EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,093
Ndio nimeamua kuolewa at last……but at my own conditions. Kwa kweli nimechoshwa na masharobaro wa hapa mjini, yaani uwizi mtupu, usanii and too many heart breaks, I have to come to conclusion love is not meant for me.
Niko katika mchakato lakini nataka hii ndoa iwe purely of benefits more or less marriage of convenience. Sitaki kuolewa kwa love cause it doesn't and never worked with me, sitaki kuwa nyumba ndogo, sitaki kuzaa na mume wa mtu, sitaki kuzaa nje ya ndoa, sitaki kulea mume, sitaki kuruka ruka kila siku.
Ninachotaka ni kukidhi matamanio ya mwili, kuendeleza kizazi (tukijaliwa), awe responsible dad to his kids kwasababu sitaki niwe single parent at same wakose mapenzi ya baba yao. Tutasaidiana maisha half half hasa yanayohusu watoto wetu. LOL
Now the challenging part, nataka mawazo yenu, nini nifanye ili hii marriage ionekana attractive kwa mume mtarajiwa. Naomba brainstorming zenu kabla sijaweka bandiko. Maana its like contract and going to be renewable see if we fit, au precaution gani nichukue......
Mtambuzi , Kongosho , Kaunga , The Boss , ndyoko , Preta , Eiyer , King'asti , na Nyani Ngabu na wengineo wote naombeni busara zenu.
MadameX,
Dah hii ngumu, but katika maelezo yako kuna kitu muhimu sana umekiongea "Hutaki kuruka ruka, hutaki watoto walelewe na upande mmoja wa mzazi, kushare matumizi ya watoto" Ambavyo hivi ndivyo nguzo kubwa kabisa katika huo mkataba na huyo utakayeingia naye. Kwa haya uliyoyaeleza hapa nahisi huo mkataba mtakaoingia ili kukidhi vigezo hivi basi utakuwa ni everlasting contract ingawa "Happy or Sad" hiyo haijalishi sana unless baadae mje mreview some of the elements za contract hiyo.
Sasa challenge ipo kwenye mtu ambaye utaingia mkataba naye, unajua when it comes to matamanio ya kimwili ni lazima kweli uwe unamtamani huyo mtu and its not like unaweza kufake matamanio, ukilazimisha kufake matamanio basi yatakuwepo mwanzoni lakini baadae inaweza kufail. So kuwa makini na mtu utakayeingia naye contract.
Ngoja nifikirie mengine ntarudi
Last edited by a moderator: