Nimekumbuka zamani!!

Sisi kuwe na wageni, halafu ujikalishe sebuleni, kuna jicho mumy atakukata utainuka mwenyewe, nakupotea.
Yani...unajua kabisa muda wako wa kusalimia umeisha maongezi ya wakubwa yanaanza!
 
Kwakwl me nikikumbuka yaliyonitokea shule ya msingi enzi hizo huwa nacheka halafu nahuzunika . nakumbuka wkt niko darasa la nne,siku moja nilienda shule nkasahau kuvaa chupi.sasa nikawa nacheza rede wakati wa breki nje ya ofisi nikajimwaga niwezavyo bila kujua km sina kufuli .mwalimu akaona vitu akanipeleka nyumbani na kumsubiria mama kumpasha.aisee housegirl ilibakia kidogo ale mkong'oto siku hiyo. jambo jingine nakumbuka wakati bado niko msingi,nilikuwa naharibu sana viatu na mabegi .wakati niko darasa la 5,zikaingia raba kali ziliitwa 'victoria a.k.a Lakuchumpa'(vilitoka baada ya ajali ya mv bukoba).ukiwa nazo wkt huo kwnu mambo safi.basi nilivililia vile viatu baba akaelewa somo akaninunulia pamoja na begi jipya.ndani ya mwezi nikaharibu vyote vikawa kama takataka.mama akakasirika akanisema sana.kesho yake akaniletea begi la turubai na njumu.yaan nilikuwa nachekwa mstarini kila siku mpaka nkaanza kuona shule chungu.
 
Hahahaha Festi Ledi umenifurahisha!Uliweka mambo hadharani aisee!!Hapo kwenye kuharibu viatu wengi sana tumepitia!Unakuta unavikanyagia mpaka kile cha nyuma kinataka kukatika!Alafu kulikua kuna kuvaa mabuti siku za mvua ila nilikua sipendi kwahiyo mi nlikua navaa viatu tena na soksi nyeupe baada ya kukatazwa kuvaa kwa ajili ya matope!Natoka kimya kimya kimya alafu naaga nikifika barabarani!Wakati wa narudi zile soksi hazifai kwa tope...nikazivua nikazitupilia mbali!
 
:coffee:Jamani wewe Lizzy Maembe mabichi unaweka kwenye uji,Hiyo ladha inakuwaje mpenzi ,kweli utoto mzuri sana
no mawazo no anything kila kitu tambarare ,
Mie nakumbuka nilipokuwa darasa la tatu tuko group la watoto tuliiba mahindi kwenye shamba la watu,Mwenye mahindi akatukamata kipigo tulichopata ni cha mbwa mwizi
Kurudi home tukadanganya wazazi tumepigwa kuna mtu katusingizia tumeiba mahindi yake namkumbuka rafiki yangu JJ maskini sijui yuko wapi sasa , wazazi wakamfata huyo mdingi mida ile ile ,yule mbaba kuwaonyesha lundo la mahindi tulilovunja shambani kwake ,tulipewa adhabu ya kumwagilia matofali ya shule kwa muda wa week nzima ,
na kulima matuta na kupanda viazi.
Hivi hawa watu naona kama walituonea adhabu ilikuwa kubwa kupita umri wetu kwa kipindi hicho.??
Bado nakumbuka niko darasa la nne nikavunja mkono kisa ilikuwa saa nne ile mida ya break kengere imegonga tu tukakimbilia kwenye miti ya mizambalawe nikateleza nikaanguka mie ,LOL:A S 20:
 
Kwakwl me nikikumbuka yaliyonitokea shule ya msingi enzi hizo huwa nacheka halafu nahuzunika . nakumbuka wkt niko darasa la nne,siku moja nilienda shule nkasahau kuvaa chupi.sasa nikawa nacheza rede wakati wa breki nje ya ofisi nikajimwaga niwezavyo bila kujua km sina kufuli .mwalimu akaona vitu akanipeleka nyumbani na kumsubiria mama kumpasha.aisee housegirl ilibakia kidogo ale mkong'oto siku hiyo. jambo jingine nakumbuka wakati bado niko msingi,nilikuwa naharibu sana viatu na mabegi .wakati niko darasa la 5,zikaingia raba kali ziliitwa 'victoria a.k.a Lakuchumpa'(vilitoka baada ya ajali ya mv bukoba).ukiwa nazo wkt huo kwnu mambo safi.basi nilivililia vile viatu baba akaelewa somo akaninunulia pamoja na begi jipya.ndani ya mwezi nikaharibu vyote vikawa kama takataka.mama akakasirika akanisema sana.kesho yake akaniletea begi la turubai na njumu.yaan nilikuwa nachekwa mstarini kila siku mpaka nkaanza kuona shule chungu.
Dah!!
 
Duh.............. Thx for nice Memories!!
Nakumbuka std 5 Kulikuwa na Mwalimu wa hesabu alikuwa anaogopwa kwa fimbo zake akiingia tu anapiga mkwara kwa kusema waliopata chine ya 50% mtajamba cheche!! basi kuna siku alimpiga Mwanafunzi mmoja yule dent si akajifanya amezimia then teacher akiwa na uoga kidogo wa kufikiri kamzimisha dent akajikakamua na kusema "My God... Aliyezimia huwa ananyanyua mkono wa kushoto" dent aliyejifanya kazimia akanyosha kweli bwana, Teache alimpa stick za Chapchap jamaa kuona vile akatoka nduki.... utoto bwana!!! week iliyofuata alinicharaza bakora hadi nikavimba mkono nilichofanya ni kumwekea upupu kwenye dawati, siku hiyo alikaa dakika 10 tu darasani coz dakika zote zilizofuata alikuwa anajikuna, hadi akaomba ruksa kwa mwalimu mkuu ili aende home kuoga!!!!! very funny lakini those where the days!!!
 
Tulikuwa tunatembea kilometa ishirini kuifuata shule, mahindi ya kukaanga katika chupa iliyo na maji ili kuyalainisha na sometimes tunapikiwa ugali alfajiri.
 
Nakumbuka kuficha Compass ya Mdada Jirani yangu, Kushtuka mwalimu akaingia, akashitaki kuibiwa Compass yake, Nikajua kuwa nimepatikana, Mwalimu akaruhusu tusachiwe darasa zima na kwa kuwa hakukuwa na mtu aliyetoka nje, Nilipata Hofu sana, lakini hawakuiona hiyo kitu japo nilikuwa natfanya utani lakini nilishindwa kuirudisha. Guess nilificha wapi??? Kwenye mkono wa Jaketi, Nikaukunja kisha nikatundika Jaketi langu kwenye kiti chake, Hakulisachi ndio ikawa salama yangu.
 
:laugh:..nimecheka sana mpaka wenzangu ofisin wananiuliza vipi mbona unachekelea screen ya computer...unavituko sana ww. ngoja :coffee: be right back with full memory

Nakumbuka tulikuwa tunasoma na Vince kwao walifuga sungura waliokuwa na uwezo wa kucheza karata,basi Vince alikuwa na marafiki wengi kwa kuwa kwao kulikuwa kama zoo ya kwenda kucheki wanyama japo walikuwepo sungura tu........

Nakumbuka siku moja Vince alinidanganya tukaenda nyuma ya nyumba akaniambia vua sketi yako,ile naanza vua,mama yake akatokea,Vince akakimbia,mama yake akanipeleke home,nlipofika tu mama yangu akanivua chupi.....sijui ili aone nini????
Vince alipigwa sana lakini bado akawa anaendelea na tabia yake,na vile kwao walikuwa wana sungura wacheza karata na nilipenda kuwaona nilikuwa nakubali tu kuvua........lol
 
:laugh:..nimecheka sana mpaka wenzangu ofisin wananiuliza vipi mbona unachekelea screen ya computer...unavituko sana ww. ngoja :coffee: be right back with full memory

ha ha ha ah,usitake kusema yale mengine,la sivyo nami ntasema ulivyokuwa hujui......lol:msela:
 
:coffee:Jamani wewe Lizzy Maembe mabichi unaweka kwenye uji,Hiyo ladha inakuwaje mpenzi ,kweli utoto mzuri sana
no mawazo no anything kila kitu tambarare ,
Mie nakumbuka nilipokuwa darasa la tatu tuko group la watoto tuliiba maembe kwenye shamba la watu,Mwenye maembe akatukamata kipigo tulichopata ni cha mbwa mwizi
Kurudi home tukadanganya wazazi tumepigwa kuna mtu katusingizia tumeiba mahindi yake namkumbuka rafiki yangu JJ maskini sijui yuko wapi sasa , wazazi wakamfata huyo mdingi mida ile ile ,yule mbaba kuwaonyesha lundo la mahindi tulilovunja shambani kwake ,tulipewa adhabu ya kumwagilia matofali ya shule kwa muda wa week nzima ,
na kulima matuta na kupanda viazi.
Hivi hawa watu naona kama walituonea adhabu ilikuwa kubwa kupita umri wetu kwa kipindi hicho.??
Bado nakumbuka niko darasa la nne nikavunja mkono kisa ilikuwa saa nne ile mida ya break kengere imegonga tu tukakimbilia kwenye miti ya mizambalawe nikateleza nikaanguka mie ,LOL:A S 20:

Hahahhahaha....mama wa kwanza we acha tu...huo utamu wake ni balaa!!Unakua mchachu kwa mbalii....alafu kila ukichota na kipande cha embe basi ule utamu/uchachu unachanganyika na uji!!Raha tupu!!!Bila kusahau kusahau karanga za kukaanga...nazo zilikua zinanogesha kweli uji!!!

Hahahahhaha....yani mlitaka kumgeuzia mwenye mali kibao???Mi nakumbuka nimewahi kuiba maembe sana ila sikuwahi kukamatwa....nikishaokota mawili matatu nakimbia zangu shule....sasa kuna wale wengine mpaka yawalemee wabebe na sketi ndo waridhike!!By the time wanakamatwa mimi ni kama sikuwepo.
 
Nakumbuka kuficha Compass ya Mdada Jirani yangu, Kushtuka mwalimu akaingia, akashitaki kuibiwa Compass yake, Nikajua kuwa nimepatikana, Mwalimu akaruhusu tusachiwe darasa zima na kwa kuwa hakukuwa na mtu aliyetoka nje, Nilipata Hofu sana, lakini hawakuiona hiyo kitu japo nilikuwa natfanya utani lakini nilishindwa kuirudisha. Guess nilificha wapi??? Kwenye mkono wa Jaketi, Nikaukunja kisha nikatundika Jaketi langu kwenye kiti chake, Hakulisachi ndio ikawa salama yangu.

Lolzzz....ulijikuta unaiba kwa lazima!!!
 
Tulikuwa tunatembea kilometa ishirini kuifuata shule, mahindi ya kukaanga katika chupa iliyo na maji ili kuyalainisha na sometimes tunapikiwa ugali alfajiri.

Dah noma kweli....hapo mvua haijanyesha!!!Siku hizi sehemu ya kwenda dkk 10..15 wanagombania dalala!!!
Ndo maana zamani watoto hawakua vibonge sana...fikiria huo mwendo na bado hujacheza....yani ni zaidi ya mazoezi!!!
 
Sisi kuwe na wageni, halafu ujikalishe sebuleni, kuna jicho mumy atakukata utainuka mwenyewe, nakupotea.

umenikumbusha mbali sana, wakija wageni ni full kujiachia wakiaga unataman uondokea nao. Hayo majicho hata mumy wangu alikuwa anatukata , ukishaliona fasta unapotea.
 
Nakumbuka kila jumatano nilikuwa siendi shule sababu ya table (orodha) mwl wa hesabu alikuwa hatari hasa table ya 7 na ya 9. Darasa la tano nilikuwa namuuzia mwl vibagia basi navila halafu nasingizia watoro wamekopa, mwl alivyojua nikaacha kwenda shule , bibi akanidunda then akalipa deni. Kuna nyimbo za kuruka kamba kama anayeingia tumfanye wakwanza manu amanuliwe kamba ikikukwama unavutwa juu juu, hadi unachaniwa chupi. Those days bana achaa.
 
Hii thread imenifanya nikumbuke mengi sana enzi za utoto!!
Nakumbuka nilikamatwa na Barua nimemwandikia Monitress nilipokuwa darasa la kwanza.
Nakumbuka nilikuwa nacheza michezo yote ya kike ingawa mimi wa kiume.
Nakumbuka enzi za KOMBOLELA lazima nikajifiche sehemu 1 na mrembo inapita michezo 3 hamjaonekana!!
Nakumbuka.............................!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom