Elections 2010 Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu

Status
Not open for further replies.
Kura yangu unayo Dr. Nakutakia kila la Heri, na Afya njema.
 
Tumshukuru Mungu kwa kukupa nguvu na tunamwamboa aendelee kukulinda na waTZ wote wapenda amani. Kila la heri.

Nasikitika kura yangu utaikosa kwani niko nje ya eneo la kura.
 
Pole na uchovu wa Kampeni mzee/Rais wangu mtarajiwa.

Asante kwa nasaha zako masaa/dakika hizi za mwisho yanatujenga kuendelea kuwaelimisha wale ambao bado wana Imani ngumu na wanaamini T-shirt, wali, pombe, 2,000TZS ndiyo njia ya kijikomboa.
 
Mungu akubariki na tunakutakia heri ushinde kwa kishindo. Mchango wangu ni kuwashawishi watu wangu wa karibu wakupigie kura!
 
I was waiting for so long for a new day to come....now i can see with my eyes, it is here it is Slaa, my blood my tears!!! it is him i will fight for, it is him changes will come through, no easy way to success! Rise up brethren for OUR HERO is here
 
Rais wangu ni Dr. W P Slaa.

Watanzania tukapige kura kesho na kuhamasisha ndugu na jamaa zetu kupiga kura. Mabadiliko tunayoyataka yatapatikana kwa sisi wenyewe kuwa Wakala wa hayo Mabadiliko. Kura yako ni kuelekea Tanzania Bora, nchi ya Ahadi. Dira na Uelekeo kufikia hapo imewekwa na CHADEMA tukiongozwa na Dr. Slaa.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.
 
Nimeguswa sana muheshimiwa raisi.

Kura yangu pamoja na wengine 100 wa mtaani kwetu, marafiki na ndugu zote ni kwako Dr Slaa.

You are my president regardless of results!! I wish you all the best!!
 
Mh. Dr. Slaa rais wetu mpendwa,

Sisi saa hizi tuko Zambia tukisubiria usafiri wa Train ya TAZARA na tunasikitika kwamba hatutakuwa pamoja huko Mbeya lakini tunakuahidi kwamba tutapiga kura kesho kama kawaida.

Tumeacha kazi na tuko watu 10 hapa stendi ya Kasama. Usiwe na wasiwasi utakuwa rais wetu wa 5. Mwambie Sugu tuko pamoja. Mungu akubariki sana. Wana Chadema damu damu!
 
Tupo pamoja Dr. Slaa (PhD). Umenikumbusha ile speech ya "I had a Dream" by Martin Luther King.....

Last edited by a moderator:
Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimeona mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

JK yeye kaona mvua inayonyesha huko Maswa!

Kura umepata Dr. Slaa. Hakikisheni tu wasimamizi wenu wana means ya kuwasiliana na nyie kadri kura zitakapokuwa zinahesabiwa. Nina imani kuna network coverage ya simu kila maeneo nchini na pia kwamba mmeshachagua mtu maalumu wa kucooordinate matokeo kila yanapokuwa tayari.

All the best
 
Your name tells me a lot about you.
I dont think Slaa needs to waste his second for this Crap!!
His time is much needed for something more important than this.
Umenielewa wewe kudadeki?

Daktari Slaa,

Kama unataka kura yangu, una masaa kama 20 hivi ya kujibu maswali yangu haya kabla sijaingia kwenye chumba cha kupigia kura.
  • Naomba unieleze vipi mfuko wa cement unaweza kuuzwa TZS 5,000 (about USD 3.34 @ exchange rate of USD 1 = TZS 1,500) kwa mfuko. Naomba utupe CIF price ya mfuko mmoja mpaka bandari ya Dar es salaam) halafu ongeza gharama ya kusafirisha kontena kutoka bandarini mpaka warehouse na gharama za wapakuaji. Tueleze nini gharama ya kusafirisha mfuko huo wa cement kutoka warehouse ya Dar es salaam mpaka huko Arusha na gharama zingine za kupakia na kupakua hiyo mifuko kwenye gari. Na tuambie hao waagizaji wanaweka faida ya kiasi gani mpaka wanahakikisha mfuko wa cement unauzwa kwa shillingi za Kitanzania buku tano?
  • Baada ya kuweza kuondoa ushuru wa forodha na VAT kwenye vifaa vya ujenzi pamoja na cement, je utalinda vipi viwanda vya ndani na ajira ya Watanzania. Kwa bei ya sasa hivi ya cement kutoka Pakistan, wenye viwanda wanalalamika kuwa wanashindwa kushindana bei na bei za cement ya Pakistan. Je wewe ukiondoa hizo kodi zote si viwanda vyote vya kuzalisha cement nchini vitafungwa? Na Watanzania elfu kadhaa kukosa ajira? Je utafanyajefanyaje hii issue?
  • Naomba utueleze hiyo treni ya umeme uliyoahidi kujenga ndani ya mwaka mmoja ambayo itakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka Mwanza mpaka Dar es salaam kwa masaa 3, pesa hizo utazitoa wapi hasa ukizingatia kuwa umeahidi kufuta kodi nyingi tu. Pia utatumia maajabu gani kukamilisha huo ujenzi ndani ya mwaka mmoja? Na hiyo treni itakuwa inasafiri kwa kasi (speed) gani na tueleze kama kuna treni yoyote duniani ambayo inasafiri kwa kasi hiyo sasa hivi.
  • Maisha yako yote umesomea mambo ya dini yako ya Kikristo na mpaka PhD yako ni ya sheria za kanisa. Hii ikakupa wewe sifa zote za kuwa mtumishi wa mungu na ukafanikiwa kuwa Padri wa kanisa la Kikatoliki. Ulipoupata huo updari uliahidi kwa mungu wako kuwa utamtumikia kwa uwezo wako wote na utafuata masharti yake yote. Wakat unaendelea kumtumikia mungu wako ulishindwa kujizuia na ulikuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ulizaa naye watoto wawili kinyume na maagizo ya mungu wako. Sasa kama ulishindwa kutimiza ahadi yako kwa mungu, ni nini hasa Watanzania wanacho zaidi ya mungu cha kukufanya wewe usivunje hizi ahadi unazowapa kwenye kampeni za uchaguzi?
 
Dr,
Leo toka asubuhi nilikuwa napita kwa kadri niwezavyo kushawishi watu wakupigie kura....90%+ wanakuunga mkono....all the best for tomorrow.Uanze rehersals za kuapishwa kabisa
 
Shughuli za kampeni ni ngumu na muda always ni mchache. Kitendo cha Dr. Slaa kuja hapa jamvini na kuongea na sisi ni ishara kuwa anajali sana pamoja na kwamba ratiba yake iko tight. Tunakushukuru kwa hilo.

Kura yangu ulishaipata tangu ulipotangaza kugombea katika ngazi hiyo. Ni wakati mzuri tu kuwakumbusha wa jamii wenzangu kuwa tuhamasike na kijitokeza kwa wingi kupiga na kulinda kura zetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Amenitumia kwenye inbox yangu FaceBook nimeona tushee wote hapa.
Usome kisha utume kwa wengine wengi hata ukiuchapisha ukapiga fotokopy, na kuugawa nyumba kwa nyumba
Ndugu wana JamiiForums, Mtandao wa IssaMichuzi, wana FaceBook na mitandao mingine na Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimena mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang’amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung’ang’ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.

DR W P SLAA - MGOMBEA WA URAISI CHADEMA 
 
Dr. Slaa, tupo nawe sasa na hata baada ya kura. Tumewashawishi watu wengi kwa nia ya simu, e mail, mazungumzo ya ana kwa ana ili wakupigie kura, na wote wameahidi kufanya hivyo. Ubarikiwe sana, na Mungu ibariki Tanzania.
 
Ndugu wana JamiiForums, Mtandao wa IssaMichuzi, wana FaceBook na mitandao mingine na Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimeona mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang’amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung’ang’ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika
Mtumishi wa watanzania,
Ninaomba ujiandae kuapishwa na si vinginevyo.HAPPY BIRTHDATE MKUU WANGU
 
Amenitumia kwenye inbox yangu FaceBook nimeona tushee wote hapa.
Usome kisha utume kwa wengine wengi hata ukiuchapisha ukapiga fotokopy, na kuugawa nyumba kwa nyumba
Asante mheshimiwa Rais wetu, ni kichaa peke yake asiyejua umuhimu wa wewe kuwa Rais. Nipo njiani naelekea Dodoma nilipojiandikisha ili nikakupigie kura kesho.
Mungu yupo upande wetu ninaamini atatutoa kwenye makucha ya dhuluma,ukandamizaji,kiburi cha watawala, ubadhirifu,dharau,manyanyaso na hila.
Kupitia wewe Dk Slaa Tanzania itaheshimika, watanzania tutajisikia huru kuwepo nchini mwetu,Tanzania yenye Neema itapatikana. Mungu akupe maisha marefu Dk Slaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom