Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Ibrah,

Nadhani Mzee Es anatuletea hoja hapa tuzijadili kama zilivyoletwa na huyo Tambe..Pia sidhani kama anaziamini maanake navyojua watu wa CCM wakiwa na swala kama hili hawawezi kulitoa hadharani kujajadiliwa.. husubiri hadi Uchaguzi kisha hushusha mashuzi yao! wajinga wengi watashindwa kutumia hekima kupeta pumba. fumba fumbua CCM mshindi yeye.
Maadam Mzee es, katurushia sisi - kazi kwetu!...
 
Serikali ya awamu ya nne ilipoingia na kukuta asilimia 79%, ya vijana waliofaulu hawakuwa wamepata nafasi ya kuendelea na masomo, ikashughulikia tatizo hilo kwa haraka na kuwezesha watoto asilimia 55%, zaidi kuongezewa, na hivyo kuifikisha asilimia 76% ya watoto wote waliofaulu kuendelea na elimu ya sekondari.

Tumeona juhudi kubwa zikiendelea kufanywa ili kuhakikisha watoto wote watakaofaulu kuendelea na masomo ya sekondari. Haya ni mafanikio makubwa kwa kuwa katika mpando wa maendeleo wa Millenium, kwa nchi yetu iliyojiwekea lengo la kufikisha watoto asilimia 80%, ifikapo mwaka 2010.



.......Coming Up Next.............!

Sekondari za Juuu, ( High School)
 
Mzee Bob,

Heshima mbele mkuu, tunajaribu pia kuleta mawazo toka nje ya forum, katika ishu muhimu zinazotula akili hapa forum, ili kuona tuko wapi kimawazo na katika kutoa alternatives, kwa ishu sugu za kitaifa,

na the best of all kukosoa pia mawazo ambayo hayaonekani kuwa katika level ya kulisaidia taifa letu kusonga mbele, zaidi ya kurudi nyuma, haya ni mawazo ya Tambwe, kiongozi wa zamani wa upinzani, kuna ninayo yakubali, na kuna ambayo sikubaliani nayo,

Lakini, ni muhimu kuyaangalia na kuyafanyia kazi, na ni kazi kwa kila mwanachi!
 
Mzee Es,
nakupata vizuri sana!...
Mimi hawa wanasiasa na wasomi wetu huwa nina shida nao moja kubwa sana...
Mathlan mwaka 1999 tunajua ni zaidi ya 1,000,000 waliojiunga na shule za msingi darasa la kwanza..lakini hawa hawa unapowatazama wakiwa darasa la saba 2006 ni karibu asilimia 20 walikatisha masomo!...hatuambiwi!
kisha waliokaa mtihani ni karibu ni nusu ya walionza darasa la kwanza miaka saba iliyopita... hatuambiwi!..
Haya tazama walioshinda mtihani na kujiunga na secondary utakuta pia haifiki asilimia 20 ya wanafunzi wote ila hutangazwa asilimia kati ya walioshinda mtihani na waliopata nafasi ya kuendelea!...jumla ya hesabu kwa walioshindwa mtihani plus walioshindwa kupata nafasi... hatuna hesabu yake kimaandishi!...
sasa hapa kwa mdanganyika kama mimi nitatazama hizo asilimia 30 zikiongezeka kila mwaka hadi kufikia 60 mara leo tunaambiwa 75 ya watoto wote waliofaulu toka wanafunzi waliokaa mtihani wa mwisho.

Hili neno asilimia ya watoto waliofaulu mtihani lina kificho kikubwa kwangu mimi kwa sababu haikupi picha ya walioshindwa kuendelea mbele na masomo mbele toka waingie darasa la kwanza!. Na sidhani kama ni rahisi kufanya utafiti kufahamu sababu zilizowakumba hawa vijana wetu kutoweza kufanya vizuri!..
Lugha hii iliyotumika hapa ni sawa sawa na ile nayoshindwa kuielewa wanapozungumzia ongezeko la mauzo ama pato la serikali.. Kwa mfano wanaweza sema mwaka 1982 pato la taifa lilikuwa 20 billioni lakini kufikia mwaka 2006 pato la taifa limeongezeka hadi 200 billioni, hapo utaambiwa ongezeko la asilimia blaa blaa blaa!.
Sasa ikiwa mwaka 1982 hizo billioni 20 tuliweza kujenga mathlan Airport ya JKN lakini leo hii hizo billioni 200 zilizopatikana haziwezi kujenga hata runway ya Uwanja wa ndege. Je, hapa kweli kuna ongezeko la mapato ama mimi mwenyewe ndio najichanganya kimahesabu!
 
Nadhani itafika wakati akina Tambwes wote waliojichomeka Upinzani watarejea CCM.

Ukifika wakati huo ndo ntatafakari kuingia uwanjani!
 
Ushauri kwa Tambwe afanye rejea kwenye hotuba ya Nyerere aliyoitoa mwaka 1978 pale karimjee akiwahutubia wabunge aliposema

"Kwani elimu yenyewe hii ya miaka saba kwani elimubwana?
Mtoto wa siku hizi akimaliza miaka saba hata kusoma hajui.kwa hiyo afadhali tuongeze ongeze kidogo"

N a mimi nasema kuwa kwani elimu yenyewe si ndio hii hata waalimu hakuna?mbona tunakimbilia kuangalia takwimu tuu bila kujali ubora wa hiyo elimu?
 
Mkapa kieleweke,
mbona tunakimbilia kuangalia takwimu tuu bila kujali ubora wa hiyo elimu?
Mjomba umenikuna penyewe kabisa!.. takwimu bila ubora wa elimu yenywe haina maana kabisa! sawa na hizo Takwimu za fedha bila kujali thamani ya fedha yetu!
Ni upotoshi mkubwa sana kwa wananchi!
 
Upande wa sekondari za juu (High School) wanafunzi waliongezeka kutoka vijana 5,206 (1.1%) mwaka 1995, hadi 12,253 (2.1%) kwa mwaka 2005 kabla MMES haijapamba moto ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 135.4%, kwa kifupi hatua tuliyopiga ni kubwa ingawaje bado kuna mengi ya kuboresha, lakini hili ni changamoto la mafanikio.

Elimu ya chuo kikuuu, hapa napo tumepiga hatua kubwa sana kutoka wanafunzi 7,785 mwaka 1995/96 hadi kufikia wanafunzi 32,681 kwa mwaka 2003/04, ongezeko la asilimia 319.8%, na sasa tumefikia takribani 40,000 bila ya kusahau kwamba mkoloni hakutuachia, hata chuo kimoja, na hata tulipoanzisha chuo kishiriki cha Makerere, ambacho baadaye kilikuwa na kuwa Chuo kikuuu Mlimani, kilianza na wanafunzi 14 tu!

Najua kuna wanaowapotosha wananfunzi wetu huko Mlimani, na kuwaambia wagome na kubeba mabango ya kudai mbona rais wetu alisoma hapo tena buree kwa asilimia 100%, bila ya kuangalia idadi ya wanafunzi katika miaka hiyo ya nyuma na uchumi wetu wa sasa hivi, kuwa havifanani!

...........Coming Up Next............

Barabara Zetu!
 
Mzee Es,

Samahani mkuu najaribu kuelewa hapo juu!
Inakuwaje vyuo vikuu vina wanafunzi wengi kuliko high schools kwa karibu ya hesabu ya mara tatu?
 
Subiri kidogo, inabidi nirudi kwenye posts za nyuma kabisa ili nijue Tambwe Hiza ni nani il niweze kupata uhondo wote. Nakumbuka tu kuwa alikuwa kiongozi fulani wa CUF kule Temeke au alihusika sana na uchaguzi wa CUF Temeke. Ila najua kuwa si mwana CUF tena na wala sijui anafanya nini sasa. Kabla sijauliza, niache niache nikasome kule nyuma mwenyewe.
 
Subiri kidogo, inabidi nirudi kwenye posts za nyuma kabisa ili nijue Tambwe Hiza ni nani il niweze kupata uhondo wote. Nakumbuka tu kuwa alikuwa kiongozi fulani wa CUF kule Temeke au alihusika sana na uchaguzi wa CUF Temeke. Ila najua kuwa si mwana CUF tena na wala sijui anafanya nini sasa. Kabla sijauliza, niache niache nikasome kule nyuma mwenyewe.


This is Tambwe: bioghraphed by Ansbert Ngurumo (Tanzania Daima: 30/5/2007):


Tambwe Hiza ni nani?

Hiza si msomi wa viwango vya Bagenda. Hajulikani kwa uandishi wa ama vitabu au makala. Lakini kumbukumbu za maisha yake ya kisiasa zinaonyesha kuwa Tambwe Hiza amekuwa mwana CCM hadi 1992 alipojiunga na CUF.

Alikaa ndani ya CUF hadi 1995, akakumbwa na mvuto wa Mrema na NCCR-Mageuzi akajiunga na chama hicho. Mwaka huo aligombea ubunge wa Temeke kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

Alishindwa na kufungua kesi ya kupinga matokeo dhidi ya mshindi, Ali Kihiyo, wa CCM. Baada ya Mahakama kutengua ushindi wa Kihiyo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikatangaza uchaguzi mdogo, NCCR-Mageuzi ilimteua Mrema agombee badala ya Hiza. Hiza akachukia, akahama na kurejea CUF mwaka 1996.

Tangu hapo amegombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF mwaka 2000 na 2005; akashindwa. Kwa hiyo, miongoni mwa wababe wa Hiza ni Kihiyo, Mrema, Khadija Kusaga na Zubeir Mtemvu.

Akiwa CUF, aliteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali za uandamizi, zikiwamo Ujumbe wa Baraza Kuu la CUF, Ukatibu wa Kamati ya kuhamasisha uhai wa chama hicho mkoani Dar es Salaam, Uenyekiti wa CUF Wilaya ya Temeke, Ukurugenzi wa Mipango na Uenezi; Ukurugenzi wa Habari na Uenezi wa Sera.

Hiza alipoteza kazi CUF Aprili 28, 2006, baada ya chama hicho kumvua nyadhifa zake kwa kumhusisha na mambo kadhaa yaliyokinyima ushindi mwaka 2005. Haikuzidi miezi mitatu, Hiza akajiunga na CCM Julai 29, 2006.

Alipohojiwa na gazeti la Nipashe mwaka jana, Hiza alitoa sababu iliyomwondoa CUF na kumrejesha CCM. Kwanza alisema hakuwahi kuwaza kurejea CCM. Pili, alisema, na hapa namnukuu: “Ni kweli nimeamua kujiondoa kutoka CUF kutokana na sababu mbalimbali, kubwa zaidi zikiwa zinahusu mambo binafsi na ukweli wa hali halisi.”

