Nimeita mmoja wamekuja wanne

Kama una 10,000/= mfukoni unaita binti baa ili iweje? Mapenzi na Mkono wa Birika haviendani - Kama huna pesa acha kusumbua mabinti zetu - Endeleaa na shule na mambo yakishakaa sawa utakuwa na uwezo wa kualika hata Baba na Mama yake binti pale Giraffe weekend moja...
hahahah!!hii yenyewee aseee
 
Usikute huyo aliye mwita ndo anataka awe girlfriend sasa kaja na team nzima kama TP Mazembe.

hahahaa umenivunja mbavu kaka TP MAzembe tena....hahaaa yaani juzi nilipanda na waandishi wa habari wa TP MAzembe kwenye ndege wana makelele mpaka basi
 
Ndio hivo siku hizi mmezidi kukopa kw hiyo na wao wamebuni njia ya kulipwa kabla, hii ikitokea umemkopa hata haimuumi sana, wale ushasema watoto ndio wanavyokuwa siku zote, kwanza ni kuwaonyeshea wenzake anae mtu anaeweza kutumia, maskini bila kujua yule jamaa atawapitia wote mmoja baada ya mwingine
 
Dawa ya nini? kama wamekula wenyewe na wameacha...!! Tatizo lako unajifanya unazo ndo maana wamekuja kukuchuna...!! kwani lazima ulipe? Mbona Kenya hata kama ni Girlfriend wako hatoki ukimtoa out mpaka umwakikishie kua gharama zote juu yako otherwise lazima aje na mshiko wake, tatizo sisi wabongo tunapenda sifa za kijinga halafu tukuja kulalamika.

we utakua mwanachuo na unatabia hizo. huajelewa somo unaanza kupandisha jazba.
mwenzio kamwita mmoj, labda kwa huyo angemudu kila kitu cha gharama yoyte, ila sasa wamekuja wanne na wanaagiza vya bei ya juu na bado hawatumii.

Me kiukweli nawaachia zigo.nalipa gharama za huyo nilomwita na zangu.
 
We **** kweli kama ushalipa unataka ushauri gani tena, ungekuwa hujalipa tungekwambia mlipie uliyemwita, hiyo ndo kufa kisabuni, kama umewalipia wote kweli walikukomoa. Hiyo tafsiri yake kwa wenye akili ni kwamba huyo demu amekufanya ATM ambayo haina namba ya siri. yaani ameshawaambia twendeni tukanywe kuna **** mmoja huwa hana bajeti, anatoa tu. ni dharau ya hali ya juu. Huyo kwa anayempenda haendi hata na rafiki mmoja.

Kama utaendelea na ujinga huo usingae ukaendelea kubaki mpangaji na kwenu huna msaada hata kitenge cha mama. Toka na mmoja tu na kuwa mwangalifu.
 
tatizo mara nyingi tunapenda kuishi maisha ambayo si halisi na jinsi tulivyo.kama unataka kumtoa out,mpe ukweli mapema."sitaki uje na group".tosha.kama atakuja nao,gharama ni za kwao...
 
dawa kaka ndogo, aither walipe wenyewe we mlipie tu uliyemualika tena bila hiyana, au lipia ulivyotumia wewe then waage. Utaona sura zao na itakuwa ni fundisho kwa wote
kwa huku rchugga madent kama hao wanaokula halafu wanasusa wanaachwa wanalipa wenyewe hapo watajifunza kwa wengine kutokana na makosa yao.
 
Kuna hii tabia ya mabinti (hasa wa vyuo) unapomwita mmoja bar wanakuja watatu mpaka watano, halafu wakifika baada ya kuagiza vinywaji vya gharama (Redbull, Savanna, nk) hudai kwamba hawajala, wanaagiza chipsi kuku kila mmoja. Wanakula kiduchu halafu wanaacha eti wameshiba. Hii huwa inanikera sana, nani anaweza kuwa na dawa yake?

dawa yake utakayemuhita mwambie aje ni kinywaji chake na chakula.
 
Kuna hii tabia ya mabinti (hasa wa vyuo) unapomwita mmoja bar wanakuja watatu mpaka watano, halafu wakifika baada ya kuagiza vinywaji vya gharama (Redbull, Savanna, nk) hudai kwamba hawajala, wanaagiza chipsi kuku kila mmoja. Wanakula kiduchu halafu wanaacha eti wameshiba. Hii huwa inanikera sana, nani anaweza kuwa na dawa yake?

Kuna kisa kimoja kilitokea zamani kidogo hoteli ya kilimanjaro, jamaa kampa demu ki-date wakutane kilimanjaro hotel, yule demu kwa akili take akaona aende na wadogo zake watatu. walipofika wakamkuta jamaa kaagiza bia anakunywa nawao wakaagiza wine tena bila kuagiziwa, wakanywa na kula mpaka saa tano hivi, jamaa akaenda kaunta akauliza bili yake akalipa, wale mademu bili yao ilikuwa kama elfu 30,000 vinywaji na chakula. Jamaa akaondoka bila kuaga..

Hiyo ilikuwa miaka ya 90, hawakuonana mpaka majuzi kwenye 2007, kila mtu amekuwa mtu mzima na anafamilia
Kwakifupi kilichowapata wale mademu nikwamba waliosha vyombo mpaka alfajiri

Kwahiyo mzee yakikufika hayo lipia yako na ukipenda ya uliyemwalika kisha ondoka zako
 
Kuna hii tabia ya mabinti (hasa wa vyuo) unapomwita mmoja bar wanakuja watatu mpaka watano, halafu wakifika baada ya kuagiza vinywaji vya gharama (Redbull, Savanna, nk) hudai kwamba hawajala, wanaagiza chipsi kuku kila mmoja. Wanakula kiduchu halafu wanaacha eti wameshiba. Hii huwa inanikera sana, nani anaweza kuwa na dawa yake?

that is bad habit!yameshanitokea but naweza kusema ni ushamba wa maendeleo.
 
Very simple,kumlipia uliyemuita tu au unaona soo itakula kwako mwazo mwisho we waendekeze tu
 
Very simple,kumlipia uliyemuita tu au unaona soo itakula kwako mwazo mwisho we waendekeze tu

Hata uliyemuita hakuna kumlipia kwani hana adabu, mimi toka enzi hizo za ujana wangu, ukinipa kidate halafu bado sijakuzoea au sikuelewi elewi nakupa kabisa taarifa nakuja na rafiki yangu au niko na wenzangu wawili siwezi waacha nikiruhusiwa naenda nae/nao nisiporuhisiwa na mimi sijisikii kwenda peke yangu basi siendi. so hiyo ni tabia mbaya sana lazima uulize kwanza
 
Mzuanda; I did the same back then,tulimfanyia (mcheza mpira mmoja hivi wa yanga,jina kapuni).mi nilienda na wasichana wa class nzima(marafiki zangu na wasiokuwa marafiki zangu pia),nia ilikuwa ni ku mkomoa, mtu mzima ovyo kwenda kunitongoza msichana wa form three.
tulikula na kunywa,uzuri ilikuwa ni soda tu na chipsi maini. then akalipa,tukarudi shule,hajanitafuta tena.demu akikufanyia hivyo ujue hakutaki


Ushamba tu na utoto utakuwa unakusumbua mtu wa hivyo!

YES, maybe ulikuwa utoto coz at that time i was 17 years old,(we are talking about years ago) But i dont regret for what i did, and im proud of it till now.
 
Dawa yake mbona rahisi... Wakifika omba namba za simu kwa kila mmoja, Then anza kutongoza mmojawapo hapohapo (sio huyp uliyemuita). Wengine wapotezee na hata stori usipige nao. Wataboreka, wataondoka, na siku nyingine ukimwita huyo wako atakuja peke yake...
 
we utakua bado unatongoza... anawaleta wenzie kuthaminisha

enzi zangu hapo unajitahidi kuchukua namba za hao wenzie, yani hilo bonge la opportunity sema ndio uzee tayari:ballchain:

Samora10 nimekugongea senki!! Yaani mi ndo naombaga kimoyomoyo aje nao tu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom