Nyota Mtibwa Sugar: Bila kumpa pesa Mexime hupewi nafasi ya kucheza

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,161
24,109
tnw7cc


Mchezaji ambaye amecheza timu ya Taifa wa miaka 12 mfululizo huku akichezea klabu moja tu maishani na kubeba majukumu ya unahodha klabuni na timu ya Taifa anaweza kushindwa kuwa kocha bora mwenye mafanikio endapo tuhuma za kuomba pesa kwa wachezaji ili awapange katika mechi zitafika mbali na kuainika ni za kweli.


Kila kitu kina madhara Fulani kwa kitu kingine, mathalani ' Nondo ni mharibu wa vitambaa au nguo za manyoya, na Kutu hula chuma kigumu bila shida yo yote'. Kuna wakati akili zetu wanadamu huwa kamili na wakati mwingine huwa si nzima-huwa leguvu kwa kujiendesha. Hivyo basi, ' Sumu ya Mtu ni Kijicho na Chuki' Chuki ina madhara na kijicho kina aibu kubwa kuliko kitu chochote ambacho si halali kwa fikra au kwa tendo la kushawishi mtu kula kitu hicho hata kama kina ' ladha' nyingi kinywani.


Kiungo mshambulizi wa Mtibwa Sugar ( Jina linahifadhiwa kwa sasa) amesema kuwa kuvurunda kwa timu hiyo msimu huu ni sababu ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Mexime. Mchezaji huyo anayejiandaa kuachana na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu ameweka wazi kuwa Mecky ( mchezaji –nahodha wa zamani wa timu hiyo na timu ya Taifa, Taifa Stars) amekuwa akiwapanga timu yake kwa sababu zisizo za kimpira- Kifupi ni lazima umpatie pesa ili upate nafasi ya kucheza Mtibwa Sugar.


" Tatizo la Mtibwa ni kocha ( Mecky), ukitoa sababu nyingine, mwalimu huyo amekuwa akipanga timu yake kama mchezaji utampatia pesa" anasema mchezaji huyo alijiunga na Mtibwa mwaka 2011 wakati timu hiyo ikinolewa na Mkenya, Tom Olaba. Kwanza niseme wazi kuwa Mecky ni mchezaji wa zamani ambaye Taifa linamchukulia kama mfano wa kuigwa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa wakati alipokuwa mchezaji wa Stars kwa miaka 12 mfululizo.


Nyakati za mwisho za uchezaji wake, Mecky alijiingiza katika mafunzo ya ukocha huku akiichezea klabu yake ya Mtibwa na mara baada ya kustaafu soka la ushindani miaka mitatu iliyopita Mecky alipewa kazi ya ukocha msaidizi katika klabu hiyo aliyoichezea kwa maisha yake yote na kushinda mara mbili ubingwa wa ligi kuu, 1999 na 2000.

Wakati akiwa msaidizi wa Olaba, Mecky alisimamishwa na uongozi wa klabu hiyo baada ya kundi kubwa la wachezaji kwenda kwa utawala wa juu na kulalamikia kitendo cha Mecky kuwashawishi wachezaji kucheza chini ya kiwango ili timu ifanye vibaya na kocha mkuu Olaba aonekane hafai.


Mecky alihitaji haraka nafasi ya ukocha mkuu pale Mtibwa Sugar, akiamini kuwa uzoefu na mbinu za ufundishaji alizowahi kupata kutoka kwa walimi John Simkoko, Mshindo Msolla, Burkard Pape, James Siang'a, Salum Mayanga, Olaba, Marcio Maximo, Jan Poulsen zingeweza kumpatia mafanikio ya haraka.

Mtibwa ilimuajiri Mecky kama kocha mkuu mara baada ya kumalizika kwa mkataba wa Olaba msimu wa 2011/12 na timu hiyo iliporomoka hadi nafasi ya Tano ikimaliza nyuma ya Simba SC waliotwaa ubingwa, Azam FC waliomaliza nafasi ya pili na Yanga SC na Kagera Sugar ambazo zilikamilisha orodha ya timu nne za juu.



Yalikuwa ni matokeo mabaya zaidi kwa Mtibwa katika kipindi cha ' Muongo Mmoja' lakini imani kwa Mecky ilikuwa kubwa kwa kuwa aliingia klabuni na mtazamo wa kuijenga upya Mtibwa ikitumia zaidi wachezaji vijana kutoka timu ya pili na si kusajili wachezaji wengi wanaotemwa katika klabu za Yanga na Simba.

Lakini mpango kama huo unahitaji muda zaidi, bila shaka klabu na Mecky mwenyewe walikuwa wakitambua hilo ndiyo maana wameendelea kufanya kazi pamoja licha ya timu hiyo kuporomoka hadi nafasi ya Tisa msimu uliopita.


" Ili kocha akupe namba ni lazima umpe kocha pesa, hafanyi kwangu tu ni wachezaji wengi wanakutana na hali hiyo" anaendelea kusema mchezaji huyo ambaye alifanya vizuri mno msimu uliopita licha ya timu kumaliza katika nafasi mbaya tangu ilipopanda daraja mwaka 1997.

Mtibwa itacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga Jumatano hii wapo nafasi ya nane katika msimamo baada ya kucheza michezo 18 na kukusanya alama 23 ilianza vizuri msimu huu na kuongoza ligi kwa miezi mitatu mfululizo lakini wamefanikiwa kushinda mara moja tu tangu kuanza kwa mwaka huu na sababu kubwa wachezaji wanasema ni Mecky. Naendelea kumtafuta mwalimu huyo na chochote atakachosema nitawajuza.

Chanzo: ShaffihDauda Blog

 
Hata kama ni kwenye blog, uandishi wa namna hii umepitiliza ukanjanja. Hakupaswa kuleta habari bila kupata maoni ya Maxime kwanza. Akiandika maoni hayo baadaye kuna wengine kwa sababu moja au nyingine hawatayaona lakini watabaki na picha ya upande mmoja kuhusu Maxime. Hii ni character assination.
 
Hata kama ni kwenye blog, uandishi wa namna hii umepitiliza ukanjanja. Hakupaswa kuleta habari bila kupata maoni ya Maxime kwanza. Akiandika maoni hayo baadaye kuna wengine kwa sababu moja au nyingine hawatayaona lakini watabaki na picha ya upande mmoja kuhusu Maxime. Hii ni character assination.

Yani fb alikopost hii nmemchana live huu ni ukanjanja wa waziwazi.
Sasa naungana na uzi wa balumbe aliosema shafii ni mropokaji.
 
Last edited by a moderator:
Lakini lisemwalo.....lipo,kwa soka la kibongo linawezekana kabisa..,AU mmesahau Mansour Magram alikuwa anawanyia nini wachezaji?,Kibadeni jee?...
 
Tujiulize swali la hali halisi ya Timu zetu.... Hawa wachezaji wanalipwa kiasi gani hadi wapate na za kumhonga kocha????????? Mpira wa Tanzania umejaa majungu na wachezaji wa maji mara moja yaani mwaka huu anavuma na mwaka unaofuata anakuwa gharasha ambalo halistahili hata kuwekwa benchi. Huyu mchezaji ni wazi anaweza kuwa anaugulia maumivu ya kutochezeshwa kutokana na kushuka kiwango..... Napata shaka na shafii kuitoa hii taarifa maana amezidi udaku na kujidai analijua soka la bongo.
 
Mpira wetu umepitia katika vipindi tofauti kama mdau alivyotoa mfano wa magram kiukweli kuna mambo mengi kocha anataka sio kuheshimiwa bali kunyenyekewa na kuengwaengwa. Kama mpo safari basi mkiingia hotel bill una clear wewe yaani kama ni safari ya mwezi inakuta Kocha hajawahi jinunulia chakula sasa akikuona hujipendezi kwako ndo beef kama hizo. But ni mapema kumuhukumu mexime.
 
Mpira wetu umepitia katika vipindi tofauti kama mdau alivyotoa mfano wa magram kiukweli kuna mambo mengi kocha anataka sio kuheshimiwa bali kunyenyekewa na kuengwaengwa. Kama mpo safari basi mkiingia hotel bill una clear wewe yaani kama ni safari ya mwezi inakuta Kocha hajawahi jinunulia chakula sasa akikuona hujipendezi kwako ndo beef kama hizo. But ni mapema kumuhukumu mexime.

kwani timu inaposafiri kila mtu anajigharamia kivyake? namaanisha chakula, maji etc? ufafanuzi tafadhali
 
Miaka hiyo nayokueleza system ilikuwa hiyo mnaweza kupewa posho ya wiki coz sidhani kama mnakuwa kama watoto wa primary mnaingia hotel kisha mwalimu anawalipia na sina uhakika kama mfumo utakuwa umebadilika sana.
 
ndio maana kwa upande mwingine naunga mkono mswada wa serikali kuwadhibiti watu kama hawa nilitegemea angeleta taarifa ambayo iko balance kumbe kasikiliza upande mmoja huu ndio mtindo wa waandishi wengi wa sasa wananchukua maelezo ya upande mmoja halafu wakimfata mwingine akikanusha pia wanaandika
 
Hao wachezaji wanaoitwa Nyota ndio wanajifanya maFaza wa Team, waambie waache uvivu wafanye mazoezi sasa hivi Damu changa zinakimbiza. Maxime anajua mpira waache fitna.
 
Back
Top Bottom