudumu daima katika mtandao wao wa wanyonyaji wa nchi yetu.

Hadi leo tumeendelea na mtindo wa kuongeza vyama vya siasa mpaka tumefikia 17. Hii ni idadi ambayo haiingii akilini eti kwamba vyote hivi vimetimiza masharti ya kusajiliwa, likiwepo lile la kuwa na wanachama 250 katika kila mkoa, ikiwepo ile ya Pemba.

Ikichukuliwa kwamba CUF na CCM wana zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa Pemba kama wanachama wao, na CHADEMA asilimia 5, basi hivyo vyama vingine 14 vikigawana hiyo asilima 10, haviwezi kufikia idadi ya 250 inayotakiwa kusajili chama cha siasa kwa kudumu.

Je, Msajili wa Vyama vya Siasa ametekwa nyara pia na hawa walarushwa wanaotegemea udhoofu wa upinzani bungeni ili kuendelea “kula”? Mbona hata TAKURU wasitumike kusaidia Msajili kupata wanachama wa dhati?

Si kosa la jinai kuwa mwanachama wa chama zaidi ya kimoja na kumpotosha Msajili katika uandikishaji upya wa vyama? Kwa nini vipengele hivi vya Sheria na Katiba havitumiki? Hii inadhihirisha dhana kwamba usalama wa taifa umegeuzwa kuwa usalama wa chama tawala.

Tukirudi katika kukua kwa CHADEMA, mbinu zetu za kushirikisha kila rika, jinsia na vikundi vya kijamii zilituwezesha kukua haraka. Mwisho wa 1993 tulipotakiwa kupima uwezo wa vyama vipya vya siasa katika uchaguzi mdogo wa Ileje, tulikubaliana na NCCR- Mageuzi kwamba tungewaunga mkono Ileje endapo nao wangetuunga mkono katika uchaguzi mdogo wa Kigoma-Ujiji ambao ulikuwa ufanyike baada ya wiki kadhaa. NCCR-Mageuzi waliibuka chama cha pili baada ya CCM kutokana na umoja huo.

Katika uchaguzi mdogo wa Kigoma-Ujiji, CHADEMA tuliweka nguvu zetu zote na Kamati Kuu tulihamia Kigoma kumpigia debe Amani Walid Kabourou, tuliyemleta toka Amerika ambako alikuwa mkufunzi.

CCM walimsimamisha Azim Premji, mfanyabiashara, na wao pia walijikita kumfanyia kampeni kubwa ya kitaifa, mpaka hata Rais Mwinyi mwenyewe kama Mwenyekiti wa CCM, akaja na ndege ya serikali kupingana na sisi.

Matokeo ya kura yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi yalimpa Premji ushindi wa chupuchupu, licha ya kwamba ilikuwa ni lazima kurudia kuhesabu katika vituo kadhaa tulipohisi tume ilikuwa inampendelea Premji.

Kabourou alikwenda Mahakama Kuu akisaidiwa na kuwezeshwa na CHADEMA, kutaka matokeo yatenguliwe kwa misingi kwamba kura hazikuhesabiwa kiusahihi, kampeni hazikuwa za kisheria na za sawa kwa vile vifaa vya serikali vilitumika, na pia kwamba Premji hakuwa raia halali wa Tanzania.

Baada ya muda ambapo kesi iliahirishwa mara nyingi, huku Premji akihudhuria Bunge kama mbunge halali, Mahakama Kuu ilitengua uchaguzi na kuamuru urudiwe. Ilikubaliana na Kabourou kwamba vifaa vya serikali vilitumika kinyume cha sheria na Premji hakuwa raia halali wa Tanzania. CHADEMA tulishangilia, tukijiamini kwamba tungeing’oa CCM pindi uchaguzi utakaporudiwa.

Tulishangazwa na CCM pale ilipokata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, badala ya kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi. Rufaa ilichukua muda mrefu kusikilizwa rasmi, majaji wakitupiga tarehe na kuahirisha usikilizaji kwa sababu mbalimbali.

Mwishoni rufaa iliposikilizwa na kutupiliwa mbali, ilikuwa imebakia miezi michache tu kabla ya Uchaguzi Mkuu, ambapo sheria inatamka uchaguzi mdogo usifanyike katika kipindi hicho.

Kwa hiyo, mbinu zilitumika kuhakikisha CCM haikai pamoja na mbunge wa upinzani katika lile Bunge. Na wananchi wa Kigoma-Ujiji wakaendelea bila mwakilishi bungeni mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 1995 wakati Kabourou alipochukua kiti chake kwa kumbwaga tena Premji wa CCM.

Uchaguzi Mkuu wa 1995 na wa 2000.

Uchaguzi Mkuu wa 1995 ulifanyika wakati CHADEMA tukiamini kwa dhati kwamba ni lazima vyama vishirikiane ili kuishinda CCM au hata ili kupata viti vya ubunge vya kuridhisha na kutoa changamoto stahiki kwa chama tawala.

Kwa hiyo, CHADEMA kilimuunga mkono Augustine Lyatonga Mrema aliyeingia katika kinyang’anyiro cha urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi. Mrema hakushinda, lakini NCCR iliibuka chama cha pili, baada ya CCM, ikichukua nafasi yetu.

Tulishindwa kwa sababu nyingi, lakini hasa kwa vile vyama vishiriki havikuweza kuachiana viti ili kujiimarisha dhidi ya CCM. Vivyo hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2000, CHADEMA tuliiunga mkono CUF ili Profesa Ibrahim Lipumba achaguliwe rais. CHADEMA pia hapa tuliibuka chama cha tatu, na CUF tuliyoiunga mkono ikawa ya pili baada ya CCM.

Kutokana na mafunzo haya, CHADEMA tulianza mapema kujaribu kuimarisha chama na kuamua ni lazima katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 tuweke mgombea kiti cha urais. Pamoja na kujaribu kufufua chama kuanzia ngazi za shina mpaka taifa, tulitathmini kwa kina muundo, sera na mikakati ya chama, tukijaribu kuingiza vijana wenye vipaji na wanazuoni katika ngazi mbalimbali za uongozi wa chama.

Kutokana na kuporomoka kwa maadili kitaifa, rushwa na ufisadi kuzidi na umaskini wa kutupwa kukithiri nchini, sera na dira ya taifa ni lazima itilie mkazo uzalendo na elimu ya uraia mwema katika mwelekeo mpya wa taifa.

Sera zetu endapo tutachukua dola ama katika kuchangia bungeni kutoa changamoto kwa chama tawala, ni lazima zisisitize tathmini ya mikataba mibovu inayolipeleka pabaya taifa letu katika utekelezaji wake.

Uchaguzi Mkuu wa 2005

CHADEMA tuliendelea na msisitizo wetu wa kusimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2005. Mwenyekiti wetu mpya kuanzia 2003, Freeman Mbowe, akishirikiana hasa na wabunge wenzake wa CHADEMA, waliweza kuhamasisha ufufuaji wa chama nchi nzima.

Tulimchagua awe mgombea urais wa CHADEMA, papo hapo tukikaribisha vyama vingine kushirikiana nasi katika Uchaguzi Mkuu huo. Lakini badala yake, vyama vilivyosimamisha wagombea urais vilikuwa vinane, vingi kuliko wakati wowote katika historia yetu.

CHADEMA tulionyesha ubunifu wa hali ya juu na tuliweka wagombea ubunge na udiwani wengi kuliko wakati wowote katika historia yetu. Nahisi CCM ilichekelea kuona kwamba mbinu zake za kuwagawa wapinzani kwa kuongeza idadi ya wagombea zilifaulu.

Licha ya kwamba mgombea wetu alikuwa na mvuto wa aina yake na wananchi wengi walifurika kwa maelfu kwenye mikutano yake kumsikiliza, CCM na mgombea wao Jakaya Kikwete walimwaga fedha za ukarimu na zawadi za khanga, vitenge, fulana, kofia na mavazi mengine Tanzania nzima kiasi cha kutisha.

Chama tawala kilikwisha kujitengenezea uhalali wa kuwapa wananchi hongo hiyo ya vyakula, vinywaji na mavazi kwa kupitisha sheria katika Bunge lao kutamka kwamba hiyo “si rushwa bali ni utamaduni wa ki-Tanzania kutoa takrima!”

Si tu katika Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, bali hata katika uchaguzi wa ndani miongoni mwa wana-CCM, mizengwe na kuhongana kwa hali ya juu kulitia fora, wakisema ni “utamaduni wa takrima Tanzania!”

Ili kuleta uwazi na demokrasia ya kweli katika kumpata mgombea wetu wa kiti cha rais, Mbowe, awali ya yote alikuwa amechaguliwa na mikutano mikuu ya CHADEMA katika kanda sita za Tanzania. Wana-CHADEMA waliojitokeza kuwania huo ugombea walipewa fursa ya kuhutubia mikutano kadhaa katika kanda, wakielezea jinsi wangetekeleza sera katika Ilani ya CHADEMA kama zilivyoainishwa.

Hawa wagombea walipigiwa kura na wajumbe wa hiyo mikutano mikuu ya Kanda, na Mbowe aliibuka na ushindi wa takriban asilimia 84. Ni ubunifu huu uliosababisha CHADEMA kujivunia kuwa mgombea wao alikuwa safi na kwamba hakukuwa na chembe ya mizengwe kama katika teuzi nyingine, ukiwepo ule wa chama tawala.

Hata hivyo, licha ya uwazi na umahiri wa mgombea wetu, fedha zilizowekezwa na wale wote wanaotaka kudumisha utawala wa CCM zilifanya kazi.

Iliwezekana kwa CHADEMA kukodisha ndege ya helikopta ili imwezeshe mgombea wetu kuwafikia Watanzania wengi iwezekanavyo na katika maeneo ambayo miundombinu yake haingeruhusu kufikiwa kwa wakati huo.

Mbowe aliweza kufanya mikutano hata zaidi ya sita kwa siku na Watanzania wengi walitambua hali halisi ya nchi yao kupitia msemaji wa CHADEMA.

Mwishoni uchaguzi ulifanyika tarehe 14 Desemba, 2005. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo wapinzani wameipigia kelele kuhusu muundo wake na uteuzi wake tangu mwanzo wa demokrasia ya vyama vingi, ikafanya mambo yake.

Katika majimbo karibu yote ambapo wapinzani walikuwa na nguvu, wasimamizi wa NEC walichelewesha kutangaza matokeo kwa sababu ambazo hazikuweza kuelezeka.

Matatizo mengine yaliyotokana na kutokuwa na wakala wa vyama vya upinzani katika vituo vingi nchini ni mengi. Kwa mfano mahala ambapo ndugu wa karibu wa mgombea walipigia kura, matokeo yalionyesha kuwa mgombea hakupata kura yoyote!

Basi ni kwamba kule ambako wagombea ubunge CCM walikuwa hawakupingwa, labda mgombea wao wa urais, alipewa kura zaidi ya asilimia 100.

Kwa mantiki hiyo, mimi binafsi sikuona ni ajabu kwamba matokeo yaliyotangazwa mwishoni yalimpa Kikwete zaidi ya asilimia 80, hasa ikijumuishwa kwamba umaskini uliokithiri Tanzania uliwafanya wengi wauze kura zao kwa waliowakarimu, itaonekana ni dhahiri kwamba CCM “ingeshinda”.

Wahenga wanasema siku za mwizi ni arobaini. Kwa bahati nzuri kwa Watanzania, Mahakama Kuu imetengua Sheria ya Takrima kwa kutamka kwamba ni batili na ni kinyume na katiba yetu.

Jinsi siku zinavyosonga mbele, maofisa mafisaidi wanafichuliwa, licha ya ufisadi wao kuendelea kulemea wananchi maskini na kufanya maisha yao yawe na ugumu usiovumulika.

Papo hapo vijana wabunifu, wajasiri na wasio na woga wanaongezeka siku hadi siku chini ya mwavuli wa CHADEMA wakichambua madhara haya na kuwafanya wananchi wawe jasiri kuamua ni chama gani na kiongozi gani atawakomboa. Iko siku kitaeleweka!

Mwandishi wa makala hii, Edwin Mtei aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Waziri wa Fedha na mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Anapatikana kwa simu namba 0754 387 177
 
Naamini mara baada ya kusoma na kutafakari kwa kina kuna kila sababu ya wale wote ambao lengo lao ni kuupotosha ukweli waweze kusoma na kuelewa baadhi ya haya ili kuweza kuleta tija kwenye taifa letu na nchi yetu kwa ujumla.

Tuangalie jinsi ambavyo bunge letu kule Dodoma linavyofanya mambo ya aibu hebu fikiri kama wapinzani wasingekuwa kule Dodoma je tungesikia mambo gani kwa hali hii ya aibu?

Upinzani umefanya kazi kubwa na ya maana sana kwenye nchi hii hebu tuwe wakweli na wenye kuona mambo ya kweli pale ambapo yanaonekana .

Tuache ushabiki ila tuzungumze ukweli halisi wa mambo.
 
Well, zitaandikwa makala ndeeefu lakini the bottom line ni kwamba upinzani na idea ya alternative path for our country inakwazwa na aina ya viongozi wa upinzani tulio nao. We are stuck between a rock and a hard place. We may have monsters running the government now, but the type of the opposition we have now would be disastrous.

Here is my take of those at least making the news:

Ibrahim Haruna Lipumba – the only serious chap in the pack, but the real CUF power resides in Zanzibar therefore Maalim Seif, a decent and honourable man by the way, is the real broker. The good Prof. is simply being used. He is of better use in the lecture hall.

John Momose Cheyo – a delightful and jolly chap whom I would rather have as a beer buddy, but not my commander in chief. He squandered his riches in profligacy (due to poor education I reckon) and drove UDP, with a potentially strong Sukuma constituency, into a fringe party. You know what I would love to see replayed? His shouting match with Amani Jidulamabambasi. Priceless!

Augustine Lyatonga Mrema – His transformation from the most feared man in the country to a frail wisecrack was sad to watch. I would rather see him acquire a spot in the Ze Comedy.

Joseph Mbatia – Mbatia who?

Christopher Mtikila – lawsuit anyone?

Freeman Aikaeli Mbowe – the transformation from a lazy BOT receptionist, to a Disc Jockey, to a heavily indebted struggling businessman, to a Commander in Chief of the Armed Forces of the United Republic of Tanzania would be one for the history books. His efforts to master Thomas Hobbes, as a way to propel the transformation, is delusional. Intellectualism and leadership cannot be feigned. A love affair with colonialism and slavery is not what the people of Tanzania want in their leader. How about a chat with Rashid Kawawa, Aboud Jumbe, Abdalla Natepe, et al – to appreciate, for better or for worse, what this country is made of.

In the end, I think the idea ya Wachina kuandaa viongozi toka mapema is brilliant hata kama it is boring kwasababu it is predictable. Sisi tunabahatisha tu...hata DJ, baada ya kuwaona wacheza disco wenzake wanakuwa Mawaziri, ndio inakuwa motivation yake kuingia siasa na anataka kuwa Rais. This is a disaster for our country, I am telling you.
 
...mrushiano wa madongo!

...wengine ngoja tuangalie nani atapata vumbi zaidi!

...ila tunafaidika kufahamu mambo!
 
"We are stuck between a rock and a hard place. We may ('we have') have monsters running the government now, but the type of the opposition we have now ------" mugongo mugongo # 10, - is incapable of launching the second liberation of Tanzania. A new crop of leaders has to emerge from within CCM and the waShindanis. Otherwise, we're headed for trouble for a long time.
 
"We are stuck between a rock and a hard place. We may ('we have') have monsters running the government now, but the type of the opposition we have now ------" mugongo mugongo # 10, - is incapable of launching the second liberation of Tanzania. A new crop of leaders has to emerge from within CCM and the waShindanis. Otherwise, we're headed for trouble for a long time.

I agree with your re-formulation.
 
Upinzani is almost dead, there is no Upinzani in Tanzania. What Tanzania have is bunch of greed people gather together for their personal interest either economically or socially.

We have few who are real opposition, but due to a lot of dubious in there parties they're facing natural death. Zito Kabwe is very energetic, young star, however he is still perform college politics. When you fight with giant like CCM you have to set strategies, plan and then program.

Here is what upinzani can do to rise and help Tanzanian people.

First, All those greed leaders who leads for years because they are founders of those parties need to go.This includes Cheyo,Lipumba, Mrema and alot of others.

Second, politics is like a soccer, if your team don't play well you don't change rules, what you does is you create a competitive team. However competitive team start at the grass root, so what you do is, you change the whole spectrum of your parties and you attract more people, example CHADEMA.

Third, you create short and long term goals, and for those short term goals you put more pressure on them and make sure they're achievable.

Those are just few of the ideas that Upinzani need to do. Honest 15 years as just pass by.
 
.., Lakini Sasa Hivi Baba Huyo Huyo Anakadi Ya Chadema Lakini Anaendesha Gari Ambayo Kwambele Katika Kioo Kuna Kabendera Cha Ccm Pale

Sikumoja Alikuwa Anafungua Shule Yake , Basi Kule Wizarani Wakamfanyia Mbovu Sana Kwa Sababu Yeye Hakuwa Mwanaccm Enzi Hizo Mwaka 1995 Alitakiwa Achangie Chama Cha Mapinduzi Akakataa Kwahiyo Wakaondosha Hawakusajili Shule Yake

Ahsante


Shy,
Rejea kauli ya Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Sumaye,

Alipokuwa Moshi alisema hivi" Wafanyabiashara mkitaka mambo yenu yafanikiwe basi jiungeni na CCM!"

Mambo ndo hayo lakini iko siku historia itaandikwa upya.
 
Tokea vianzishwe vyama vya upinzani,baadhi yao vimekuwa havisikiki. Ni vyama viwili tu CHADEMA na CUF ndio vimekuwa mstari wa mbele kujaribu kuleta mabadiliko ya mawazo kwa watanzania wengi maskini.

Chadema kinajulikana kwa sera zake za marekebisho kwenye uchumi, na CUF vilevile kina sera zinazolenga mabadiliko ya kiuchumi. Pamoja na sera zingine kuhusu jamii na siasa.

Chama tawala CCM kipo madarakani tokea enzi hizo kila mtu anajua hilo. Kimejikita vilivyo na kuwa na mizizi sehemu zote. Chama tawala ndicho kinafaidi matunda ya kutawala. Kina pesa za kutumia kwa kuwa kimeshikilia hazina ya taifa na kinaweza kuomba pesa ya "wafadhili" kama zimepungua na hata bajeti ya Tanzania inafadhiliwa na nchi "wahisani" wakiipitia kwanza kabla ya ku-approve! na ndio inasomwa bungeni kwa mbwembwe.

Chama tawala kimeweka mfumo wa ulaji ndani yake. Humo kama wewe unataka kuwa mbunge basi ni lazima uwe mwanachama (hai) na hata kama umesoma kufikia u-professor na unaona mambo sio mazuri katika fani yako basi itabidi uchanganye na ubunge na matokeo yake wasomi wengi kwa sasa wameingia CCM na kuacha kazi zao za utafiti au NGOs.

Siasa za Tanzania bado ni za kukatisha tamaa.Kuna tabia ya watu kutumia wapiga kura kwa kuwadanganya kwa sera hizi na zile halafu mtu anaingia bungeni kwenda kutanua na kulitumia Bunge na Serikali kujinufaisha wao na familia zao na mpaka ukoo mzima.

Sasa vyama vya CUF na Chadema vina jukumu la kuhakikisha vinaunda chama kimoja chenye nguvu. Nasema hivo kwa sababu vyama hivi viwili tayari vina mtandao nchi nzima na hata nje ya nchi. Tulio nje tunahitaji kuvisaidia vyama hivi kimawazo, kifikra na hata kimipango kusimama ili "at least" tuwe na spika wa upinzani na zaidi ya wabunge nusu walio wapinzani.

Pili, vyama hivi vikiishaungana itabidi atafutwe mtu mahili katika ulingo wa siasa. Mtu huyu ni lazima awe mwenye "calibre" na "stature" ili aweze kuleta nidhamu hasa katika masuala ya mwafaka yanayochezeshwa marimba kwa sasa. Mtu huyu ni yule atakaeweza kugeuza meza kwa hoja zenye nguvu zitazoichemsha CCM na kuifanya ibadilishe strategy zake za kuyumbisha upinzani Tanzania.

Waheshimiwa Lipumba, Mzee Hamad, na Mbowe wawe na "vision".Ikumbukwe kwamba kwenye ulingo wa siasa kuna vigor,strategy,dedication,na committment vinahitajika sana katika karne hii ya 21.Haiwezekani mpaka leo ruzuku ikatoka katika chama tawala ni lazima kuwe na "special funds" ili ku-boost number of membeship applicants na suppoters.

Waheshimiwa naomba kutoa hoja.
 
Hoja yako ni nzito.. inabidi tuifikiri kwa kina. Hata hivyo swali la msingi ni wapinzani wanastahili kuaminiwa na wananchi? maana inaonekana wananchi wameshakata tamaa na wapinzani. Maana kila kukicha wao wanalalamika tu, tujiulize ni kitu gani wapinzani wafanye kujijengea Imani na kurudisha matumaini?
 
Kama wananchi kweli wamekata tamaa na wapinzani then we are doomed. Maana hao CCM ni mijizi ya kutupwa na hilo halina ubishi kwa sababu ushahidi upo zaidi ya kutosha. Sasa wapinzani bado hawajapata fursa ya kutuonyesha wanaweza kufanya nini lakini inaelekea watu wamewakatia tamaa...Wow!!!
 
Nyani, inabidi waoneshe uongozi kwenye vyama vyao kwanza kabla hawajapewa nchi. Kabla ya Uhuru vyama vya TAA na TAAA na vile vya wafanyakazi vilionesha uongozi na walipompata Mwalimu waliweza kukaa pamoja na kuunganisha vyama hivyo kikazaliwa TANU. Uongozi wa TANU haukuwa wa watu wenye mawazo yale yale lakini walijua ni nini wanachopigania na wengi wao waliweka pembeni matamanio yao binafsi na kuweka mbele ujio wa taifa lao jipya. Ni kutokana na mawazo hayo ndio maana machifu wetu wote walikubali kupoteza hadhi na nafasi za vyeo vyao na kuliweka Taifa mbele. Viongozi hawa walionekana KABLA ya Tanzania kuwa huru hivyo tunapopata uhuru na miaka 10 baadaye Tanzania ilikuwa inaanza kujitosheleza kwa kiwango kikubwa kiuongozi. Hata lilipotangazwa Azimio la Arusha 1967 ambapo waasia na wageni wengi waliamua kuondoka nchini wakitarajia kuwa Tanzania itavunjika, kuna wale waliobakia tukabanana nao humu humu.

Tatizo la wapinzani ni kuwa miaka 15 baada ya mfumo wa vyama vingi wameshindwa kujionesha wanastahili uongozi. NI kwa sababu hiyo ndio maana wengine tunajaribu kuwasaidia ili waonekane kama viongozi ili watakapopita tena kuomba nafasi ya uongozi basi watu watawaamini. Kwa jinsi wanavyoendelea sasa watu wanawaona wao ndio wasanii zaidi kuliko wale walioko madarakani.
 
Lakini kweli...hoja ya Leadership hata mimi nakubaliana nayo. Bado hawajainyesha Leadership kwenye mambo mengi. But kwa jinsi mambo jinsi yalivyo sijui ni kwa nini inachukua muda kupata uongozi makini. Nadhani kwa vile upinzani bado ni mchanga therefore it will take time. Hata Civil Rights struggles zilichukua muda kumpata MLK...kabla yake walikuwepo but it just needed that one person..him...to take the struggle to another level.
 
Nyani.. jambo ambalo linanisumbua sana ni kuwa bado kwenye upinzani hakuna watu ambao wengi wao hawajawahi kuwa CCM. Labda hati watakapoanza kuonekana watu ambao katika maisha yao hawajawahi kuwa CCM.
 
Sisi chadema pamoja na matatizo hayo ya kutoka kwa Akwlimbe lakini hauyumbi,Akwilombe alikuwa mtu mdogo sana,pamoja na uzuri wake katika jukwaa,sie bado ni watu makini.
 
maneno ya halikuniki ni mkosaji hayo, mana hata akitoka mnyika mtasema hivyo hivyo.

lakini ukweli CCM imepigapabaya, na si vyema CHADEMa kukurupuka wake chini wajipange wajiulize sana tena sana maana kuna kitu, tena kuanzia juu hadi chini.

mie siamini kule kigoma kama wale wote walipewa pesa kama tunavotakiwa tuamini.


ushauri ni kuundwa chama chengine kipya na hawa wazee wakae pembeni, wamejitahidi tuangalie nafasi ya wengine
 
Back
Top Bottom