Nimeambukizwa magonjwa ya zinaa na mpenzi wangu wa chuo kikuu (nisaidieni cha kufanya)

Wana.JF Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo kikuu tumekubaliana kwa mapenzi ya mungu tunaweza kuwa mwili mmoja,kwa kweli tumekuwa tukikutana kimwili tulikuwa tuna tumia KONDOMU,Ikafikia hatua tukasahau KONDOMU,SASA NIMEJIKUTA NA MAGONJWA YA ZINAA.NINA UHAKIKA YEYE NDIO KANIAMBUKIZA SIJAMWAMBIA,SASA NIMUACHE AU NIMWAMBIE.NISAIDIENI.

Itabidi umwambie ili wote wawili mpate tiba...then kitakachofuata ni juu yako!
 
asa kuandika chuo kikuu ili iweje?tujueje au ulikuwa unamaanisha nini?chuo kikuu nao ni wazinzi kama watu wengine ambao hawajabaatika kwenda darasani,jitahidi ukatubu kwa mungu kwa ajili ya uzinzi uliofanya na umwambie mwenzako kama anakupenda kweli muoane haraka ili msiwe wazinifu.nenda hospital mkatibiwe wote..

umeniibia wazo langu. pamoja mkuu
 
yuko wapi huyo mzee serengeti, mbona kajificha kupokea ujumbe wake.? Kama upo naomba nijue huyo mpenzi wako yuko chuo gani then ntakuambia namna gani hawa she/he wa chuo walivyo na how to avoid kukuambukiza.! Nyw kapime na upate tiba ya magonjwa yako.

Acha kujumlisha tabia za watu na chuo wewe....

Yaani eti umwambie walivyo unachanganya tabia na chuo.....

Shindwa katika jina la Yesu..............
 
Pole sana usitahamaki, nakumbuka kuna mdada nilimsimamia harusi alipata case kama hiyo mumewe alikasirika akawa tayari kumuacha kabisa sababu alikuwa anajiamini hajatembea na mwanamke mwingine zaidi ya mkewe,wakaenda hsptl kupima mkewe akawa hana kabisa ugonjwa kama mjuavyo mwanaume akipata maambukizi asubuho after some few hrs inajitokeza

baada ya kufanya uchunguzi sana wakagundua kumbe mumewe alijisaidia choo cha kukaa ofisini na sio yeye peke yake kapata bali kuna wababa wengine wawili....ndio kesi ikapoa yaani unaweza pata kwenye public toilet na yeye pia anaweza pata huko chuoni msaidie kwa kumwambia mwende hsptl akatibiwe
 
Hayo ni baadhi ya matokeo ya ngono zembebado na kubwa zaid linakunyemelea nenda mapema kapime hiv km vp anza dozi
 
Wakati mdada amechanganya viuno hadi unasimamia kucha ulikuwa unasikia raha hadi ukavua Condom ukiamini ndizi hailiwi na maganda.,sasa umekwaa gonjwa la zinaa badala ya kwenda hospitali unakuja kuomba ushauri ufanyaje.,unategemea sisi tukwambieje zaidi ya kwenda hospitali kuokoa vikojoleo vyenu.
 
Wana.JF Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo kikuu tumekubaliana kwa mapenzi ya mungu tunaweza kuwa mwili mmoja,kwa kweli tumekuwa tukikutana kimwili tulikuwa tuna tumia KONDOMU,Ikafikia hatua tukasahau KONDOMU,SASA NIMEJIKUTA NA MAGONJWA YA ZINAA.NINA UHAKIKA YEYE NDIO KANIAMBUKIZA SIJAMWAMBIA,SASA NIMUACHE AU NIMWAMBIE.NISAIDIENI.
Wakati unamtongoza au mnatongozana mbona hukutuomba ushauri? Je iwapo asingekuambukiza magonjwa ungetujulisha vile vile? Jaribuni kuwa mnatatua matatizo mengine peke yenu.
 
You thought that the grass was greener, on the other side you made your bed now lay on it. Remember to see your Doctor.
 
Pole sana usitahamaki, nakumbuka kuna mdada nilimsimamia harusi alipata case kama hiyo mumewe alikasirika akawa tayari kumuacha kabisa sababu alikuwa anajiamini hajatembea na mwanamke mwingine zaidi ya mkewe,wakaenda hsptl kupima mkewe akawa hana kabisa ugonjwa kama mjuavyo mwanaume akipata maambukizi asubuho after some few hrs inajitokeza

baada ya kufanya uchunguzi sana wakagundua kumbe mumewe alijisaidia choo cha kukaa ofisini na sio yeye peke yake kapata bali kuna wababa wengine wawili....ndio kesi ikapoa yaani unaweza pata kwenye public toilet na yeye pia anaweza pata huko chuoni msaidie kwa kumwambia mwende hsptl akatibiwe

Haya we serengeti jicho lako na lione hapa!
 
Eti nini? Unauliza? Unayeumwa katibiwe. Nakushangaa! Na unajuaje kakuambukiza yeye. Mwanaume mwanakharamu wewe! Acha kusingizia mtoto wa watu, magonjwa umuambukize halafu na shutuma juu! Hata aibu huna. Loh!
 
Mwambie na muende wote kwa daktari na mfanye vipimo vyote hadi hiv ili mpate ushauri hata kama ni ule wa kuishi kwa matumaini.
Na huko chuo ulienda kusoma au kufanya ngono tena ngono zembe?
Jamani jamni hii ni 'network'!!! Sasa na huyo demu si naye akamchukue mwenzake aliyemletea hayo madudu naye akapimwe?!
 
Mwambie na muende wote kwa daktari na mfanye vipimo vyote hadi hiv ili mpate ushauri hata kama ni ule wa kuishi kwa matumaini.
Na huko chuo ulienda kusoma au kufanya ngono tena ngono zembe?
si unajua tena ujana maji ya moto? vp mpenzi?
 
Wana.JF Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo kikuu tumekubaliana kwa mapenzi ya mungu tunaweza kuwa mwili mmoja,kwa kweli tumekuwa tukikutana kimwili tulikuwa tuna tumia KONDOMU,Ikafikia hatua tukasahau KONDOMU,SASA NIMEJIKUTA NA MAGONJWA YA ZINAA.NINA UHAKIKA YEYE NDIO KANIAMBUKIZA SIJAMWAMBIA,SASA NIMUACHE AU NIMWAMBIE.NISAIDIENI.
<br />
<br />
mwambie kisha nenden wote hospitali.
 
una uhakika ndiye au unaamin? nahisi nawe una kajamaa kengine. ila ka umepewa zinaa jiandae na ugonjwa mkubwa
 
Ikugonge na ngoma kabisa,kila siku mnahubiriwa juu ya ngono zembe mitaan,uzinzi makanisani lakini bado hamsikii,sasa unataka nini,hukumu hicho kiungo chako kilichokusababishia hayo yote,kikate kabisa utakuwa umetatua tatizo na haitakaa ijitokeze tena hiyo ni full prevention method.
 
Mwambie na muende wote kwa daktari na mfanye vipimo vyote hadi hiv ili mpate ushauri hata kama ni ule wa kuishi kwa matumaini.
Na huko chuo ulienda kusoma au kufanya ngono tena ngono zembe?
Ushauri mgumu ambao hauzoeleki ni huu wa kuishi kwa matumaini
 
Back
Top Bottom