CAPO DELGADO
JF-Expert Member
- Aug 31, 2020
- 7,617
- 16,713
Hakika ngoma aliimbwa, Airport Man of The Match Super League, Jezi no 6 mgongoni
Tarehe 20, October majira ya jioni kabisa nilikuwa nimekaa na mtaalamu wa kusoma mchezaji wa mpira (scaut) kutoka Timu moja ya London, ambaye pia ni Coach na Game analyst.
Tulikuwa tumekaa kutizama mpira katika Uwanja wa Benjamin Mkapa (Lupaso) nikiwa na mgeni wangu kama mwenyeji wake na Mentor, ninapata madini mengi mno kutoka kwake.
Niende moja kwa moja kwenye mada kuu.
Nilibahatika kuangalia mchezo laikini jicho langu liliamua kumuangalia na kumfuatilia mchezaji mmoja tu.
Nilijikuta siwezi kufanya analysis ya mchezo badala yake nilikuwa nimejikita kumtizama kijana mmoja kutoka Congo Kinshasa Zaire ya Mobutu. Nikimtazama mchezaji mrefu mweupe futi 6.2.
Nilimuona akiwa kiungo, kweli kweli katika ubora wa hali ya juu mno akidhihirisha uwezo wake mkubwa kuwa amecheza Timu kubwa kama As Vita na Raja na Timu ya Taifa ya Congo. Alipiga pass karibuni zote kwa usahihi, na alicover eneo kubwa sana katikati ya uwanja.
1. Uwezo wa kusambaza pasi: Nilimuona Ngoma akiwa na uwezo mzuri wa kutoa pasi za uhakika kwa wenzake, kuendesha mchezo, na kusaidia timu kudhibiti mpira.
2. Uwezo mkubwa wa kiakili na maamuzi: Nilimuona Ngoma akiwa na maamuzi ya haraka katikati uwanja. Akiweza kutumia akili kusoma mchezo na kuchukua maamuzi sahihi kwa kila tendo lake katikati ya uwanja.
3. Uwezo wa Kupiga Mashuti: Nilimuona Ngoma akirotate mpira na kupiga mashuti ya hatari kuelekea lengo la Al Ahly na kuwakosa kosa.
4. Kujitolea kwa Ulinzi: Nilimuona pia Ngoma akidrop down katikati ya walinzi wawili Inonga na Chemalone. kuanzia kuchukua mipira kusambaza pasi nk.
5. Uwezo wa Kukaba na Kuiba mpira: Ngoma pia alionyesha uwezo wa kukaba, kupora mipira, japo si mzuri sana katika hilo. Simba hapa wanapaswa kutafuta Kiungo Mkabaji mwenye uwezo mkubwa atakayekuwa wa kukaba na kuilinda back four yake, na hili ndio eneo linalowaponza zaidi Simba kwa sasa.
6. Ujuzi wa Kimwili na Stamina: Nilimuona pia Fabrice akiwa ametawaka mipira ya juu kama Kanute kuwa na uwezo wa kukimbia kwa muda mrefu uwanjani, kuwa na nguvu za mwili, na kuwa tayari kwa juhudi za kazi nzito.
7. Uwezo wa Kuwasiliana na Timu: Nilimuona pia Midfielder Teacher kwa uwezo mkubwa wa kutoa maelekezo, kuwasiliana na wenzake, kuanzia akina Chama, Inonga, Saido nk.
Hizi sifa zote niliweza kuziona kwa Midfielder Teacher Fabrice Luamba Ngoma.
Baada ya mchezo nikaulizwa huyu kiungo ni Mtanzania kweli? Baada ya kurudi nyumbani dipo nikarudi kwenda kuutazama mpira vizuri, possession mashuti nk.