Niko njia panda yenye maumivu moyoni: Biashara yangu imelala sana je, niende kwa mganga?

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,844
13,102
MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI.

INTRODUCTION:

Mimi ni mtumishi wa umma Ila pia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa sanaa...

Na nikiri NAPENDA HELA SAA.
Yaani ukitaka niwe na Amani basi laki kadhaa ziwe kwenye wallet yangu.

Katika kukimbiza ndoto zangu niliamua kufungua biashara ya vinywaji ya Jumla na rejareja (jina la mtaani tunaita Depo).

Nilikusanya mtaji nikiwa tayari nina idea na ilipofika mil 9 nikafungua depo.
Mil 6 bidhaa na mil 3 sunk cost kama kodi, Matengenezo frame na mengine yale ya maandalizi ya biashara.

Nauza vinywaji vyotee vikali na baridi, kwa jumla na reja reja, na kwasasa biashara yangu ina mtaji wa mil 25.

SCENARIO
Biashara ilianza vizurii mpaka nikawa nadata, yaani wateja walikuwa wengii.

Hawa wakani-force kukuza mtaji fasta mpaka kufika hizo mil 25.

Pia nikawa na vijana wa3 wa dukani, yaani ni fast delivery. Yaani mteja akikata tu simu basi bidhaa ipo mlangoni mwake.

Aisee nilipata jina fasta na kubwaa sanaa.

Mauzo yangu yalikuwa makubwa ya mil 3 Kwa siku na siku nisipouza yalikuwa hayashuki mil 1.

Kwasasa Nina Miaka kadhaa kwenye biashara (from July 2020).

Ila ndugu sasa biashara sielewi..

PROBLEM
Tokea January 2023 BIASHARA IMEKUWA NGUMU mnooo.

Mauzo mil 1 Tena jana ndio Majanga, nimefunga na laki 5..!!!

Pia hapa Nina miamala ya simu, na juzi (01/02) nililipwa commission ya 150k kwa mitandao yotee mi 4.

Wakati nilifika commison ya laki 5 kwa mitandao yote mi4.

Wateja simu sizioni, wakati Kuna kipindi walikua wanapiga simu mpaka saa 7 usiku kuniomba niwauzie bidhaa.

Hiyo saa 7 usiku watakukodia boda utakuja kufungua store utawauzia, wanakulipa na boda inakurudisha gheto kwa gharama zao.

Nina masters na bachelor ya mambo ya biashara, hivyo nimejaribu marketing skills kibao kama za kutuma sms kila asubuhi kuomba order kwa wateja, kupost status za WhatsApp ila 2023 bado ngumu kwenye biashara.

Sasa nimeshauriwa na raia NIENDE KWA MTAALAMU NIKAPIKWE.

Naambiwa, nilikua na nyota kalii hivyo competitor wameona waizime ili wao wauze.

DILEMA
Nimedata mwenzenu, ukicheki hii biashara ndio naitegemea kuwa ndio tobo la kunifanya nije kuachana na ajira za serikali ya CCM ila MBELE NAONA GIZA.

Nina mengi aisee siwezi kuandika yote, mfano: siku hizi nafungua saa 1 kamili asubuhi na kufunga saa 5 usiku.
Na hata kazini (halmashauri) nimepasusa naona pananichanganya tu (wiki yotee hii (Tokea 30/01)SIJAFIKA KAZINI.

KUHUSU VITABU-
Hivi vitabu sijui vya Robert koyasaki na wengine NIMESOMA SANAAA.
Tokea 2020 nishasoma vitabu kama 30 hivi vya mambo ya biashara na fedha na Robert Koyasaki pekee yake ni vitabu vi5 kuanzaia Rich Dad mpaka Money Quadrant.

Vingi vinazungumzia "Kwenye financial world Usikate tamaa, pambana"" ila nahisi Kuna kamba ipo nyuma ya mapambano yangu inanivuta nyuma.

NAPAMBANA NYIE...
1. Muda wote duka nalifanya safi
2. Rangi zinavutia (mashelf na ukuta)
3. Kama elimu, Nina degree mbili za biashara (bachelor + masters)
4. Kama ni experince, nishauza sanaa biashara za watu Tena bila mshahara (kipindi najifunza biashara)
5. Kama ni ukarimu, basi ni mkarimu sanaa. Humu Kuna watu wawili tulishaongea sanaa Japo kwa simu (kama wako comfortable wanaweza thibitisha hapa).

Kifupi nafanya mengii ila 2023 imekua ngumu.
Imefikia mpaka kupunguza wafanyakazi dukani kutoka 3 mpaka 1..!!!

Na kilichonifanya nipost ni baada ya commision kushuka kutoka 500k mpak 150k kwa Jauary/2023.

Huwezi amini:-
Jumapili ya wiki hii sikufungua, ili tu nione upepo wa wateja, ila chakusangaza mpaka unaingia usiku sijapokea simu hata ya mteja mmoja kulalamika "Mbona nimefunga"

Kwasasa sijui si-exist kwenye phone book zao..!! Niko kudata balaaa yaani waliokuwa wakinipigia simu usiku nao hawapigi hata mchana..!!!

Kazini sijaenda wiki maana kichwa ni cha moto balaaa.

Nipeni mawazo wajasiliamali wenzangu.
Nipeni mawazo wafanyabiashara wenzangu.

Nishapitia msoto mkubwa sanaa kwenye maisha ya uyatima, kazini, kwenye ujana wangu ila Jambo gumu linapogusa biashara NADATA KABISAAAA.

Nahitaji kuacha Kazi na hili ndio TOBO LANGU.

MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI?

#YNWA
 
Naam hivi ndivyo allah huadhibu waja wake, wewe si humtambui? kwasababu tu ulijiona umejitosheleza.

"hapana! sivyo hivyo!, hakika mwanadamu ni mwenye kuvuka mpaka mno, pale anapojiona amejitosheleza."

Quran 96:6-7

Tiba ya hayo mambo sio kwenda kwa waganga huko sasa unaenda ulimwengu mwingine na hasara zitakuzidi mpaka utajinyonga, rudi kwa mola wako muombe msamaha na unyenyekee kwake, atakufungulia milango ya rizki na baraka nyingi, hakika yeye ni msamehevu mwenye huruma mno.
 
Mimi (as for me,simsemei mtu) naamini biashara ni kuwa na bidhaa sahihi kwa wakati sahihi na location sahihi bila kusahau kauli nzuri kwa wateja pia kuheshimu mtaji hakuna mganga wa kukupa mafanikio ktk biashara yako zaidi ya Mungu na juhudi zako ukitaka kuniamini nenda kaloge halafu weka mali mbovu uone kama utauza.

Tuliza akili omba Mungu ni upepo tu usipagawe bado mapema and by the way nimekuwa nakusoma soma humu hutaki kuowa wewe ungekuwa na watoto unapeleka shule saizi ungekuwa ushatoboa kwa njia nyengine maana ubongo ungeuchangamsha zaidi ya hapo.
 
Naam hivi ndivyo allah huadhibu waja wake, wewe si humtambui? kwasababu tu ulijiona umejitosheleza.

"hapana! sivyo hivyo!, hakika mwanadamu ni mwenye kuvuka mpaka mno, pale anapojiona amejitosheleza."

Quran 96:6-7

Tiba ya hayo mambo sio kwenda kwa waganga huko sasa unaenda ulimwengu mwingine na hasara zitakuzidi mpaka utajinyonga, rudi kwa mola wako muombe msamaha na unyenyekee kwake, atakufungulia milango ya rizki na baraka nyingi, hakika yeye ni msamehevu mwenye huruma mno.

😳😳😳 Nimuombe msamaha Allah, NIMEFANYA KOSA GANI?

#YNWA
 
MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI.

INTRODUCTION:

Mimi ni mtumishi wa umma Ila pia nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa sanaa...

Na nikiri NAPENDA HELA SAA.
Yaani ukitaka niwe na Amani basi laki kadhaa ziwe kwenye wallet yangu.

Katika kukimbiza ndoto zangu niliamua kufungua biashara ya vinywaji ya Jumla na rejareja (jina la mtaani tunaita Depo).

Nilikusanya mtaji nikiwa tayari nina idea na ilipofika mil 9 nikafungua depo.
Mil 6 bidhaa na mil 3 sunk cost kama kodi, Matengenezo frame na mengine yale ya maandalizi ya biashara.

Nauza vinywaji vyotee vikali na baridi, kwa jumla na reja reja, na kwasasa biashara yangu ina mtaji wa mil 25.

SCENARIO
Biashara ilianza vizurii mpaka nikawa nadata, yaani wateja walikuwa wengii.

Hawa wakani-force kukuza mtaji fasta mpaka kufika hizo mil 25.

Pia nikawa na vijana wa3 wa dukani, yaani ni fast delivery. Yaani mteja akikata tu simu basi bidhaa ipo mlangoni mwake.

Aisee nilipata jina fasta na kubwaa sanaa.

Mauzo yangu yalikuwa makubwa ya mil 3 Kwa siku na siku nisipouza yalikuwa hayashuki mil 1.

Kwasasa Nina Miaka kadhaa kwenye biashara (from July 2020).

Ila ndugu sasa biashara sielewi..

PROBLEM
Tokea January 2023 BIASHARA IMEKUWA NGUMU mnooo.

Mauzo mil 1 Tena jana ndio Majanga, nimefunga na laki 5..!!!

Pia hapa Nina miamala ya simu, na juzi (01/02) nililipwa commission ya 150k kwa mitandao yotee mi 4.

Wakati nilifika commison ya laki 5 kwa mitandao yote mi4.

Wateja simu sizioni, wakati Kuna kipindi walikua wanapiga simu mpaka saa 7 usiku kuniomba niwauzie bidhaa.

Hiyo saa 7 usiku watakukodia boda utakuja kufungua store utawauzia, wanakulipa na boda inakurudisha gheto kwa gharama zao.

Nina masters na bachelor ya mambo ya biashara, hivyo nimejaribu marketing skills kibao kama za kutuma sms kila asubuhi kuomba order kwa wateja, kupost status za WhatsApp ila 2023 bado ngumu kwenye biashara.

Sasa nimeshauriwa na raia NIENDE KWA MTAALAMU NIKAPIKWE.

Naambiwa, nilikua na nyota kalii hivyo competitor wameona waizime ili wao wauze.

DILEMA
Nimedata mwenzenu, ukicheki hii biashara ndio naitegemea kuwa ndio tobo la kunifanya nije kuachana na ajira za serikali ya CCM ila MBELE NAONA GIZA.

Nina mengi aisee siwezi kuandika yote, mfano: siku hizi nafungua saa 1 kamili asubuhi na kufunga saa 5 usiku.
Na hata kazini (halmashauri) nimepasusa naona pananichanganya tu (wiki yotee hii (Tokea 30/01)SIJAFIKA KAZINI.

KUHUSU VITABU-
Hivi vitabu sijui vya Robert koyasaki na wengine NIMESOMA SANAAA.
Tokea 2020 nishasoma vitabu kama 30 hivi vya mambo ya biashara na fedha na Robert Koyasaki pekee yake ni vitabu vi5 kuanzaia Rich Dad mpaka Money Quadrant.

Vingi vinazungumzia "Kwenye financial world Usikate tamaa, pambana"" ila nahisi Kuna kamba ipo nyuma ya mapambano yangu inanivuta nyuma.

NAPAMBANA NYIE...
1. Muda wote duka nalifanya safi
2. Rangi zinavutia (mashelf na ukuta)
3. Kama elimu, Nina degree mbili za biashara (bachelor + masters)
4. Kama ni experince, nishauza sanaa biashara za watu Tena bila mshahara (kipindi najifunza biashara)
5. Kama ni ukarimu, basi ni mkarimu sanaa. Humu Kuna watu wawili tulishaongea sanaa Japo kwa simu (kama wako comfortable wanaweza thibitisha hapa).

Kifupi nafanya mengii ila 2023 imekua ngumu.
Imefikia mpaka kupunguza wafanyakazi dukani kutoka 3 mpaka 1..!!!

Na kilichonifanya nipost ni baada ya commision kushuka kutoka 500k mpak 150k kwa Jauary/2023.

Huwezi amini:-
Jumapili ya wiki hii sikufungua, ili tu nione upepo wa wateja, ila chakusangaza mpaka unaingia usiku sijapokea simu hata ya mteja mmoja kulalamika "Mbona nimefunga"

Kwasasa sijui si-exist kwenye phone book zao..!! Niko kudata balaaa yaani waliokuwa wakinipigia simu usiku nao hawapigi hata mchana..!!!

Kazini sijaenda wiki maana kichwa ni cha moto balaaa.

Nipeni mawazo wajasiliamali wenzangu.
Nipeni mawazo wafanyabiashara wenzangu.

Nishapitia msoto mkubwa sanaa kwenye maisha ya uyatima, kazini, kwenye ujana wangu ila Jambo gumu linapogusa biashara NADATA KABISAAAA.

Nahitaji kuacha Kazi na hili ndio TOBO LANGU.

MGANGA ATANIRUDISHA KWELI KWENYE RELI?

#YNWA
Nina experience ya zaidi ya miaka kumi (10) kwenye biashara ya Pombe both beer, spirits na soft drinks!
Nachoweza kukushauri in summary ni hichi, “ acha wenge” tulizana biashara ipo na ni nzuri!
If u need profit forecast and what to expect kutoka kwa biashara yako waweza uliza more chief! Ila kwa sasa nikushauri utulie kwanza
 
Mimi (as for me,simsemei mtu) naamini biashara ni kuwa na bidhaa sahihi na kwa wakati sahihi,kauli nzuri kwa wateja pia kuheshimu mtaji hakuna mganga wa kukupa mafanikio ktk biashara yako.

Tuliza akili omba Mungu ni upepo tu usipagawe bado mapema and by the way nimekuwa nakusoma soma humu hutaki kuowa wewe ungekuwa na watoto unapeleka shule saizi ungekuwa ushatoboa kwa njia nyengine maana ubongo ungeuchangamsha zaidi ya hapo.

1. Nina watoto wawili wako Shule...
Mmoja darasa la 3 mwengine kaanza la kwanza.

Wote wapo Dar wanasoma Private, Kazi yangu ni kutuma ada na school bus fees.

2. Nisiende kwa waganga ila NIMUOMBE MUNGU 😳😳😳😳
MGANGA huwa anamuomba nani?

Nakumbuka nilisoma mwaka wa 1 bachelor kwenye foundation of Faith (African religous Vs. western religoous facts).

Anyway MUNGU YUPO.

#YNWA

#YNWA
 
Huwezi kuwa huna makosa, kupiga zumari humu na kuwahamasisha watu kwenda kinyume na mfumo wa maumbile na kuishi kama wanyama kupandana na kila anaetokea mbele yako ni kosa tosha.

Sijaelewa....

Hayo uliyoandika Yana uhusiano gani na Biashara yangu?
NB:- Madhambi yangu anaihukumu biashara, "Business is separate legal entity" Kwani Allah halijui hili?

#YNWA
 
Hali yankawaida kwa january. Sababu za kushuka

1. January.
2. Bei za mshindani wako na yeye unaweza amecopy kupaste mshindani wako.
3. Unaweza ukongeza coverage ya wateja wako kama unausafiri. Kama ulikuwa unauza urefu wa km1 toka dukani kwako ongeza 2km
Mkuu jibu la swali lako liko hapa wala usiangaike kwenda kwa waganga watakulaghai na kukufilisi zaidi.
Mwezi wa January ni changamoto kwa watu wote.
Huu mwezi wa January wateja huwa wamevurugwa, wanapunguza matumizi kutokana na stress za kulipa ada za watoto wao na kulipia kodi.
Kuwa mvumilivu uangalie trend ya mwezi February na March utapata majibu sahihi.
 
umezidiwa kete..

chunguza waliokuwa wateja wako siku hizi wananunua wapi mzigo.

ukishajua wanaponunua anza kufatilia ulipozidiwa, yawezekana huko walikohamia kuna bei rahisi.

biashara ni kuchunguzana, ulipokuwa unapiga hizo pesa tayari kuna wazee wa fursa walishaanza kukuchunguza wametumia mwanya, yawezekana wafanyabiashara baada ya kukuchunguza wao wanauza bei ya chini kuzidi wewe, wanafanya delivery mpaka usiku, wapo location inayofikika kirahisi, n.k. na pia inawezekana ni vijana wako wa hapo hapo dukani nao wamejiongeza wamefungua vistoo vyao bubu wateja wakija wanawapeleka huko.

ukichunguzwa na wewe wachunguze, tit for tat !! tatizo wengi wanapokosea huwa wanaacha uchunguzi biashara ikianza kumeremeta, mda huo umerelax kuna watu wanapanga mikakati, kuja skustuka chali wateja washahama.

Kiukweli hata mimi niliyeishia form 4 unanipa mashaka hio elimu yako uliyosomea mpaka masters unashindwaje kuitumia.
 
Sijaelewa....

Hayo uliyoandika Yana uhusiano gani na Biashara yangu?
NB:- Madhambi yangu anaihukumu biashara, "Business is separate legal entity" Kwani Allah halijui hili?

#YNWA
Siijui imani yako na sihitaji kuijua ila kwa tunaoamini ktk hizi imani tunaamini kama kipato kinachotokana na kazi fulani kama biashara kuajiriwa etc hakitumiki vizuri mirija inakatwa.

Kama hela unanywea pombe hovyo,ukinywa unaokota okota wanawake hovyo hela unanyanyasa nayo watu haiwezi kuwa na baraka hata kama siyo Mungu nature ya utu inakataza hivyo so angalia pia ktk hizo angle

Sikulazimishi kuamini lakini.
 
Usilazimishe nature ifanye kwa your willing.
-5789484382090803414_120.jpg
-5789484382090803414_120.jpg
20210717_171641.png
FdqJzYnWYAA3SqK.jpeg
1183fabd7d714ca8ace54a2e3b7a4ba1.jpg
 
Naungana na wadau wanaosema kuwa mvumilivu na ulisome soko la miezi kadhaa ijayo.

Biashara kuflop sometimes ni kutokana na tabia za wateja, wateja hupenda machimbo mapya na hupeana habari juu ya machimbo mapya siku zote. Sio siku zote huwa ni makosa ya mfanyabishara.

Kuhusu cha kufanya mie mwenyewe sina cha kushauri.
 
Back
Top Bottom