Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,329
- 23,873
Ayayaya...nakumbuka nikiwa form one...shule moja hivi huko kilimanjaro.
Shule yenyewe ilikuwa na 5% boys 95% girls.
Sasa siku moja tukatangaziwa kuna wanafunzi kutoka sweden watakuja kutusalimia alafu wangependa kucheza na sisi mpira wa miguu.
Basi tukawa tunatolewa darasani wiki nne mfululizo saa tisa kwenda mazoezini. Kwaiyo kwa mwezi mzima sisi tukawa tunakosa vipindi vya jioni.
Basi siku ya siku wageni wakaja tukawa tunapiga nao kitabu wiki nzima then Ijumaa tukaenda kwenye mechi...mimi nikijua kabisa nimepiga zoezi la kutosha na namba yangu namba nane naimudu vizuri.
Wakapanga kikosi bana...tena na jezi nshavaa..mara nashtuka mpishi ndo amevaa jezi af akaingia namba yangu. Kabla sijaelewa vizuri si mechi ikaanza. Nikaambiwa nitaingia second half.
Haya nikangoja kipindi cha kwanza kikaisha..mpishi hata kucheza hajui..anabutua mpira tu...yani dah nkawa najipa moyo nikiingiaaaa...watanijua.
Kipindi cha pili kikaanza.mtu mzima nishapasha kabisa tayari kuingia mara sista anakuja kuniambia ati huwezi kuingia kisa wale wazunggu wana miili mikubwa eti wataniumiza mara ooh..daah iliniumaje??!
Nililia siku ile jamani...nililia....daah..yani kila nkikumbuka ile siku hasira huwa inanipandaga ghafla..kiukweli nlipokua form one nlikua na umbo dogo sana ila hata dk 10 niwaonyeshe wat i could do.
Af nkifikiria nimepoteza mwezi mzima sijaatend vipindi vya jioni nliumia sana..mwishoni wanakuja kumweka mpishiiiiiii....dah..
Ngoja niachie apa nsije lia tena...