Ningelikuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya awamu ya tano ningelifanya haya

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,401
3,938
Ningelifuta vyuo vikuu vyote visivyokuwa na sifa ya kuitwa vyuo vikuu.

Ningelitengeneza vyuo vingi vya ufundi yaani VETA huku nikitoa kipaumbele cha hali ya juu kwenye ubunifu wa mitambo ya kutengeneza na kuchakata mazao ya kilimo.

Ningelifuta kidato cha sita badala yake mwanafunzi angemaliza Form Four na kwenda Foundation coarse ya kusomea anachokipenda kwenye maisha yake.

Ningelileta mitihani ya aina tatu kwa vijana wa Form four yaani Mitihani ya wanafunzi wanaojiweza zaidi yaani Extended examinations ambayo itakuwa graded kulingana na ufaulu wa mwanafunzi yaani kuanzia A to U.

Ningelileta mitihani ya wanafunzi wa kati na wa wenye uwezo mdogo slow learner yaani Core Examinations ambapo the highest score ni C hata akipata alama 100 anawekewa C grade.

Ningeliboresha miundombinu ya mashuleni kuanzia maabara Vifaa vya kujifunzia nk.

Ningelileta utaratibu wa Mwalimu kuongezewa masilahi yake maradufu huku nikiweka mashariti ya mwalimu awe ni mwanafunzi mwenye ufaulu mkubwa yaani A* student ndiye mwalimu.

Ningelijenga nyumba za kisasa za walimu na kuwaletea utaratibu wa kuagiza magari bila ushuru kwa kufanya hivyo nitawavutia waalimu kutoka private schools na kuja government schools na hapa nitatengeneza mazingira rafiki ya wazazi kuleta watoto wao shule za serikali hii itaibua vipaji vya watoto wengi wanaosahauliwa na mfumo mbovu wa Elimu tulio nao usawa utatawala rushwa itapungua sana maana hakuna kulingishana kwa sababu watoto wa masikini na matajiri watachanganyikana.

ITAENDELEA
 
Umesahau kitu kimoja muhimu sana. Kwa Africa na hasa kwa Tanzania ya leo waziri hatekelezi maono yake, bali huelekezwa na Rais mambo muhimu ya kufanya kwa mujibu wa MATAKWA ya Rais na ilani ya uchaguzi.

Hivyo usiseme ningekuwa waziri wa elimu; labda useme ningekuwa Rais. Ukuwa rais unaweza kufanya hayo! Sihitaji kukupa mifano kuhusu nguvu za Rais katika kutekeleza maono yake; maana ipo mingi tu na inaonekana wazi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom