Elections 2010 Ninaomba kura zenu ili niwe Rais wenu

Status
Not open for further replies.
Bila shaka zawadi pekee kwa siku yako ya kuzaliwa ni kura yangu na wote wanaonitegemea katika familia yangu.
 
Dr. Slaa Nakuhakikishia hapa Bukombe tunao mwamko wa ajabu wa kutaka mabadiliko naweza kusema ni mlipuko wa uelewa wa ajabu ambao ni wewe ndiyo umeusababisha baada ya kutangaza nia ya kugombea kiti kikuu.Kifupi hapa Bukombe unazo kura nyingi na mbunge utapata Prof.Kahigi.Kwa hakika kuna umoja wa ajabu hadi wenzetu wa CCM tunao ila hawajionyeshi tegemea kura za kimbunga.Mungu akubariki sana
 
Dah,this is really touching!
Dr.Slaa,mimi sitapiga kura kwa sababu ya uhuni tulio fanyiwa chuoni UDSM,ila nime shawishi watu wengi kadri nilivoweza!

Nafurahi kwamba hata waliokua hawataki mabadiliko sasa wamekukubali kwa kuwaeleza ukweli wa tulipo na kwa sababu gani.
Ina niuma sana kukosa nafasi hii adimu katika maisha yangu,ila nitakutambua kama raisi wangu utakae leta mabadiliko katika Tanzania.

Ushinde au usishinde tutakua pamoja katika harakati za kuelimisha watanzania ili tupate mabadiliko ya kweli,...
Inaniuma sana kutoweza fika dar es salaam kupiga kura,ila naamini UTASHINDA na hata ikitokea otherwise usikate tamaa maana harakati baada ya kushindwa (bahati mbaya ikitokea ) nitakua msitari wa mbele zaidi katika ushiriki huo,.....

Nitakuwa wakala makini na mwaminifu ili Tarime iendelee kuwa chini ya chadema.....

I've full of tears about to drop down,...
Mapenzi ya Mungu na yatimie.
 
Go Slaa Go... For the voices of the oppressed and the blood of the innocent ones is heard from a distance, the flesh of the poor children who were denied their right to live is vivid, nothing can stop them, the cry is everywhere, Go Slaa Go, NO river to stop you, no mountain to downslip you!

Go Slaa Go, for the harvest is ready, go now for the sky has heard our prayers and our Ancestors are with you, go as MAN go, never dare to look back, for hundreds are with you, Go to serve them. Mpiganaji Elli
 
Dr wa ukweli rest assured that u have ma vote. Mimi na majirani zangu tutakuchagua wewe.

Asante for a heart touchin message, u a indeed a God send presidaa. Be blessed.
 
. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Baba tuko pamoja. Nina watu 20 nyuma yangu kwa ajili ya kura za mabadiliko CHADEMA kuanzia Urais mpaka udiwani.
Wapenzi wote wa mabadiliko, ukiamka asubuhi kesho wakumbushe washirika, wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwa njia ya simu kama hawako karibu wapige kura ya kukomboa Taifa. Siku ya ukombozi ni kesho 31/10/2010.
 
Kura zetu na za ndugu zetu utapata, kwani kura yangu ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa langu. Sitauza, Sitaacha kuitumia na pale nitakapoitumia nitaitumia kwako, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote mliyotuahidi mtayatimiza na zaidi.
 
Dr.Slaa,

Mimi binafsi kura yangu umeipata,nimejaribu pia kuwashawishi wazazi,ndugu jamaa na marafiki ili wakupigie kura wameniahidi watafanya hivyo lakini naelewa mwisho wa siku kura inabaki kuwa ni siri ya mtu.

Ninachokuomba/Kukushauri,usisahau maombi/kusali kwa mwenyezi Mungu hasa usiku huu wa leo_Omba Mungu akulinde na atume malaika wake walinzi wawaguse wale wote ambao bado hawajaguswa na kuona umuhimu wa mabadiliko ili kesho waweze kukupigia kura wewe Dr.Slaa.

Watanzania tumechoka tunataka mabadiliko. Mungu akubariki,Mwenyezi Mungu utusaidie.Amina.
 
Nimewasiliana na ndugu zangu wote wa wamenihakikishia kukupa kura za ndio,na sasa nafanya kampeni kwa njia ya simu na mtandao kuhakikisha kila anayenifahamu anakupa kura ya ndio.

La muhimu hapa ni kuhakikisha unaleta mageuzi ya uongozi na mtazamo wa maendeleo ya kweli kwa TAIFA na sio kwa mtu binafsi kama ilivyo sasa.

....Mungu akulinde na akupe nguvu na ujasiri wa kuwa na subira na uvumilivu pale utakapoona kuna fedheha ukae mbali na ibilisi kwasababu maamuzi yako yanaweza kuchukua maisha ya watu na taabu na njaa vikawakabili watanzania.

...hatuna imani sana na serekali iliyoko madarakani kama kweli wanaweza kupokea matokeo kushindwa kirahisi tuu kama inavyojionesha,ninachokuomba sana rais mtarajiwa uwwe na roho ya uvumilivu sana.maamuzi yafanywe na chama kwa ujumla wake na uwe kama mchangiaji tuu ili dunia ione jinsi tanzania inavyoongozwa na Jeshi badala ya Raia wa kawaida kama ilivy maafikiano.
 
yangu no, yafamilia yangu no, ya mtaa wetu no,ya kijiji chetu no, ya tanzania utapata 10%

Yako ukimnyima sawa lakini ya familia yako, mtaa wako na kijiji chako si siri yao? au kadi zao tayari umeshazinunua zote ikiwamo ya mkewo?
 
Go OUR HERO Go, go beyond the borders of corruption, and the hills of oppression, our tears and the innocent shed blood of our brethren has made the land wet, evryone is crying whether silently or loudly but there is a cry!!!
Go beyond unfulfilled dreams of the sons and daughters of the land, go now go, remember, the voices of our enemy can not stop Us, we are many and dtermined to achieve a common goal for us and for the children of our children!! Go Slaa GO!!! mie mwana wa Nchi ELLI
 
Mimi na nyumba yangu tunakupa kura zetu Dr Slaa. Mwenyezi Mungu na akutangulie...
 
yangu no, yafamilia yangu no, ya mtaa wetu no,ya kijiji chetu no, ya tanzania utapata 10% originally posted by Malaria Sugu

Duh wewe uko juu!kumbe nilikuwa sijui kama una kura ya veto,mtaa utaamua utakavyo,kijiji kiutakavyo!!au unajivunia wizi wa CCM???This is stupidity!!!
 
Dr. Slaa,
Tunakushukuru sana kwa upendo wako. Binafsi nakutakia afya njema na tunakuombea kwa mungu akusaidie uweze kutuongoza vyema watanzania.

Tunakuhakikishi mimi, familia yangu na ndugu zangu ambao tunakuunga mkono kuwa kura zetu umepata na tutazilinda na kwamba hatuhitaji malipo kulinda kura zetu.

Mungu akubariki sana
 
Daktari Slaa,

Kama unataka kura yangu, una masaa kama 20 hivi ya kujibu maswali yangu haya kabla sijaingia kwenye chumba cha kupigia kura.
  • Naomba unieleze vipi mfuko wa cement unaweza kuuzwa TZS 5,000 (about USD 3.34 @ exchange rate of USD 1 = TZS 1,500) kwa mfuko. Naomba utupe CIF price ya mfuko mmoja mpaka bandari ya Dar es salaam) halafu ongeza gharama ya kusafirisha kontena kutoka bandarini mpaka warehouse na gharama za wapakuaji. Tueleze nini gharama ya kusafirisha mfuko huo wa cement kutoka warehouse ya Dar es salaam mpaka huko Arusha na gharama zingine za kupakia na kupakua hiyo mifuko kwenye gari. Na tuambie hao waagizaji wanaweka faida ya kiasi gani mpaka wanahakikisha mfuko wa cement unauzwa kwa shillingi za Kitanzania buku tano?
  • Baada ya kuweza kuondoa ushuru wa forodha na VAT kwenye vifaa vya ujenzi pamoja na cement, je utalinda vipi viwanda vya ndani na ajira ya Watanzania. Kwa bei ya sasa hivi ya cement kutoka Pakistan, wenye viwanda wanalalamika kuwa wanashindwa kushindana bei na bei za cement ya Pakistan. Je wewe ukiondoa hizo kodi zote si viwanda vyote vya kuzalisha cement nchini vitafungwa? Na Watanzania elfu kadhaa kukosa ajira? Je utafanyajefanyaje hii issue?
  • Naomba utueleze hiyo treni ya umeme uliyoahidi kujenga ndani ya mwaka mmoja ambayo itakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka Mwanza mpaka Dar es salaam kwa masaa 3, pesa hizo utazitoa wapi hasa ukizingatia kuwa umeahidi kufuta kodi nyingi tu. Pia utatumia maajabu gani kukamilisha huo ujenzi ndani ya mwaka mmoja? Na hiyo treni itakuwa inasafiri kwa kasi (speed) gani na tueleze kama kuna treni yoyote duniani ambayo inasafiri kwa kasi hiyo sasa hivi.
  • Maisha yako yote umesomea mambo ya dini yako ya Kikristo na mpaka PhD yako ni ya sheria za kanisa. Hii ikakupa wewe sifa zote za kuwa mtumishi wa mungu na ukafanikiwa kuwa Padri wa kanisa la Kikatoliki. Ulipoupata huo updari uliahidi kwa mungu wako kuwa utamtumikia kwa uwezo wako wote na utafuata masharti yake yote. Wakat unaendelea kumtumikia mungu wako ulishindwa kujizuia na ulikuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ulizaa naye watoto wawili kinyume na maagizo ya mungu wako. Sasa kama ulishindwa kutimiza ahadi yako kwa mungu, ni nini hasa Watanzania wanacho zaidi ya mungu cha kukufanya wewe usivunje hizi ahadi unazowapa kwenye kampeni za uchaguzi?
 
Happy Birthday to you again DR. SLAA. Tunauhakika kuzaliwa kwako katika tarehe hio ambayo ni siku muhimu leo hii katika mapambano yako ya kuwania Uraisi si jambo dogo.

Tunashukuru mungu katupatia mtu muhimu sana kama wewe katika nchi yetu inayokuhitaji sana.

TUPO PAMOJA MORE THAN 100%.
 
DR.SLAAA kura yangu, mke wangu, baba yangu, mama yangu na wadogo zangu wanne unayo watu (8) na Arusha mjini wote na vitongoji vyake na watz wema watakupa kura yao, cha msingi jiandae kuapishwa usifikirie tena kura.....................
 
I love you Dr. Slaa. We all love you. My family is travelling to vote for you. On their way they are singing "Dr. Slaa for presidency". BRAVO MTANZANIA HALISI.
 
Nathubutu kuto kukosa kuchagua kiongozi wangu safari hii na staki wengine wakose lakini kikubwa ni kuomba mungu hata wasio na mwelekeo kesho wakupigie kura wewe tuu Dk Slaa.

Najaribu kuwashawishi na vijana wengine wengi wakakupigie kura pia kura yangu ni yako nakukabidhi kama ndio hazina yangu iliobaki chini ya sisiem nitakufa kihoro bure tuu!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom