Nimejiridhisha kwamba CCM imekita mizizi, kama vyama vya kikomunist vya China na Korea Kaskazini

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,607
Hii ni baada ya kuzunguka kwenye taasisi kubwa za kielimu hapa nchini na kubaini kwamba asilimia kubwa ya hawa tunawaita wasomi wa ngazi za juu ni wana CCM kindakindaki na bado wana imani kubwa na dola iliyopo.

Ukitembea kwa walala hoi mikoa mbali mbali, huwaambii kitu kuhusu CCM.

Ukija kwenye hivi vinajiita vyama vya upinzani ukivichambua haswaaa na ukavichimba, unakuja kuona kwamba ni wale wale tu CCM. Maana wanatembea mule mule kwenye njia za CCM.

Yaani hivi vinajiita vyama vya upinzani wanachogombea ni viti vya ubunge wapate ruzuku maisha yaende, ukichunguza sana bado unaona hamna chama cha upinzani ambacho kipo tayari kuunda serikali.

Na hiki ni chama ambacho kimetawala nchi miaka inaenda sitini sasa.

Hujapita kwenye taasisi za ulinzi na uasalama, nako huko kumejaa wenye mapenzi na CCM kindaki ndaki.

Ndo mana nasema, CCM imejichimbia mizizi kama chama cha kikomunisti cha China. Wamewezaje kufanya hivo, sijui.

Ila ifike mahala sasa wananchi, tuwaombe CCM wawe wanatuletea viongozi wenye akili, na kama ikibidi hata system ihusike, kuhakikisha taifa linapata viongozi wenye akili ya ku drive growth ya nchi.

Iwe kama tu chama cha kikomunisti cha China, system inahakikisha nchi inatawaliwa na watu wenye bongo na sio hawa utopolo ambao wanatembelea brand ya CCM kwa kujua kwamba itatawala milele.

I wish mpinzani ninayemkubali mimi 'Tundu Antiphas Lissu' angekuwa tu ni mwana CCM, maana nimegundua huko upinzani ni watu wachumia tumbo tu na watu hopeless.

Najua ntapokea matusi yote, lakini najaribu kuwa realistic, huwezi kupambana kwenye hakuna.

N.Mushi
 
Sio kweli, mbona mwendazake aliipangua na kuweka watu waka na sera zake kama alivyotaka
 
Lakini mwendazake si CCM huyo huyo? Hapo tofauti ni kwamba ndani ya CCM kutakuwa na itikadi tofauti... ila chama ni hicho hicho kimoja.

Yaani ni kama kubadilisha imamu ila msikiti ni ule ule
 
Hata kama wana imanj na ccm lkn maisha ,ukosefu wa ajira unawanyoosha sana , mpk akili zinawakaa
 
Njaaaa.

Kuabudu pesa na madaraka kwa watu ndio kunakotumiwa na CCM kudhoofisha watu.

Mbinu pekee wanatotumia CCM ni kula na kila mtu yeyote wanayemuona ana ushawishi kwenye jamii. Kuanzia Vyama vya siasa ( Ruzuku na Teuzi ), vyama vya wafanyakazi, viongozi wa dini, wasomi wakufunzi vyuoni, wasanii, vikosi vya ulinzi, Vyama vya wakulima, chama Cha wamachinga.

Na Rais wa CCM anafanya teuzi zaidi ya asilimia 90. Na hata zile ambazo siyo teuzi bado ana ushawishi kwa 90%.

Biblia inasema, palipo na Mzoga ndipo wakusanyikapo TAI, maana pale panaponuka msosi ndipo wanapojaa watu.

Nakuhakikishia hata Sasa hivi iingie madarakani CHAUMA, zaidi ya 90% ya wanaojifanya CCM watahamia CHAUMA.

In short, Hakuna chama kinachopigania watu. Watu ni Daraja tu kufikia mambo yao.

Ili watu mfaidike binafsi naamini mpaka kusiwepo na chama chenye Monopoly kwenye maamuzi, Basi.
 
Pamoja na kuwa CCM imenikuza, Pamoja na kuwa CCM imeniangusha. Hata siku moja-au Kamwe siwezi kuiita ya Kikomunisti.

Na ukipata mda ...please Define Ukomonisti.

Hiyo ni lugha ya Ukimbari, Ni lugha inayotumika kuwahadaa Vijana wa Ulaya na Magharibi yake.

Haina mshiko tena katika korido za Kimataifa na ni za wale wa Mlengo wa Kulia- Kulia (Far-Right) Yaani wale wanaohusishwa na Ushetani. Msitumezeshe sumu zenu.

Ni Propaganda Hasi.

Utaeleweka.
 
Ukomunisti ndo una tabia ya kukita mizizi kila kona.. kwenye idara zote za elimu, ulinzi, sanaa... nk.

We hujiulizi... wasanii asilimia 98% ni CCM, walimu wa vyuoni, vyombo vya usalama, halafu unasema nisikiiete kwamba ni chama cha kikomunisti?
 
Una ushauri gani kwa vya upinzani.

vifutwe au wafanya nini kushika dola mkuu.
Ushauri wangu ni bora tusiwe na vyama vya upinzani... maana gharama za uchaguzi ni kubwa sana, hizo pesa zingepelekwa kusaidia maendeleo..

Kutumia mabilioni kugharamia uchaguzi ambao mshindi ashapatikana, huo ni ukichaa...
 
Subiri uone mikutano miwili tu ya Hadhara watajuta kuruhusu mikutano ya siasa.

Hapa Tanzania CCM ilishakataliwa.

Acha kuandika hisia.
Hiyo mikutano ineruhusiwa na nani???... tukubali tukatae.. ukiona mpaka mikutano ambayo ipo kisheria inaamuliwa na matakwa ya CCM, wewe mpinzani utasemaje kwamba una ndoto za kuitoa CCM madarakani?

Hiyo mikutano ya kisiasa nanialiizuia? Na nani anairuhusu??..

Nijibu
 
Hii ni baada ya kuzunguka kwenye taasisi kubwa za kielimu hapa nchini na kubaini kwamba asilimia kubwa ya hawa tunawaita wasomi wa ngazi za juu ni wana CCM kindakindaki na bado wana imani kubwa na dola iliyopo.

Ukitembea kwa walala hoi mikoa mbali mbali, huwaambii kitu kuhusu CCM.

Ukija kwenye hivi vinajiita vyama vya upinzani ukivichambua haswaaa na ukavichimba, unakuja kuona kwamba ni wale wale tu CCM. Maana wanatembea mule mule kwenye njia za CCM.

Yaani hivi vinajiita vyama vya upinzani wanachogombea ni viti vya ubunge wapate ruzuku maisha yaende, ukichunguza sana bado unaona hamna chama cha upinzani ambacho kipo tayari kuunda serikali.

Na hiki ni chama ambacho kimetawala nchi miaka inaenda sitini sasa.

Hujapita kwenye taasisi za ulinzi na uasalama, nako huko kumejaa wenye mapenzi na CCM kindaki ndaki.

Ndo mana nasema, CCM imejichimbia mizizi kama chama cha kikomunisti cha China. Wamewezaje kufanya hivo, sijui.

Ila ifike mahala sasa wananchi, tuwaombe CCM wawe wanatuletea viongozi wenye akili, na kama ikibidi hata system ihusike, kuhakikisha taifa linapata viongozi wenye akili ya ku drive growth ya nchi.

Iwe kama tu chama cha kikomunisti cha China, system inahakikisha nchi inatawaliwa na watu wenye bongo na sio hawa utopolo ambao wanatembelea brand ya CCM kwa kujua kwamba itatawala milele.

I wish mpinzani ninayemkubali mimi 'Tundu Antiphas Lissu' angekuwa tu ni mwana CCM, maana nimegundua huko upinzani ni watu wachumia tumbo tu na watu hopeless.

Najua ntapokea matusi yote, lakini najaribu kuwa realistic, huwezi kupambana kwenye hakuna.

N.Mushi
Ccm ni chama kujifichia makucha ya ufisadi ,Kama nadanganya fuatilia wote wajifanyao ccm kindakindaki ,utashangaa
 
Ukomunisti ndo una tabia ya kukita mizizi kila kona.. kwenye idara zote za elimu, ulinzi, sanaa... nk.

We hujiulizi... wasanii asilimia 98% ni CCM, walimu wa vyuoni, vyombo vya usalama, halafu unasema nisikiiete kwamba ni chama cha kikomunisti?
Sawa Mkuu,
Hakika najiuliza Wasanii gani? Manake kudai Wasanii karibu wote 98% naona kuna ukinzani hapo....

Vilevile uwepo wa Wanachama wa CCM katika sekta tofauti za Kiserekali, kwangu sioni kama hiyo hoja inaqualify Kuwaita CCM wakomunisti....

Define Komunisti unavyoelewa basi....

Halafu jibu hili....Au nionyeshe au uniambie ni Nchi gani zaidi ya China ambayo Haina Wanachama katika sekta hizo ulizozitaja

Unataka kusema kuwa hakuna Wanachama wa vyama vingine katika hizo sehemu ulizotaja?
Tuendelee
 
Sahihi kabisa....

Ccm ni mabepari uchwara japo walianzia kwenye ujamaa.
Proved,
Kiuhalisia Muafrika wa enzi ni, na wa sasa bado ni ya Mibepari, tofauti na tulivyo /ambavyo tunahadithiwa.

Ujamaa hauna ushirikiano mahususi wowote na Ukomunisti, ninavyoelewa mimi.

Nakubalina na ulichosema bali naona ni the other way Round.
 
Sawa Mkuu,
Hakika najiuliza Wasanii gani? Manake kudai Wasanii karibu wote 98% naona kuna ukinzani hapo....

Vilevile uwepo wa Wanachama wa CCM katika sekta tofauti za Kiserekali, kwangu sioni kama hiyo hoja inaqualify Kuwaita CCM wakomunisti....

Define Komunisti unavyoelewa basi....

Halafu jibu hili....Au nionyeshe au uniambie ni Nchi gani zaidi ya China ambayo Haina Wanachama katika sekta hizo ulizozitaja

Unataka kusema kuwa hakuna Wanachama wa vyama vingine katika hizo sehemu ulizotaja?
Tuendelee
Kuna kitu tunaita kwa kimombo 'Non-partisan' ni maarufu sana kwenye siasa za magharibu, ikiwa na maana kwenye vyombo kama vya ulinzi na usalama, vinatakiwa viwe na hii principle ya kutoegemea upande mmoja...

Ila ukiwa na vyombo kama hivi vimejipambanua kuwa CCM wazi wazi, hapo ndo nikashindwa kuvitofautisha na vyama vya kikomunist ambavyo vinatawala China na N.Korea.

Achana na habari ya ku define ukomunist kwa sasa, jibu ni kwamba mfumo wa CCM ume adopt muundo wa mifumo ya dola ya nchi za kikomunisti, ambayo kwayo, huwa wanataka kutawala kila kitu kwa ngazi zote..

Nadhani sasa umenielewa
 
Ccm ni chama kujifichia makucha ya ufisadi ,Kama nadanganya fuatilia wote wajifanyao ccm kindakindaki ,utashangaa
Je kujificha makucha kunakufanya uwe Mkomunisti?

Nirudie, lugha hii inayotumiwa kuita Nchi au Chama kuwa ni ya Kikomunisti ni ya kuchagaza, na Propaganda hiyo hasi Inatumika pale wale wamagharibi wanaposhindwa kupenya katika, Siasa na Roho za watu.
Sioni kama ina mshiko Kimataifa kwa sasa. Dunia Imebadilika.

Sikukatazi kuamini hivyo, ila fanya utafiti kidogo ujitosheleze na mawazo mbadala.
 
Hiyo mikutano ineruhusiwa na nani???... tukubali tukatae.. ukiona mpaka mikutano ambayo ipo kisheria inaamuliwa na matakwa ya CCM, wewe mpinzani utasemaje kwamba una ndoto za kuitoa CCM madarakani?

Hiyo mikutano ya kisiasa nanialiizuia? Na nani anairuhusu??..

Nijibu
Hilo swali lako mbona jepesi sana? Sikutegemea kuulizwa na wewe mtalaam
 
Back
Top Bottom