Nimeamua kuacha kazi ili nijiajiri

Wazo kama wazo ni zuri sana

Tatizo ni sababu ya kuacha kazi na je ukishaacha unakwenda kufanya nn au unahamia ofisi gani?

Kwa sababu ulizosema mfano boss anakubana hilo halipaswi kukuachisha kazi na kwenda mtaani kujiari labda uhamie kampuni nyingine

Lingine ni furaha, katika hili lazima uwe makini kwa sababu unaweza acha kazi ukaenda kujiari ukafikiri utapata furaha lkn kiukweli kujiajiri hasa miaka miwili ya mwanzo ni stress sana hakuna furaha coz itakubidi uwe busy sana ikiwezekana kampani zako za kula bata uzikache kabisa!

All in all kujiajiri ni jambo jema sana, cha msingi wazo hilo litoke moyoni na ujiamini kua utaweza.
 
shaurimbaya jiulize tena kabla ya kusepa, umefika miaka 45?, Umeandaa familia na ndugu zako kuishi kama mfanyabiashara? na mwisho uko tayari ku absorb shock tokana na risk za kibiashara?

Miaka najua kama uko below 45 utakuwa unapenda matumizi kwahiyo lazima uwe na tahadhari zaidi kwa maisha mapya unayoanza.

Pili, Familia za watumishi huwa zinaishi maisha ya juu ya kawaida. Misosi, nguo na matumizi huwa juu maana mzee akipiga bomu anakuja kufidia kwahiyo hawajui kujinyima....unatakiwa kuanza kuwabadilisha kidogokidogo je umefanya hilo ili waikubali hali mpya?

Mwisho, Shetani akikujaribu mil 18 ikapotea yote je uko tayari kusema utaanza upya hata kuuza icecream tena?

Lakini bado nasema uamuzi nu mzuri tu....ukijiajiri utapata mafanikio na nafasi hata ya kushiriki kazi za kijamii zaidi kuliko ukiwa mtumishi ofisi za watu


kuhusu umri nipo 28, nina familia changa, mke na mtoto mmoja.

mke wangu ni mwajiriwa pia. yeye ataendelea na kazi yake aliyonayo.

jukumu la chakula ndan ya nyumba ni la mke wangu. tulishagawana majukumu.

mi nimesave pesa ya kulisha familia for almost a year kama back up. wife akikwama au matatizo yakitokea.

also artwork nina ujuzi mkubwa sana. nilifanya kazi part time kwenye workshop ya t shirt nilivyomaliza form 4 na likizo ya form 6 pia nilikuwa kwenye t shirt workshop ya I print.

inshort najua hii industry vizuri
 
Last edited by a moderator:
Wazo kama wazo ni zuri sana tatzo ni sababu ya kuacha kazi na je ukishaacha unakwenda kufanya nn au unahamia ofisi gani! Kwa sababu ulizosema mfano boss anakubana hilo halipaswi kukuachisha kazi na kwenda mtaani kujiari labda uhamie kampuni nyingine
Furaha lakini lazima uwe makini sababu unaweza acha kazi ukaenda kujiari ukafikiri utapata furaha lkn kiukweli kujiajiri hasa miaka miwili ya mwanzo ni stress sana hakuna furaha coz itakubidi uwe busy sana ikiwezekana kampani zako za kula bata uzikache

tatizo sina furaha na kazi yangu..

inshort siipendi kazi yangu kabisa. hata kama bosi anifanyeje..

inshort naboreka kila nikifikiria kwenda kazini.

nimeichoka sana na sana.

artwork ni passion. hata kama nisipoingiza kitu. but nafurahi tu navyotengenezea logo tofauti na kuzi transfer kwenye t shirts.
 
Km unafanya usirudi nyuma acha kazi usimsikilize yeyote tena wanavyokua na wasiwasi na ww ukasimamia msimamo wako lazima utakomaa!

Halafu nimekaa krb na watu wa painting na graphic design waliokua serious wote sasa wako vizuri ndani ya 5yrs tu, wanaocheza hawajaendelea lakini tunakesha nao bar kila siku!

Kwa kifupi designing and printing inalipa haijalishi unaprint nn hata mabango na bissness card unapata pesa nzuri tu
 
Nimekuelewa vizuri Sana wala hujanikwaza....wanaokera ni wale tunaoamini watasimamia hizi biashara lakini wanakuwa ndio wauaji,biashara ndogo ndogo hizi usiposimamia mwenyewe hesabu maumivu

Ni kweli na ndio maana sisi tunaofanya kazi nje hurudi masikini nyumbani despite expectations tunazokumbana nazo kwa extended family zetu, unawekeza wanakula kwa imani kwamba maadamu wewe umefungua ka mgahawa ka chips hukategemei maana wewe unahela nyingi kumbe wapi. Inauma na inakera sana maana inarudisha maendeleo nyuma.
 
Habari brothers and sisters,

Nimefanya kazi 4 years. My salary ya sasa ni 2.3m gross,

Niliajiriwa kama inventory controller since 4 yrs ago.

Sababu ya kusepa najiona kabisa I am not happy with my job na najihisi kabisa mimi sijapangiwa niishie hapa.

Kazi inanibana sana na my boss ni mkali sana ananitegemea sana na ananibana kweli kweli nami nashindwa kufanya passion yangu.

Inshort nina passion na art work na nina knowledge kubwa sana ya t shirt printing nataka nikaifanye serious mtaani wakati nasepa job.

Nimejitahidu kwenye miaka yangu 4 kazini nimejenga kajumba changu ka 2 rooms na kila kitu ndani na kununua ka IST.

Nimesave kiasi kidogo cha kunifanya ni-survive for 10 months ahead.

Nimechungulia NSSF nina kama m 18 point something.Nataka nikazi-draw ni invest a half of them kwenye baadhi ya vifaaa nyetu nizamie mazima kwenye T shirt Art work designing.

Kiukweli naondoka kazini sababu sina furaha kazini, siipendI kazi yangu and to me happiness come first.

Artwork ni furaha yangu hata kama silipwi tangu ujanani nafurahi navyofanya artworks za t shirt designing.

Swali kubwa kichwani, uamuzi naoufanya ni sahihi? Maana mama yangu mzazi anasikitika sana na hata mama watoto wangu anasikitika.

Sina uhakika kama hutajutia uamuzi wako, kwani hata mimi baada ya miaka 7 sasa kazini natamani kutoka licha ya mshahara mkubwa nitakaopata baada ya kumaliza masomo (karibu mara 3 ya unachopokea).

Lakini watu hutofautiana sana kwa kila kitu, wengine kama wewe hujali zaidi uhuru na kufanya kile upendacho kutoka moyoni bila kushurutiswa au kusukumwa. Nina mwelekeo kama wako kwa hali ya juu sana hadi wakati mwinginie nafikiri kwamba pengine I take things for granted.

Lakini nakushauri cheki kwanza hali ilivyo, kama unaweza basi anzisha biashara yako ya t-sheti ukiwa bado kazini, na ikishika kasi kiasi cha uhakika basi quit mara moja.

Nasema hivi kwasababu wakati mwingine yaweza kuwa ni kishawishi tu na ukisha acha kazi basi unajikuta ukiwa na majuto makubwa na pengine hutaweza tena kurudi kazini.
 
Ni kweli na ndio maana sisi tunaofanya kazi nje hurudi masikini nyumbani despite expectations tunazokumbana nazo kwa extended family zetu, unawekeza wanakula kwa imani kwamba maadamu wewe umefungua ka mgahawa ka chips hukategemei maana wewe unahela nyingi kumbe wapi. Inauma na inakera sana maana inarudisha maendeleo nyuma.

mimi ni victim wa hilo mkuu, nimejifunza hard way.........ndio maana nashauri mtu yeyote anayeanzisha biashara asimamie mwenyewe,kwa hali hii huwezi kufanya kazi na biashara,upande mmoja utadoda tu na utatoa hitimisho ambalo si sahihi.
 
Kajiajiri bwana, achana na kutumikishwa kwa faida isiyo kuwa yako. Kitu ni chako bwana, go ahead!!!!
 
Mimi pia sikuungi mkono ongeza miaka 4 tena atleast ufungue kaujasiria mali ukiwa kazini then ikitulia unaweza ukaacha.

BIG NO
Huyu anakuingiza chaka. Anataka uendelee kuwa mtumwa kwenye kazi usiyoifurahia. Kama umesevu vya kutosha hadi ku-survive miezi kumi, piga chini mzigo. Kuanza ni kugumu, lakini ukishaanza utajiona kuwa umefanya uamuzi sahihi kabisa. COPY from ME. Niliacha net salary ya kumzidi kwa mbali afisa wa TRA na kufuata roho inachotaka. Siko pabaya sana ila nimefanya maamuzi sahihi na matunda nayaona. Mleta mada, Ingia inbox tushauriane nikujuze namna ya kuanza bila kukwama, BURE!
 
Tatizo waleta mada kama izi huanza kwa kudanganya kuhusu salary ili atushtue tuone ajabu!sema naacha salary laki 3 au 5,ili twende sawa
 
uwamuzi mzuri, japo mwanzon itakupashida kidogo ila utakuja simama tu kujiajiri nijambo bora sana
 
Kaka nimefanya kazi jeshini miaka 25, miaka yote sikupata Ujuzi/Mtaji. Nashukuru niliwekeza kwenye real asset na Muda. Miaka 25 ya utumishi ardhi ili appreciate nikauza nikapata mtaji ndipo nikaaomba voluntarily retirement. Miaka miwili sijajuta hata kidogo. Thanks God
 
Back
Top Bottom