Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,259
Binafsi siamini katika kuungaunga. Hii inatokea sana kwa watu wanaosoma masomo ya arts, tofauti na wewe kwamba hupendi ualimu; wengine wanaunga kwa kuwa wako incompetent na hawawezi wakashindana katika ulimwengu wa ajira. Kwao kuunga wanadhani inawaongezea nafasi ya ajira na pia maslahi, lakini kumbe sivyo. Ukirudi utamkuta mtu mwenye degree moja ambaye ana experience kiasi kwamba hata mkienda interview watamchukua yeye, wewe wanakubwaga.
Limekuwa ni tatizo kwa watanzania kusoma vitu ambavyo hawavipendi kwa kuwa tu wanaona kuna scholarship au sponsorship. Wengine wanaenda kusoma course ambazo hawezi hata kuja kuzitumia au hazipendi ila tu kwa sababu tu labda inafanyika Ulaya au Marekani. Huu ni ujinga.
Sasa mkuu sikuelewi kwamba umepoteza miaka mitatu kwa ajili ya kitu usichokitaka, na bado wataka kupoteza mwaka hadi miaka miwili kwa kitu usichokijua. Ukitegemea ushauri wetu utaishia kusoma kitu ambacho hukipendi hata kama kina maslahi mazuri, maana ualimu pia una maslahi mazuri kwa baadhi ya waajiri ukilinganisha na profession nyingine. Ungeenda kazini ungejua sehemu gani ina soko zuri, hii ingekusaidia kufanya maamuzi sahihi ya degree ya pili.
Lakini pia nachelea kuhisi wewe wafikiria kuajiriwa tu. Hizo mentality zife kwa sasa. Usisome kwa sababu unataka ajira fulani, soma kwa ajili ya kutaka ya kupata mwanga wa kukusaidia kitu fulani katika maisha. Kafanye kazi bwana, kazi yoyote uipendayo; hata huo ualimu. Shule zipo tu, na kozi mpya zaibuka kila siku. Hujazaliwa ushinde kusoma darasani, kuna masomo makubwa yanapatikana mtaani.