Nikaenda kumzika ibilisi wangu....!

Mtambuzi ulikuwa huna haki miliki ya kazi zako mkuu hii huku imeibiwa no copyright
 
Last edited by a moderator:
Chenge,
Hii story ni ya kweli kaka? Ulisema somewhere kwamba ulikwenda kupima DNA kule South Africa. Unaweza kuelezea kidogo hilo la kupima DNA?
Asante
 
Pole sana Mkuu lakini naamini Mungu yu mwema kaza buti angalia mbele ipo siku utayasahau yote. Kubwa hapa ni funzo kwetu tuwe na tahadhari wakati wote.
 
Pole sana ndugu yangu, popote tulipo yupo pia ibilisi na ndiyo chanzo cha MAOVU yote haya, yote mwachie Mungu, kwani yeye hujidhihirisha kwetu wanadamu na kutupa mafunzo kwa njia mbalimbali. Mungu aliona atumie njia hii aweze kutufanya tuamini kwambe yeye ndiye Mungu na ndiye mweza wa yote. Yote Mwachie Mungu. Mzee wa Kale.
 
sasa hiyo ni hadhithi au ni ukweli? Au simulizi la kwenye riwaya, mh kama ni kweli pole sana kwa mapigo yoote uliyoyapata. Ila tafuta mupenzi wa kukuliwaza tuu ila urimpende saaana na kumuamini kama ulivyofanya kwa mkeo maana bila hivyo utakua mtu wa majonzi kila 7iku poolée samehe tuu.4
 
Inasikitisha..na inaakisi uhalisia wa ndoa zetu ambazo kwa juujuu tunataka ionekane ni yenye furaha na uaminifu mkubwa lakini sirini ni ndoa zilizosheheni usaliti, unafiki na uzinzi uliokubuhu tena kwa pande zote: kikeni na kiumeni.
 
Duuuuuuuu!!!!!!!!!!!

Kila kona mambo haya yapo. Yanasikitisha sana!!!!

Ndio maana kuna usemi

"Maisha ya Ndoa ni sawa na Bahari kwani kuna mawimbi mengi, na samaki wakali mno"

"Tulio ndani ya ndoa tunatamani kutoka, na walio nje ya ndoa wanatamani kuingia"

"Maisha ya ndoa ni matamu na chungu"



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Duuuuuuuu!!!!!!!!!!!

Kila kona mambo haya yapo. Yanasikitisha sana!!!!

Ndio maana kuna usemi

"Maisha ya Ndoa ni sawa na Bahari kwani kuna mawimbi mengi, na samaki wakali mno"

"Tulio ndani ya ndoa tunatamani kutoka, na walio nje ya ndoa wanatamani kuingia"

"Maisha ya ndoa ni matamu na chungu"



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Baadhi ya wanawake ni wanyama kabisa! mi sioi karibuni hadi nizeeke!
 
Pole mkuu
Ila hapo kwenye aina ya gari NISSAN PAJERO itakua wakati unaandika majonzi yalikua mengi kupita kiasi
 
Kwenye mahusiano niliyoko mpaka sasa na mpenzi wangu ambaye soon tutafunga ndoa(miaka minne sasa), nilishamfumania na message kama hizo kwenye simu yake. Kusema ukweli mpaka sasa nina kidonda kikubwa sana moyoni.

Mara nyingine nahisi uchizi nikijiuliza, kwanini aliamua kufanya hivyo? But yote namuachia Mungu as long as anaelewa hatari ya kudanganya,,, ni kifo cha aibu(UKIMWI etc) na pia Jehanam.

Mungu atuongoze
 
Mkuu mtambuzi hapa napata shida kidogo na huyu mwanaume..hivi kweli uko na mke wako kwa karibu miaka nane sasa yet unasema kuna droo ambazo yeye hakuruhusiwa kufungua..i mean hakuwa na access nazo na kuwa mkewe alikuwa akizificha bila yeye kujua zilipo na bado akawa ameridhika kwa muda wote huo...under normal circumstances na kama kweli kwa jinsi alivyosema walikuwa wanapendana mno na kuaminiana that was IMPOSSIBLE situation as far as real love is concerned!!!Huyu anatudanganya nadhani walikuwa wanaishi kila mtu kivyake..hakuna kushika simu yangu na wewe sishiki yako..ntakachokifanya usinifuatilie..that's the kind of life they were living...otherwise the whole story ni HADITHI and not the TRUE STORY. Pia najua mwanamke asingeficha barua kama zile ndani ya chumba angekuwa akizisoma then anazi destroy hapohapo...mana zilikuwa hazina ulazima wa kuwepo kama kumbukumbu..lbda vitu kama hati ya nyumba nk ndo angeweza ficha chumbani..otherwise hii ni hadithi ya KUSADIKIKA!!!!!!
 
Nilizoe kusoma mikasa ya mapenzi,kwenye simulizi za magazetini,vijarida na vitabu.siku moja nikiwa mkoa fulani ,niliamua kumtafuta rafiki yangu ambaye tulipotezana kwa muda kidogo baada ya kumaliza chuo.Nilipompigia simu alifurahi sana na akanihimiza nifike haraka sana nyumbani kwake.siku hiyo nilikua niko na jamaa yangu mwingine.Basi tulipofika nyumbani kwake nikamkuta yuko na jamaa mwingine, wote walikua wanyuka suti maridhawa.Lakini hali ilibadilika ghafla, siyo kama vile tulivyoongea kwenye simu,kwani yule jamaa mwingine alikua mnyonge sana.Ndipo ikabidi niulize kulikoni?

Mwenyeji wangu akafunguka kuwa muda ule walikua wametoka kanisani, na yeye akiwa Bestman lakini Bibi harusi alikua Kala kona.walijitahidi kumtafuta bila mafanikio."Nilipigwa butwaa kwani nilizoea hadithi kumbe huwa inakua kweli"Basi kama kawaida ikabidi tuanze na kufarijiana na busara za uongo na ukweli zilitawala.Yule jamaa alikuwa ni mwl na mwezi huo ilikua aende UDSM kujiongezea shule,lakini kutokana na pilikapilika za ndoa, na maisha mapya aliamua kuahirisha shule yake hiyo.Kitu nachokumbuka kumshauri,ni kwamba 1:Ajikubali kwamba imemtokea kwani ndio hatua moja wapo ya kuanza upya maisha.2:Ilikuwa imebaki wiki moja chuo kufunguliwa-hivyo nilimshauri ajaribu kuwasiliana na uongozi wa chuo kama wangemruhusu aendelee na chuo,kuliko kuendelea kukaa pale mkoani.

Nilipiga zangu castle zangu, na baadae nikaaga.Kwa jinsi tulivyoongea na yule Bwana,akapenda tuondoke wote kwani na yeye alitaka kurudi nyumbani.basi tuliondoka wote,kufika sehemu tukaona kijiwe, ikabidi niombe tupige mbili tatu,na ikawa hivyo.nilifanya hivyo ili kuwa na uhakika kuwa yule bwana akitoka pale,asiende kujitundika,kwani ningehuzunika sana kwa kutomsaidia.Tuliendelea na maongezi mpaka nilipoona ile hali yake ya huzuni iliyopitiliza imemtoka.
Ndipo tuliagana na huku akitushukuru sana,kwani alisema alikua kachanganyikiwa sana,lakini kwa wakati ule atleast alipata mwanga wa wapi pa kuanzia maisha yake mapya.

Baada ya siku mbili tatu tukapata taarifa yule Bibi harusi alitoroshwa na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye aliokuwa amewasili toka SA.Hakuonekana pale mkoani kwa muda wa miezi yapata mitatu.Then kuna siku,nikiwa na jamaa yangu mmoja, tulipishana na binti mmoja mtaani.jamaa yangu akaniuliza kama namfahamu nikamwambia hapa.Ndipo aliponifahamisha kuwa huyu ndio yule binti,aliyeingia mitini wakati wa harusi,nilimuangalia huku tukipishana,nikijaribu kumkariri ili siku nyingine asije akamkimbia mtu mwingine mbele ya macho yangu.

Baada ya miezi kadhaa ,aliyekuwa anapaswa kuwa Mpambe wa bibi harusi nikapata taarifa kuwa kapata ajali na kufariki.Nilisikitika sana kwani nilikua nikimfahamu yule biti,huku wakati tukio hili likiendelea sikua nimejua kuwa yeye ndie aliukua mpambe wa BIBI HRUSI wetu.

Na simulizi yangu ndio inaishia hapo.

Dingi swayo,nakuomba tu ufuatilie hizi simulizi na kujifunza kutoka kwa yaliyowatokea wengine.Ila usiombe ikakukuta wewe,siku hiyo naamini utavaa kaptula kichwani.Kwani inaweza kukukuta kwa stahili tofauti.Na pia ujue haya matukio hutokea pasipo kujarajia.
 
Mtambuzi always u made ma day, Thx kwa hii simulizi,pamoja na fundisho la uaminifu lakini hutakiwi kuusemea moyo wa mtu aise, kilicho moyoni mwa mtu ni siri yake mwenyewe.

Mimi simuamini mtu yeyote, hata babangu namwamini Mungu peke yake tu
 
Baadhi ya wanawake ni wanyama kabisa! mi sioi karibuni hadi nizeeke!

Hatuwezi kukwepa kuoa, lakini yatubidi tusiaminiane kisaaana.

Na inakuwa mbaya zaidi pale unapofanyiwa hivi na mtu unayemuamini na kumpenda.

Waweza kutafuta kamba na kujining'iniza.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom