Nimeambiwa Simba SC wakitumia Low Block na Counter Attack Wydad Casablanca FC anatupeleka Semi Finals CAFCL

Binafsi sijafanikiwa kuangalia mechi za Mamelody ila nafikiri ifike muda timu za bongo tujifunze kwa Memolody jinsi ya kuwafunga waarabu mana huwezi kuacha kukutana nao, kwa sababu wamelishika soka la Afrika, timu zao zinapatika katika hatua mbalimbali za mashindano.

Hivi hao Mamelody wanatumia mbinu gani kuwafunga hawa waarabu mana walikuwa wameishashindikana ila kwa sasa Mamelody anajipigia tu Waarabu.

Juzi kampiga Belouzdad goli 3-1, na Belouzdad alikuwa nyumbani.
Wewe hukuangalia mechi mpaka mwisho, Mamelodi wamempiga Mwarabu goli 4 kwa 1 kwao, wanasubiliwa sasa waende South Africa waoneshwe kaburi la Al Ahaly walipozikwa.
 
Napenda kolo atinge semi final ingawa hatutokua na amani mjini kwa makelele yao.

Bunafsi nawaombea wafike semi final. Kivipi watafikaje?
1. Watumie surprise attacks kama walivotufanyia kwenye derby. Wapush mapema maana mwarabau atakuja akijua kwamba yeye ndo ana haki ya ku attack.

2. Watumie ule mfumo wa Nabbi kule Nigeria. Back 3 watatu na mid fielder 5, huku back wings zikisogea na kurudi nyuma. Alaf Saido asiwepo kwenye squad, awepo Kibu. Chama aambiwe hii sio mechi ya kutafuta umwamba. Atoe pass faster.

3. No 6 awepo wa kuzunguka uwanja wote anakata umeme kama alivo Ngolo Kante. Pia kila mchezaji ahakikishe ana push na kujitoa 100 ya uwezo wake. Ikitokea wamefungwa goli moja, waambizane kifanya technical attack ya kupush kupata goli.
 
Aina ya wachezaji wa Mamelody ni tofauti na Simba, mchezaji tegemeo Simba ni chama, spidi ya konokono, wengine wazee, mwarabu inatakiwa umpeleke spidi mwanzo mwisho, utawezaje timu imejaa vibabu kina Onyango?
Hiyo Mamelod ina mataji mangapi ya CAFCL kama waarabu ni wazee?
Wanachuakuaje kombe wazee mbele ya vijana?

You have a poor argument

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Nami GENTAMYCINE nauliza je, wakiongezea na High Pressure yaani tucheze Mifumo yote Mitatu ya Low Block, High Pressure and Counter Attack kwa mfumo wa 4-1-4-1 Mwarabu hatochapika Kwao Mohammed V Stadium Siku ya Ijumaa na Mnyama ( Simba SC ) kutinga kwa mara ya Kwanza CAFCL Semi Finals?

Karibuni wana Simba SC Wenzangu wote hapa JamiiForums tulijadili hili Kiufundi na tafadhali kama unajijua Wewe ni Shabiki wa Mganga Kasema Jini linataka Damu za Wanachama Wetu 500 Tu Ili Tushinde kwa Kishindo Jumapili FC usipoteze muda wako Kuchangia au Kushauri chochote kile kwani tunawajua kwa Unafiki Wenu na Kamwe hamtutakii mema.

Cc: SAGAI GALGANO
Ujue Wewe tu mbinu hiyo wao chini ya kocha bora kuliko wote kuwahi kutokea kucheza na timu za Tz asijue
 
Mkuu safari hii mnatumia fundi wa wapi mbona kimya-kimya?
Fundi wao alipigiwa kitabu na waarabu mpaka ile mvua aliyozoea kuachia ikabackfire, Na goli likapatikana moja kama la dawa, Sasa nafikiri wameenda nae moroco kwenye ule msafara lakini anaweza akalipukiwa matunguri yake uko uko maana waarabu si mchezo kwa kitabu!
 
Fundi wao alipigiwa kitabu na waarabu mpaka ile mvua aliyozoea kuachia ikabackfire, Na goli likapatikana moja kama la dawa, Sasa nafikiri wameenda nae moroco kwenye ule msafara lakini anaweza akalipukiwa matunguri yake uko uko maana waarabu si mchezo kwa kitabu!
Kitabu gani? Kama ni Quran basi hakuna jipya

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Kocha wa Simba ajifunze kutoka Mamelody jinsi anavyowafunga Waarabu mana kwa sasa hakuna Mwarabu anayefurukuta kwa Mamelody nje ndani
 
Wewe hukuangalia mechi mpaka mwisho, Mamelodi wamempiga Mwarabu goli 4 kwa 1 kwao, wanasubiliwa sasa waende South Africa waoneshwe kaburi la Al Ahaly walipozikwa.
Hata hapo juu nimesema sikuangalia hiyo mechi, nilihadithiwa tu na huwa siwafuatilii Mamelody ila kuanzia mechi ijayo lazima nianze kuwatazama nione wanatumia mbinu gani kuwanyanyasa Waarabu nje ndani.

Huu ni msimu wa pili Al ahly hafurukuti kwa Mamelody nje ndani. Belouzad naye kachezea.

Hata hao Wydad nahisi wangechezea goli nyingi kwa Mamelody. Simba alichezea nafasi mbili za muhimu, alipaswa apate goli tatu na kuimaliza game.
 
Back
Top Bottom