Nimeamua kuolewa......

Ndio nimeamua kuolewa at last……but at my own conditions. Kwa kweli nimechoshwa na masharobaro wa hapa mjini, yaani uwizi mtupu, usanii and too many heart breaks, I have to come to conclusion love is not meant for me.

Niko katika mchakato lakini nataka hii ndoa iwe purely of benefits more or less marriage of convenience. Sitaki kuolewa kwa love cause it doesn't and never worked with me, sitaki kuwa nyumba ndogo, sitaki kuzaa na mume wa mtu, sitaki kuzaa nje ya ndoa, sitaki kulea mume, sitaki kuruka ruka kila siku.

Ninachotaka ni kukidhi matamanio ya mwili, kuendeleza kizazi (tukijaliwa), awe responsible dad to his kids kwasababu sitaki niwe single parent at same wakose mapenzi ya baba yao. Tutasaidiana maisha half half hasa yanayohusu watoto wetu. LOL

Now the challenging part, nataka mawazo yenu, nini nifanye ili hii marriage ionekana attractive kwa mume mtarajiwa. Naomba brainstorming zenu kabla sijaweka bandiko. Maana its like contract and going to be renewable see if we fit, au precaution gani nichukue......

Mtambuzi , Kongosho , Kaunga , The Boss , ndyoko , Preta , Eiyer , King'asti , na Nyani Ngabu na wengineo wote naombeni busara zenu.

MadameX,
Dah hii ngumu, but katika maelezo yako kuna kitu muhimu sana umekiongea "Hutaki kuruka ruka, hutaki watoto walelewe na upande mmoja wa mzazi, kushare matumizi ya watoto" Ambavyo hivi ndivyo nguzo kubwa kabisa katika huo mkataba na huyo utakayeingia naye. Kwa haya uliyoyaeleza hapa nahisi huo mkataba mtakaoingia ili kukidhi vigezo hivi basi utakuwa ni everlasting contract ingawa "Happy or Sad" hiyo haijalishi sana unless baadae mje mreview some of the elements za contract hiyo.

Sasa challenge ipo kwenye mtu ambaye utaingia mkataba naye, unajua when it comes to matamanio ya kimwili ni lazima kweli uwe unamtamani huyo mtu and its not like unaweza kufake matamanio, ukilazimisha kufake matamanio basi yatakuwepo mwanzoni lakini baadae inaweza kufail. So kuwa makini na mtu utakayeingia naye contract.

Ngoja nifikirie mengine ntarudi
 
Last edited by a moderator:
MadamX hapo kwa hayo masharti labda uzae wako na umfundishe hayo unayotaka kwa ulimwengu huu wa sasa mwanaume wa hivyo HAYUPO!!!!
 
M'Jr , asante kwa ushauri wako, kama ni matamanio ya mwili sina mwili wa kabati kwahiyo nafikiri nina mvuto, my worries ni kuwa kitabia hatutaenda na thats I dont want to make an issue about it, asinibadilishe and I won't do the same, purely business.

Halafu nakusubiri kwa mengineo.
 
Last edited by a moderator:
M'Jr , asante kwa ushauri wako, kama ni matamanio ya mwili sina mwili wa kabati kwahiyo nafikiri nina mvuto, my worries ni kuwa kitabia hatutaenda na thats I dont want to make an issue about it, asinibadilishe and I won't do the same, purely business.

Halafu nakusubiri kwa mengineo.
MadameX,
Nimekusoma lakini i meant matamanio kwako wewe maana nawe lazima uwe umemridhia huyo mtu ili usije ukajilazimisha kuwa na hisia za kuungaunga kwasababu tu huenda umeona mtu huyo ana vigezo baadhi lakini kwenye mvuto kukakosekana.

Wewe sina tatizo na mvuto wako "Najua geji inasoma on top"

Subiri mengine niko kwenye kikao nikimaliza tu nakushushia
 
Last edited by a moderator:
hasara za kuzaa nje uya ndoa kijana alipata mchumba alipomuonyesha baba yake ,baba akamwambia
asimuoe ni ndugu yake ila mamaya ke hajui wa pili hivyohivyo wa tatu hivyo hovyo basi kijana akaamua
kumwambia mamayake mamayake akamwambia amuoe tu yule sio dada yake kwani huyo nae sio baba
yake ila asimwambie kwani hajui pia


Aiseeeee, duniani kuna mambo...........
 
Okay back to topic MadameX,

Katika kutafuta mwenzi wa kuishi naye whether ni for a heart surrender or business as usual au hiyo ya kwako ya purely benefit contract ni lazima uwe na vigezo kama ulivyoviweka hapo kwenye post yako. But kwenye hili huwa kuna challenge ambayo watu wengi huwa wanaiface kwenye swala hili, moja kubwa ni kujikuta wanakuwa dissappointed kwa kujikuta hakuna mtu anayekidhi vigezo vyote hivyo kujikuta ka muda kanakwenda na wanaanza kuwa desperate. Na unajua siku zote desperate time needs desperate measures ambazo huwa sio nzuri sana maana zinakupeleka kwenye whoever comes first.

Hapa ninachosema ni kwamba its good to have your own set qualities of the person you need but pia weka timeframe of the saint you want to appear inapozidi then unareview vigezo ili kuona maybe ni kipi wanachokikosa na namna gani ukiwa na mtu anayekosa kigezo hicho wewe unaweza kukiaccomodate. Binadamu wote tuko tofauti so ndio maana ndoa inaitwa committment ambayo inakutaka wewe u release some of your rights na huyo mwenza afanye vivyo hivyo ili mfikie kwenye compromising point then mnasonga mbele.

Nahisi kwa leo nimekupa maneno ya kutosha kama una la ziada niulize tu....................
 
Last edited by a moderator:
Akitokea mweye mawazo kama yako hakuna shida ndoa yenu yaweza kudumu maana kila mmoja atakuwa anaangalia hizo benefits zaidi. Ila katika hali ya kawaida ndoa bila mapenzi ni kama gunia la chumvi! zito asikuambie mtu! Btw MadameX mbona umenawa ile makeup shosti? Au ndio maandalizi ya kutafuta mchumba? Urembo wa asili kwa sana. Lol!
 
Last edited by a moderator:
Akitokea mweye mawazo kama yako hakuna shida ndoa yenu yaweza kudumu maana kila mmoja atakuwa anaangalia hizo benefits zaidi. Ila katika hali ya kawaida ndoa bila mapenzi ni kama gunia la chumvi! zito asikuambie mtu! Btw MadameX mbona umenawa ile makeup shosti? Au ndio maandalizi ya kutafuta mchumba? Urembo wa asili kwa sana. Lol!


Thanks for the Input MwaJ, imebidi nichange look maana hata mwili pia nimeupunguza.
 
Back
Top Bottom