Nilichojifunza kwenye msiba wa kaka

kyanyangwe

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,147
2,746
Kaka yangu amefariki last two weeks.

Alikua Mtumishi wa Umma wa cheo kikubwa tu wizara fulani.

Ofcoz, siwezi kudanganya serikali iliuchukua huu msiba serious, sijajua ni kwa sababu ya miongozo yao au ni kwa sababu ya ukaribu kati ya bro na boss wake. Anyway bro alifaraiki ghafla sababu tuliyoambiwa na Madaktari ni heart attack.

Msiba wa kaka umehudhuriwa na wananchi wa kawaida sana kuanzia wachimba kaburi mpaka waombolezaji.
Kipindi cha uhai wa kaka, kuna kipindi niliwahi kumsikia kwa maskio yangu akiongea na mpaka Raisi wa nchi kuhusu masuala fulani kaka leo kafariki kwenye mazishi yake nimesikia tu salamu za waziri wake.

Nilichojifunza, hivi vyeo vya duniani ni nonsense mbele ya Mungu. Leo kaka kafariki wanaomuogesha ni wananchi wa kawaida tu tena wa kule kijijini kwetu na wanafamilia.

Tutende mema tukiwa hai, nilichokishuhudia kule mortuary na nafasi aliyokua nayo kaka ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Kwanza nikupe pole kwa msiba. Mungu azidi kuwapa nguvu.

Maswali yangu ni machache tu mkuu.
Je, pale mortuary ulitarajia awe katika hali gani kulingana na status yake?

Ndugu, jamaa na marafiki ni kawaida na heshima na utamaduni kupata fursa ya kuuhudumia mwili mpendwa wao, je ulitarajia nani afanye hayo? Unaringanisha na utaratibu upi tofauti uliowahi kuuona wapi?
 
Pole sana.Kifo chake,kiache funzo kwenu mliomfahamu na hata waliomfahamu baada ya yeye kuondoka hapa duniani.Tuishi na watu vizuri.Ikitokea umerudi nyumbani,ishi na wanakijiji vizuri.Hao(wanakijiji),ndiyo hulala msibani,huogesha miili,huchimba makaburi,hugawa chakula msibani n.k.

Kwa ufupi watu wa kawaida,ndiyo huwa kila kitu.Huwezi kumkuta mbunge, waziri, Rais au watu tunaokunywa nao bia mjini,wanachimba kaburi,kuosha maiti n.k.

Tuheshimiane.
 
Pole ndugu kwa kuondokewa na kaka, huwa tunawadharau tukiwa kwenye hizi nafasi, lakini tukifa wale tuliowapuuza ndio wanaotujali.

Siku moja pasipo kutarajia nikiwa natoka stendi gari ilizima ghafla, nikajaribu kuiwasha laa, wakati huo gari zingine na mabasi yameshaanza kupiga honi maana nimezuia barabara. Alitokea kijana mmoja mchukua mizigo, akaisukuma gari mpaka sehemu salama.

Nikashuka ili nimshukuru , sikumuona mtu, alikuwa ameshaondoka. Kwa kweli tukio hili sitalisahau na lilinifundisha kumheshimu kila mtu.

Toka siku ile kila mtu awe mtoto, tajiri, maskini wote nawapa heshima zao, hujui ni nani atakusaidia lini
 
Kwanza nikupe pole kwa msiba. Mungu azidi kuwapa nguvu.
maswali yangu ni machache tu mkuu.
Pale mortuary ulitarajia apewe awe katika hali gani kulingana na status yake?

Ndugu, jamaa na marafiki ni kawaida na heshima kupata fursa ya kuhudumia mwili mpemdwa wao, je ulitarajia nani afanye hayo? Unaringanisha na utaratibu upi tofauti uliowahi kuuona wapi?
Enzi ya uhai alikua na hadhi yake kwa kweli,gari la serikali lenye mafuta full tank muda wote.ila leo nashangaa anaogeshwa na wananchi wa kawaida kabisa kule kijijini.

Wale maboss waliokua kila muda wako home kwake osterbay siwaoni hata wakishiriki shughuli yoyote ya mazishi zaidi ya kuaga mwili tu.
 
Pole mkuu, BTW kwa kuwa uliwahi kumsikia anaongea na Rais ulitegemea akifa aje kuzikwa na mawaziri?? Ukifa ni umekufa shughuli yako imeishia hapo, cha msingi hakikisha kabla ya kufikia umauti umejitahidi kuishi kwa kuiridhisha nafsi yako bila kubugudhi wengine
 
Enzi ya uhai alikua na hadhi yake kwa kweli,gari la serikali lenye mafuta full tank muda wote.ila leo nashangaa anaogeshwa na wananchi wa kawaida kabisa kule kijijini.wale maboss waliokua kila muda wako home kwake osterbay siwaoni hata wakishiriki shughuli yoyote ya mazishi zaidi ya kuaga mwili tu.
Kuuaga mwili ndiyo nafasi yao, mengine wanapaswa kuwaachia ndugu wasimamie majukumu ya mpendwa wao.
Unadhani ingeleta picha gani iwapo marafiki ma wafanyakazi wenza wangeyafanya hayo majukumu mengine? Lazima ugomvi ungeibuka au malalamiko kuwa marafiki wamewatenga ma kuwaingilia.
Marafiki, mwajili ma wafanyakazibwenza wanaishia kufanya logistics tu, mengine ni ya kifamilia na kimila zaidi.
 
Back
Top Bottom