Nikiongea na wanawake, naambiwa mimi ni mkali sana nisaidieni

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari za wakati huu..

Wakuu kila nikiwa na mazungumzo na wanawake wananiambia mimi ni mkali sana na ninaongea kwa msisitizo sana.. sijui tone ya sauti yangu imekaaje napo ongea nao japo mimi najiona wa kawaida tuu na naongea kawaida sana...

Wana nambia naongea kwa ukali sana na msisitizo sana, na nipo serious sana mpaka wanaogopa sana, jambo ambalo na waambia mbona nipo kawaida sana ila hawataki kuamini kabisa.

Hii hali imeniletea hadi utata kwenye kutongoza ndugu zangu, nilikua naipuuza ila inaleta utata sana . Hata mwanamke nae mtongoza akinisikiliza na kuniangalia usoni anasema hivyo hivyo kua naonekana serious sana na mkali sana. Sasa sijui ni pepo lime nivaa au ni nini wakuu.

Wakuu nielezeni ni fanyaje hii hali initoke
 
Tupia hapa short voice ukiongea umuhimu wa JF kwenye Afya yako ya Akili..au Umuhimu wa Social media

Kisha kwa Wanawake tulio hapa tutakusikiliza na kuona kua kweli unalo hilo tatizo au la

jjs2017
Niwazo zuri sana ila sauti yangu inajulikana sana na watu wengi kwa sasabu na hudumia jamii kubwa kwa siku , hivyo na kutana na watu si chini ya 500+ katika kazi zangu za kujitafutia kipato. kuiweka hapa haitokua vizuri kwa upande wangu wa faragha.

Ila Asante
 
Habari za wakati huu..

Wakuu kila nikiwa na mazungumzo na wanawake wananiambia mimi ni mkali sana na ninaongea kwa msisitizo sana.. sijui tone ya sauti yangu imekaaje napo ongea nao japo mimi najiona wa kawaida tuu na naongea kawaida sana...
Uliza wanaokuzunguka, waombe ushauri wa kweli sio wa kuficha ficha.
Kama na wao wanasema ni ya kawaida, basi huna haja ya kujitetea kwa mwanamke yoyote.
Ila akikuambia upo serious sana japo unajiona kawaida mjibu ndio nipo serious sana mpaka mzee Magu alinipa tuzo nimeibandika ukutani kwangu chumbani.
 
Back
Top Bottom