Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,611
Hii ni baada ya kuzunguka kwenye taasisi kubwa za kielimu hapa nchini na kubaini kwamba asilimia kubwa ya hawa tunawaita wasomi wa ngazi za juu ni wana CCM kindakindaki na bado wana imani kubwa na dola iliyopo.
Ukitembea kwa walala hoi mikoa mbali mbali, huwaambii kitu kuhusu CCM.
Ukija kwenye hivi vinajiita vyama vya upinzani ukivichambua haswaaa na ukavichimba, unakuja kuona kwamba ni wale wale tu CCM. Maana wanatembea mule mule kwenye njia za CCM.
Yaani hivi vinajiita vyama vya upinzani wanachogombea ni viti vya ubunge wapate ruzuku maisha yaende, ukichunguza sana bado unaona hamna chama cha upinzani ambacho kipo tayari kuunda serikali.
Na hiki ni chama ambacho kimetawala nchi miaka inaenda sitini sasa.
Hujapita kwenye taasisi za ulinzi na uasalama, nako huko kumejaa wenye mapenzi na CCM kindaki ndaki.
Ndo mana nasema, CCM imejichimbia mizizi kama chama cha kikomunisti cha China. Wamewezaje kufanya hivo, sijui.
Ila ifike mahala sasa wananchi, tuwaombe CCM wawe wanatuletea viongozi wenye akili, na kama ikibidi hata system ihusike, kuhakikisha taifa linapata viongozi wenye akili ya ku drive growth ya nchi.
Iwe kama tu chama cha kikomunisti cha China, system inahakikisha nchi inatawaliwa na watu wenye bongo na sio hawa utopolo ambao wanatembelea brand ya CCM kwa kujua kwamba itatawala milele.
I wish mpinzani ninayemkubali mimi 'Tundu Antiphas Lissu' angekuwa tu ni mwana CCM, maana nimegundua huko upinzani ni watu wachumia tumbo tu na watu hopeless.
Najua ntapokea matusi yote, lakini najaribu kuwa realistic, huwezi kupambana kwenye hakuna.
N.Mushi