Stories of Change - 2023 Competition

sideuka

Member
May 18, 2023
5
5
Maisha ya siku hizi yamegubikwa na vitu vingi sana ambavyo kiuhalisia vinaficha uhalisia wa maisha yetu waafrika, Ninaweza kusema kuwa haya ndiyo maendeleo lakini isifike mahali tukasahau kabisa tulikotoka na kuuvaa umagharibi moja kwa moja katika chapisho hili ninakwenda kuikumbusha jamii baadhi ya vitu ambavyo vimesahulika na baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kurekebishwa na kukumbushwa, Neno mwanangu katika chapisho hili linawakilisha watu wa jamii ya kiafrika karibu katika kuongeza maarifa.

Mwanangu kwanza tambua Dunia saizi imeoza mwalimu wa Dunia amekuwa kipofu anafundisha huku akiwa haoni kile anachofundisha kinatoa matunda yake au la! Yeye anasema atakae elewa ameelewa na asiyeelewa hajaelewa, pia nikukumbushe saizi mama afundishi unafundisha ulimwengu yaani ule msemo walio usema wahenga yakwamba asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu sasa ndio upo kazini katika siku za maisha yako mama hana nafasi yakukufunza wewe isipokuwa ulimwengu.

Niamini baba ako nakuambia siku za maisha yako hakimu wa maisha yako ni kichwa chako kwa sababu siku za maisha yako wanasema ni siku za utandawazi, hapo sasa naweza sema kuwa aliyetunga msemo wa macho hayana pazia alifaulu kwakuwa siku za maisha yako utaona vingi ambavyo hukupaswa kuona. Mwanangu enzi za utoto wangu baba yako mtu akifariki watoto tulikuwa tunafichwa ndani tulikuwa tukiambiwa kuwa tukichungulia nje tutaliwa na samba au jini, pia tuliambiwa tukipita malaloni/makaburini tuangalie pembeni kwani tukiangalia makaburi tutakatika kidole gumba hivyo ilikuwa sharti ujikang`ate dole gumba ili kuzuia kidole pale inapotokea bahati mbaya umeangalia makaburi.

Lakini siku za maisha yako unavijua vingi ambavyo hata baba yako sifikirii kama unavijua, vitu vingi ambavyo unavifahamu mwnangu kwa siku za maisha yako ni laana kwa siku za maisha ya baba. Nahisi huenda kuwa bado hujanielewa lakini naomba utumie akili na utashi wako katika kuelewa kile ambacho ninahitaji uelewe, kwanza fahamu walimu wako ni walimwengu na sifa kuu ya walimwengu ni hii Hata kama ukafaulu kwa asilimia tisini naukafeli kwa asimia kumi walimwengu watahesabia kuwa umefeli kwa asilimia mia hapo sasa ndio unaambiwa zakuambiwa changanya na zako.

Kwa siku za maisha yangu mwanangu ilikuwa nirahisi sana kuishi kwa sababu heshima kwetu ilikuwa katika utu na heshima lakini siku za maisha yako ni ngumu kuishi kwa sababu ili mtu akusaidie nilazima uwe na pesa utu na heshima vipo nyuma wakati sisi pesa ilikuwa nyuma ngoja nikukumbushe kidogo si unajua pesa ndio iliyomfanya nabii yetu Yesu asalitiwe na pia unakumbuka pesa ndio iliyomfanya delila amuuze samsoni kwa wafilisti?

Mwanangu pesa sio mbaya lakini ubaya unakuja pale unapoweka tamaa kwenye pesa, siku za maisha yangu pesa zilifananishwa na shetani lakini kwa siku za maisha yako pesa zinafananishwa na sabuni ya roho.

Siku za maisha yangu nilikuwa nikisafiri nilikuwa sina haja yakuandaa pesa yakulalia katika nyumba ya wageni kwani ilikuwa ni rahisi sana nabisha hodi nyumba yeyote kisha najieleza mimi ninaitwa Davidi msigwa natokea wilayani Soje Kata ya kijafa tafadhari naomba hifadhi ya usiku waleo na wenyeji walinihifadhi lakini siku za maisha yako ukiwa mgeni mahali huongei na mtu kwanza unaongea na mabango kisha unaishia kuongea na kitabu cha wageni na mwisho kabisa unamalizia na matumizi ya pesa.

Nakuasa sana mwanangu kuwa makini na walimwengu na wewe epuka kuwa mlimwengu achana na wanaosema sheria duniani haki mbinguni, wewe anza kutenda haki ukiwa duniani ili ukifika mbinguni ukapewe mamlaka achana na wanaohitaji haki ya mbinguni mwanangu usione hasara wewe ukose ili kumi wapate maana walimwengu wanapenda kuwa wao wawe wakwanza na wengine wafuate wewe angalia ikiwa ni haki yao wawe wakwanza basi waache wawe wakwanza usitake kupata kitu bila ya jasho mwanangu simaanishi kuwa usiwe unapokea zawadi hapana ila naomba uwe makini na kile kitu unachokifanya epuka rushwa kwani ilikatazwa toka enzi za mababu zetu.

Naomba usiwe kama mvuta sigara anaetembea na sigara bila kibiriti, kila unachopanga naomba upange vyema maana walimwengu wanapenda kukuona ukifeli mwanangu elewa hivyo mwanangu, ukifanya jambo na ukafeli walimwengu watakuambia wewe si wakwanza kwani hata aliyevumbua pesa alikufa kwa madeni, watakuambia maneno mengi ambayo yatakufariji ukikaa nao lakini mkiachana wanakucheka au usiwe kama wanafunzi ambao wakivaa sare wote wanaonekana wapo sawa lakini wakirudi nyumbani kila mtu anavaa magwanda yake mpaka wengine huona bora washinde na sare za shule mda wote ili wasijulikane kuwa wanamaisha magumu.

Nina vingi vya kukuambia mwanangu ila kabla sijaendelea mbele naomba nikuambie kuwa zingatia mlo sahihi na sio kila kitu kitamu basi ndio kinajenga mwili kuna vingine vitamu lakini ni sumu kwenye mwili penda sana kula vyakula vyenye faida kwenye mwili wako ukifanya hivyo nauhakika kuwa hata wajukuu wangu watakuwa rijali kama ulivyokuwa baba yao, nasema hivi sababu najua mpaka wewe kufika umri huo nilikulisha nini na ndio maana una akili timamu, penda sana vyakula vya asili achana na vyakula vyakiwandani akija mgeni kwako mlishe kile unachokula wewe sio kile anachotaka yeye akija mchinjie kuku na ugali wa dona.

Muepushe mke wako na vikao vya akina mama wenye lengo la kuharibu mahusiano ya watu hasa pale ambapo wanapoona kuwa mnasonga mbele mpe misimamo thabiti juu ya maisha yenu na sio juu ya maisha yao, penda kujamiiana na jamii acha kujitenga mwangu ukijitenga utakuwa chuya. Na kama ujuavyo chuya katika mchele hufanya mchele kuonekana mbaya hata kama kuna chuya kumi katika mchele kilo moja.

Huu ujumbe nakupa mwanangu lakini ukiona umekufaa mpe na wenzio maana nimesikia watu wanasema kizuri kula na mwenzio hivyo sio mbaya kama nawewe ukawapa wenzio wasome kile nilichokupa baba yako ili nawao watoke kwenye kiza cha walimwengu na waje upande wapili wakula wali na sio walimwengu maana walimwengu ni wabaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom