Majumuisho ya mapitio ya mkataba WA YANGA na Sport Pesa

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
*VIVA YOUNG INTERNATIONAL GROUP*

*MAJUMUISHO BAADA MAPITIO YA MKATABA WA UDHAMINI WA TIMU YA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB NA KAMPUNI YA SPORTSPESA LIMITED*

*MAY, 2017*

*1. UTANGULIZI*

Tarehe *08/05/2017* Klabu ya Yanga ilisaini mkataba wa udhamini kwa miaka mitano (5yrs) kati yake na Kampuni ya *SportsPesa Limited* wenye thamani ya jumla ya shilingi milioni mia tisa hamsini *(950m)* za Kitanzania kwa mwaka.

Mkataba huo ulisainiwa mbele ya Kamati ya Utendaji, Baraza la Wadhamini la Klabu ya Yanga huku ukishuhudiwa na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo kwenye makutano ya mtaa wa Twiga na Jangwani eneo la Kariakoo.

Baada ya mkataba huo kusainiwa Wanachama na Wapenzi wa klabu hiyo walikuwa na haki ya kuuona Mkataba huo ili kujua yaliyomo kwakuwa ulisharidhiwa kwa matumizi ya wanachama baada ya kusainiwa rasmi.

Mkataba huo ulianza kuonwa na baadhi ya wanachama mbalimbali, likiwemo kundi linalojumuisha washabiki na wanachama wa timu ya Yanga almaarufu *(VIVA YOUNG INTERNATIONAL).*

Kundi hili kama yalivyo makundi mengine mengi linapatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Whatssapp.

Baada ya kujitokeza kwa maoni mbalimbali dhidi ya mkataba huu kundi hili mnamo *28/05/2017* (siku ishirini na moja baada ya kusainiwa kwa mkataba) liliona ni busara kuteua wajumbe kumi na nne (14) ili wapitie mkataba huo na baadaye kuleta mapendekezo kwa kundi zima ili kurahisisha majadiliano.

*2. KAMATI ILIYOTEULIWA:*
Kamati iliyoteuliwa ilijumuisha wajumbe wafuatao;
1. Aaron Nyanda – Dar es Salaam
2. Angu Shadrack - Njombe
3. Deo Mutta – Dar es Salaam
4. Dr. Jonas Tibohora – Dar es Salaam
5. Herman Ngurukizi - Moshi
6. Mohamed Bhinda – Dar es Salaam
7. Maximilian Luhanga – Dar es Salaam
8. Mickness Mahela - Misungwi
9. Omary Kimossa– Dar es Salaam
10. Patricia Mateja – Dar es Salaam
11. Ray Kigosi – Dar es Salaam
12. Said Mrisho – Dar es Salaam
13. Saguda George – Dar es Salaam
14. Samwel Korosso – Dar es Salaam

*3. MAJUKUMU YA KAMATI ILIYOTEULIWA (HADIDU ZA REJEA)*
Kamati iliyoteuliwa na wanakundi ilikasimiwa majukumu yafuatayo;

a) Kuusoma mkataba kwa kina,

b) Kutoa maoni na mapendekezo,

c) Kuwasilisha maoni na mapendekezo yao kwa wanakundi ndani ya siku tano.

Baada ya kuwasilisha maoni na mapendekezo kwa wanakundi, jukumu litabakia kwa wanakundi kuona ni njia gani nzuri ya kuwasilisha maoni hayo baada ya majadiliano mengine na wanakundi kabla ya kuyawasilisha kwa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga kwa hatua zaidi. ,

*4. MPANGO KAZI WA KAMATI ILIYOTEULIWA*
Wajumbe wa kamati walikubaliana kupitia Mkataba huu na kujadiliana online ili kupunguza gharama za kukutana kwakuwa wajumbe wanatoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Wajumbe walikubaliana kuwa watapitia mkataba Ukurasa kwa ukurasa hivyo waliugawanya mara nne kwa vipengele kama ifuatavyo;
a) Jumapili Tarehe 28/05/2017 Kipengele namba 1-5 (Clauses);

b) Jumatatu Tarehe 29/05/2017 Kipengele namba 6 - 8 (Clauses);

c) Jumanne Tarehe 30/05/2017 Kipengele namba 9 -13 (Clauses);

d) Jumatano Tarehe 31/05/2017 Kipengele namba 14 -16 (Clauses); pamoja na viambatisho 1-2 (Schedues);

e) Alhamis Tarehe 01/06/2017 Kuwasilisha taarifa kwa wanakundi kwa ajili ya mapitiio na majadiliano.

Wajumbe walikuwa wanapitia mkataba kila mmoja kwa wakati wake na kufanya majadiliano online kila siku kuanzia saa tatu usiku hadi saa tano usiku kwa siku zote *(09:00 PM - 11:30 PM).*

*5. MAPITIO YA KIFUNGU KWA KIFUNGU;*

*5.1 Jumapili Tarehe 28/05/2017 Kipengele namba 1-5 (Clauses);*

Ukurasa wa kwanza (Page.1) wa mkataba kati ya Klabu ya Yanga na SportsPesa aya ya pili (Paragraph ya pili) - Hakuna anwani ya Posta wala anwani ya eneo la Klabu ya Yanga mahali ilipo. (No Postal address neither Physical address for the Club). Hii ni hatari sana kwakuwa kisheria hapa SportsPesa kaingia Mkataba na mtu asiye na anwani.

Kamati imeona kuwa huu ni ukosefu wa umakini huenda kutokana na uharaka wa waingia mkataba ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Wajumbe wamependekeza kuwepo kwa anwani hizo ili kurahisisha ufahamu wa waingia mkataba (The Postal and Physical address should be included for clarity).

Kipengele namba mbili (Clause no. 2) Kwenye maana ya Klabu,

Kamatu ilionyesha wasiwasi wa mkataba kuhusisha hadi timu ya vijana chini ya umri wa miaka ishirini (Under 20) kwakuwa wengine wanakuwa wako chini ya miaka kumi na nane (below 18 yrs) hivyo kuwahusisha na uchezaji wa kamali ni jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.

Kipengele namba tatu (Clause 3) Definition; Item d:
Kamati imeomba kupata ufafanuzi juu ya tofauti pana kati ya *SportsPesa Limited* na *SportsPesa Group.*

Timu ya Yanga imeingia Mkataba na Kampuni ya SportsPesa Limited lakini kipengele cha tatu (Clause 3; Item d) kinasema *“SportsPesa Group means SportsPesa Limited and all its subsidiaries”* Sehemu hii inaonyesha kuwa klabu ya Yanga itabanwa mpaka kwenye SportsPesa Group.

Swali ambalo Kamati imejiuliza ni; Je SportsPesa Group itakuwa na makampuni mangapi?

Klabu ya Yanga itanufaika vipi na upana huo wa Makampuni ya SportsPesa? Hapa ina maana (The economies of scale ya SportsPesa). Kamati ilienda mbali zaidi kwa kujiuliza kwa mfano Bakhresa Group ina makampuni zaidi ya kumi (10), sasa unapoingia mkataba na Bakhresa Food Products halafu unaambiwa utawajibika pia kwa Azam Marine inawezekanaje?

Kamati imependekeza Sportspesa awe wazi (Specific) ili hapo baadaye SportsPesa ikiwa na makampuni mengine isije ikaifanya klabu ya Yanga kutumika hovyo kwa kampuni nyingi kwa ada ile ile ya milioni mia tisa hamsini.

Aidha kwa upande wa klabu ya Yanga inaonekana Sportspesa imeingia mkataba na *Young Africans Sports Club* lakini ukiangalia kipengele cha pili (Clause No. 2) haiko wazi, nainukuu *"The club is Sports Club that participates in domestic and overseas international competitions and includes a Men's first team football squad, associate U20 and other development teams under the "Yanga" name"*

Hata hivyo Kamati ilihoji pia kuwa; Kwa kuwa mkataba ulisainiwa kabla ya ligi kuisha na kukubaliana kuwa Mkataba unaanza maramoja (immediately) baada ya kusainiwa na kwakuwa wakati wa kukabidhiwa ubingwa mjini Mwanza kwenye mapokezi ya timu Jijini Dar es salaam Mapokezi yalihusisha matangazo ya SportsPesa. Kwa mnasaba huo basi ipo haja ya Klabu ya Yanga kupewa milioni mia moja (100milion) ya ubingwa na SportsPesa.

*ANGALIZO*
Klabu ya Yanga iwe makini sana kwasababu neno *Group* linaweza kuwa na mambo mengine zadi ya shughuli za kucheza Kamali (gaming activities).

Hapa Yanga inapaswa kuwa macho kwenye matangazo (promotions).
Ukurasa wa Pili wa Mkataba (Page 2). Ukurasa wa Pili item 1; schedule 3; hakuna appended club logo Hivyo inashauriwa iwekwe.

Kipengele namba 4.1 (Clause 4.1) ambacho kinaonyesha kuanza kwa mkataba (commencement of the contract) ni lazima pia sponsor aonyeshe tarehe au muda wa kuanza kufanya malipo.

Aidha Sponsor anawajibika kutoa pesa in advance itakayoiwezesha klabu isajili kwa wakati ili baadaye mdhamini anufaike na hao wachezaji.

Mapungufu yaliyopo ni kuwa malipo ya Sponsor ya robo yapo wazi na hayajazingatia mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili (free and pegged to time without considering the registration calendar).

Suala kubwa hapa ni kuwa Sponsor lazima ajue uhalisia wa soko la mpira. Kushindwa kusaidia hilo kutapelekea kusajili mabaki ya wachezaji ambao hawatamsaidia kwenye malengo yake ya kibiashara *(Marketing and Promotions)* aliyoikusudia.

Usajili wa Yanga unahitaji asilimia 50% ya pesa iliyokubalika kati ya Yanga na Sportspesa kwa msimu.

Wanakamati walikubaliana kuwa Sportspesa atoe 1/3 ya hitajio ili kumudu gharama za uhamisho wa wachezaji (facility to support players' transfers).

Ukurasa wa pili (Page 2 item w); - Image Rights – Klabu na wachezaji wa Yanga lazima wahusike katika kunufaika, la sivyo mikataba ya wachezaji na timu ya Yanga lazima iandaliwe upya ili kuendana na mahitaji ya Sportspesa. (The player’s contract with the club should be formatted to suit SportsPesa demand). Bila marekebisho au mapitio haya muhimu mzigo wote utabakia kwa klabu ya Yanga hivyo hili siyo sahihi.

Ukurasa wa tatu wa Mkataba (Page 3) – Hapa hakukuwa na lolote lililojitokeza kuwa na kasoro.

Ukurasa wa nne wa Mkataba (Page 4) kipengele cha 4.2 (Clause 4.2). Nanukuu kipengele husika “SportsPesa will however have the first option to renew the Sponsorship of the club at the expiration of the terms agreed herein). Hapa wajumbe wa Kamati waliona ni bonge la mtego; Yaani ndani ya miaka mitano (5 Years) mkataba uhuishwe kwa makubaliano yaleyale (renewed on the same terms). Hii haikubaliki hata kidogo.

Mapendekezo ya Kamati kwenye kipengele hiki ni kipengele kufanyiwa maboresho na kusomeka kama ifuatavyo; *“SportsPesa will however renew the sponsorship as expiration of the terms to mutually agreed later on separate arrangement”*

Kipengele cha tano (clause 5) hapa ndiyo kwenye msingi mkuu wa maboresho ya mkataba huu (this is the cornerstone of contract amendments).

Kipengele cha 5.3 (clause 5.3). Vipindi vya malipo visiwe kwenye vipindi vilivyopendekezwa (Payment Installment should not be quarterly) bali iwe kwenye mtiririko wa pembe tatu (pyramid shape) kama vile 0.4, 0.3, 0.15, nk.

Wajumbe wa Kamati walienda mbali zaidi na kushauri kuwa si jambo zuri kabisa kuchukua pesa hiyo kwa mtindo uliokubalika kimkataba kati ya Sportspesa na Klabu ya Yanga kwasababu uendeshaji wa timu upo zaidi kwenye mishahara, gharama za kambi, gharama za safari, pamoja na posho na bonasi za wachezaji. *it is even worthless to take this money in quarters because the management of the team is based on salaries, travel and allowances/bonuses*.

Hitimsho la mjadala likapendekeza kuwa malipo yafanyike kwa kila mwezi (monthly) kwa kuwa mfano halisi (Reference) ni wakati wa Mkataba kati ya timu ya Yanga na TBL.

Kipengele cha 5.6.2; (Clause 5.6.2). Bonus ni ndogo sana kuliko wigo mpana (coverage) watakayopata Sportspesa. Kwa mnasaba huo wajumbe walipendekeza marekebisho ya kina hapa yafanyike haraka sana.

Kipengele cha 5.8; (clause 5.8); Kipegele hiki kinahusu Sportpesa kughalimia mkutano mkuu (AGM) kwa milioni ishirini. Wajumbe waliona haina shida wala mashaka kwakuwa kama kutakuwa na maboresho ya kimkataba basi kipengele hiki kitabadilika pia.

*5.2 Jumatatu Tarehe 29/05/2017*
Kipengele namba 6-8 Clauses;
Ukurasa wa tano wa mkataba (Page 5) – (Clause 6 “The Club's Obligation/ Right Of Sportpesa)
Kipengele namba 6.1.1 (Clause 6.1.1) - Wajumbe wameshauri kuwa ni vizuri neno “at the discretion of Sportpesa" liondoke ili kupunguza nguvu ya sponsor kuipangia klabu kwenye kila jambo.

Kipengele namba 6.1.6.2 (Clause 6.1.6.2) Asilimia 70% branding ya eneo (space) kwenye mechi ni kubwa sana kulingana na hela ndogo anayotoa sponsor. Hapa wajumbe walipendekeza sponsor apewe angalu 50% tu.

Kipengele namba 6.1.2 (Clause 6.1.2) - Hiki Kipengele kirekebishwe ili klabu iwe na kazi ya kuwezesha kupatikana kwa mchezaji. Kama mchezaji huyo ana mkataba unaohitaji kulipwa (responsibility to compensate players) iwe kwa Sportpesa kulingana na mahitaji yao kwa tukio la aina hiyo.

Kipengele namba 6.1.3.3 (Clause 6.1.3.3) - Kipengele hiki kina mtego sana; wajumbe walishauri kisomeke Kama ifuatavyo *"With respect to the rights in using club players' sound and image (still and motion) for promoting and marketing purposes, the club will engage SportPesa to mutual agreement on terms of which club and player will be benefited"*
Hapa lazima kuwe na makubaliano tofauti.

Kipengele namba 6.1.6.2 (Clause 6.1.6.2) - Hapa asilimia 70% iliyokubalika kimkataba ni kubwa sana kiasi kwamba hata kama klabu inapata sponsors wengine haiwezi kutumia asilimia 30% tu iliyobakia.

Hivyo basi wajumbe wameshauri asilimia hizi zishuke hadi 50% inayoleta uwiano katika win win situation.

Kipengele namba 6.1.17 (Clause 6.1.17) - Hii ya kutumia wachezaji mara mbili kwa mwaka katika mashindano wanayoandaa Sportpesa ni tatizo. Kuwatumia wachezaji zaidi kutasababisha kuwachosha sana (body fatigue) kwakuwa ukizingatia kipengele namba 3; f kwenye definition kinachosema " *Player means every member of the club's first team squad from time to time during the term* Ina Maana kwenye mashindano hayo watatumika wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Kipengele namba 6.1.2 (Clause 6.1.2) Wajumbe wameshauri kuwa mikataba ya klabu na wachezaji msimu huu viongozi wawe makini kwenye kipengele hiki la sivyo klabu itawalipa fidia wachezaji kwa ushiriki wao kwenye mashindano ya ziada ya sportpesa promotions and marketing.

*ANGALIZO*
Kila kipengele chenye neno Group kifanyiwe marekebisho na kusomeka Sportspesa Limited.

Ukurasa wa 5 (page 5) kipengele kidogo cha 6.1.3 (sub clause 6.1.3) - Gharama za mchezaji kusafirishwa kwenda kwenye matukio ya Sportpesa hazijagusa chakula, afya, gharama za safari na bima anapokuwa kwenye matukio hayo.

Wajumbe walihoji kuwa je wajibu huu niwa nani kati ya Sportspesa na Yanga?. Mfano ni kwamba je mchezaji akipatwa na matatizo ambayo moja kwa moja yamesababishwa na ushiriki wake nani atayabeba?.

Wajumbe walishauri kuwa vipengele hivi virekebishwe ili kutoa nafasi kwa sponsors wengine kuingia kwakuwa vipengele vilivyopo vinaonyesha wazi kuwa hakutakuwa na sponsor atakayevutiwa pindi akipata fursa ya kuona huu mkataba hususan eneo hili.

*USHAURI WA JUMLA WA KAMATI KWENYE KIPENGELE CHOTE CHA SITA*
Uamuzi wa jumla kwenye kipengele namba sita pamoja na vipengele vyote vidogo kwa ujumla ni kuwa: inashauriwa vijadiliwe upya ili viwe na tija kwa waingia mkataba wote

Wajumbe wote walijiridhisha kuwa matatizo mengi hasa yaliyopo kwene kipengele namba sita (Clause 6) pamoja na vinginevyo yanaletwa na asili (aina) ya mkataba wenyewe *"Sponsorship and Marketing Agreement Between Young Africans Sports Club and SportsPesa LTD".*

Maneno haya ambayo yapo kwenye mkataba huu naya nukuu *“Sponsorship and Marketing Agreement”* mwisho wa kunukuu, yanaleta maana pana sana kwenye lugha za kimkataba.

Lengo la Sportspesa kwenye mkataba huu moja kwa moja ni kuitumia Yanga kwenye matangazo na ndiyo maana Sportspesa ameweka masharti magumu katika kuwatumia wachezaji bila ya win win situation.

Wakati wa mapitio Ilionekana wazi kuwa huenda mijadala ya mkataba wa Sportspesa na Yanga imetokana na tathmini zisizo rasmi za kuendesha timu kwa mwaka ama kwa kutokujua, au kwa makusudi au kwa ukosefu wa weledi kwasababu matumizi ya timu ya Yanga hayalingani kabisa na kilichokubalika kimkataba.

Kwa muktadha huo wajumbe wamejiridhisha kuwa ufinyu wa malipo ya mkataba (milioni 950) kati ya Sportspesa na Yanga umesababishwa na tathmini isiyo rasmi na kukosa weledi kutoka kwa waliofanya tathmini hiyo.

Yanga imepewa majukumu mengi ndani ya mkataba huu kiasi kwamba, nafasi ya kumpata mdhamini mwingine inakuwa finyu kwa kuwa mdhamini (Sponsor) mwenye interest atakosa sehemu ya kujitangaza maana Sportspesa ameenda mbali sana hadi kwenye mazoezi na vifaa vyake.

Wakati wa mapitio wajumbe walikubaliana kuwa klabu kama Yanga inahitaji kubwa zaidi ya alichoahidi Sportspesa kwa vigezo vifuatavo vya kitafiti;
a) Kiasi anacho toa Sportspesa kwa kuangalia millage aliyojipa ni kidogo sana hivyo mapitio ni lazima yafanyike.

b). Kwa kiasi kikubwa Sportspesa amewafunga Sponsors wengine wakubwa kuingia kwakuwa amebana maeneo yote muhimu kwa gharama isiyolingana na alichoahidi.

c). SportsPesa amejimilikisha zaidi ya asilimia 80% kwa millage anayo itaka, hili halikubaliki hata kidogo,

d). Kuanzia branding na kwenye mambo yote ya Yanga anachukua takriban asilimia 70%, sasa akija sponsor mwingine atafaidika na lipi?

e). Ni haki kabisa kwa Sportspesa kuonekana kwa zaidi ya asilimia 30% ambapo kwa kawaida branding hupewa 35%-40% kwa 100% ya udhamini kwenye masuala kama vile press conference.

Kilichoonekana baada ya kulibaini hili ni kuwa yote haya pamoja na vifungu vyote kwenye mkataba huu kuonekana kumpa millage kubwa sana Sportspesa.

Wajumbe wanaamini kuwa SportsPesa alipaswa kutoa udhamini wa Zaidi ya asilimia 75% kwa Klabu ya Yanga kwenye jumla ya bajeti yote.

Japokuwa kipengele namba 8.1 kinatoa mwanya wa kuongeza Sponsors kwakuwa Sportspesa ndiye mdhamini mkubwa (exclusive Sponsor) na anaruhusu Yanga kuwa na wabia wengine (partners) ili mradi tu wasiwe wachezesha Kamali. Lakini pia hata huyo asiyechezesha kamali lazima ruhusa itoke kwa Sportspesa.

Kipengele cha 7 (Clause 7) - *None Disclosure and Confidentiality* Hapa hakuna tatizo lolote.

Ukurasa wa kumi wa Mkataba (Page 10) - Clause 8 – Non Exclusivity
Kipengele namba 8.3 (Clause 8.3) kisomeke “The club must notify Sportpesa to the right of any additional sponsors prior to signing any such agreement " Hapa wajumbe wameondoa maneno “Club must consult Sportpesa to discuss"

*5.3 Jumanne Tarehe 30/05/2017*
Kipengele namba 9-13 Clauses (9-13)
Wajumbe pia walishauri kiongezwe kifungu cha kumbana sponsor kila wiki yenye mechi kuwepo na ten spots za tangazo la mechi kwenye media zinazokubalika.

Kipengele cha 10.1.1 (Clause 10.1.1) hapa hakuna shida bali ni kusisitiza kipengele namba 10.1.2 (Clauze 10:1.2) kuondolewa kabisa.

Kipengele namba 9 (Clause 9) hakikuwa na kitu chochote cha kufanyia marekebisho.

Vipengele namba 10.1, 10.1.1 Na 10.1.2. Vipengele hivi havina shida kwa klabu ya Yanga.

Vipengele namba 10.1.3 na 10.1.4 inabidi vifutwe kwakuwa havina masilahi kwa klabu ya Yanga.

Kipengele namba 10.2.1 mahali penye neno Sportpesa liwekwe neno club.

Wajumbe wametoa angalizo kuwa; moja kati ya vitu muhimu vya kuangalia ni matumizi ya Nembo ya Klabu ya Yanga (Club Logo).

Kama Sportpesa Group wana maduka, wanaweza kuchapisha fulana pamoja na vifaa vya mbalimbali kwa kutumia nembo ya Yanga kwa nia njema (in a good will) na kusambaza jezi za Yanga kwa kuziuza na Yanga isifaidike na mauzo hayo.

Wajumbe wameomba kupata ufafanuzi wa neno Good will kama lilivotumika kwene mkataba huu. Aidha Wajumbe wameenda mbali zaidi kwa kushauri kuwa mkataba huu unadilishwe jina na kuitwa; *“SPONSORSHIP AGREEMENT BETWEEN YOUNG AFRICAN AND SPORTPESA LIMITED”* na siyo
*“SPONSORSHIP AND MARKETING AGREEMENT BETWEEN YOUNG AFRICAN AND SPORTPESA LIMITED*.

Udodosi wa kina umeonyesha kuwa waingia mkataba wameshindwa kuwa wazi katika matumizi ya jina kwenye mkataba na kuonekana kama Yanga inashirikiana na makampuni matatu ambayo yameonekana kujirudia mara kwa mara kwenye mkataba kama ifuatavyo;
1) Sportpesa Limited,
2).Sportpesa Group na
3). Sportpesa.

Wajumbe wametoa angalizo5 la kutoruhusu mkanganyiko huu kwenye mkataba huu.

Kipengele namba 10.1.2 cha mkataba kinazungumzia matumizi ya nembo ya Yanga. Nembo hii kwa kifungu hiki inaweza kutumika kwenye branding activities japo wajumbe wamejiuliza kuwa kwa aina za biashara anazozifanya Sportspesa ambayo ni kamali hawana uhakika kama sportspesa anaweza fanya biashara kwa kutumia logo ya klabu kwa kupitia mkataba huu.

Ushauri wa Kamati hapa ni Klabu ya Yanga kukubaliana kwa uwazi kwenye eneo hili kama tahadhali tu.

Kipengele namba 10. 1. 4 (Clause 10.1.4). Wajumbe wamependekeza kifutwe mara moja kwakuwa hakina maslahi kwa klabu ya Yanga.

Eneo hili linaweza kusababisha utumiaji wa nembo ya Klabu bila malipo yoyote. (Logo in loyalty without charge). Matumizi ya aina hii ndiyo tafsiri ya neno kukopesha au Kukodisha.

Kipengele namba 11.2 (Clause 11.2), Wajumbe walihoji kwenye neno claim kipengele namba 11.2 ambacho kinatoa siku kumi na tano (15 days). Je zinatosha kwa klabu kuweza kufanya maamuzi?

Hapa wajumbe walihoji iwapo hiyo claim itahitaji approval ya Mkutano Mkuu (AGM). Aidha wajumbe walienda mbali zaidi kwa kuhoji Katiba ya Yanga inasemaje kuhusu ajenda za Mkutano Mkuu (AGM) huwa zinatolewa muda gani kabla ya kikao?

Kutokana na utata huo wajumbe waliomba kupata ufafanuzi sahihi wa neno Claim lililotumika.

Je maana sahihi ya claim kwenye mkataba huu ni nini? Kwasababu neno claim lina maana nyingi kama zilivofafanuliwa hapa;

*Verb* - State or assert that something is the case, typically without providing evidence or proof.

*Noun* - an assertion of the truth of something, typically one that is disputed or in doubt.

A demand or request for something considered one's due.

Au maana ya claim inaweza kuwa Cost, Time, Bonus, Penalty, Interest and Compensation.

Vipengele namba 13.1 na 13.3 (Clauses 13.1 & 13.3) viondolewe kabisa.

Kipengele namba 14 - Matokeo baada ya pande mbili za Mkataba kuvunja/ kusitisha mkataba kwa ujumla wake hayana tatizo kwa maana mkataba ukivunjika undugu umeisha kila mtu anachukua chake.

Kipendele namba 14.2.6 Sportspesa amejielezea upande wake tu kuwa anaweza kuvunja mkataba wakati wowote bila kutoa sababu ili mradi atoe notisi ya siku arobaini na tano. Swali walilojiuliza Wajumbe je Yanga kwanini hawezi kuvunja mkataba kwa vigezo hivyohivyo?

Vipengele namba 15 na 16 vipo mara mbili na kila kimoja kina maana tofauti hivyo wajumbe wameshauri virekebishwe.

Kipengele namba 15 (Clause 15) - *DISPUTES and LAW AND JURISDICTION* Hiki hakina shida.

Kipengele namna 16 Clause 16) - *NOTICE* Hiki hakina shida pia.

Tatizo hapa lipo kwenye - *GENERAL PROVISIONS* Eneo hili ndiyo mahali pekee ambapo Yanga inaweza kuukataa huu mkataba kwakuwa pana upuuzi mwingi kwenye mkataba huu.

Mwisho kabisa kwenye SCHEDULE 1 na DRAFT HEADS OF TERMS vyote viandaliwe upya Maana vinatafsiri uozo mwingi unaokataliwa ndani ya mkataba huu.

Hapa ndipo kwenye chimbuko la mambo mapya yasiyo na masilahi kwa Klabu ya Yanga mfano Sponsor kupewa tiketi kadhaa kwenye mchezo zisizoendana na uhalisia.

*USHAURI*

1. Wachezaji wa Under 20 wasivalishwe Jazz za Sports Pesa kwakuwa kufanya hivyo kunakiuka haki za watoto kwa kuwafanya watangaze kamali wakati Sheria hairuhusu.

2. Sports Pesa watoe pesa ya Jazz na siyo kutengeneza Jazz. Jazz zisimamiwe na Club ili kutoruhusu Logo kutumiwa Tofauti.

3. Spotspesa wawe na mipaka ya kuweka Matangazo yao kwa kuwa specific. Siyo kuilazimisha Club kuweka Matangazo yao kwenye kila ligi.. Mfano kombe la Azam, Kombe la Kitu kingine chochote. Maana yake hapa ni kwamba waseme wao kwa pesa hiyo kiduchu wanadhamini club kwa ligi ipi.

4. Mechi za away Sportspesa wawekewe mipaka kwakuwa wametaja home ground kwenye mkataba hivyo wasiruhusiwe kuweka matangazo kwenye viwanja nje ya hivyo.

*HITIMISHO LA UJUMLA*

*(1)* Wana Yanga tujenge Umoja, Mshikamano na Ushirikiano wetu kwa kufanyika Ushawishi wa hali na mali ili Mwenyekiti arudishwe kundini na iwekwe mikakati ya kuzuia mpasuko au mgogoro wa aina yoyote katika kipindi hiki cha mpito.

*(2)* Mkataba ufanyiwe marekebisho haraka sana iwezekanavyo mara baada ya vikao vya mashauriano ya pande mbili.

*(3)*. Viambatanisho vya Exclusive Rights na Draft Heads of Terms vifutwe vyote kwa ujumla wake na vitajadiliwa upya baada ya marekebisho ya mkataba.

*(4)* Katiba ya Yanga ifanyiwe marekebisho kwa kuweka Kamati ya ushauri wa mikataba itakayojumuisha wataalam wa biashara, masoko, sheria na mikataba pamoja na wawakilishi wa matawi n.k

*(5)* Iandiwe ratiba ya muda wa utekelezaji wa mapendekezo yote,

*MWISHO KABISA*
TAMKO LA KAMATI - Tuna imani kubwa na viongozi wetu, tunawashukuru kwa kuweza kumpata mdhamini waliyeingia naye mkataba. Tunaamini wataheshimu muda ambao umetumika bila malipo kupitia mkataba huu kwa manufaa ya Yanga.

Kwa mnasaba huo tunaamini kuwa watafanya mapitio mapema sana ili kuinusuru Klabu ya Yanga yenye wapenzi wengi ndani nan je ya Tanzania.

Aidha kuchelewa au kutofanya mapitio kutatuwezesha kuwasilisha maoni yenu kwenye vyombo vya Habari ili wanayanga wengi waweze kujua mapungufu ya mkataba ili iwasaidie kuelewa zaidi mkataba ambao ni haki yao kuujua.

*YANGA KWANZA MTU BAADAYE*
 
Dah!
Cha kwanza, hadi viongozi wanakubali kusaini huo mkataba ni kweli walijiridhisha na vipengele vyote?
Kama ni kweli hao viongozi awastahili.

Sababu ukiangalia mdhamini amejiangalia yeye kwenye kila kitu, mfano pale timu ikipata mdhamini mwingine wa kuongezeka ni hadi SportPesa ikubali.

Wawe makini na huo mkataba ingali bado mapema
 
22d9a5fa549c7ab920151d61bb75ce5f.jpg
Na samaki mfuge kujiongezea kipato
 
Back
Top Bottom