Nimemaliza Degree ya Ualimu nataka niunge, je ni kozi gani nzuri niombe?

Binafsi siamini katika kuungaunga. Hii inatokea sana kwa watu wanaosoma masomo ya arts, tofauti na wewe kwamba hupendi ualimu; wengine wanaunga kwa kuwa wako incompetent na hawawezi wakashindana katika ulimwengu wa ajira. Kwao kuunga wanadhani inawaongezea nafasi ya ajira na pia maslahi, lakini kumbe sivyo. Ukirudi utamkuta mtu mwenye degree moja ambaye ana experience kiasi kwamba hata mkienda interview watamchukua yeye, wewe wanakubwaga.
Limekuwa ni tatizo kwa watanzania kusoma vitu ambavyo hawavipendi kwa kuwa tu wanaona kuna scholarship au sponsorship. Wengine wanaenda kusoma course ambazo hawezi hata kuja kuzitumia au hazipendi ila tu kwa sababu tu labda inafanyika Ulaya au Marekani. Huu ni ujinga.
Sasa mkuu sikuelewi kwamba umepoteza miaka mitatu kwa ajili ya kitu usichokitaka, na bado wataka kupoteza mwaka hadi miaka miwili kwa kitu usichokijua. Ukitegemea ushauri wetu utaishia kusoma kitu ambacho hukipendi hata kama kina maslahi mazuri, maana ualimu pia una maslahi mazuri kwa baadhi ya waajiri ukilinganisha na profession nyingine. Ungeenda kazini ungejua sehemu gani ina soko zuri, hii ingekusaidia kufanya maamuzi sahihi ya degree ya pili.
Lakini pia nachelea kuhisi wewe wafikiria kuajiriwa tu. Hizo mentality zife kwa sasa. Usisome kwa sababu unataka ajira fulani, soma kwa ajili ya kutaka ya kupata mwanga wa kukusaidia kitu fulani katika maisha. Kafanye kazi bwana, kazi yoyote uipendayo; hata huo ualimu. Shule zipo tu, na kozi mpya zaibuka kila siku. Hujazaliwa ushinde kusoma darasani, kuna masomo makubwa yanapatikana mtaani.
 
Cha msingi mkuu kapige kazi kwanza kama miaka 2 hivi kwani hata mie nataka kufanya hivyo as long as nasubiria post
 
Kama Ulienda Ed. Kwa ajili ya Kupata Mkopo,manake Ada ya kusoma Degree nyingine Haukua nayo!
Sasa Unataka Ushauriwe Masterz nzuri yenye Mkopo Au!Manake Masterz siyo Bure!
Kafanye Kazi acha Mawenge!
 
Mm ni mwl nimemalza mliman last year.kaka kama umepata chanel ya kusoma nenda kasome,achana kbsa na mawazo ya kwenda kufanya kazi.ualim ni kibarua.c kaz.ukishaanza kushika chake kuna hatar ya kupoteza kabisa mwelekeo wako wa maisha.jaman hakuna kazi isiyo na maslah kama ualim,yani utaish maisha ya umaskini na manyanyaso.mshahara wa sasa wa mwl ni 469600.hii ni basic,wakikata unabak na laki 3 na upuuz hv.soma kwanza,kaz ipo 2 kaka.
Usikilize moyo wako,unataka uwe nani?au huna vision?pia angalia dunia/tanzania inahtaj wataalam gan sokon then decide wht to study.
 
Jamani wana jimvi nimemaliza shahada ya ualimu ila nataka kuunga ila kwa kubadilisha course kwasababu sikuwa na wito wa kufundisha ila niliingia ualimu kwa madhumuni ya kupata mkopo na sikitu kingine.sasa jamani niombe course gani nzuri kwa ajili ya masterz.nawakilisha.

Kwa hiyo mpaka unamaliza 1st degree haujui ndoto zako ni kuwa nani?Hakuna profession of your dream?Unataka watu wakuchagulie profession.Kazi kwelikweli!
 
Kama ulisoma education ili upate mkopo, umejipanga vp kwa hiyo master, au unafikiri nako utapata mkopo. Kumbuka bodi inakudai sasa. Kapige kazi kwanza acha bwebwe.
 
Jamani wana jimvi nimemaliza shahada ya ualimu ila nataka kuunga ila kwa kubadilisha course kwasababu sikuwa na wito wa kufundisha ila niliingia ualimu kwa madhumuni ya kupata mkopo na sikitu kingine.sasa jamani niombe course gani nzuri kwa ajili ya masterz.nawakilisha.

Hayo ni maneno ya kashfa kubwa, ambayo mtu kama wewe ulitakiwa usiseme hadharani. Tatizo kubwa la TZ ni Waalimu, hatuna walimu, wewe unakuja unasema eti umekwenda shule just kwa njia ya uwalimu ili umpate mkopo? hii ni shame. Shame on YOU.

Kumbe UFISADI upo kila kona.
 
Mm ni mwl nimemalza mliman last year.kaka kama umepata chanel ya kusoma nenda kasome,achana kbsa na mawazo ya kwenda kufanya kazi.ualim ni kibarua.c kaz.ukishaanza kushika chake kuna hatar ya kupoteza kabisa mwelekeo wako wa maisha.jaman hakuna kazi isiyo na maslah kama ualim,yani utaish maisha ya umaskini na manyanyaso.mshahara wa sasa wa mwl ni 469600.hii ni basic,wakikata unabak na laki 3 na upuuz hv.soma kwanza,kaz ipo 2 kaka.
Usikilize moyo wako,unataka uwe nani?au huna vision?pia angalia dunia/tanzania inahtaj wataalam gan sokon then decide wht to study.

Kwa ushauri kama huu nchi hii haitokaa ikaendelea kamwe! siamini unaweza toa ushauri kama huu, kumbuka huyu mtu amepewa mkopo unaotokana na kodi zetu ili apate elimu ya kuwafundisha watoto wetu. kila siku tunalalamika ukosefu wa walimu huko shule za kata wewe leo hii unakuja kutoa ushauri kama huu. Oldonyo nenda kafundishe kwanza, shule zipo tu. Habari ya maslahi ni muhimu lakini kama kila mara serikali inaposomesha walimu halafu wanakuwa na mawazo kama yako ya kutopenda kufundisha na ukujumlisha na watu wanaotoa ushauri kama huu ahpo juu, ni lini maslahi hayo yataboreshwa! maana kila siku kutakuwa na upungufu so serikali itawekeza zaidi katika kuzipa pengo hilo. mazee nenda kapige kazi utusaidie kuziba pengo ili serikali sasa ielekeze nguvu katika kuboresha maslahi yenu walimu!
 
kozi uliyosomea ni kimeo ndugu yangu, bora urudi shule tena ukasomee hotel managemant, ila ni bora tungejua jinsia yako maana kama ni dada ni bora ukasomee ubamedi nao unalipa kinoma.
 
Mwaya jifunze ujasiriamali ndugu utafurahia maisha yako kama ndegewa angani hizo ajira za msiahara baada ya miezi 3 laana jiajiri ujilipe mwenyewe kama mzee aliacha vile vigari ama vibanda ingia banki komaa nao usije filisiwa kama patco
 
we jamaa mi nakujua,cha msingi kama umepata sponsor nenda kasome ila kama huna nenda kazini ucje teseka na master ya kupiga lampad.vipi mduma na manyanda wapo?,kitima na dk safari? Dk elikioni je?
 
Jamani jamani hivi kweli mtu ambaye amesoma mpaka kapata dgr anatamka madudu kama haya kuwa coz ya ualimu ni kimeo basi huyu bila shaka ameikomboa elimu na elimu haija mkomboa kabisa.Afute kauri kwanza na awe na mtazamo chanya kuhusu ualimu.
 
Kilembwe!ndugu yng co kwamba mm c mzalendo,la hasha! Nilichomshauri yeye ni kwenda kusoma,kazi ipo tu,hata akirud akitaka kushika chaki na ashike,kwani kakatazwa?
Kama kuna tatizo la walim je serikal imefanya jitihada gani kuhakikisha kua inaboresha maslah ya walim?tofaut ya nyongeza ya mshahara wa walim wa shule ya msingi ya mwaka jana na mwaka huu ni TSH 200.sasa huu c utani na manyanyaso ya serikal kwa walim hawa?kama serikal yenyewe imekosa uzalendo kwa kutowajal wataalam wake,je sisi wataalam tutaupata wapi uzalendo?acha majibu ya siasa,be realistic,ualim si wito ni kazi.iweje daktar wa digrii 1 alipwe laki 8,wakati mwalim mwenye digrii 1 alipwe laki 4.huu ni usaliti na una wanyanyasa walim,kwani hufanya baadhi ya taaluma ni muhimu kuliko nyingine.kumbuka daktari,mhandisi,mwanasiasa,wote hao wamefundishwa na mwalimu. TEACHERS MAKES ALL PROFESSIONS POSSIBLE.lazma wapewe umuhimu unaostahili.
 
fanya kazi kwanza upate experiens kama upo BAED halafu soma masters ya public administration..FAIDA yake ni kuwa zinauhusiano ni rahisi hata kufanya utafiti ni rahisi kupata kazi kama program officer afisa utumishi na nafasi za utawala katika masuala ya elimu na jamii serikarini na sekta binafsi.Hata mimi nina mpango huo afta 2 yrs

Wengi huamini hivyo, lakini napenda nikushauri Mkuu kwamba hiyo sio kweli. Mimi nimesoma HRM na nipo katika field hiyo kwa muda wa miaka minne sasa. Nimefanya kazi Serikali Kuu na sasa nipo katika agency mojawapo za serikali. Mitazamo hiyo huwapotosha wengi na hivyo kujikuta wanaonekana kuwa hawana good professional background katika HRM. Kinachoweza kumpa mtu kazi ni First degree, na hivyo masters ni added advantage tu baada ya kuwa na first degree.
 
we jamaa mi nakujua,cha msingi kama umepata sponsor nenda kasome ila kama huna nenda kazini ucje teseka na master ya kupiga lampad.vipi mduma na manyanda wapo?,kitima na dk safari? Dk elikioni je?
<br />
<br />
kaka wote wapo wazima wa afya
 
kaka naomba tubadilishane mimi nikupe vyeti vyangu vyote,yaani cheti changu cha kuzaliwa,cheti changu cha form four, cheti changu cha form six na cheti changu cha degree, mimi nimesomea uchumi wa maendeleo ya jamii BACHELOR OF ARTS IN COMMUNITY ECONOMIC DEVELOPMENT(BA-CED),Napenda sana kuwa mwalimu,kama utakuwa tayari ni pm.
 
Back
Top Bottom