Nikiweka fixed deposit 10M naweza kulipwa kiasi gani na bank kila mwezi?

Sijaweka hela huko ili nifanye biashara na UTT..nimehifadhi ili biashara yangu itakapokaa vzr nitoe hela huko niingize kwny mzunguko. Hiyo 10m nimeipata kwny hiyo biashara yangu ambayo kwa sasa haifanyi vzr.

Tuelewane hapa: sifanyi biashara inayoitwa UTT. kule nimehifadhi km tu benki sema benki hawana tija ukifananisha na UTT. Nfkr nimeeleweka. Over
Wenye hela za mawazo tunapenda sana kujifanya washauri kwa wenye hela kweli kweli
Yani anaona kila mtu yupo kwa ajili ya kufungua baro za mtumba mabanda ya chips na kununua bodaboda

Kitu cha kwanza alitakiwa ajiulize wewe hiyo million 10 umepata wapi na ushauri wake hapo.

Mtu anasema uvivu wa kufikiri kuweka 10M UTT wakati katika kuchangamka kwake kote unakuta hajawahi weka hata 5M kwa pamoja.

JF kuna ujuaji mwingi sana mzee.
 
Na kila siku hua nawauliza Hawa wanaoponda kwmb mtu amefikishaje Milioni 10 km sio mfanyabiashara mchapakazi?
 
Na kila siku hua nawauliza Hawa wanaoponda kwmb mtu amefikishaje Milioni 10 km sio mfanyabiashara mchapakazi?
Humu JF kuna watu wanapenda kuwaingilia sana watu mkuu na una moyo sana kuwajibu kila siku

Kuna wakati Biashara hazisomi mtu unakaa pembeni wao wanakuja na ushauriiii.

Halafu watoa ushauri karibu wooote ushauri unafanana bodaboda, banda la chips, nunua mpunga, forex, weka odd 2.

Unajua hawa watoa ushauri waganga njaa wenzangu.
 
Watu binafsi wanapokea ndio na kima cha chini inategemeana na mnada wa hisa zao kwa wakti huo. Ila hata 500k unaweza kuweka ingawa return itakuwa ndogo sana labda uwe unafanya kama uwekezaji wa muda mrefu sana.

Kila ijumaa wanatoa seminar kwa wanaohitaji kufahamu mambo ya uwekezaji kwenye hati fungani zao,kawasikilize mkuu.

Semina inafanyikia wapi?
 
Kwanini uweke kiasi kingi hivyo cha hela Bank? Huko utapata faida kama ya 1% kila mwezi au 10% kwa mwaka, ambayo naamini kama ukiwekeza hiyo hela kwenye uwekezezaji wowote mzuri unaweza kupata hela zaidi ya hiyo. Nenda hata maeneo mapya ambayo yameshakuwa ya uswahili kutokana na population ya watu kuongezeka, nunua kiwanja hata kwa 1M kisha jenga vyumba viwili, sebule, jiko na choo ndani kisha pangisha huwezi kukosa 200,000 au zaidi kwa mwezi na bado utakuwa na nyumba. Biashara zipo nyingi za kufanya kukuingizia kipato kikubwa hadi 1M kwa mwezi kwa hela hiyo. Wekeza, wekeza, wekeza na sio kuweka akiba!!
10 Milion Unaweza Jenga Vyumba 2 , Sebule , Jiko ,Choo ?
 
Hamna mtaji wala hela inayoongezeka ni ufinyu tu wa maarifa yako ya maswala ya fedha ndio inakufanya uone hivyo,Uki weka hiyo 100M kwa malipo ya 750K kila mwezi-hiyo unayolipwa ni thamani ya kiasi ambacho hela yako inapoteza thamani kila siku ikiwepo huko.
Huyo ni wakala wa UTT

Kingine watu hawaelewi kuwa thamani ya pesa yetu imeshuka sana mwanzo mwaka jana dollar ililiwa 2360, leo ni 2425
 
Naombeni msaada?
Je utt liquid fund ina gawio kwa kila mwezi kwa mwekezaji? Au ni lile ongezeko la thamani ya kipande pekee?.Na kama kuna gawio linaanza kwa mwekezaji aliwekeza kiasi gani cha fedha?
 
Millioni kumi. Tafuta chuo kikuu haps dsm chenye demand kubwa ya wanachuo , angalia eneo zuri ununue ujenge vyuumba vya kupsngisha wanachuo tena kama ukipata eneo la million 3 , ukajenga vyumba 15 (au ndan yake 6 ni self) ukaongezea pindi ikipelea ,,aseewe hiyo investment itazalisha hela Vitukuuu na vining'ina....
 
Eneo lililokaribu na chuo kikuu liuzwe million 3?
Lenye uwezo wa kujenga vyumba 15?
Self contained bedroom 6?

Nyie jamani Nyie mbona mambo ya kufikirika haya.
 
Back
Top Bottom