Niliyoyaona jimboni Karatu

Mujumba

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
853
306
safari ya kwenda loliondo ilinipa nafasi ya kufika jimboni Karatu na kujionea mambo mengi yaliyonivunja moyo na kunikatisha tamaa kabisa juu ya uwezo wa Dr Slaa! nilikutana na msururu wa kinamama wakiwa na ndoo wakienda sehemu za mbali kutafuta maji,pia kwa macho yangu niliweza kuona foleni ndefu sana za maji hii ilithibitisha kuwa kuna shida kubwa ya maji,pia niliweza kuona watoto wengi wa shule wakiwa hawana viatu miguuni,pia wananchi kwa ujumla walionekana wamekata tamaa ya maisha na nyuso zao zilionyesha hivyo! nikajiuliza hili si ndio jimbo la bwana slaa ambalo aliltumikia kwa miaka mingi,sasa kwanini alishindwa kutatua hizi kero za wananchi?? miaka yote alikuwa anafanya nini kama mbunge? kama jimbo dogo hili limemshinda je nchi angeiweza? nilijiuliza maswali mengi sana ambayo nilishindwa kuyapatia majibu kabisa
(Hii ni email niliyofowadiwa na rafiki yangu Mussa Mosha anayemiliki kampuni ya utalii pale Arusha na mfuasi mzuri wa chadema)
 
mkuu unaamini ya kuambiwa?? Nenda mwenyewe ukaone.. hayo ni matatizo ya watanzania wengi kwenye majimbo mengi! ulitaka atatue kwa mshahara wake??
 
Wewe unawasemea wanakaratu kama nani? Hawana shida kama hao wa jimbo lako la kiccm. Mbona JK yuko magogoni lakini mtaa wa pili hauna maji wala umeme? dk. Slaa hana fedha bali uongozi shupavu
 
Kashaga bila shaka brain yako ina handfull amount of viral diseases, I hope babu atakusadia ili urudi kwa wenye busara
 
mkuu unaamini ya kuambiwa?? Nenda mwenyewe ukaone.. hayo ni matatizo ya watanzania wengi kwenye majimbo mengi! ulitaka atatue kwa mshahara wake??

Yeye kama mbunge wa pale kwa miaka zaidi ya kumi alipambana vipi na hizo changamoto? huwezi kujivuna utaliletea taifa neema ikiwa kwako yamekushinda! wako wabunge wanaoweza kujivuna kutatua kero mbalimbali sasa yeye alifanya nini miaka yote?
 
Temeke:
Tanzania_mothers_459847artw.jpg

Ilala:

4.jpg
 
safari ya kwenda loliondo ilinipa nafasi ya kufika jimboni Karatu na kujionea mambo mengi yaliyonivunja moyo na kunikatisha tamaa kabisa juu ya uwezo wa Dr Slaa! nilikutana na msururu wa kinamama wakiwa na ndoo wakienda sehemu za mbali kutafuta maji,pia kwa macho yangu niliweza kuona foleni ndefu sana za maji hii ilithibitisha kuwa kuna shida kubwa ya maji,pia niliweza kuona watoto wengi wa shule wakiwa hawana viatu miguuni,pia wananchi kwa ujumla walionekana wamekata tamaa ya maisha na nyuso zao zilionyesha hivyo! nikajiuliza hili si ndio jimbo la bwana slaa ambalo aliltumikia kwa miaka mingi,sasa kwanini alishindwa kutatua hizi kero za wananchi?? miaka yote alikuwa anafanya nini kama mbunge? kama jimbo dogo hili limemshinda je nchi angeiweza? nilijiuliza maswali mengi sana ambayo nilishindwa kuyapatia majibu kabisa
(Hii ni email niliyofowadiwa na rafiki yangu Mussa Mosha anayemiliki kampuni ya utalii pale Arusha na mfuasi mzuri wa chadema)

Kumbee!! Basi kamwambie kikwete akatalii na huko akajionee mwenyewe watanzania wanavyotaabika. ila mwambie huko hakuna bembea.
Mwambie pia akienda loliondo kwa babu angalie miundombinu, wilaya ya Kubwa la Mafisadi na mbunge wao milele(Loliondo imegawanywa kutoka monduli recently). kashaga nenda!
 
hizi ndizo fikira zilizogota .... pumba si pumba .... crap si crap basi tu ilimradi iti ametoa challenge JF ..... huu ni uparamama
 
Huyu jamaa anaishi wapi huyu HADI ANAFIKIA kushangaa matatizo ya watanzania ya toka enzi na enzi?
Usilete ubeba-box wako hapa bongo bana!
Tunasubiri mtimize ahadi hizi kwanza, na ndipo uanze kushangaa!

AHADI ZA KIKWETE KWA WAPIGA KURA KATIKA KAMPENI ZA URAIS 2010.
Je atazitekeleza?...Mimi na wewe ni Mashahidi, na kama zitatekelezwa tuweke tiki!
Lakini kinachotisha zaidi, ahadi hizi gharama yake ni jumla ya shs trilioni 90!...upo hapo?

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
35. Kulinda haki za walemavu- Makete
36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
42. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Kashaga umetumwa na nani? kwanza ukweli wako umejidhihirusha kwa sababu safari ya Loliondo unapitia mto wa mbu kwa Lowassa, sasa kama umewaona watu wa huko sio dr. Slaa. Historia ya karatu huijui acha umbea!

Nenda karatu jionee mwenyewe. au kapone hilo ligonjwa lako lililokufanya uende kwa babu ndio uende ukaone vizuri karatu kwa macho yako.

CCM hata wafanyeje karatu hawaokoti kitu!
 
Yeye kama mbunge wa pale kwa miaka zaidi ya kumi alipambana vipi na hizo changamoto? huwezi kujivuna utaliletea taifa neema ikiwa kwako yamekushinda! wako wabunge wanaoweza kujivuna kutatua kero mbalimbali sasa yeye alifanya nini miaka yote?

Mkuu,
we huwa unafuatilia Bunge?? Mbona mara kibao mheshimiwa SLAA amekuwa akiweka wazi maendeleo jimboni kwako. Na hata baadhi ya wabunge wamekuwa wakimpa sifa.
Mie binafsi sijafika huko Karatu,
wewe pia hujafika huko..hebu kafuatilie kama hizo taarifa zako ulizopewa zina ukweli kiasi gani halafu uje u-comment hapa!

Mkapa kabla ya kuwa rais alikuwa mbunge kule Masasi.. Umefika Masasi na kuona wana matatizo gani? lakini Mkapa alikuja kuwa raisi
 
Wewe unawasemea wanakaratu kama nani? Hawana shida kama hao wa jimbo lako la kiccm. Mbona JK yuko magogoni lakini mtaa wa pili hauna maji wala umeme? dk. Slaa hana fedha bali uongozi shupavu

mimi siwezi kuwa mnafiki jimbo langu ni la moshi mjini ambalo nimeishi zaidi ya miaka 20 sasa,lakini ki ukweli ndugu Ndesamburo amefanya mengi sana pale na ndio maana unapokuja uchaguzi tunaweka vyama pembeni a kumchagua huyu mzee kwani yeye kama mbunge amefanya mengi sana na hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuonyesha aliyofanya mzee Ndesa si kwenye maji tuu,Ndesa kasaidia,mashule,barabara,hospitali,masoko,michezo etc,sasa Slaa yeye kwanini jimbo lake liko kwenye hali duni hivi,miaka yote alikuwa anafanya nini?
 
Kama hiyo haitoshi, Mtu na Waziri mhusika, wapo kufungua Bomba la Maji ili akina mama wapate maji kwa urahisi.

Kama BAJAJI vile kwa akina mama Waja wazito...... Heheheee!!!!!

mugumu.jpg
 
Kwa kweli mimi nashindwa kuwashangaa watu wanaopoteza muda kuchangia thread zisizo na tija yoyote zinazoanzishwa na kashaga & co.
Dawa yao ni kusoma utumbo wao halafu unachapa lapa!!
 
mimi siwezi kuwa mnafiki jimbo langu ni la moshi mjini ambalo nimeishi zaidi ya miaka 20 sasa,lakini ki ukweli ndugu Ndesamburo amefanya mengi sana pale na ndio maana unapokuja uchaguzi tunaweka vyama pembeni a kumchagua huyu mzee kwani yeye kama mbunge amefanya mengi sana na hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuonyesha aliyofanya mzee Ndesa si kwenye maji tuu,Ndesa kasaidia,mashule,barabara,hospitali,masoko,michezo etc,sasa Slaa yeye kwanini jimbo lake liko kwenye hali duni hivi,miaka yote alikuwa anafanya nini?

Karatu huijui Moshi mjini huijui!

Peleka PUMBA zako huko!
 
Back
Top Bottom