mr pipa
JF-Expert Member
- Jul 26, 2021
- 2,330
- 4,854
Kwanza niseme mimi ni baba mwenye mke na watoto, ni mfanyakazi wa Serikali katika kitengo cha ulinzi na usalama ambacho jamii yangu inayonizunguka hawaelewi ninafanya kazi gani mpaka sasa maana wanaweza nikuta nusu ya mwezi ni nyumbani halafu nusu yake huwa sionekani nyumbani hivyo inawafanya wawe na maswali na kuniuliza wanashindwa sababu sijajenga mazoea na mtu mzima,
Tukiacha hilo tuje kwenye mada, nimekuwa mtu wa tofauti kidogo hasa likija suala watu wa kupiga nao stori, muda wangu mwingi huwa natumia kupiga story na watoto kuliko watu wazima wenzangu, yaani ni rahisi sana hata nikiwa ugenini, kumzoea mtoto, kuliko mtu mzima mwenzangu na hii imenifanya mtaani ninapoishi kujulikana zaidi na watoto kuliko watu wazima
Sasa jamii kidogo imekuwa ikinihisi tofauti kama mimi ni mshirikina hata mali nilizonazo napata kwa njia za kuchukua nyota za watoto, nimejitaidi kuacha mazoea hayo ila niseme nimeshindwa mana kuna muda watoto watatoka majumbani kwao na kunifuata pasipo mimi kuwaita
Wakuu msaada wenu