Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Tatizo kwenye vyama vya upinzani ni ukosefu wa demokrasia ya ndani. Ni vema viongozi wakawapisha wengine na wao wakabakia wanachama waaminifu na wapiganaji.Kufanya hivyo watapata nafasi ya kuona matatizo wakiwa nje ya uongozi. Kwa sasa kukimbiwa na viongozi mbalimbali ni kutokana na hao kuona kuwa mbele kumezibwa. Tunawaheshimu viongozi hao waliokaa zaidi ya miaka kumi na historia itawajenga kama wakiachia ngazi badala ya kung'ang'ania madaraka. Si lazima tufuate, lakini nchi nyingi kiongozi hujudhuru iwapo ameshindwa kukiingiza chama chake madarakani..
 
Tatizo la vyama vya upinzani Tanzania nadhani haliko kwenye viongozi zaidi, bali liko kwenye mfumo mzima wa nchi kuhusu vyama vya siasa. Kwa vile chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu, inabidi kihudumiwe na wanachama wake wenyewe badala ya kutegemea ruzuku. Inawezekana nia ya serikali kutoa ruzuku kwa vyama ilikuwa nzuri lakini mfumo unaotumika unakipendelea chama tawala na kudumaza vyama vya upinzani. Kwa upande mwingine, serikali imakuwa inatumia mamlaka yake vibaya kuwanyanyasa watu wanaochangia vyama vya upinzani, na hivyo kuvifanya vitegemee ruzuku ndogo wanayopata kujiendesha. Maoni yangu yanarudi kwenye kutaka mabadiliko ya katiba kama ifuatavyo:
  • Kila chama kilichosajiliwa kwa msingi wa sheria kiwe na haki ya kupata ruzuku. Ruzuku inaweza kuwekwa mkatika makundi mawili au matatu: Vyama vikubwa, vyama vya kati na vyama vidogo kulingana na idadi ya wanachama wake na idadi ya matawi yake. Ni jukumu la ofisi ya msajili ku-audit vyama ili kuona kama kweli vinakidhi masharti ya kuwekwa katika kundi fulani. Kwa hiyo kunakuwa na viwango vitatu vya ruzuku. Kwa mfano vyama vikubwa vyote vitakuwa vinapewa ruzuku inayolingana bila kujali kuwa vilipata kura ngapi au vina wabunge wangapi, vile vile vyama vya kati na vyama vidogo. Ni vibaya kukinyima chama ruzuku eti kwa sababu hakikupigiwa kura wakati tunajua kuwa kila raia alikuwa na nafasi ya kupigia chama kimoja tu. Kama nia ya serikali katika kutoa ruzuku ilikuwa ni kutaka vyama viweze kujiendesha ili kuimarisha demokrasia, mtu unaweza kusema kuwa chama kilichokosa kura ndicho kipewe ruzuku zaidi kwa vile ndicho kinahitaji kujijenga zaidi kuliko kile kilichopata kura.

  • Kwa vyovyote ruzuku ya namna ya (a) hapo juu inaweza isitoshe kuendesha baadhi ya vyama vyenye ambition kubwa, kwa ni hiyo ni wajibu wa kila chama kuhamasisha wanachama wake kukichangia ili kiweze kujindesha badala ya kutegemea ruzuku. Michango ya vyama iwekewe utaratibu unaozuia watu wachache tu kukichangia chama fedha nyingi sana na kukifanya kama mali yao.
  • Serikali iwajibishwe kila inaponyanyasa raia wanaoshabikia vyama vingine zaidi ya chama tawala. Miaka ya tisini kuna wafanya biashara wengi walioshabikia vyama vya upinzani na kuvisaidia kifedha ili visitegemee ruzuku, lakini serikali ikatumia nguvu zake za dola kuwanyanyasa raia hawa kiasi kuwa wengi wao waliachana kabisa na shughuli za kisiasa na wengine waliamua makusudi kujiunga na CCM ili kulinda biashara zao. Mfumo huo ambapo serikali ilitoa upendeleo kwa wanachama wa chama tawala na kuwanyanyasa wale walioko upinzani bila kuangalia kuwa wao wote walikuwa ni watanzania wenye haki sawa mbele ya serikali ilikuwa ni makosa makubwa ambayo lazima yasahihishwe katika katiba. Katiba itenganishe kabisa kazi za serikali na kazi za vyama vya kisiasa.

Uyumbaji wa viongozi wa upinzani ni matokeo ya ruzuku kwa maana zote mbili: ruzuku kubwa ya CCM inatumika kununua viongozi na wanachama wa vyama vya upinzania, na ruzuku ndogo kwa vyama vya upinzani inawafanya viongozi ambao hawana njia nyingine za vipato kushawishika kirahisi na ruzuku ya CCM.
 
