Nilichukia sana nilipogundua kuwa baba ndiye mchumba wake mama...

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,986
156,264
Nilikuwa najua baba na mama ni ndugu. Kamwe sikujua kuwa ni watu kutoka koo mbili tofauti.

Mama yangu mdogo alipo olewa, alivaa nguo nzuri sana. Mimi na wadogo zangu tukaletewa nguo nzuri sana kutoka ng'ambo.

Hamu na kiu yangu sasa ikawa ni kuona mama naye akiolewa, ili apendeze na sisi tupate tena nguo toka ng'ambo.

Nilipo ona mama anakawia kuolewa, nikamuuliza baba, mama ataolewa lini kama anti Tutti ili tuletewe nguo toka ng'ambo?

Baba akafunguka, akasema yeye ndio mchumba wa mama, na tayari amesha muoa.

Akaingia chumbani na kutoka na kitabu kikubwa. Akaanza kunionyesha picha zao za harusi. Nichukia sana.

Hapo nilikuwa na miaka mitano tu.

Je wewe unakumbuka ni kisanga gani ulichokifanya ulipokuwa mtoto?
 
teheee...aisee we mdau sijakuona kitambo.
mimi nina visa viwili, kimoja hakifai hata kuweka humu,mwenye kiu nacho ani PM
hiki cha pili cha kawaida: kuna mmama fulani alikua rafiki yake mama, alikua anapenda kuja home...
basi mimi kila akija nilikua namfuata mama namnong'oneza nakumwambia "mama mimi nikikua nataka nimuoe huyu mama" hapo nilikua na miaka kama 6,...majuzi nimekutana na yule maza, ni mtu mzima kinoma...akanitania...akanambia wewe si ulisema utanioa? hahahaaa...
 
Hahahahhahaaa Bujibuji unataka mama yako aolewa mara ya pili ili ipate nguo hahahahahhah
 
Last edited by a moderator:

Hebu ni PM mzee unipe hicho cha kwanza
 
True story niikumbukayo katika hili , nakumbuka nikiwa na 6 yrs.
Kuna magari yalikua yakiitwa Factor films yakipita kila mkoa ama wilaya kwa mwezi mara 1 yakionesha sinema, na hiyo ndiyo siku ya mgao wetu tr. 23 monthly!
Baba alishanipa warning mapema kua sitakiwi kwenda sinema siku hiyo kwakua mapema ya hiyo siku nilionekana nina symptoms za malaria.
Warning ya Baba haikufanya kazi mi nikaenda, niliporudi alinipa kichapo cha haja.
Baada kichapo nikamfata Maa nikamuuliza "hivi mama , huyu baba ni ndg yetu?"
akaniuliza , "kwanini ? " nikamwambia kanichapa akaniuliza tena "kwa hiyo unataka tumfanyaje?" nikajibu
"kwanza leo asile kwetu, usimpe chakula chetu alafu tumfukuze kwetu"
 
I was a litle girl nina 6 years kuna uncle wetu alikuwa apenda sana kuja kwetu sasa kuna siku mama alinunua kabati wakati linaingizwa ndani yule uncle akawa anasaidia nkamwambia aache asijipendekeze kwenye kabati letu akenda mwambia mama nlichapwa nkaambiwa nimuombe radhi
 
Jaamani..huyo anko alikuonea tu.
Sasa hivi umefikisha miaka mingapi??! :p
 
Basi kwa kuwa mm nmesahau nlikua na miaka mingapi nitatumia 6..
Nlipokua na miaka sita..siku moja tumepika pilau ya haja na nyama ya kuku iliyorostiwa pembeni.
Basi kwa mazoea tulivokua wadogo tunakulaga chakula kwanza then nyama mwishoni.
Kwa bahati mbaya siku hiyo wakaja wageni bila taarifa wakatukuta tunakula. Ikabidi nao wakaribishwe walau waache baraka.
Na kwa kuwa tulikua tushapakua tukawa tumemaliza nyama zote kwenye hotpot ila tulikua nazo kwenye sahani kama mbilimbili kila mtu.
Kimbembe kilikuja tulipoambiwa tuwagawie wageni nyama moja moja..mimi ya ngu nikaificha nikadai imeisha.
Tulipomaliza kula nikanyanyuka nayo sasa wakati napishana na mgeni pale akannigonga mkono bahati mbaya nkaangusha nyama yangu..nilipatwa na aibu.
Af kama haitoshi wageni walipoenda kulala tu baba akanifuata..alinipigaje...mpaka nakumbuka ukutani pale nliandikaga i hate u daddy...dah ila ulikua utoto...
I love my dad sioooo much.
 
mmmmh sheshe la mwaka mume wangu jg nimecheka had tumbo laniuma

Mi nina meng ila hebu skia hii nilikua na umri mdogo kama miaka mitano ivi mara nying nilikuan nasimamia harusi sasa siku hiyo nimesimamia harusi vizuri tuu ghafla aunt yangu akawa anpita ukumbin mi si ndo nikamuona bana nikamwita aunt kwa sauti tena nilikua namfuata pale ukumbin nikarudishwa nkaendelea na sherehe ila sasa kilichojiri kesho yake nilikula mkong'oto ka jambaz mtoto
 
Enzi hizo nakumbuka nilikuwa na miaka kama 5 tulikuwa tunaishi victoria dar,tulikuwa tunaishi maghorofani tena ghorofa ya juu,siku moja nikamuuliza mdogo wangu(mtoto wa mama mkubwa) eti ukiwasha moto halafu ukishawaka ukiumwagia mafuta ya taa utawaka ama utazimika?tukaenda kufanya experiment nikampa mafuta ya taa,mi nikachukua kiberiti mpaka chumbani kwa mama tukajifungia ndani,nikafungua kabati la nguo nikawasha nguo kwa kiberiti ilipowaka nikamwagia mafuta ya taa,,kilichotokea,moto ukawa mkubwa,tunaogopa kutoka tutapigwa,moto unazidi kupamba moto,wazazi hawapo,,tulikuja okolewa na majirani ingawa mfanyakazi wetu aliungua mguuni.
 
True story niikumbukayo katika hili , nakumbuka nikiwa na 6 yrs.
Kuna magari yalikua yakiitwa Factor films yakipita kila mkoa ama wilaya kwa mwezi mara 1 yakionesha sinema, na hiyo ndiyo siku ya mgao wetu tr. 23 monthly!
Baba alishanipa warning mapema kua sitakiwi kwenda sinema siku hiyo kwakua mapema ya hiyo siku nilionekana nina symptoms za malaria.
Warning ya Baba haikufanya kazi mi nikaenda, niliporudi alinipa kichapo cha haja.
Baada kichapo nikamfata Maa nikamuuliza "hivi mama , huyu baba ni ndg yetu?"
akaniuliza , "kwanini ? " nikamwambia kanichapa akaniuliza tena "kwa hiyo unataka tumfanyaje?" nikajibu
"kwanza leo asile kwetu, usimpe chakula chetu alafu tumfukuze kwetu"

Afukuzwe baba? Labda mama awe anafanya kazi njaa ingewafanya mmkumbuke kesho tu na ungetamani arudi teh teh utoto una mengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom