Nimepata msiba wa Mama yangu mzazi

Mungu ampumzishe kwa amani mama. Pole kwa kuondokewa na mzazi, familia ya JF ipo nawe leo hata kesho!
 
Mkuu TETE-A-TETE,

Pole sana ndugu yangu!

Habari za kifo zisikie tu kwa jirani, lakini kwasasa najua how u feel, i have been in the like situation just two months ago!

Mungu akutangulie ndugu, Mungu wa Mbinguni ndiye atakayekufariji kikweli na kukufuta machozi!

Lakini zaidi, Shughuli hii na iende kwa usalama na kwa mipango iliyoandaliwa, huku BWANA akiwa ndiye kiongozi na msimamizi mkuu!

Farijika ndugu- JIPE MOYO MKUU!
 
Pole sana Tete.
Kufiwa ni kitu kigumu sana. Ila Mungu atakupa nguvu.
Safari njema na natumaini mazishi na mipango mingine itaenda vizuri mumpumzishe mama yenu salama
 
Duh Pole mno tete.....RIP mama...tupo pamoja kwenye hili....Mungu akupe nguvu
 
Pole kwa msiba mzito wa kufiwa na mama mzazi.Mtihani ulioko mbele yako ni ule wa kumkosa na kukumbuka malezi yake na mapenzi yake.

Mimi nakuombea dua Mungu akujaze subira na kukupa moyo wa uvumilivu.Mwenyezi Mungu sisi wote ni waja wake na kwake tutarejea.alale mahali pema peponi mama huyu mpendwa.Amin.
 
pole sana ndugu yangu mungu atakupa nguvu na utaenda salama na utarudi salama mungu ailaze mahali pema peponi Amen
 
Wana jfs nimefiwa na mama yangu mzazi leo kcmc bado nipo dar nataraji kuondoka kesho kuelekea moshi naomben sala zenu ktk kipindi hiki kigumu
My number 0719354556
Pole sana mkuu tete'a'tete,

Utapata simu kutoka Support Office za JF zilizopo Dar es Salaam, watataka kufahamu jinsi ya kuonana nawe na kuwasilisha rambirambi toka JF.

Kwa wana JF ambao wangependa kuchangia kwenye rambirambi hizi kwa mkuu tete'a'tete basi wanaweza kuwasiliana na ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam.
 
Pole sana mkuu kwa msiba huo wa mama. Mwenyezi Mungu ailaze Mahala Pema Peponi Roho ya Mama - Amen
 
Pole Sana Mkuu....kwa msiba wa mama.... Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
 
Pole sana ndugu yangu Mungu akupe subira. Ni subira tu ndio inayotakiwa katika kipindi hiki kigumu cha msiba! Mungu akufanyie wepesi.
 
pole sana ndugu yetu TaT!
Ni tukio la kustua na kuhuzunisha sana kufiwa na mzazi. Mungu akupe nguvu kuhimili majonzi, simanzi na ombwe utakalolisikia.
RIP mama....
 
Kwakweli msiba ni usikie tu umetokea lakini ukikufika ni Balaa.Pole sana tete kwa kuondekewa na NGUZO kuu ya Kidunia..yote hayo ni mapenzi yake mungu.Roho ya Marehemu mama Ipumzike kwa Amani...Amen..Pole sana naomba maulana akutie nguvu katika mapito haya magumu ya kidunia
 
Back
Top Bottom