Nimewakamata wezi wa ajira mtandaoni!

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Baada ya kuapply tangazo lao la kazi huko Uranium Songea,fasta wakanipigia simu wakadai wapo kwenye mchakato wa kuita watu kwenye interview lakini tutangulize kwanza laki 2 kwa M-PESA, nikawakubalia...nikaja hapa jamvini kuhoji uhalali wa hii kampuni kwa kiasi kikubwa hivyo kabla hata hatuajiriwa. Nikachukua mawazo yote ya wanaJF, nikatengeneza maswali yangu kadhaa naomba uyajibu.

Halafu nikampandia hewani yule jamaa aliyejitambulisha kama Ishe Mboma, simu ikaitaaaa weeee, hadi ikakatika haikupokelewa. Baada ya kama dakika 5simu yangu ikaaza kuita, kucheki yule jamaa ananipigia. Nikapokea!! Akaniambia alikuwa kwenye KIKAO.

Maongezi yakaanza kama ifuatavyo: Nilianza kumwambia kwamba nina fedha mkononi na nipo dukani Mpesa tayari kuzituma, ila nina mawali matatu tu naomba uyajibu kabla sijatuma.

Swali la kwanza nilimuuliza, Je hiyo ni kampuni au ni Recruitment Agent(RA)? Akanijibu yeye ni HR wa ndani ya kampuni na sio RA.
Nikamuuliza huo mgodi unaochimba Uranium upo wapi? Akanijibu upo songea na mpaka kijiji akanitajia...nikamwambia kwanini asiniajiri kwanza halafu tufanye makubaliano mshahara wangu wa kwanza nimkabidhi huo mzigo, akakataa!!,
Nikamuuliza Wewe mwenyewe na hiyo kampuni mpo wapi(nikajua wapo dar)..akanijibu wapo Songea mjini 2 km kutoka pale mjini.
Nikamwambia kama upo Songea basi na mie nipo hapohapo Songea unaonaje tukionana halafu nikakukabidhi mzigo ana kwa ana....!!

Hapo jamaa aliniachia vumbi baya!! Akaniambia ''This thing is very confidential and we are not allowed to have personal meeting'' Nikamwambia NIMEKUKAMATA MWIZI MKUBWA WEWE. AKAKATA SIMU.

SO TUWENI MAKINI JAMANI NA HAWA JAMAA WANAOTOA KAZI HALAFU WANATAKA FEDHA KWANZA, BILA KUJA HAPA JF NISINGEPATA MAWAZO YA KUULIZA STRONG QESTION YULE BWANA,MANAKE ALISHANIBAMBA.
 
Hao wako wengi kwa design tofauti tofauti kabisa. Wanatumia cm zetu kutuma jumbe mbalimbali na namba za nje ya Tz kabisa. NAfikiri wengi tuko makini siku hizi maana wametapakaa sana. Kuna wengine tena wanaiba line za watu hasa tigo na wanazitumia kuiba fedha hasa kwa wafanyabiashara. Waambie kabisa kama mfanyakazi wako akipigiwa simu au sms na namba yako huku akitakiwa kutuma pengine hela ya mauzo au kutoa kitu cha thamani ni bora aache. Kama una line mbili hakikisha zote wafanyakazi wanazo ili wakipata wasiwasi na moja wanakutafuta na nyingine tena wakupigie simu na wala si sms.
 
mmepiga hatua kwasababu mmeanzisha hii website? acha izo bwana....mbona masikini wamejaa mtaani?ombaomba kibao...huo ni mkoa mgumu sana kufanya kazi,ukipangiwa kazi tabora kutoka ni ngumu sana...labda kama utakuwa nzega uwe mwizi au mnunuzi wa madini ya wizi wanayoiba wachimbaji wa Lusu...
 
Mbona kama hii yako haina uhusiano wowote na mada iliyopo? Au ndo umepandikiza post ndani ya post?
 
mmepiga hatua kwasababu mmeanzisha hii website? acha izo bwana....mbona masikini wamejaa mtaani?ombaomba kibao...huo ni mkoa mgumu sana kufanya kazi,ukipangiwa kazi tabora kutoka ni ngumu sana...labda kama utakuwa nzega uwe mwizi au mnunuzi wa madini ya wizi wanayoiba wachimbaji wa Lusu...

Ina uhusiano gan na mada? Au nyny ndo walewake.
 
Back
Top Bottom