Ni Wendawazimu kujificha kwenye Kichaka Cha Dini. Ni kupoteza Uelekeo na kufunika Kichwa Ardhini Ukidhani wenye akili Hatukuoni

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,728
12,129
assalaam alaikum wa rahmatullahi wabalakatuh... huu naandika nikiwa nimekasirishwa na matukio ya watu kadhaa kuamua kujificha katika dini ili kudendeleza tabia cao chafu za njaa, unafiki na chuki. ni aibu kuwa sasa hivi kama Mtu atamkosoa Rais Samia itadaiwa ni sababu ya Dini yake. Huu ni upumbavu wa hali ya juu sana. Waliokuwa wanamkosoa Magufuli walikuwemo Wakristo wengi hadi wa Dhehebu lake. hawakuangalia wala kuzungumzia dini au dhehebu lake.

walimwangalia Magufuli kama binadamu mwingine yeyote yule. wanakuja wapumbavu wanataka mtetea Rais Samia kwa kigezo cha Dini na si utendaji wake halafu na sisi tunajifunika Shuka hilo hilo lenye chawa na kunguni ndani yake tukiamini kuwa litatusitiri kwa muda mrefu. Huu ni wazimu, huu ni wendawazimu

mimi si Mkristo. ila siwezi bebwa na ujinga huu wa baadhi ya watu kutetea viongozi kwa minajiri ya Dini zao. Huu ni upuuzi wa kiwango cha hali ya juu ya mwisho kabisa katika SIasa. kiongozi ambaye anaaamua kutumia Dini, Kabila au Kanda katika siasa zake ni mtu ambaye tayari ameshaishiwa sera. hana mwelekeo ameshapotea hana mbele wala nyuma sasa anatafuta huruma ya wanadini,kabila au kanda yake kumbeba. huyo ni Mchawi, Jambazi, Gaidi, Shetani, Jini na Mchafu kuliko aia yoyote ya uchafu. hawana tofauti na ndege ambaye anajificha kwa kufunika kichwa ardhini na akiamini haonekani.

Mimi nilikuwepo katika watu ambao tuliambiwa "Huyu ni mwenzetu" na ninafahau harakati zote ambazo zinafanyika kwenye vikao vyet. nafahamu hawa wanaoambiwa wasiache kumtetea kwenye mitandao na majukumu waliyopewa kwa kigezo cha Dini. nakataa kutumika kama Zuzu, Zezeta , Zombie, Msukule na Zebwe. NItakataa na kumkataa Shetani na mambo yake yote akiwa katika rangi na mavazi yoyote yale.

vya kwanza kuundwa vilikuwa vidole kisha watu wakaunda Uma. Iliumbwa Tanzania kwanza na watu wake then wakaja watu na Dini zao kutengenisha watu kwa minajiri mbali mbali . tufuate Dini ila tusiache akili nyuma. Huu utakuwa Wendawazimu wa Kiwango cha PHD kabisa.

wabillah tawfiq.
 
Back
Top Bottom