Ni wazi sasa CCM imewabana CHADEMA bungeni

Yan wanapopitisha bajeti kama hile ni wazi wanamsaidia dhaifu jk.
 
ushindani bungeni ni hoja sio vijembe na taarabu.wabunge wetu kwa sasa hawana hoja wanaimba tu taarabu

Wabunge wa ccm wametishiwa kama bajeti haikupita rais atavunja bunge na kuitisha uchaguzi! Uroho wa madaraka na kiwango cha juu cha usaliti ndicho kinachoendelea sasa hivi Dodoma. Lakini hakuna shida, bajeti itapita, makampuni makubwa yatalindwa, na wapambe wengine wataendelea kutumbua nchi. That's CCM.

2015
 
Sijui huu ni mkakati Maalum wa Spika Dhidi ya wabunge wa Chadema na wapinzani?
ktk hotuba ya bajeti inavyoendelea utagundua kuna mkakati umepangwa na CCM dhidi ya wabunge wanaonekana wanazungumza sana kwa ukali kutoka chadema.

Mbunge wa Chadema akimaliza kuchangia, ameandaliwa mbunge maalum wa CCM kwa kazi maalum na anaelingana sifa za maneno na kejeli kama alivyo wa chadema.
Kwa mfano, alipomaliza Lissu akaja Mchemba. na sote tulivyoona
alipomaliza kafulila- Akaja Lisinde. na kila mtu aliona jinsi ya Lusinde alivyombana kafulila huku Naibu SPika akicheka na kumrudisha Lusinde kurudia kauli yake huku akidai hajasikia.
alipotaka kumaliza Mnyika, kaandaliwa Mbunge machachari wa Mara.
Akimaliza Msigwa. unaweza ukaona nyuma yake yupo mbunge mwengine wa CCM anaelingana kwa kejeli na vijembe bungeni

nadhani jinsi ya wachangiaji wa Chadema walivyopangwa. basi nyuma kuna beki aliepewa kazi ya kukaba. na Mpaka sasa washambuliaji wa Chadema wamekwama


Hakuna kitu hapo. Wanachofanya CCM ni kama kwenye mpira timu inacheza deffeceve bila kushambulia. Kila mpira ukija wanatoa kona au wanasababisha free kick au penalt. Matokeo yake watafungwa goli jingine baada ya lile la jana na mshambuliaji machachari Mnyika.
 
Mbona bunge lililopita Dr Slaa alijizolea umaarufu mkubwa kwa wananchi,hii ni kwa kuwa alikuwa anajenga hoja sio kucheza ngonjera kama hizi za kina mnyika
Kwa taarifa yako Mnyika kwenye medani za siasa tokea jana yupo juu kichizi mwaka huu wenu mtapiga yowe sana
 
mkuu kinachoonekana kule dodoma bungeni ni kuwa hakuna mjadala ila wako kwa ajili ya kujibu mapigo ya chadema.ila ninachoelewa ni kuwa mpaka itakapofika september 2012 mwisho wa bunge hili lazima chadema wataibuka washindi.nawashukuru sana chadema kwa kuongea point zenye maana sana na zinazogusa maisha ya kila mtanzania kuliko kuzungumzia mambo ya mipasho yanayofanya na watu kutoka kwenye chama kingine.
 
BUNGE LA KIISTAARABU LA CHIFU ADAM SAPI MKWAWA NA USHINDANI MKALI MIJADALA KWA NGUVU ZA HOJA' HIVI SASA NI JUKWAA LA WANAMIPASHO, WAIMBA TAARAB NA MIDOMO KAYA MIGUUNI MWAKE JOB NDUGAI

Mkuu 'Nipo Hapa',

Hakika inasikitisha kweli kweli kuona bunge linageuzwa kuwa soko la WAPIGA KELELE MAHIRI, walanguzi, na mizabizabina (Rweyemamu et al, Kurugenzi za Mawasiliano Magogoni, 2011) ambapo wenye HOJA ZA NGUVU, MIPASHO NA MATUSI hupewa nguvu zaidi na kiti cha spika huku wenye kukosoa bajeti kwa faida ya walalahoi wakikejeliwa na wakati mwingine hata kutupwa nje ya bunge.

Mpaka hapa wala si siri tena kwamba kwa mara nyingine baadhi ya wabunge wa CCMwameamua kwa makusudi kutugeuza WaTanzania walipakodi kuwa ni watu wa mzaha na kuchezewa ovyo tu jinsi mtu yeyote apendavyo ilmradi tu mbele ya jina lake kuna maaneno ya 'Mheshimiwa M<bunge' basi tu.

Naam, ndio kusema y kwamba ni nani aliyetarajia sehemu panapoitwa bunge kuweza kusheheni lugha zisizo na staha kiasi kile, je ni nani aliyetarajia kuona kiti kinachotarajiwa kusimamia U-Mwanana wa MIJADALA YA KISTAARABU NA USHINDAANISHAJI WA NGUVU ZA HOJA (na si hoja za nguvu) pale sebuleni pindi anapobadilika ghafla na kudondosha filimbi yake chini na kuanza kuwakabili vilivyo wabunge wa ushindani kwa mtindo ule tena kwa mshaangao mkubwa wa taifa zima????

Kama kuna kitu mwananchi wa kawaida anatafuta kusikia kutoka Bungeni Dodoma wakati wote ni jinsi gani Ugali utakavyoongezeka zaidi mezani kwake kutokana na mikakati murua kwenye Bajeti ya serikali. Hivyo, ni vema serikali kupitia bunge ikawapa sikio pana zaidi hasa wenye KUKOSOA BAJETI KWA LENGO LA KULIBORESHA ZAIDI kuliko kutafutaa kuwaziba midomo kwa mikakati ya kitoto kiasi kile cha kupanga KIKOSI CHA WAPIGA KELELE mbele yaake ili hoja yake isifue dafu.

Ni vema ikaeleweka bayana kwamba Bajeti ni mali ya serikali na wapinzani kwa pamoja hivyo kila anayezungumza anayo maslahi pale na wala si kuwaona wengine kuwa kama tishio vile kwa ajenda za KIFISADI kibao zilizofichwa ndani ya hii Bajeti ya Mgimwa'.

Ni wazi pia kwamba Bajeti isiopembuliwa KISAWASAWA mwisho wa siku hukosa kuleta tiza za ki-maendeleo kwa wananchi. Hali ya aina hii inapotokea siku zote husalimiwa na maandamano mengi, madai ya ufisadi na kero nyingine za aina hiyo.

Sasa kwa vile nguvu za hoja huonekana kupewa kisogo na wanamipasho kupata kuunganishiwa vipaza sauti zao ghafla tu kwenye amplifier ya Spika Ndugai pale mbele hadi hapo ni kwamba kwetu sie huku mitaani ni kwamb Bunge sasa lishaageuzwa kuwa kilabu cha pombe ki-aina vile.

Nasema hivi kwamba wala si utani kwamba Watanzania tuliowengi hivi sasa tunajihisi zaidi kuchukuliwa mzaha na sehemu kubwa ya wabunge wa CCM kwenye kile kinachotarajiwa kuwa ni JUKWAA RASMI NA LENYE KUSTAHILI HESHIMA TELE kitaifa na vile vile kuwa ni sehemu au kikao cha wastaarabu tupu Dodoma Bunge sasa kuwa kama kikao cha mapunguani vile kule Mirembe Hospital.

Na ni kwa maan hiyo hiyo hapo juu ndio maana vile vile nikaonelea kua ni vema huyu ndugu yetu NIKO HAPA naye akatuomba radhi wana-CHADEMA pamoja na wapinzani wote bungeni kwa ujumla wetu tena bila kusita. Sifa hizo ulizoziainisha hapo chini za VIJEMBE NA KEJELI hata siku moja hutozikuta kwa wabunge wa upinzani maana kamwe hatuna haja nazo wala haziongezei Mtanzania mhangaikaji unafuu wowote katika maisha yake.

Kimsingi, inashangaza tena sana kuona kuna MJADALA MZITO BUNGENI kuhusu NAMNA GANI YA KUBORESHA BAJETI YA TAIFA ili ikatufae zaidi sisi walipa kodi wa nchi hii na baadhi ya wabunge wa CCM (wapo wengine ambao ni waelewa sana mle tofauti na hao vilaza uliowataja wewe hapo chini) wakiendelea tu kuonyesha umahiri wao wa kugeuza mijadala ya kiwabunge wenye sifa hizo.

Lakini, yote juu ya yote, wapiga kura wa nchi hii UWEZO TUNAO wa kuondokana na wabunge wa aina hii siku za usoni ili kule Dodoma wapate kwenda tu wale wtu ambao wanajua nini sisi walipakodi tunahitaji kusikia kikijadiliwa kwenye bajeti pale sebuleni na wala si kuonyeshanga UMAASHUHURI KATIKA MEDANI HIZO aDIMU ZA nani-mjinga zaidi vile.


Sijui huu ni mkakati Maalum wa Spika Dhidi ya wabunge wa Chadema na wapinzani?
ktk hotuba ya bajeti inavyoendelea utagundua kuna mkakati umepangwa na CCM dhidi ya wabunge wanaonekana wanazungumza sana kwa ukali kutoka chadema.

Mbunge wa Chadema akimaliza kuchangia, ameandaliwa mbunge maalum wa CCM kwa kazi maalum na anaelingana sifa za maneno na kejeli kama alivyo wa chadema.
Kwa mfano, alipomaliza Lissu akaja Mchemba. na sote tulivyoona
alipomaliza kafulila- Akaja Lisinde. na kila mtu aliona jinsi ya Lusinde alivyombana kafulila huku Naibu SPika akicheka na kumrudisha Lusinde kurudia kauli yake huku akidai hajasikia.
alipotaka kumaliza Mnyika, kaandaliwa Mbunge machachari wa Mara.
Akimaliza Msigwa. unaweza ukaona nyuma yake yupo mbunge mwengine wa CCM anaelingana kwa kejeli na vijembe bungeni

nadhani jinsi ya wachangiaji wa Chadema walivyopangwa. basi nyuma kuna beki aliepewa kazi ya kukaba. na Mpaka sasa washambuliaji wa Chadema wamekwama
 
Mchemba na Zitto leo asubuhi katika kipindi cha jambo Tanzania, Karibu mtu alie, Marini hasan nae mchokozi kweli, ndio sababu hapati ubosi pale TBC, Sera zake zinakaribia ha Tido. Aliyeshuudia aseme ilikuwaje
 
Hawajacna kitu. Wameshikwa hadi wanaunda kamati ya mawaziri 6 kuokoa bajeti! Wanaona jahazi linazama.
 
Wakati mwingine kwenda shule siyo lazima uelimike unaweza ukawa umefuta ujinga tu.
 
Wananchi wa kusini wasipopelekewa maendeleo wahamie Malawi - Komba
 
KATIKA GAZETI LA MAJIRA LA LEO, KUNA KICHWA CHA HABARI TFF yazitaka Simba na Yanga kukaza buti!! '' Habari inaanza kwa kusema Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limezitaka Simba na yanga kuhakikisha zinalibakisha kombe la Kagame, linaloandaliwa na vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na kati (CECAFA). Kauli kama hii ni nzuri ila kinachonisikitisha hapa nakuona ni jinsi gani hata viongozi wetu wa soka wamejaa siasa za Simba na Yanga ni Kitendo cha kuzitaka Simba na Yangu tu bila Kuzungumzia Azam!!!. Tunakwenda wapi kwa staili hii. Hivi kichwa cha mwendawazimu kitaaisha. Itakuwaje kwa viongozi wa TFF pale Azam itakapolichukua kombe?. Au Azam si timu ya Tanzania hata isizungumziwe ? Nawaasa viongozi wanguwa tiefu efu acheni hizo. Kichwa cha mwendawazimu kinaanzia kwenu na unazi wa kijinga!
Wazungu wanamsemo ambao wanapenda kuutumia kwa mtu mkubwa mwenye akili ya kitoto au anayefanya utotototo....wanasema '''SHAME ON YOU'''. Namimi nasema shame on TFF
 
nipo Pwani hapa kwa mkuu wa kaya...watu wanfuatilia bunge huku wakichapa kazi....anapozungumza mbunge wa CCM watu hawashangai.Ila anaposimama mbunge wa CHADEMA, redio zinaongezwa sauiti na hata TV....WAKO MAKINI KWELI.


nASHINDWA ELEWA NI KWAMBA WANIPENDA chadema AU NI KWMABA WAVIZIA KUSIKIA wabunge wa watanzania kupitia CHADEMA wakiboronga wapate cha kuozungumza?
 
Bajeti yetu bungeni safari hii ni sharti itenge fedha kwa ajili ya MAENDELEO kwa asilimia 75 % na fedha kwa ajili ya gharama za UTAWALA, POSHO NA MIKONGAMANI safari hii kamwe isizidi asilimia 25 %.

Fedha kwa ajili ya Mikopo Elimu ya Juu nayo lazima iende juu 4 fold ili Tanzania yetu iweze kuwekeza zaidi katika elimu kuongeza ubora wa watu wetu kushindana kwa tija katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Back
Top Bottom