Huu ni uchambuzi "Yakinifu" mzee kichuguu!

Serikali yetu inawa-miss watu wa caliber yako.

Hitimisho lako ni kichomi kwa wengi, sometimes inabidi ukweli ukubalike kuwa 'ndiyo hali halisi'
 
Mimi nina mawazo tofauti kidogo. Upinzani Tanzania upo na upo strong sana tu, ila kuna kitu watu hawataki kukiweka wazi. CCM ni chama kikubwa, chama dola chama ambacho kila mtu mwenye nafasi ya ulaji atakitetea, kuanzia, Usalama wa Taifa, Polisi, Jeshi na hata watoa haki tunao waamini( Mahakama). Kinachofanyika sasa ni CCM kutumia fedha za walipa Kodi katika Research za mambo makuu matatu.
1. Ni jinsi gani watawahadaa wananchi na ulimwengu kwa ujumla kuonesha kuwa kuna Uwanja tambarare wa siasa

2. Ni jinsi gani watavuruga uchaguzi kisayansi pale wanapoona mambo mabaya kwao,( rejea uchaguzi 1995, Dar na 2005 Kifo cha Jumbe ( mgombea mwenza CHADEMA)

3. Ni jinsi gani wataweza kuiba KURA na kutumia ubabe kujitangaza washindi ( Hii ni mikakati, ambayo CCM inayokuanzia uchaguzi unapokamilika na mpaka mwingine unapofika)

Hapa ni kwamba hata CUF, CHADEMA,TLP na wengine wote wajiunge bado hakuna kitakachosaidia, kilichopo hapa ni wapinzani kuhamasisha wananchi nchi nzima, iwe maandamano kila siku mpaka katiba itakayo weka huru tume ya uchaguze na mambo mengine yapatikane.

Kwa mtazamo wangu Ili kuwe na Democrasia ya kweli lazima wapitikane "sacrificial lambs". Hapa nina maanaisha wapinzani wenyewe wawe tayari kufungwa au hata kupoteza maisha katika kudai democrasia, wakianza wao wananchi watawaamini. Lakini sio ku organise maanadamo halafu wewe unasema upo London kwenye Safari za kichama.

CCM itakuwa tayari kusikiliza wapinzani pale wapinzani watakapo pata Sauti ya Umma, Mfano 2001, CUF ilipoandaa maandamano na watu wakajitokeza pamoja na vitisho vya Kina Sumaye, Mkapa, mahita na WALA NCHI Wote, iliishitua CCM na ndio maana leo mnaona CCM inatumia Strategy ya Kununua muda kwa Muafaka ili CUF ikose nguvu ya Umma baada ya wananchi kukata tamaa na CUF na hapo CCM itaibuka kidedea. Msimamo wa CUF kutangaza Kilichojiri trh 15 aug 2007 uwe ni huo na wasibadilike, hapo Umma utawaamini kuwa kweli wapo makini na wanafanya wanachokizungumza. Wakinywea tu kwao ni Bao CCM inapata credit. Ukweli ni Kwamba CCM haipo tayari kuchangia nchi na chama chocho kile kwani watakuwa wanaingia mamluki wa kuyaweka mambo yao nje kitu ambacho si sera ya CCM, wao wanaongelea ndani hata kama mtu kaiba mabilioni ya nchi.

Wapinzani wawe tayari kupambana na kila mtu ambaye mrija wake upo kwenye buyu la asali la nyuki(a.k.a Tanzania), the whole system.
 
Halikuniki, kupoteza Makamu Mwenyekiti na Naibu Katibu siyo jambo dogo.

Mwanakijiji,

Kwanza lazima ujue kuwa kualalamika ni njia mojawapo ya kutoa taarifa kwa umma. Wapinzani wasipolalamika katikauonevu wa mfumo huu tulionao tutawashangaa. Kilio chao ndicho kitatumika kuwaamsha na wengine wanaoumia, na kuwashtua wanyanyasaji kwamba ubaya wao umejulikana zaidi na zaidi. Kuna mlalamishi kuliko Nyerere alipokuwa mpinzani? Ulalamishi wa TANU ndio ulioitangaza na kuikomaza. Bahati nzuri ya TANU wakaoloni weupe wa wakati ule walikuwa na dhamiri hai . (Conscience) Walitafsiri kilio cha Watanganyika, wakasoma alama za nyakati...njia kueleka uhuru ikawa nyeupe. Hawa wakoloni weusi wanaishi kama hawana dhamiri, ni wakatili na hawasikilizi, ndiyo maana hata wakiiba ukawakamata, hawajiuzulu ng'o!

Upinzani sasa unapambana na mijitu isiyosikia iliyo tayari hata kuua systematically. Halafu tunawalaumu? Hapana, mwanakijiji, hii siyo haki wanayostahili. Laiti wewe ungekuwa ulishashiriki harakati hizo mwenyewe physically, usingekuwa unasema hayo. Wewe unazungumza kinadharia tu. Njoo uonje joto la jiwe, tuone utaskuwa unasema nini baad aya miaka 13 ya kuteswa, kunyanyaswa na kudharauliwa, huku you don't see light at the end of the tunnel.

Sisi tunaoshuhudia manyanyaso yao, kwanza tunastaajabia ujasiri walionao hawa wanaoendelea kubaki opposition, na ndiyo maana tunasema ipo siku wapambanaji halisi watabaki wakati walio dhaifu wakijiondokea na kurudi CCM kupumzika. Ukombozi utapatikana.

Pili, kuhusu CHADEMA. CHADEMA hakitapoteza makamu mwenyekiti. Kaburu alikuwa mzigo kuliko msaada kwenye chama. Uzuri ni kwamba CHADEMA kimekuwa chama kidogo hado Mbowe alipochukua uongozi wa juu. zaidi ya hayo kimekuwa chama pekee kinachojua kushughulikia migogoro ya ndani bila kelele - a sign of maturity - wakati huo huo kikikosa watu wa kutosha wa kushiriki uongozi. Hiyo ndiyo sababu iliyomfanya Kaburu asijulikane ubovu wake.

Tangu chama hicho kilipokuwa targeted na serikali, ndipo tunakisikia sana kwenye vyombo vya habari. Lakini ukiondoa mchango wa kukisimika chama Kigoma katika miaka ya mwanzo ya harakati, Kaburu hakuwa na mchango mwingine uliohitajika sasa kwenye chama hasa baada ya kuzuiwa kuchota mapesa kama alivyokuwa amezoea. Kwa hiyo alipondoka chama kilipumua. Hivi wewe hushangai chama hakijajaza nafasi yake kwa zaidi ya mwaka licha ya mwenyekiti kuwa masomoni nje ya nchi? Hakuwa na kazi, na labda wameona wasiijaze sasa waende taratibu kwani ilikuwa waiz muda mrefu!

Akwilombe, sawa. Ila naye ameondoka kama waliomtangulia na watakamfuata ama kurejesha hesabu za kazi waliyotumwa miaka mingi, au kutafuta mahali pa kuponea nbaada yua kuhangaikia kwenye opposition bila matumaini ya kupata chohcote kesho. Ni haki yake ya kidemokrasia ingawa inamdhalilisha.
 
Skraga,

1st Post and lovely one! Keep such a move. Nikukaribishe jamvini... Karibu! Naomba kukunukuu:

Kwa mtazamo wangu Ili kuwe na Democrasia ya kweli lazima wapitikane "sacrificial lambs". Hapa nina maanaisha wapinzani wenyewe wawe tayari kufungwa au hata kupoteza maisha katika kudai democrasia, wakianza wao wananchi watawaamini. Lakini sio ku organise maanadamo halafu wewe unasema upo London kwenye Safari za kichama.

Mbuzi/kondoo wa sadaka waliisha! Labda tumlengeshe mwingine. Wengine wanajaribu lakini si ajabu ukasikia naye 'amerejea' kundini baada ya kugundua kuwa 'alidanganywa'.

Leo mimi na politiki tu :)
 
Niulize swali dogo:

Hivi hawa wanaokosa vyeo wakabadilika na kuhama chama kwenda kingine wakapokelewa kwa shangwe, hamwoni kama wao na wanaowapokea wana matatizo zaidi ya tudhaniayo?

Binafsi sipendezwi kabisa na watu wa namna hii. Tambwe Hizza sikutarajia hata siku moja awe alivyo sasa. Kabourou, Akwilombe etc. Upinzani unamong'onyoka kila kukicha. Nahisi upinzani hauko strong kama tunavyoambiwa hapa. Something is missing...

Wapi tunaelekea?
 
Niulize swali dogo:

Hivi hawa wanaokosa vyeo wakabadilika na kuhama chama kwenda kingine wakapokelewa kwa shangwe, hamwoni kama wao na wanaowapokea wana matatizo zaidi ya tudhaniayo?

Binafsi sipendezwi kabisa na watu wa namna hii. Tambwe Hizza sikutarajia hata siku moja awe alivyo sasa. Kabourou, Akwilombe etc. Upinzani unamong'onyoka kila kukicha. Nahisi upinzani hauko strong kama tunavyoambiwa hapa. Something is missing...

Wapi tunaelekea?

Kwa kuangalia mwenendo wa utendaji wa serikali usioridhisha, malalamiko ya wananchi yasiyoisha, upinzani uko strong. Tatizo sisi tutnaangalia upinzani kwa kuwatazama viongozi wa vyama. Ndiyo maana wanatajwa hapa wanaohama. Kwani Tambwe alipohama CUF walikosa mtu wa kufanyakazi yake? Ameondoka na wangapi? CUF imekwama wapi kwa sababu yake? hakuna mtu ambaye ni indispensable. Wataingia watatoka, mfumo utaendelea.

Kinachokosekana ni ujasiri wa wananchi kuwaunga mkono viongozi wachache waliojitokeza na wanaoendelea kuongoza harakati. Kama ni hoja zinasemwa sana. Wananchi wanaitikia "ni kweli" lakini wakiwa kwenue vilabu vya pombe au nyumbani kwao. Wakiitwa njoo tuandamane wanakumbuka ya Pemba, hawaendi! Utawaumu viongozi?

Tuna serikali dhalimu. Watu wanataka kuishi hata katika shida. ndiyo maana wanavumilia ujinga wa mfumo ili kuogopa virungu vya FFU. Ni taifa la watu waoga! Binafsi siwezi kubeza nguvu waliweka viongozi wa upinzani tangu mageuzi yapipoasisiwa. Wanakabiliana na serikali dhalimu, viongozi na watawala wahuni!

Tazama serikali ilivyo-freeze biashara za watu waliokuwa wamejitoa kusaidia upinzani kuanzia mwaka 1995. Wote mmoja baad aya mwingine wamerejea CCM, au wameachana na siasa, au wamekuwa wafadhili wa CCM kuendelea kukandamiza upinzani. Hata wengi wanaoandika hapa, wanalaumu tu lakini si jasiri kiasi cha kusema haya sasa tupambane na wadhalimu tukomboe nchi. Haya yanasemwa kwenye kompyuta. Ni wangapi miongoni mwa wana Jambo Forum wamesaidia kukuza mawazo ya kimageuzi?

Lakini kama kwa kuangalia udhaifu wa kiutendajiwa serikali na ubabe inaotumia kuwanyamazisha wapinzani, ni rahisi kuona kwamba upinzani una nguvu ila unakua pole pole kwa sababu ya udhaifu wa kizazi hiki ndumila kuwili!
 
Good discussion!!

Wadau,
Ni kweli tunahitaji watu mahili ktk upinzani ili kuwa-convince ile 80% iliyokataa vyama vingi. hii ndio kazi kubwa iliyonayo upande wa upinzani.

Hili gundu la "hatuko tayari kwa vyama vingi" bado wananchi tulio wengi tunalo vichwani mwetu......na hii inakuwa reflected hata ktk matokeo ya kura ktk vipindi vya chaguzi zote zilizopita....jaribu kukumbuka.

Wachache tunaoelewa maana ya upinzani........hii iwe changamoto kwetu kuwaelimisha wasioelewa faida za kuwa na upinzani na hivyo support yao ni muhimu ili kuleta uwajibikaji serikalini na hatimaye maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Baadhi ya watu niliofikiri mahili ktk upinzani.............duh naona wengine wamerudi CCM sijui walikuwa mapandikizi??!!!

Somo la chama mbadala inabidi lifanyiwe kampeni kubwa sana (pengine kampeni yake iwe zaidi ya ile ya elimu ya UPE na elimu ya watu wazima) ili wananchi waweze kuelewa kuwa chama mbadala maana yake si vita bali ni mchakato wa uwajibikaji wa viongozi wetu wa kisiasa kwa wananchi.
 
Good discussion!!

Wadau,
Ni kweli tunahitaji watu mahili ktk upinzani ili kuwa-convince ile 80% iliyokataa vyama vingi. hii ndio kazi kubwa iliyonayo upande wa upinzani.

Wachache tunaoelewa maana ya upinzani........hii iwe changamoto kwetu kuwaelimisha wasioelewa faida za kuwa na upinzani na hivyo support yao ni muhimu ili kuleta uwajibikaji serikalini na hatimaye maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Somo la chama mbadala inabidi lifanyiwe kampeni kubwa sana (pengine kampeni yake iwe zaidi ya ile ya elimu ya UPE na elimu ya watu wazima) ili wananchi waweze kuelewa kuwa chama mbadala maana yake si vita bali ni mchakato wa uwajibikaji wa viongozi wetu wa kisiasa kwa wananchi.

Nadhani una hoja, ila mashauri tifanye hivi. Wana Jambo tuache porojo tushiriki siasa moja kwa moja. Tusijifanye wachungu na nchi kumbe porojo tupu kwenye mtandao, tunabaki kulaumu wachache jasiri waliojitokeza, wakawekeza nguvu, muda na raslimali zao na kukatishwa tamaa, na sisi tunarukia kuwahukumu.

Hii elimu iondoke kwenye mtandano iende vijijini wanakoihitaji, maana hap naona tunapiga domo sana, lakini tumeganda tu kwenye kompyuta. Labda ndiyo maana Mnyika hayupo hapa amengundua kwamba anazungumza na wasiohusika, kwamba muda wa kuiridhisha intellectual enquiry kwenye mjadala wa mtandaoni umekwisha. Kijana yupo kazini mitaani kwa wanaohusika, yaano hizo asilimia 80 unazosema.

Kama unamaanisha unachosema na wewe ng'oka moja kwa moja hadi kwetu Sumbawanga utuamshe. Mimi nitafanyia kazi Usukumani ninapoishi, na kina Mukandara warudi kwao 'visiwani' wafanye kazi. Hapo nitaona tuko serious.
 
Siku vyama vitakapo jitambulisha kwa mrengo na sera zake ndipo wananchi wataweza chagua chama cha kweli. Upinzani hata ukiwa na nguvu kiasi gani haiwezi kusaidia kitu kwa sababu wananchi leo hii wanatazama list ya first 11 wanaoingia uwanjani - WATU!
Ni akina nani wako upande gani kama vile timu za mpira wa miguu. Uwezo wa timu kifedha kuweza kununua wachezaji wazuri na ndivyo CCM wanavyofanya. Nimeyaona sana hata ktk kijiwe hiki watu wakiuliza Chadema kuna akina nani?...hapo huwa wanaona magoli tu hakuna ushindi!
Ni kweli kabisa kuwa CCM leo hii ina wachezaji wazuri wa legue ya Taifa, na ndicho wananchi wanachotazama wakifikiria lengo la chama ni kuhsinda magoli tu!..
Kwa hiyo hata tunapotaka kupiga kura zetu wananchi hutazama uwezekano wa chama gani kushinda na ndipo huweka kura zao kama vile kamari!.

Na ndio maana utasikia CCM lazima ishinde na ukimuuliza mtu why?..utachekwa wewe pasipo kupewa sababu ya msingi nje ya list ya wachezaji wake. Mrengo na sera vyote ni mapambo ambayo wananchi asilimia 80 ya wapiga kura hawafahamu.
Fanya uchunguzi waulize watu mia moja nini mrengo na sera za CCM utaulizwa kwanza mrengo ni kitu gani na sera hapo kidogo watababaisha na kusema kwani wewe hufahamu?..
Kwa hiyo mind set ya wananchi ni mtihani mwingine mkubwa kwa vyama vya Upinzani na kusema kweli kila anapoondoka mtu alwatan ni pigo kubwa kwa vyama hivi kulingana na mazingira yetu.
 
Niulize swali dogo:

Hivi hawa wanaokosa vyeo wakabadilika na kuhama chama kwenda kingine wakapokelewa kwa shangwe, hamwoni kama wao na wanaowapokea wana matatizo zaidi ya tudhaniayo?

Binafsi sipendezwi kabisa na watu wa namna hii. Tambwe Hizza sikutarajia hata siku moja awe alivyo sasa. Kabourou, Akwilombe etc. Upinzani unamong'onyoka kila kukicha. Nahisi upinzani hauko strong kama tunavyoambiwa hapa. Something is missing...

Wapi tunaelekea?

Hilo niliwahi kuliongelea huko nyuma kuwa tatizo jingine tulilo nalo katika siasa za nyumbani kwetu ni la umaskini na tamaa ya mali ambapo wengi wa wanasiasa wetu wanategemea siasa ili kujipatia mali. Hawaingii kwenye siasa kwa kufuata itikadi za vyama. Nadhani swala la imani ya itikadi bado liko mbali kidogo na wanasiasa wetu wengi. Hata hivyo imani yangu ni kwamba chini ya matatizo hayo, jambo tunalotakiwa tufanye kwanza ni kuweka vyama vyote katika level ground ya resources; baada ya hapo ndipo watu watajikuta wanafuata itikadi. Kwa sasa hivi kuna wana CCM wengi ambao hawapendi kuona jinsi chama chao kinavyoendesha nchi lakini kwa vile CCM ndiyo ina resources nyingi na ina uwezo wa kuwavurugia mambo yao, basi wanabakia kule kule: siwezi kuamini kabisa kuwa mtu kama Lamwai eti anaipenda CCM hasa ninavyomjua alivyokuwa akichambua matatizo ya wananchi na jinsi CCM ilivyoyaleta, wakati matatizo hayo bado yapo na CCM haijabadilika. Vile vile kuna wana-upinzani wanaojua fika kuwa wanalofanya kama wapinzani ndilo jema zaidi kwa nchi lakini kutokana na njaa zao wanaamua kwenda kule kwenye resources nyingi ili watoto wao wasife njaa.
 
Quote #1,

1. "Tatizo la vyama vya upinzani Tanzania nadhani haliko kwenye viongozi zaidi, bali liko kwenye mfumo mzima wa nchi kuhusu vyama vya siasa"

Mzee Kichuguu, kwenye hilo juu ninawalaumu upinzani waliohusika na kusaini mkataba wa kuanzishwa kwa vyama vingi pale Ikulu, maana wangekuwa makini na kutafakari kwa kina what CCM was offering them at the table, ninbawakumbuka sana waliosaini aliwemo Mheshimiwa Mtei, Marehemu Ngwillulupi, Seif Hamadi, Lipumba, Mtemvuu, Cheyo, na Masha. On one hand, tunawashukuru kuwa angalau tuna something kuliko tungeendelea na chama kimoja, lakini on the other hand the misery we are in, ni matokeo ya vision zao hao viongozi wa waasisi wa upinzani wetu, maana behind this miseryy we are in as a natin ndio hasa what was the CCM's vision!

Quote #2,

"Kwa vile chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu, inabidi kihudumiwe na wanachama wake wenyewe badala ya kutegemea ruzuku. Inawezekana nia ya serikali kutoa ruzuku kwa vyama ilikuwa nzuri lakini mfumo unaotumika unakipendelea chama tawala na kudumaza vyama vya upinzani."

CCM na serikali yake haiwezikulaumiwa au kuwa responsible na matokeo ya sheria iliyokubalika na pande zote mbili wakati wa kuanzishwa mfumo huo, yaani upinzani na CCM, hapana, ni ukosefu wa vision nzuri kwa taifa letu na kukimbilia madaraka, kwa pande zote mbili za siasa kuanzia CCM, mpaka upinzani, ndio tatizo lililo tufikisha hapa, vyama vyote viwili ni lazima vibebe responsibility hii, lakini ukweli ni kwamba kuna sheria moja ya siasa katika dunia nzima, ni kwamba the incumbent hata siku moja huwa hapati ruzuku sawa na the sideliners, yaani upinzani!

Quote #3,

"Kwa upande mwingine, serikali imakuwa inatumia mamlaka yake vibaya kuwanyanyasa watu wanaochangia vyama vya upinzani, na hivyo kuvifanya vitegemee ruzuku ndogo wanayopata kujiendesha. Maoni yangu yanarudi kwenye kutaka mabadiliko ya katiba"

Hiii ni hoja hafifu sana, Serikali haijamnyanyasa mtu au watu wanaochangia vyama vya upinzani, the matter of fact mwenyekiti wa Chadema ni one of the most successful business man in Tanzania, na Mbunge wa Chadema Ndesamburo, sasa hii serikali inanyanyasaje wachangiaji na kuwaacha wapokeaji? Ukweli ni kwamba serikali hiyo hiyo ya CCM huwasaidia sana hawa viongozi wa upinzani wasifilisiwe na benki zetu, kutokana na kujikita sana na madeni yasiyolipika, na ndio hasa mfano wa kiongozi wa upinzani Cheyo, ambaye serikali ya CCM imamsaidia sana asinyang'anywe nyumba yake kutokana na kushindwa kulipa mkopo wa benki moja hapa bongo, kwa hiyo hii hoja hafifu sana!

Quote #4,

"Maoni yangu yanarudi kwenye kutaka mabadiliko ya katiba"



Hiii ndio hoja ya msingi sana, lakini the call za kuibadili hii katiba yetu, isiwe na nia ya kuilaumu CCM, hapana iwe ni kukubali kuwa wakati tunaanzisha hizo katiba, hatukuwa na vision nzuri ya matokeo yake, mbele ya safari, na ni makosa yaliyofanywa na pande zote mbili, yaani CCM na upinzani, unless ni sheria iliyoanzishwa enzi za chama kimoja!

Kwa kumaliza, ninasema kwamba vyama vyetu form CCM to upinzani, vyote vinahusika kwa lawama samba samba kabisa, na matokeo ya misery we are in as a nation kwani wote walihusika na kusaini walisaini uke mkataba in the 90s!
 
Field Marshall ES said:
Hiii ni hoja hafifu sana, Serikali haijamnyanyasa mtu au watu wanaochangia vyama vya upinzani, the matter of fact mwenyekiti wa Chadema ni one of the most successful business man in Tanzania, na Mbunge wa Chadema Ndesamburo, sasa hii serikali inanyanyasaje wachangiaji na kuwaacha wapokeaji? Ukweli ni kwamba serikali hiyo hiyo ya CCM huwasaidia sana hawa viongozi wa upinzani wasifilisiwe na benki zetu, kutokana na kujikita sana na madeni yasiyolipika, na ndio hasa mfano wa kiongozi wa upinzani Cheyo, ambaye serikali ya CCM imamsaidia sana asinyang'anywe nyumba yake kutokana na kushindwa kulipa mkopo wa benki moja hapa bongo, kwa hiyo hii hoja hafifu sana!

Nadhani inawanyanyasa selectively. Kuna wafanyabishara wengi waliokuwa supporters wa upinzani mkoani Kilimanjaro walikuwa wananyanyaswa sana na TRA kwa kwa sababu za kisiasa zaidi. Walipoamua kuhamia CCM tena kwa mbwembwe, kero za TRA zikaisha na wakaendelea na biashara zao kwa utulivu. Zaidi zaidi mwulize Lamwai yaliyompata kwenye biashara yake ya uanasheria.
 
Mzee Kichuguu,

Quote #1,

"Nadhani inawanyanyasa selectively. Kuna wafanyabishara wengi waliokuwa supporters wa upinzani mkoani Kilimanjaro walikuwa wananyanyaswa sana na TRA kwa kwa sababu za kisiasa zaidi. Walipoamua kuhamia CCM tena kwa mbwembwe, kero za TRA zikaisha na wakaendelea na biashara zao kwa utulivu."

Mzee Kichuguu,

Heshima mbele, binafsi sina info za kutosha on this Kilimanjaro's ishu, lakini ninafahamu kwamba serikali haiwezi kumuonea mwanachi na makosa ya kodi kama hana kabisa kosa la kodi, sheria zetu ziko wazi kabisa on that, na ningetegemea mwananchi wa mkoa wa Kilimanjaro, tena mfanya biashara ambaye yuko radhi kununua suti ili tu akasikilize kesi mahakamani, leo aonewe na serikali kwa ajili ya kodi ambayo alishailipa ipasavyo kisheria, ni hoja ambayo inaonekana kutokuwa kamilifu. Wangekuwa ni wananchi wa mikoa mingine labda ningeamini, lakini sio mikoa kama Kilimanjaro na Arusha!

lakini pia ninaamini kuwa ni uamuzi wa serikali on when, why, and who, katika kufuatilia ulipwaji wa kodi kisheria, I hope that was the case huko huko Kilimanjaro, lakini ni hoja inayo-qualify as a political gossip!

Quote #2,

Zaidi zaidi mwulize Lamwai yaliyompata kwenye biashara yake ya uanasheria.

Dr. Lamwai, amekuwa akitumiwa sana katika ku-exaggerate hoja ya kuilaumu CCM na mahusiano yake na viongozi wa upinzani na wanaohamia upinzani, lakini ukweli ni kwamba huyu alifanya makosa mengi kisheria, alipokuwa kiongozi wa upinzani, the matter of fact alitakiwa kufungwa jela kutokana na baadhi makosa aliyoyafanya huko nyuma, ikiwa ni pamoja na kutoa kashafa nyingi against serikali na viongozi wake, ambazo alipotakiwa kuzithibitisha kama sheria zetu zinavyoatka, alishindwa, kwa hiyo kujisalimisha na kwenda jela, akahamia CCM, lakini hoja kwamba kazi zake za uansheria zilikuwa na utata, ina walakini maana Bob Makani, mwenyekiti wa zamani wa Chadema, ni mwanasheria pia na mpaka leo anaendelea na kazi zake bila matatizo. Dr. Lamwai hajawahi kuwa masikini au kwenye dhiki ya kufikia kuomba msaaada kwa CCM, hiyo si kweli kabisaa, yeye na Kaburu, wamesoma shule zinazoeleweka sana na dunia, hapa bongo watu wamesoma M<zumbe tu na hawalali na njaa sasa iweje hawa wenye kisomo babu kubwa?
 
Hatuhitaji wapinzani mahili(ri) bali tunahitaji wapinzani makini. Umahiri unamsaidia/utamsaidia nini mtanzania wa kawaida zaidi ya wao(wapinzani) kupata ulabu walio nao wenzao kwa sasa?

Upinzani unaochipua na kukua kutoka katika changamoto kama hizi wanazokumbana nazo sasa ndio zitakazosaidia kujengeka kwa upinzani makini endapo tu wataacha kukimbilia kuangalia mapungufu ya wanao wakimbia na kuangalia mapungufu walioyonayo wao wanaoendelea kubakia.....

Tanzanianjema
 
Komandoo Es,
lakini ukweli ni kwamba huyu alifanya makosa mengi kisheria, alipokuwa kiongozi wa upinzani, the matter of fact alitakiwa kufungwa jela kutokana na baadhi makosa aliyoyafanya huko nyuma, ikiwa ni pamoja na kutoa kashafa nyingi against serikali na viongozi wake, ambazo alipotakiwa kuzithibitisha kama sheria zetu zinavyoatka, alishindwa, kwa hiyo kujisalimisha na kwenda jela, akahamia CCM

Mzee wangu, kwanza samahani kwa kuopoa hoja ndani ya maelezo yako. Hapa uncle umenishtua sana kuona kuwa CCM ina nguvu kiasi kwamba mtu aliyetakiwa kwenda jela kaachiwa mara tu alipojiunga na CCM.
Je, huoni kama hii ni mbinu chafu sana yaani unasalimu amri kusaliti chama pinzani ili upate msamaha wa CCM... ambao sii mahakama!.

