Nimepata Msiba WanaJF

Pole ndugu, Mungu akupe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Tumshukuru Mungu kwa sababu pia uliweza kulelewa na Babu yako na kumjua.

R.I.P Babu wa sipo.
 
wabongo bana fyetele sana....sasa mtu anasema ana msiba mnampa thanks!!!???
binafsi sioni haja ya kusikitika kama utakuwa muumini wa hizi dini zetu...tushangilie maana kasogea katika ufalme wa Mungu..
 
Ndugu wana JF leo mchana nimepata msiba wa Babu yangu Mzaa Mama. Huu msiba mzito sana kwangu kutokana na maisha niliyoishi. Kwa wale ambao hawakukulia kwa Baba na Mama wanajua role ya Babu na Bibi nami ndio inayonifanya niomboleze sana. Kwa kifupi alikuwa ni Baba mzazi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe milele. Amen

Pole sana kwa kufiwa na babu
 
pole sana sipo. Mwenyezi Mungu
awalinde msafiri salama na shughuli zote
za msiba ziende salama.
Mwenyezi Mungu awafariji wafiwa wote.
RIP babu yake sipo
 
pole sana Sipo

Bwana allitoa, na Bwana ametwaa: Jina la Bwana na libarikiwe. Ayubu 1: 21b
 
Pole na msiba wa Babu yako.

Sisi kwetu wajukuu ndo tunacheza ngoma ni sherehe kubwa sana!!
 
pole sana kwa msiba wa babu yetu! what we have to know is that all human beings we are under the ownership of GOD and he can take us anytime! take courage bro
 
pole sana kwa msiba wa babu yetu! what we have to know is that all human beings we are under the ownership of GOD and he can take us anytime! take courage bro
 
Ndugu wana JF nashukuru sana kwa sapoti yenu, nadiriki kusema kuwa mmekuwa sehemu ya familia yangu kwa kiasi ambacho siwezi kukisemea hata kwa chembe ya maneno au kuitenda kwa jinsi yoyote ile kwa aina yoyote ya matendo. Nashukuru kuwa maombi na sala zenu zimetuwezesha kufika salama Arusha ingawa bado wengine wanasafiri ila ni imani yangu kuwa watafika salama wote pia.
Maziko yatafanyika Jumatatu ya tarehe 23/11/09 kijijini kwetu, hii imetokana na Dayosisi ya Mkoani Arusha kuomba nafasi ya kushiriki kwa kila hali kutokana na Marehemu Babu kuwa mtumishi wao kama Mchungaji kwa kipindi kirefu tu.
Hali ya huku kwa sasa ni mvua sasa kwa hizi local roads kunatokea matatizo ya hapa na pale lakini ndio barabara zetu tutamaliza kwa amani tu ndio imani yetu.
Nashukuru tena sana ndugu zangu "Be blessed all"
 
Ndugu wana JF nashukuru sana kwa sapoti yenu, nadiriki kusema kuwa mmekuwa sehemu ya familia yangu kwa kiasi ambacho siwezi kukisemea hata kwa chembe ya maneno au kuitenda kwa jinsi yoyote ile kwa aina yoyote ya matendo. Nashukuru kuwa maombi na sala zenu zimetuwezesha kufika salama Arusha ingawa bado wengine wanasafiri ila ni imani yangu kuwa watafika salama wote pia.
Maziko yatafanyika Jumatatu ya tarehe 26/11/09 kijijini kwetu, hii imetokana na Dayosisi ya Mkoani Arusha kuomba nafasi ya kushiriki kwa kila hali kutokana na Marehemu Babu kuwa mtumishi wao kama Mchungaji kwa kipindi kirefu tu.
Hali ya huku kwa sasa ni mvua sasa kwa hizi local roads kunatokea matatizo ya hapa na pale lakini ndio barabara zetu tutamaliza kwa amani tu ndio imani yetu.
Nashukuru tena sana ndugu zangu "Be blessed all"

pole sana mpendwa kina Pakajimmy wanataka kuhudhuria mazishi unaweza kuwapa Contact kamili ili muwe pamoja

mungu awatangulie kwa yote
 
Pole sana ndugu...

Inna Lillah Wa Inna Ilayh Rrajiuun. (Sisi wote ni wa Allah na Kwake Yeye tutarejea)
 
pole sana mpendwa kina Pakajimmy wanataka kuhudhuria mazishi unaweza kuwapa Contact kamili ili muwe pamoja

mungu awatangulie kwa yote
nashukuru FL1. NimeshamPM PakaJimmy. Thanx alot
 
Pole sana ndugu, bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe, tupo pamoja kwenye kipindi hiki kigumu,pole sana!!
 
Ndugu wana JF leo mchana nimepata msiba wa Babu yangu Mzaa Mama. Huu msiba mzito sana kwangu kutokana na maisha niliyoishi. Kwa wale ambao hawakukulia kwa Baba na Mama wanajua role ya Babu na Bibi nami ndio inayonifanya niomboleze sana. Kwa kifupi alikuwa ni Baba mzazi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe milele. Amen

Poleni sana, Tupo pamodja kiroho!
 
Back
Top Bottom