Elections 2010 Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu

Status
Not open for further replies.
Kila la heri wapenda mabadiliko kura zetu umezipata. Tunakuombea umalize vyema kampeni huko Mbeya.
 
Slaa sio mbaya umekuja na hapa nilitegemea hapa pawe mwanzo kabisa katika kutafuta ridhaa na kuombaga kura.ila kama ujuavyo mambo safari hii ni magumu sana kwa upande wako maana mliwacha kuwashawishi vijana wajiandikishe ,kampeni hizi ndizo zitakazowagharimu vibaya sana na kuwakosesha ushindi ,hongera kwa kuwavuta wananchi katika mikutano hilo halina mjadala. hofu wengi wao si wapiga kura,

Ni bora ukajitayarisha kutangaza kuyakubali matokeo vile yatakavyotangazwa na kusaini,na pia uwapoze wengine ambao wamejenga tamaa ya lolote liwalo ni lazima washinde hao ni hatari kwa Taifa na ni hatari kwako na chama chako.

Akiba ya maneno ikiwa utafanikiwa kuutwaa Ushindi basi 2015 uhakikishe WaTanzania waishio nchi za nje nao wanapiga kura huko huko waliko.
So far nakutakia kila la kheri.

Mwiba handakini.
 
kura ni siri ya mpigaji dr slaa; hata hivyo kwa upande wangu tayari nimeshafanya uamuzi; kesho nakwenda kutekeleza tu. mimi kura yangu nitakupa wewe dr ws na wagombea wa chadema;

  • bw mhembano wa jmbo la chadema dodoma mjini kwa upande wa ubunge, na
  • bw marandu wa chadema kata ya kizota kwa upande wa udiwani.
mungu akubariki sana!!!
 
"...Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu..." (Ni maneno ya Dk Slaa kupitia mtandao wa jamii forums. Mpe kura yako. Sambaza ujumbe). Hicho kipande nimekimega nikakiweka katika sms na kuanza kuwasambazia wadau. Usishangae ukakutana nacho kwenye simu yako.


 
Daktari Slaa,

Kama unataka kura yangu, una masaa kama 20 hivi ya kujibu maswali yangu haya kabla sijaingia kwenye chumba cha kupigia kura.
  • Naomba unieleze vipi mfuko wa cement unaweza kuuzwa TZS 5,000 (about USD 3.34 @ exchange rate of USD 1 = TZS 1,500) kwa mfuko. Naomba utupe CIF price ya mfuko mmoja mpaka bandari ya Dar es salaam) halafu ongeza gharama ya kusafirisha kontena kutoka bandarini mpaka warehouse na gharama za wapakuaji. Tueleze nini gharama ya kusafirisha mfuko huo wa cement kutoka warehouse ya Dar es salaam mpaka huko Arusha na gharama zingine za kupakia na kupakua hiyo mifuko kwenye gari. Na tuambie hao waagizaji wanaweka faida ya kiasi gani mpaka wanahakikisha mfuko wa cement unauzwa kwa shillingi za Kitanzania buku tano?
  • Baada ya kuweza kuondoa ushuru wa forodha na VAT kwenye vifaa vya ujenzi pamoja na cement, je utalinda vipi viwanda vya ndani na ajira ya Watanzania. Kwa bei ya sasa hivi ya cement kutoka Pakistan, wenye viwanda wanalalamika kuwa wanashindwa kushindana bei na bei za cement ya Pakistan. Je wewe ukiondoa hizo kodi zote si viwanda vyote vya kuzalisha cement nchini vitafungwa? Na Watanzania elfu kadhaa kukosa ajira? Je utafanyajefanyaje hii issue?
  • Naomba utueleze hiyo treni ya umeme uliyoahidi kujenga ndani ya mwaka mmoja ambayo itakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka Mwanza mpaka Dar es salaam kwa masaa 3, pesa hizo utazitoa wapi hasa ukizingatia kuwa umeahidi kufuta kodi nyingi tu. Pia utatumia maajabu gani kukamilisha huo ujenzi ndani ya mwaka mmoja? Na hiyo treni itakuwa inasafiri kwa kasi (speed) gani na tueleze kama kuna treni yoyote duniani ambayo inasafiri kwa kasi hiyo sasa hivi.
  • Maisha yako yote umesomea mambo ya dini yako ya Kikristo na mpaka PhD yako ni ya sheria za kanisa. Hii ikakupa wewe sifa zote za kuwa mtumishi wa mungu na ukafanikiwa kuwa Padri wa kanisa la Kikatoliki. Ulipoupata huo updari uliahidi kwa mungu wako kuwa utamtumikia kwa uwezo wako wote na utafuata masharti yake yote. Wakat unaendelea kumtumikia mungu wako ulishindwa kujizuia na ulikuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ulizaa naye watoto wawili kinyume na maagizo ya mungu wako. Sasa kama ulishindwa kutimiza ahadi yako kwa mungu, ni nini hasa Watanzania wanacho zaidi ya mungu cha kukufanya wewe usivunje hizi ahadi unazowapa kwenye kampeni za uchaguzi?

majibu ulishapewa siku nyingi ila akili yako inaonekana inasahau baada ya sekunde moja tu hivyo hata akikujibu utasahau.

hivyo kama humpi ni hiari yako. wengine tumeshaamua kumpa kura zetu
 
maana mliwacha kuwashawishi vijana wajiandikishe ,kampeni hizi ndizo zitakazowagharimu vibaya sana na kuwakosesha ushindi ,hongera kwa kuwavuta wananchi katika mikutano hilo halina mjadala. hofu wengi wao si wapiga kura,

Akiba ya maneno ikiwa utafanikiwa kuutwaa Ushindi basi 2015 uhakikishe WaTanzania waishio nchi za nje nao wanapiga kura huko huko waliko.
So far nakutakia kila la kheri.

Mwiba handakini.

Mwiba kwani wapiga kura waliojiandikisha na kufikia millioni zaidi ya 19 ni wazee?
 
Mh. Rais punguza ukali wa maneno, nimeshidwa kumaliza kusoma kwa uchungu niliopata,, kura yangu haina pa kwenda zaidi ya CHADEMA
 
Dr Slaa,

Kwa unyenyekevu mkubwa sana nakupongeza kwa ujasili wako na ari yako katika mbio hizi za Urais.

Kama nilivyokubainishia mwanzoni wakati wa uteuzi wako ndani ya chama chako. Nilisema bado kabisa kwa wewe kugombea Urais mlitakiwa kuimarisha chama chenu katika ngazi za Ubunge na udiwani ili kuleta mageuzi makubwa ndani ya bunge la muungano.

Fahamu kubwa una wapambe wengi sana LAKINI WAPAMBE SIO APIGA KURA. Ninasikitika kukambia kuwa sidhani kama utaweza kufikisha hata 12% ya kura zako katika Uraisi.

Hongera sana kwa kujaribu.
 
Kwa yoyote anayechukia ufukara wa Wa-Tanzania wengi...naamini atafanya lililo jema kesho..
Kuchagua mabadiliko hakuepukiki...Kura zetu unazo Mh.Dokta

Mungu wa Milele na asimamie haki za wanyonge wa Tanzania hapo kesho katika sanduku la kura mpaka utangazwaji wa matokeo..AMEN
 
yangu no, yafamilia yangu no, ya mtaa wetu no,ya kijiji chetu no, ya tanzania utapata 10%

hahahahahaha..... hatimae leo umefufuka haya habari za kupotea tulikumiss kweli jamvini karibu tena ila ukumbuke WATANZANIA WAMESHA AMKA SIKU NYINGI CCM INAVUTA SHUKA WAKATI KUMESHA PAMBAZUKA!

KURA ZETU WATANZANIA (MBAYUWAYU) TUNAMPA DR WA UKWELI NAYE SIE MWINGINE NI WILBROAD PETER SLAA
 
Dr. uwe na uhakika na kura yangu, na nimejitahidi sana kwa kadiri ya uwezo wangu kuwa-convince walio karibu nami wakupigie kura, wameniahidi watafanya hivyo.
All the best Rais Mtarajiwa!
 
Dr. Slaa zawadi yangu kubwa ya kusheherekea siku ya ya kuzaliwa ni KURA YANGU MIMI NA JAMAA ZANGU JUMLA TUKO 50 sina kingine cha kukupa
 
Jamani kikubwa kilichobakia ni kulinda Kura zetu.
Dr. Slaa kashapata ushindi.
 
Dr. Slaa kura yangu na weengi niliowashawishi kesho utazipata - ushindi wako ni ushindi wetu wapenda nchi. Usishangae kuwa wengine tupo concerned zaidi hata ya wewe na uchaguzi huu. Tuendelee kuhamasisha na tupo pamoja.
 
DrSlaa, u have my vote already
Godbless Lema has my vote also
Diwani wa CHADEMA has my vote too!
Ninakupenda sana Dr, ninaipenda CHADEMA!
MUNGU NDIYE TUMAINI LETU!
 
Dr Slaa,

Kwa unyenyekevu mkubwa sana nakupongeza kwa ujasili wako na hari ysko katika mbio hizi za Uraisi.

Kama nilivyokubainishia mwanzoni wakati wa uteuzi wako ndani ya chama chako. Nilisema bado kabisa kwa wewe kugombea Urais mlitakiwa kuimarisha chama chenu katika ngazi za Ubunge na udiwani ili kuleta mageuzi makubwa ndani ya bunge la muungano.

Fahamu kubwa una wapambe wengi sana LAKINI WAPAMBE SIO APIGA KURA. Ninasikitika kukambia kuwa sidhani kama utaweza kufikisha hata 12% ya kura zako katika Uraisi.

Hongera sana kwa kujaribu.

Baru x2;
Leo umekuja mwenyewe? maana siku zote ulikuwa uanamtuma Zawadi!! Hayo unayoyasema tuachie sisi; kwani U-Rais ni wa nani? Dr go on and fight the fight; kule ulikozuiwa jana unazo 95% kimkoa; maana CCM hawajui kuwa wametibua kote! DR Slaa has the power of the people!
 
Dr. Slaa kura yangu na weengi niliowashawishi kesho utazipata - ushindi wako ni ushindi wetu wapenda nchi. Usishangae kuwa wengine tupo concerned zaidi hata ya wewe na uchaguzi huu. Tuendelee kuhamasisha na tupo pamoja.


Dr. SLAA, ni kweli unakubalika. LAKINI hakikisha wewe au watu wako wanakesha kuhakikisha wapiga kura wako hawarubuniwi usiku majumbani kwao, kwenye gesti au njiani. Iweni macho hata asubuhi watu hugawa pesa. Tena, kaeni na KAMERA ZENU kuchukua matukio yooooote; ikiwa ni pamoja sura za watu, nk Mkikesha leo na kesho, MTASHINDA. Msipokesha, hola!


Hakikisheni ujumbe wa watu kukaa mita 300 unawafikia waTanzania wote, la sivyo wengine wataogopa-hasa nje ya miji.
 
Maneno ya Dr Slaa yameniuma sana, nimetokwa machozi wakati nasoma ujumbe wake hapa jamvini. Ndugu zangu,nakumbuka jana nilipanda daladala aina ya Coaster toka pale External hadi Mwenge.

Nikaanza kumpigia kampeni Doctor Slaa baada ya mama mmoja kuanza kulalamikia ugumu wa maisha wakati wa mazungumzo na jirani yake kwenye seat. Watu wote kwenye ile daladala waliniunga mkono wakisema ni vema kubadili uongozi ili tuone nao utatufanyia nini.

Naililia Tanzania ya Nyerere na Sokoine
 
Dr tulishaamua siku nyingi sana kukupa kura na tunasubiri kesho ifike salama ili tukakamilishe maamuzi yetu kwako, MUNGU AKUBARIKI UWE RAISI BORA WA TANZANIA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom