Bado nipo nipo
Member
- Nov 19, 2011
- 69
- 11
Vipi wadau wa hapa ndani, leo nimekuja kwenu kuomba msaada juu ya hili. Nina baba yangu ambaye mambo yake yamemwendea kombo sana mwaka huu, haswa kwa swala la kifedha. Na ameniambia anataka kuuza nyumba pamoja na kiwanja alicho nacho ambamo ndiko anakoishi na familia yake ili warudi kijiji walipotoka na kufanya biashara na fedha atakayopata. Je hii itasaidia ama ndio muendelezo wa matatizo endapo biashara itazorota?