Yani...unajua kabisa muda wako wa kusalimia umeisha maongezi ya wakubwa yanaanza!
Dah!!Kwakwl me nikikumbuka yaliyonitokea shule ya msingi enzi hizo huwa nacheka halafu nahuzunika . nakumbuka wkt niko darasa la nne,siku moja nilienda shule nkasahau kuvaa chupi.sasa nikawa nacheza rede wakati wa breki nje ya ofisi nikajimwaga niwezavyo bila kujua km sina kufuli .mwalimu akaona vitu akanipeleka nyumbani na kumsubiria mama kumpasha.aisee housegirl ilibakia kidogo ale mkong'oto siku hiyo. jambo jingine nakumbuka wakati bado niko msingi,nilikuwa naharibu sana viatu na mabegi .wakati niko darasa la 5,zikaingia raba kali ziliitwa 'victoria a.k.a Lakuchumpa'(vilitoka baada ya ajali ya mv bukoba).ukiwa nazo wkt huo kwnu mambo safi.basi nilivililia vile viatu baba akaelewa somo akaninunulia pamoja na begi jipya.ndani ya mwezi nikaharibu vyote vikawa kama takataka.mama akakasirika akanisema sana.kesho yake akaniletea begi la turubai na njumu.yaan nilikuwa nachekwa mstarini kila siku mpaka nkaanza kuona shule chungu.
Nakumbuka tulikuwa tunasoma na Vince kwao walifuga sungura waliokuwa na uwezo wa kucheza karata,basi Vince alikuwa na marafiki wengi kwa kuwa kwao kulikuwa kama zoo ya kwenda kucheki wanyama japo walikuwepo sungura tu........
Nakumbuka siku moja Vince alinidanganya tukaenda nyuma ya nyumba akaniambia vua sketi yako,ile naanza vua,mama yake akatokea,Vince akakimbia,mama yake akanipeleke home,nlipofika tu mama yangu akanivua chupi.....sijui ili aone nini????
Vince alipigwa sana lakini bado akawa anaendelea na tabia yake,na vile kwao walikuwa wana sungura wacheza karata na nilipenda kuwaona nilikuwa nakubali tu kuvua........lol
:laugh:..nimecheka sana mpaka wenzangu ofisin wananiuliza vipi mbona unachekelea screen ya computer...unavituko sana ww. ngoja :coffee: be right back with full memory
:coffee:Jamani wewe Lizzy Maembe mabichi unaweka kwenye uji,Hiyo ladha inakuwaje mpenzi ,kweli utoto mzuri sana
no mawazo no anything kila kitu tambarare ,
Mie nakumbuka nilipokuwa darasa la tatu tuko group la watoto tuliiba maembe kwenye shamba la watu,Mwenye maembe akatukamata kipigo tulichopata ni cha mbwa mwizi
Kurudi home tukadanganya wazazi tumepigwa kuna mtu katusingizia tumeiba mahindi yake namkumbuka rafiki yangu JJ maskini sijui yuko wapi sasa , wazazi wakamfata huyo mdingi mida ile ile ,yule mbaba kuwaonyesha lundo la mahindi tulilovunja shambani kwake ,tulipewa adhabu ya kumwagilia matofali ya shule kwa muda wa week nzima ,
na kulima matuta na kupanda viazi.
Hivi hawa watu naona kama walituonea adhabu ilikuwa kubwa kupita umri wetu kwa kipindi hicho.??
Bado nakumbuka niko darasa la nne nikavunja mkono kisa ilikuwa saa nne ile mida ya break kengere imegonga tu tukakimbilia kwenye miti ya mizambalawe nikateleza nikaanguka mie ,LOL:A S 20:
Nakumbuka kuficha Compass ya Mdada Jirani yangu, Kushtuka mwalimu akaingia, akashitaki kuibiwa Compass yake, Nikajua kuwa nimepatikana, Mwalimu akaruhusu tusachiwe darasa zima na kwa kuwa hakukuwa na mtu aliyetoka nje, Nilipata Hofu sana, lakini hawakuiona hiyo kitu japo nilikuwa natfanya utani lakini nilishindwa kuirudisha. Guess nilificha wapi??? Kwenye mkono wa Jaketi, Nikaukunja kisha nikatundika Jaketi langu kwenye kiti chake, Hakulisachi ndio ikawa salama yangu.
Tulikuwa tunatembea kilometa ishirini kuifuata shule, mahindi ya kukaanga katika chupa iliyo na maji ili kuyalainisha na sometimes tunapikiwa ugali alfajiri.
Sisi kuwe na wageni, halafu ujikalishe sebuleni, kuna jicho mumy atakukata utainuka mwenyewe, nakupotea.