Komandoo, kuna mengi ambayo hufanywa na wenyewe CCM, na ktk siasa zao wanao msemo usemao - Kuzua FITNA!
Na watakapo kuzushia Fitna mjomba huna hila kwani Wafanyabiashara wote nchini wamepitia mkono wa CCM ktk mafanikio yao. Ni lazima ktk miaka 40 ya Utawala wao mfanyabiashara yeyote kawahi kutafuta msaada fulani toka kwa watu hawa na wanafahamu ilikuwa kinyume cha sheria, moja kubwa ilikuwa ni ulipaji kodi.
Nina hakika kwamba hakuna tajiri yeyote nchini ambaye ktk muda fulani hakukwepa kodi. Utake usitake kuna wakati utajikuta unaingia mkenge kwa sababu jamaa wa TRA enzi za nyuma walikuwa wakikufuata wenyewe na kukupa offer you can't refuse. Kwa hiyo file likifunguliwa ussipokamatwa enzi za Nyerere utakamatwa enzi za mwinyi ama Mkapa yote inategemea Utajiri wako ulianza kupaa wakati gani. Kulingana na kodi zetu huwezi kutajirika hata siku moja bila kuiba kodi na ndio chunvi ktk donda siku ya siku.

Now, flip the coin tazama upande wa pili!
Huyo Cheyo kweli unaafiki CCM kuingilia kati madai ya nyumba toka mkopo wa benki kuwa ni msaada? hapa kidogo nashindwa kuelewa kama hii ni Uchafu wa CCM kuweza kumbana Cheyo ama ni fadhila. na imekuwaje CCM waingilie hata ufanyaji kazi wa Benki zetu? Je, hii sii crime kwa CCM as an associate to!

Swala la Mbowe, sidhani kama huyu kijana amepata utajiri wake akiwa kiongozi wa Chadema. Nachokumbuka Bilies imeanza kazi akiwa nje ya siasa na kama nakumbuka mwaka jana kabla ya uchaguzi kulitokea uvumi kuwa anafuatiliwa ktk maswala ya kuzua Fitna. Sasa iwe kweli kasamehewa ama CCM imemsaidia kuendesha biashara zake. Huoni kama CCM wanazidi kucheza rafu kuingilia maswala yasiyohusiana na chama?
Biashara anazofanya Freeman ni biashara ambazo hao wazee wetu wa CCM huona kama ni uhuni mtupu kwa hiyo sidhani kama unaweza kumhesabu Freeman kati ya Matajiri Tanzania, anazo kiasi za kumtosha ktk usalama wa maisha yake na familia.

Mawazo yako ktk mchango nilio wakilisha!
 
Njia ya uhakika ya kuweza kubeat hizo machinations ni kujitahidi kuwa as clean as.....

Tatizo ndugu zetu walioamua kujitwika ujemedari wa upinzani (tuwashukuru kwa moyo wao) huwa wanajisahau na kujiona wako sawa na wenzao walioshika ulabu wa Dola. Matokeo yake wanajiweka vulnerable na kuwarahisishia washindani wao kuwabana ama kuwamaliza kiulaini.

Katika siasa za kiafrika ambazo maarufu kwa jina la SIASA Za MATUMBO the only assured way to beat walioshika dola ni kuwa clean zaidi ya kutegemea smart moves kama wasemavyo...

Tanzanianjema
 
Njia ya uhakika ya kuweza kubeat hizo machinations ni kujitahidi kuwa as clean as.....

Tatizo ndugu zetu walioamua kujitwika ujemedari wa upinzani (tuwashukuru kwa moyo wao) huwa wanajisahau na kujiona wako sawa na wenzao walioshika ulabu wa Dola. Matokeo yake wanajiweka vulnerable na kuwarahisishia washindani wao kuwabana ama kuwamaliza kiulaini.

Katika siasa za kiafrika ambazo maarufu kwa jina la SIASA Za MATUMBO the only assured way to beat walioshika dola ni kuwa clean zaidi ya kutegemea smart moves kama wasemavyo...

Tanzanianjema

Uko sahihi kabisa (100%) ila tatizo ni kuwa katika dunia ya umaskini wetu ambapo tofauti kati ya walioa nacho na wasio nacho ni kubwa sana, hiyo inawataka wanasiasa wa upinzani ama waishi kam wasio nacho kabisa ambayo ni ngumu kwa wengi wao na inaweza kuwaponza kwenye propaganda za kisiasa au waishi kama wanaokaribia walio nacho na hivyo kuwa vulnerable kwa propaganda za kisiasa tena.
 
Back
Top Bottom