Hiza anasema mambo binafsi yalimwondoa CUF na kumrejesha CCM! Na siku chache baada ya Hiza kurejea CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alipokuwa akiwapokea kina Dk. Amani Kabourou na Jacob Nkomola (na Tambwe alikuwapo), alikaririwa akisema kinachowarejesha wapinzani CCM ni njaa yao!

Baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakidai kwamba kina Hiza wanachofanya sasa, baada ya kujeruhiwa mno kisiasa, ni kuomba kazi ama serikalini au CCM.

Hiza ambaye hakuwahi kuwaza kurejea CCM, amekuwa mkosoaji mkuu wa CCM, sasa anauliza swali: “hamuoni jema la CCM?”

Sijui anasijikiaje akisoma makala ya Susan Lyimo (Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA) iliyochapishwa katika gazeti hili Jumapili iliyopita. Mahali fulani, Lyimo anasema:

“Taarifa zinaonyesha kuwa, baada ya miaka 45 ya uhuru, idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu ni asilimia 0.27 ya Watanzania wote, huku idadi ya Watanzania ikikaribia kuwa milioni 40.

Hii ina maana kwamba, Tanzania ina vijana 48,000 tu, wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu. Uwiano wa wasomi na wasio wasomi katika nchi yetu ni 1 kwa 800.

Jambo la kusikitisha ni kwamba katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Msumbiji, Namibia na hata Angola ni Tanzania ndiyo inayoshika mkia kwa kuwa na idadi ndogo ya vijana wanaohitimu elimu ya chuo kikuu.

Wakati Kenya ina asilimia 1.47 ya watu wake wanaosoma vyuo vikuu, Uganda ina asilimia 1.33, Msumbiji asilimia 0.33, Namibia asilimia 4.66 na Angola ni asilimia 0.44, nchi ambazo zimepata uhuru baada ya Tanzania kutangulia.

Pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu, mazingira mabovu yaliyopo katika vyuo hivi, yanafanya wanafunzi wengi kuhitimu wakiwa na vyeti tu, au shahada na stashahada, lakini wakikosa sifa, ujuzi, fikra na utaalamu anaopaswa kuwa nao msomi wa chuo kikuu.

Hii imekuwa sababu kwa vijana wetu kuwa katika wakati mgumu wa kupambana kusaka ajira katika soko la ajira.”

Haya haya yanazungumzwa katika uchumi, kilimo, afya, na mengine ambayo wakosoaji na wapinzani wangependa yaendeshwe kwa umakini na uaminifu unaotarajiwa, unalingana na dhamana waliyokabidhiwa na wananchi.

Napata shida kuelewa Hiza anapata wapi nguvu za kutetea wale wale aliokuwa anawasimanga juzi kwamba wameshindwa kusimamia na kuendesha hata mashirika na miradi yao wenyewe?

Tumuulize Hiza anayezungumzia mema ya CCM. Yapi ambayo yeye hakuwahi kuyataja kwa miaka 15 tangu mwaka 1992?

Lililo wazi ni kwamba kwa macho ya wengi, na kwa mantiki ya kila mmoja na wasifu wake, Bagenda na Hiza ni majeruhi wa CCM, Mrema na CUF. Inaeleweka kwamba wamehama vyama kutokana na sababu binafsi zaidi kuliko za misingi ya kiitikadi au kuvutiwa na mafanikio ya CCM
 
Proffesion ya Tambwe Hiza ni "ujanjaujanja" period. Alichofanya baada ya Miaka 13 kujaribu kuwahadaa watanzania kuwa ni mwana mabadiliko ni kujirudi na kukubali his true identity. Hongera kaka Tamwe kwa kukubali ukweli na kuwa muwazi....Wapo wengi bado na mungu akipenda wataendelea kujichuja....Asante ushindi wa Tsunami....

Tanzanjema
 
Wiki iliyopita serikali ilianzisha tovuti maalumu ambayo itatumika na wananchi kwa ajili ya kutoa kero zao , na kadhia zao mbali mbali wanazokutana nazo , wakati mwingine kutoa pongezi na kutoa ushauri kuhusu mambo Fulani kuhusu serikali , wafanyakazi wake na mahusiano ya ndani ya nchi hata nje ya nchi kama mtu anakuwa na ushahidi wowote

Tembelea www.wananchi.go.tz au www.kero.go.tz ukienda hapo utaweza kusoma hiyo tovuti kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza pamoja na mengi mengine ni wewe kama mwananchi kutoa maoni ,pongezi na mchango wako katika kufanya maisha yetu yawe mazuri zaidi na yenye malengo mazuri kwa siku zijazo .

Wapinzani bado wamelala , hawajawahi na wala hawana nia yao ya kufungua tovuti kama hiyo kwa ajili ya kusikiliza pia maoni ya wananchi na kero zao , wapinzani wanabaki na mambo yale yale ya zamani na ambayo majibu yake yameshapatikana

Kuhusu Kashfa ya BOT ? Kweli hii ni kashfa kwa jina lakini hakuna mtu aliyedhubutu kutokeza hazarani kuongelea kashfa hii kwa sababu ni mambo mengine ya uwongo au ya kuhisi ambayo mtu mwenye akili zake timamu ameyatunga na kuwatumia watu kadhaa kwa njia ya mtandao .

Sio kwamba napenda mambo haya yatokee la hasha , mimi napenda watu walio wazi wanaleta hoja mbele ya jamii wawe tayari kujitambulisha wao ni kina nani , hizo taarifa wamezipata wapi au waliwahoji kina nani mpaka kupata taarifa husika .

Hapo ndio tunaweza kuita kashfa kwa sababu kutakuwa na ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwashitaki wahukumiwa , sasa tunatoa lawama kwa njia za kujificha hii ndio democrasia ya kweli ? mtu ana ngata na kukupuliza ? haya ni maoni yangu tu .

Katika magazeti ya leo wapinzani walisema watagomea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 , mpaka hapo katiba mpya itakapoandikwa na tume ya uchaguzi huru kuchaguliwa ifanye kazi yake , pengine tuulize , sasa hivi wapinzani wanajua kabisa hali ya uchumi ni mbaya dhamani ya pesa imeshuka na watu wengi hawana kazi kwahiyo serikali inakosa mapato mengi

Kuandaa katiba mpya inahitaji maoni ya watu wengi zaidi ya hao viongozi wachache wa upinzani , inahitaji muda maalumu na watu kupatiwa pesa kufanya shuguli hii , je na hali hii ya uchumi ilivyombaya itakuwaje ? je tusijenge hospitali na wodi za watoto tukaandike katiba mpya ?

Tusitengeneze daraja la Kigamboni tuandike katiba mpya au tujiandae na uchaguzi wa mwaka 2010 ? na kwa nini wapinzani wanaongelea zaidi mambo ya uchaguzi 2010 ? wana maanisha nini wanavyosema hivi ?

Naamini nchi ya Tanzania ni kubwa sana , kuna mambo mengi sana ya kujadili na kutolea majibu , mfano wangegomea kupitishwa bajeti ambayo inakata maini wananchi hapo wangeeleweka , kwanini wanaacha bajeti iendelee wakati wanajua ni mbaya halafu wadai mambo mengine ?

TUKTA inapanga kuonana na kikwete kisha ifanye maandamani nchi nzima wapinzani wangetumia nafasi hii kuungana na TUKTA na wafanyakazi wengine kuishinikiza serikali lakini wapinzani hao hao wamelala usingizi wa pono wanangoja wanafunzi wagome wakawatete kwa sababu kule watoto wao nao wanasoma au sio ?

Huyu lipumba ni mtaalamu wa uchumi , ina maana yeye binafsi hawezi kujitolea kuishauri serikali kuhusu uchumi na matumizi ? huyu lipumba amesomeshwa na hii hii CCM ambayo leo ndio mbaya wake . huyu huyu lipumba ndio alikuwa gia kubwa katika mapinduzi ya kiuchumi nchini Uganda kwahiyo ana ujuzi na utaalamu wa mambo haya angeweza kuleta changamoto zake katika mapinduzi

Tanzania tunataka mapinduzi ya kweli na sio mapinduzi ya maneno ambayo kesho watu husahau , inajulikana haswa kwamba wapinzani wa sasa hivi ni Zao la CCM miaka ya 60 `s babu zao na baba zao walikuwa ni viongozi au watu waliokuwa wanategemeana na Serikali kwa kiasi kikubwa

Kuuweka upinzani madarakani sasa hivi sio mapinduzi tunataka wapinzani wa kweli ambao hawana DAMU wala hawana MIRABA YA CCM na hii inawezekana mwaka 2020 ambapo tutapata watu makini vijana ambao watakuwa na dira njema vijana hawa ndio tuko nao sasa hivi tunakuwa nao , tunakula nao na tunafanya nao kazi mbali mbali
 
(1) Tanzania ni wananchi wangapi wanaweza kutumia kompyuta, kuingia kwenye tovuti na kuandika kero zao?

(2) Aliyetoa fununu za uovu wa za Rais Nixon mwaka 1970, aliendelea kutojulikana mpaka mwaka juzi baada ya zaidi ya miaka thelathini. Kazi mojawapo ya vyombo vya dola ni kufanya uchunguzi au upelelezi kutokana na fununu. Kwa hiyo raia aliyetoa fununu keshatimiza wajibu wake kama raia, ni kazi ya dola kutumia fununu hiyo kufanya uchunguzi ili kupata ukweli. Tuna serikali moja ambayo ina vyombo vya dola, raia siyo sehemu ya vyombo hivyo vya dola.

(3) Katiba ni ya muhimu sana kwa taifa, ndiyo dira ya taifa inayoongza serikali. Kama unaona katiba haina ulazima basi tusiwe na serikali, tuwe kama Somalia. Kuwa na serikali bila kuwa na katiba ya haki ni udikiteta.

(4) Kutayarisha katiba siyo lazima kuchukue muda mrefu namna hiyo, na kama serikali ina nia ya kukusanya maoni ya wanachi kweli kweli haitachukua muda mrefu hivyo; mbona hii ya jumuia ya Afrika Mashariki maoni yamekusanywa kwa mwaka mmoja tu. Kama una kumbukumbu zako kamili, mwezi nadhani wa May au June 1975 wakati Mheshimiwa Jumbe alipompendekeza Mwalimu Nyerere kuwa mgombea pekee wa urais, Nyerere alikubali na kushauri kuwa TANU na ASP ziungane. Mchakato wa kuunganisha vyama vile ukafanyika mwaka 1976 baada ya uchaguzi na katika kipindi hicho hicho katiba mpya ya CCM ilindikwa na chama kikazinduliwa February 5, 1977. Process nzima ilichukua si zaidi ya miezi kumi na tano.

Kuandika katiba yetu mpya haitachukua zaidi ya miezi kumi na tano pia kwa vile vifungu vingi vinavyotakiwa kufanyiwa marekebisho vinajulikana tayari.
 
kitu ninachojua ili hata hayo mambo ya muhimu kama kujenga madaraja yafanyike tunahitaji mabadiliko and very fast. kuanzia katiba na viongozi. Tumezoea kusema how high wakati wakubwa wanasema jump. Fedha za kutengeneza katiba zipo sana ila zinatumiwa na viongozi wetu for the wrong reasons. jambo la kunishangaza kabisa kweli wakuu wa mikoa 26 na spouses wao waliitwa dodoma na boss wao (you know Who) ili wakashuhudie akisoma bajeti ya wizara yake. Bajeti ambayo imeandaliwa na wakuu hao hao wa mikoa. unaweza kuimagine kiasi cha fedha ya walipa kodi iliyotumika kwa ajili ya kuwaweka hawa mjini dodoma kwa wiki moja and what is this about spouses??????????. ni mara ngapi kwa mwaka huu tu fedha za serekali tena sio fedha mamilioni yametumika kwa mambo yasiyo na msingi??????

Ninaamini for anything to happen lazima nia iwepo na sacrifices zifanyike bila hivyo tutakuwa tunaambiwa kila kukicha serikali haina pesa je ni kisingizio cha kutotaka mabadiliko? tufungue macho na bongo zetu zifanye kazi is this the kind of life we want to lead hali inakuwa ngumu kila kunapoitwa asubuhi. mimi na wewe tulio na uwezo wa kupata huduma za internet kutoa na kusoma mawazo ya wengine zungumza na ambao hawana uwezo huo wafahamu umuhimu wa mabadiliko na kwamba yanahitajiaka na sio kesho leo . kila mmoja unaye mbadilisha fikra atambadilisha na mwingine. labda mabadiliko yanaweza kutokea faster than we may think. the power is in our hand we just have wake up make some sacrifices and wake up those still sleeping.
 
Of course there is a lot to reflect on the 15 years of the politics of choice in Tanzania. Certainly the Parliament is more exciting. But my overall verdict: it will take a generation to have a decent opposition that hasn't been in bed with the current rulers. All of them have somehow been compromised by favours, deals, etc. What we have now for an opposition leader is a demagogue who cuts a sorry figure - think Mbowe (a man who would rather be a slave under the Brits because he hates being a "Freeman", an opposition leader speaking his mind freely. He hates being a businessman and entrepreneur under the Black rule).

As for the young crop of opposition politicians (Mnyika, Zitto, etc), it remains to be seen whether college agitation can turn into mature political posture. With Zitto's misjudgement (taking someone's wife who is infected with HIV/AIDS) and demagoguery, with Mnyika's ineptness - all resulting from lack of proper political grooming and guidance - I don't see hope.

Mtei, Mapalala, Marando, Fundikira, Lamwai and the crowd kick-started the idea of alternative to CCM. A coterie of opportunists - Kighoma Ali Malima, JJ Guninita, Mashaka Nindi Chimoto, et al - joined in. The result: false hope and disappointment for many Tanzanians who were looking for an alternative.

The bottom line: with the current opposition leadership, CCM is not going anywhere, despite thievery and incompetence. If you read Jambo Forum, and have not visited Nkasi, or Ileje, or Kamachumu, you would think CCM is going down tomorrow. People like Mnyika, Kabwe and Mbowe and their army of supporters spend their days here - and smell State House as a result.

I think the idea of robust opposition newspapers such as Tanzania Daima is a good one, despite its managerial issues and business difficulties. The opportunity that Tanzania Daima provides for CHADEMA cadres to communicate their grievances (that is what is being done, because I don't see a solid alternative ideas and philosophy) is certainly immense. We have the likes of Ngurumo, Kibanda, Ben (Mwanakijiji), and so on writing. But I think a party needs more than cadres with sharp pens. You need to develop cadres with a strong ideological orientation, responsive to the ideals of our nation not to the populist deformed rhetoric of a latter-day intellectual. And you can't do that by kissing the colonialists' ass, and you certainly can't do it by asking your supporters to make sacrifices that you are not willing to make, or that your pampered upbringing has not allowed you to make. You build a solid base of support by providing a message of hope, not of self-hating.

My two humble cents. I now pass you on to Abdul Mtemvu - the mercenary, according to Ngurumo. (simply because he likes Jakaya)
-------------------

Miaka 15 vyama vingi nchini: Je, yapo matumaini ya upinzani?

Abdul Mtemvu


KATIKA toleo la jarida la New African la Juni, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alifanya mazungumzo na mhariri wa jarida hilo maarufu barani Afrika, na katika moja ya maswali, aliulizwa kuhusu upinzani. Swali na jibu lake nanukuu hapa chini.
"Buffour: In your maiden speech in parliament on 30 December 2005, you said: ‘My victory and that of the CCM is, infact, a vote of confidence in our party and its policies, a vote of confidence in the dedicated leadership of my predecessor. As a CCM member, I am pleased with the results. But as president, I should like to assure everyone that we have no intention to wipe out the opposition.' That was a noble pledge, wasn't it, considering that in many African countries, opposition is a dirty word.

Kikwete: Yes, of course we need the opposition. I cannot build the opposition myself, but I am not going to take measures to strangle them. We are quite keen to see them flourish, and we give them the opportunity and the freedom they need to grow. This is all we can do. The rest of the job is theirs." Mwisho wa kunukuu.

Kwa rais wa nchi ambaye, pia, ndiye mwenyekiti wa chama kinachoongoza serikali, hayo ni maneno ama kauli nzito sana. Ni kauli iliyojaa dhamira na hata, pengine, kuonekana kama kitanzi kwake.

Hakika itakuwa ni muhali kwa Kikwete kuujenga upinzani ili uwe tishio hapo baadaye na hatimaye, kukiangusha na hata kukipokonya madaraka chama chake!

Inapokuwa dhamira na malengo ya chama cha siasa ni kutwaa hatamu za dola, inakuwa jambo la hoja bayana, kwamba, kila chama cha siasa kitafanya kila liwalo kuyatwaa madaraka na, pale, kunapokuwa chama kimeshashika madaraka, basi, lengo linakuwa kuendelea kushikilia madaraka hayo, kwa kila njia iliyo halali. Na pengine, na hata kwa baadhi ya nchi zingine, kwa njia za haramu! Ni ukweli ulio dhahiri na tumeshayaona yakitokea.

Naomba nirejee tena kwenye hoja. Nasema, midhali dhamira na malengo ya chama chochote cha siasa ni kutwaa hatamu za dola, inakuwa muhali kwa, hata, chama kilichokuwa madarakani kuachia hatamu za dola, pindi kinaposhinda uchaguzi.

Labda, kwa sisi Waafrika, tubadilishe mtazamo huu wa lengo na kusudio la chama cha siasa ili tuepukane na mfumo hasimu unaojengeka baina ya wafuasi wa vyama tofauti vya siasa.

Shuhudia CCM na CUF, hususan, kwa upande wa Visiwani. Kweli, hawa watu ni maadui wa kiwango hicho? Ndugu wawili wakatenganishwe na mitazamo tofauti ya kisiasa kiasi cha hata kufikia uhasama wa kuuana? Inaingia akilini kweli? Mimi hainiingii akilini.

Nimepata kuandika kuhusu siasa na kuainisha, mathalan, kuwa sura ya mfumo wa vyama vyingi barani Afrika, ni tofauti na sura ya mfumo huo huo kwa wenzetu walioanzisha mfumo huo. Wale wenzetu wanatofautiana kwa kupingana, sisi tunatofautiana kwa kupigana. Wale wale ambao katika mfumo wa chama kimoja walikuwa makomredi, leo hii, kwa ujio wa vyama vingi, ndio mahasimu wakubwa. Tena wa kuuana!

Nini kimeusibu mfumo wa vyama vingi Afrika hadi tumefikia hapa tulipo? Kama tumelazimishwa kuwa nao huo mfumo, inakuwaje hao waliotulazimisha tuwe na mfumo huu wa vyama vingi wao hawafanyi tunayofanya?

Hatuoni wanaoshindwa kuingia msituni wala kuanzisha hujuma dhidi ya serikali halali. Bahati mbaya kwetu sisi, chama kilichokuwa tawala katika mfumo wa chama kimoja ndicho kinachoonekana kama afriti mkubwa au adui wa wananchi katika mfumo huo wa ushindani wa vyama vingi.

Vyama vingine, na pengine viongozi wake wametoka huko huko kwenye chama kilichokuwa tawala katika mfumo wa chama kimoja, ghafla ndio wanakuwa wakombozi. Wakombozi wa nini na wanamwokoa nani dhidi ya nini, huwa haisemwi! Mradi tu, kwa mfano wa hapa kwetu, chama kama CCM kinatakiwa king'olewe madarakani!

Wachambuzi na watafiti wa masuala ya siasa wanasema kuwa, kwenye uchaguzi wowote huru na wa haki, ni vigumu kutabiri chama gani kitaibuka mshindi. Zipo ‘indicators' ndogo ndogo kama ‘opinion polls' na kadhalika isipokuwa haziaminiki kwa asilimia mia, lakini kutabiri kwa usahihi ni vigumu sana.

Kwa maana hii, chama chochote kilicho madarakani, na kwa kutaka kuendelea kuweko madarakani, kitahakikisha hata pale uchaguzi unapolazimika kuwa ‘free' basi usiwe ‘fair'! Shuhudia ya Nixon na Watergate. Kuna kuwepo na mbinu za chama kinachoendesha serikali ama kuoogoza serikali kuudhoofisha upinzani, kwa njia moja au nyingine. Ndiyo mchezo wa siasa.

Julai mosi, Tanzania tumetimiza miaka 15 ya kuhalalisha mfumo wa vyama vingi nchini. Tumeshakuwa na chaguzi tatu ambapo Jakaya Kikwete ndiye mshindi wa uchaguzi wa tatu, chini ya mfumo huo.

Upinzani haujasambaratika na wala kusambaratishwa rasmi, pamoja na jitihada za Katibu Mkuu wa CCM kuzibomoa ngome za upinzani, na hata kwa baadhi ya waliokuwa viongozi wa baadhi ya vyama vya upinzani kuingia CCM.

Labda mtu anaweza kujiuliza hii ‘bifu' ya Katibu Mkuu wa CCM na mathalan, Chadema ni ya nini? Hivi, na katika mtazamo mzima wa siasa, haiwezekani ikatokea siku moja chama cha upinzani chochote kile kikaungana na CCM? Kwani haiwezekani siku moja nayo CCM ikawa kwenye upinzani dhidi ya chama kitakachokuwa madarakani? Mbona KANU, leo hii, wako gizani?

Ni kwa nini vyama vinavyosema ni pinzani, vyote kwa ujumla wao ndiyo viwe na ‘bifu' na CCM tu? Vyenyewe kwa wenyewe havina tofauti za msimamo au ni kuwa tofauti zao ni ndogo kiasi cha kufanya tofauti zao na CCM ndiyo msingi wa uhalali wao? Na hii tofauti ni nini hasa? Haya ni maswali ambayo, kwa hakika, binafsi yananisumbua sana.

Sasa hivi, cha ajabu kwangu, ni uamuzi wa kambi ya upinzani kuanza kile ambacho nakiona ni kama ‘extra-political activities' nje ya siasa za majukwaa. Mathalan, na sielewi uamuzi wao wa kuzunguka nchi nzima kuamsha hisia za wananchi kuiona bajeti ya serikali kama ni onevu kwa wananchi, lengo lake au kusudio ni nini.

Bajeti tayari imepita au kupitishwa, sasa hao wa kuzunguka nchi nzima iweje? Na halafu itasaidia kitu gani?

Ni lini katika historia ya nchi yetu, bajeti ya serikali imekuwa kipenzi cha wananchi, hata leo hii bajeti hii kuwa kiroja? Ongezeko la bei ya mafuta ni kubwa kiasi gani hadi kusababisha manung'uniko yote kutoka kwa viongozi wa vyama vya upinzani na baadhi ya wahariri na waandishi wa makala za magazeti? Ni kweli ongezeko hilo ndiyo chanzo cha kufanya maisha ya mwananchi wa kawaida kuwa magumu au kuna lingine?

Hapa nchini, miaka yote, na imeikuwa kama utamaduni, kila unapofika muda wa bajeti, basi ni lazima wafanyabiashara watapata sababu ya kupandisha bei ya bidhaa. Huko nyuma hata baadhi ya vitu vilikuwa vinafichwa wiki kadhaa kabla bajeti.

Huu ndiyo utamaduni wa wafanyabiashara wetu, hata pale ambapo hamna sababu ya msingi ya kufanya hivyo ilimradi tu hoja ni ‘biashara ni faida'. Lakini kuna ‘element' ya ‘social obligation' kwenye kufanya biashara.

Lakini, kweli ongezeko la sh 150 hata 200 ndiyo, mathalan, mwenye teksi aongeze bei ya sh 1,000 halafu ilaumiwe serikali, ni halali kweli? Kwa nini sisi walaji tusiandamane dhidi ya wenye teksi badala ya kuilaumu serikali? Tax revenue ni moja ya sehemu ya mapato makubwa na ya msingi ya serikali.

Inasikitisha sana kuwa upinzani hadi sasa umepoteza mwelekeo wote wa upinzani na badala yake, unadakia mambo yaliyo nje ya hoja nzima na mtazamo wa kusudio la kuwepo kwa upinzani nchini.

Mwalimu Nyerere alipata kusema, na namnukuu: ‘Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndiyo ulionifanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi, nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM, au ambacho kingelazimisha CCM kujisafisha kwa kuhofia kuwa bila ya kufanya hivyo, kitashindwa katika uchaguzi ujao.' Wapinzani mpo hapo?

Inasikitisha kuwa serikali ya awamu ya nne imefanywa kama shetani wa kumlaani kwa kutupa mawe, kwa mfano wa sisi Waislam tuendao hijja. Kila baya lililopita au kufanywa na serikali za awamu za nyuma hitimisho lake ni kwa Jakaya Kikwete. Inakuwa kama vile udhaifu wa Nabii Daudi asukumiziwe Muhammad, eti tu kwa vile wote ni mitume na Mungu wao mmoja! Maajabu haya.

Majukwaa ya siasa yamehamishwa na kupelekwa kwenye vyombo vya habari kiasi cha hata kutia shaka kama baadhi ya tahariri na makala zinazoandikwa hakika si hotuba za siasa. Kulikoni?

Tatizo ni nini? Ni kwa Chama Cha Mapinduzi kuzidi kupeta katika chaguzi au kwa Jakaya Kikwete kuwa ndiye Rais wa Tanzania? Wasalaam
 
Hey Mugongo Mamboz

Ahsante Kwa Mchango Wako Hapo Juu .

Nakumbuka Mwaka 1993 Baba Yangu Alikuwa Anakadi Ya Chadema , Nilimuuliza Hiyo Ni Nini ? Hakunijibu Wakati Huo Sikujua Mambo Ya Siasa Wala Nini Na Wala Sikujua Kama Hiyo Chadema Ni Chama Cha Siasa , Lakini Sasa Hivi Baba Huyo Huyo Anakadi Ya Chadema Lakini Anaendesha Gari Ambayo Kwambele Katika Kioo Kuna Kabendera Cha Ccm Pale

Sikumoja Alikuwa Anafungua Shule Yake , Basi Kule Wizarani Wakamfanyia Mbovu Sana Kwa Sababu Yeye Hakuwa Mwanaccm Enzi Hizo Mwaka 1995 Alitakiwa Achangie Chama Cha Mapinduzi Akakataa Kwahiyo Wakaondosha Hawakusajili Shule Yake

Sasa Kabla Ya Uchaguzi Makamba Akaja Akaongea Nae , Yeye Mzee Akaamua Kwenda Nje Ya Mji Akamnunulia Makamba Nyumba Na Shamba , Akachukuwa Wale Ngombe Wazuri Wa Mama Akampatia Makamba Katika Makazi Hayo , Na Akampa Gari Moja Ya Kubebea Majani Ya Ngombe Ili Makamba Ambebe

Na Tangia Siku Hiyo Akabadilika Kabisa , Well Lakini Mimi Niliondoka Nyumbani Kwasababu Tulipingana Haswa Yakija Katika Mambo Haya Ya Masilahi Ya Maisha Na Chama

Chama Cha Mapinduzi Kimeshika Watu Kila Sehemu Watu Hawawezi Kujitoa , Kama Wapinzani Wanataka Kwenda Mbele Basi Wasiogope Kuilazimisha Serikali Itengane Na Vyama Vya Siasa , Wale Mawaziri Wasiwe Mabunge Wawe Wanaajiriwa Wakuu Wa Mikoa Pia Kwa Mtindo Huu Tutakuwa Sawa Kwa Sawa Tutakuwa Tunashindana Kwa Sera Na Sio Nguvu Na Mabavu

Nimeona Mfano Kwa Mzazi Wangu Mwenyewe Na Mambo Yake Yeye Ni Chadema Lakini Hawezi Kuwa Nda Nguvu Bila Kuwahonga Ccm Katika Maisha Yake

Ahsante
 
Hey Mugongo Mamboz

Ahsante Kwa Mchango Wako Hapo Juu .

Nakumbuka Mwaka 1993 Baba Yangu Alikuwa Anakadi Ya Chadema , Nilimuuliza Hiyo Ni Nini ? Hakunijibu Wakati Huo Sikujua Mambo Ya Siasa Wala Nini Na Wala Sikujua Kama Hiyo Chadema Ni Chama Cha Siasa , Lakini Sasa Hivi Baba Huyo Huyo Anakadi Ya Chadema Lakini Anaendesha Gari Ambayo Kwambele Katika Kioo Kuna Kabendera Cha Ccm Pale

Sikumoja Alikuwa Anafungua Shule Yake , Basi Kule Wizarani Wakamfanyia Mbovu Sana Kwa Sababu Yeye Hakuwa Mwanaccm Enzi Hizo Mwaka 1995 Alitakiwa Achangie Chama Cha Mapinduzi Akakataa Kwahiyo Wakaondosha Hawakusajili Shule Yake

Sasa Kabla Ya Uchaguzi Makamba Akaja Akaongea Nae , Yeye Mzee Akaamua Kwenda Nje Ya Mji Akamnunulia Makamba Nyumba Na Shamba , Akachukuwa Wale Ngombe Wazuri Wa Mama Akampatia Makamba Katika Makazi Hayo , Na Akampa Gari Moja Ya Kubebea Majani Ya Ngombe Ili Makamba Ambebe

Na Tangia Siku Hiyo Akabadilika Kabisa , Well Lakini Mimi Niliondoka Nyumbani Kwasababu Tulipingana Haswa Yakija Katika Mambo Haya Ya Masilahi Ya Maisha Na Chama

Chama Cha Mapinduzi Kimeshika Watu Kila Sehemu Watu Hawawezi Kujitoa , Kama Wapinzani Wanataka Kwenda Mbele Basi Wasiogope Kuilazimisha Serikali Itengane Na Vyama Vya Siasa , Wale Mawaziri Wasiwe Mabunge Wawe Wanaajiriwa Wakuu Wa Mikoa Pia Kwa Mtindo Huu Tutakuwa Sawa Kwa Sawa Tutakuwa Tunashindana Kwa Sera Na Sio Nguvu Na Mabavu

Nimeona Mfano Kwa Mzazi Wangu Mwenyewe Na Mambo Yake Yeye Ni Chadema Lakini Hawezi Kuwa Nda Nguvu Bila Kuwahonga Ccm Katika Maisha Yake

Ahsante

...taratibu haya maongezi yako!

...halafu,mawaziri always ni wanasiasa au uwaziri ni nafasi ya kisiasa.

...ndo maana makatibu wakuu ni wataalamu na si wanasiasa.

...kazi ya waziri ni kutekeleza sera za chama,katibu mkuu ni sera za serikali!ndo maana kunakuwa na mchanganyiko wa sera!
 
Hey Mugongo Mamboz


Sasa Kabla Ya Uchaguzi Makamba Akaja Akaongea Nae , Yeye Mzee Akaamua Kwenda Nje Ya Mji Akamnunulia Makamba Nyumba Na Shamba , Akachukuwa Wale Ngombe Wazuri Wa Mama Akampatia Makamba Katika Makazi Hayo , Na Akampa Gari Moja Ya Kubebea Majani Ya Ngombe Ili Makamba Ambebe

Ahsante

Tumesoma kwenye magazeti kwamba Makamba aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM June mwaka jana, miezi saba baada ya Uchaguzi Mkuu.

Sasa sijui ni "kabla ya uchaguzi" gani Makamba alienda kuongea na mshua wako ili abebwe.

Acha kutupiga fix.

Ila point yako - ya kwamba wapinzani wote wako kitanda kimoja na watawala - hiyo ni ya msingi na ina ukweli. Tatizo ni fix katika mfano wako.
 
Back
Top Bottom