PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 7,768
- 16,022
Katika mahijiano ya Dakika 50 na sekunde 3 aliyofanyiwa na Azam TV ambayo yameonyeshwa kwenye youtube channel ya kituo hicho, Fiston Mayele ameongea mambo kadhaa, lakini mimi nimeamua kuongelea suala lake la mahusiano na timu aliyoichezea, yaani Yanga pamoja na anayoichezea hivi sasa, yaani Pyramids FC.
Katika mahijiano hayo, Mayele ameonyesha kukerwa na comments za mashabiki wawili au watatu dhidi yake au familia yake na kuamua kuibebesha lawama timu nzima ya Yanga kwa comments za watu hao.
Mayele anasema alipojiunga na Yanga alipewa mkataba na aka sign, ali sign sababu alikuwa hajui kiingereza, Manager wake alikuwa hajui Kiingereza na alikuwa anachekacheka tu.
Ulipoisha msimu wa kwanza, ndipo akasmua kubadili Manager na kumtumia Jasmine ambaye kwanza alishangazwa na ule Mkataba. Akasimamia ubadilishwe, akaongezwa mshahara pia ukampa uhuru wa kuondoka ikitokea club inamhitaji.
Amesema aliahirisha kusema live alichotaka kusema sababu Tanzania ameacha watu wake (familia) ila ameshauriana na Jasmine kwamba mwisho wa msimu ndiyo aongee kila kitu.
Hayo sikuona kuwa ni big issue kivile, kilichonistua na alipoiponda hadi timu aliyoichezea sasa. Mayele anasema alipewa Mkataba na Pyramids FC, mkataba ule Jasmine akaukataa, kwa maelezo yake Mayele akasema “waarabu ni wahuni kama usupotumia akili watakukandamiza”.
Hii kauli inatosha sana kumuweka Mayele katika sintofahamu na maboss wake hao wa sasa.
Mayele anaonekana ni mtu anayependa sana social media na attention zake, siyo mbaya ila, anapaswa kuelewea negative na positive effects za social medias. Hivyo awe mwangalifu sana na aongeacho.
Wana Yanga waliokwazika na Mayele ningewashauri wasiyabebe hayo, ni kijana anajipigania, pia kati ya vitu vinavyopelekea kuwa na kauli zile ni limits aliyo nayo katika uelewa na matumizi ya lugha ya kiswahili. Anajifunza Kiswahili the hardway hali inayompelekea kutoa kauli zinazoonekana kuwa ni kero, kukosa ustaarabu n.k ila yote ni sababu ya kuwa na ufinyu wa uelewa wa lugha anayoitumia, maana anajifunza kurusha ndege huku akiendelea kufanya assembling.
Kama angetumia lugha ya kwao au Kifaransa kamwe asinge strugle. Hivyo muleweni tu na mumuache aendelee na maisha aliyoyachagua.