Ni wazi sasa CCM imewabana CHADEMA bungeni

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Sijui huu ni mkakati Maalum wa Spika Dhidi ya wabunge wa Chadema na wapinzani?
ktk hotuba ya bajeti inavyoendelea utagundua kuna mkakati umepangwa na CCM dhidi ya wabunge wanaonekana wanazungumza sana kwa ukali kutoka chadema.

Mbunge wa Chadema akimaliza kuchangia, ameandaliwa mbunge maalum wa CCM kwa kazi maalum na anaelingana sifa za maneno na kejeli kama alivyo wa chadema.
Kwa mfano, alipomaliza Lissu akaja Mchemba. na sote tulivyoona
alipomaliza kafulila- Akaja Lisinde. na kila mtu aliona jinsi ya Lusinde alivyombana kafulila huku Naibu SPika akicheka na kumrudisha Lusinde kurudia kauli yake huku akidai hajasikia.
alipotaka kumaliza Mnyika, kaandaliwa Mbunge machachari wa Mara.
Akimaliza Msigwa. unaweza ukaona nyuma yake yupo mbunge mwengine wa CCM anaelingana kwa kejeli na vijembe bungeni

nadhani jinsi ya wachangiaji wa Chadema walivyopangwa. basi nyuma kuna beki aliepewa kazi ya kukaba. na Mpaka sasa washambuliaji wa Chadema wamekwama
 
Good analysis wabunge wa chadema wanachangia bajeti ya serikali wabunge wa CCm wanachangia bajeti ya chadema,sijui aliyekwama ni yupi
 
Hukumu ni 2015 Wananchi tunafahamu vyema ni nani yupo upande wa Wananchi na ni nani yupo upande wa Chama. 2015 tutatoa Hukumu za haki.
 
Ila uzuri hii TBC inaonekana maeneo mengi nchini kwa sasa. So wananchi ndio waamuzi na watekelezaji.
 
Na huo ndio udhaifu wa wabunge wa CCM. Wanajipanga kupambana na wabunge wa CHADEMA, badala ya kupambana na bajeti mbovu.

Rais amekuwa Dodoma kwa siku kadhaa, sijui amewatishia au ametumia mbinu gani lakini wabunge wa CCM wanaonekana kutoelewa bomu lililopo kwenye bajeti. Wataipitisha na hapo ndipo watajikuta wamewapa CHADEMA mtaji mwingine wa kuwamaliza nje wa bunge. Hii bajeti imejaa madeni.
 
kwa hiyo dawa yao imeshapatikana????
hyo ina maana CCM ina majembe sema tu ilikuwa haiyatumii
 
wabunge wa sisiem ni waoga, bajeti isipopitishwa rais a.k.a dhaifu atalazimika kulivunja bunge je unategemea likivunjwa bunge kuna mbunge wa sisiem mwenye uhakika wakurudi mjengoni?kazi yao nikuzomea waone:fear::fear::fear::fear:
 
Mbona bunge lililopita Dr Slaa alijizolea umaarufu mkubwa kwa wananchi,hii ni kwa kuwa alikuwa anajenga hoja sio kucheza ngonjera kama hizi za kina mnyika
 
Back
Top Bottom