Jamani hhebu wataalamu wa masuala ya miundo ya serikali na nchi tueleimishane kwanza kabla ya kutangaza uhaini, naomba kujua, kwenye muungano wetu huu:-
1. Ni nchi gani na nchi gani ziliungana?
2. Zilipoungana je kulizaliwa nchi mpya am laa?
3. Kama kulizaliwa nchi mpya?
4. kama jibu la 3 ni NDIO, je zilizaliwa nchi ngapi moja, mbili au mia?
5. Je nchi hiyo/hizo inaitwaje/zinaitwaje?
6. Je nchi hizo zina mipaka au hazina?
7. Je nchi hiyo/hizo ni huru na zinajitawala au kuna moja inatawala nyingine?
6. Je kwenye nchi hiyo/hizo kuna serikali ngapi?
7. Kama jibu la 6 ni serikali zaidi ya moja, je inawezekana kuwa na nchi moja yenye serikali zaidi ya moja? Toa mfano
8. Mwisho je wewe ni Mtanzania, Mtanganyika, Mzanzibari, muunguja au mpemba?
9. Je unaridhika na muundo huu?
10. Kama hauridhiki, ungependa nini kifanyike?
11. Asanteni kwa kunisikiliza
Mkuu majibu ya maswali haya sio kero za Wananchi isipokuwa ni upotoshi wa makusudi. Tunashindwa kujibu maswali magumu zaidi kwa kutafuta urahisi kwani Muungano wetu ulilazimika kuwepo kutokana na hali ya kisiasa. Na ndivyo Muungano wa nchi nyingine ulipatikana na sio kwa kufikiria zaidi mipaka ya nchi isipokuwa WATU wake na MAZINGIRA yaliyokuwepo.
Hivyo sababu ambazo pekee zinaweza kuuvunja Muungano huu ni tofauti za WATU na MAZINGIRA tulokuwepo leo jambo ambalo litaamuliwa na wananchi wenyewe na sio siasa za kigabuzi kwa kutazama mipaka ya nchi badala ya wahusika. Hata nchi zote za USSR na Yugoslavia zilivunjika kutokana na kero zinazowahusu wananchi wenyewe na siii mipaka ya nchi zao au kutambulika kwa Taifa ndani ya nchi isipokuwa kumetokana na swala kubwa la KIUCHUMI au KIITIKADI.
Sisi tunapoendelea kudai Utengano kutokana na Historia ya mkoloni inaonyesha wazi bado tumetawaliwa kiakili. Tunashindwa kuyatafutia ufumbuzi maswala nyeti yaliyopo mezani tunatafuta tofauti za Uasili ya watu hivyo hata kama tukija tengana basi Pemba na Unguja watakuja tumia vigezo hivyo hivyo kutengana. Na vizuri sana ikiwa Wazanzibar mtaweka wazi kero yenu ndani ya Muungano kwani kudai kuitwa nchi au Taifa hali viongozi wenu wana mamlaka makubwa zaidi ya Muungano wowote naoujua mimi ni kufanya kufur.
Sijawahi kuona nchi moja ina Marais wawili, sasa nasikia kutakuwa na makamu wa rais na waziri mkuu (waziri Kiongozi) ktk serikali zote za Muungano na Visiwani, hii pekee inawafanya kuwa na madaraka makubwa kuliko nchi zozote ndani ya Muungano wowote ule. Na pengine haya ndio makosa makubwa yaliyowahi kufanyika kwani muungano wa nchi huondoa kabisa tabaka za kiramani ktk uongozi wa nchi. Lau kama Tanzania ingeungana pasipo kujali utaifa wa kila mmoja wetu tusingekuwa na matatizo kama haya isipokuwa lingezuka labda tatizo la Zanzibar kumezwa na Bara.
Binafsi naamini kabisa ikiwa kuna mpango madhubuti wa mgao wa urithi na mali ya Taifa zima, hii akikli ya Kitumwa ya kutazama mipaka ya mkoloni isingekuwa tatizo na hakika ni kwa jicho kama hili ndio maana Afrika tumeshindwa kudumisha Pan Africanism. Na hakika hizi ndizo athari za kutawaliwa kiasi kwamba Wazanzibar wanajisikia tofauti na karibu sana na Mwarabu (Oman) na Wabara kujisikia Uzungu huku tukitumia dini kama ndio sababu ya tofauti zetu.
Til then.. we still serving the Masters!
Balaza la wawakilishi lipo kisheria kama ilivyo kwa bunge la jamuhuri. Labda cha kujiuliza hapa ni je, baraza la wawakilishi linayo mamlaka ya kufanya mabadiliko iliyoyafanya katika katiba ya Zanzibar? Kama jibu ni ndiyo, then sioni uhaini unatokea wapi. Ndani ya mipaka ya jamuhuri, zanzibar ni nchi (lakini kimataifa hakuna nchi inayoitwa Zanzibar!)
Mimi ni Mmang'ati wa hanang so sina interest yeyote binafsi!
Mkuu nadhani nitatofautiana nawe ktk hili. Maudhui ya kuhoji Muungano ndiyo yanayokera watu kama mimi. Na siwezi kufananisha Muungano na dini kwa sababu dini ni Imani ya watu na Muungano unatokana na kutengeneza mazingira safi kwa jamii inayoungana. Hivyo tunaposhindwa kuelewa kwamba lengo kuu la Muungano ni kuunganisha WATU na swala la nchi ni kuyaweka Maingira yetu ktk hali ya kudumisha Umoja huo.Umenena vema...kitu kimoja ambacho sikipendi kuhusu huu muungano wetu ni kwamba umefanywa kuwa wa kiimani zaidi kwahiyo hautoi nafasi ya kujadiliwa.....ni kama masuala ya dini yalivo,,huruhusiwi kuyajadili jadili sana, kwanini?wanajua wao! kuna makosa yalifanywa wakati wa kuutengeneza, na kila watu wanapohoji makosa hayo, basi ile hali ya kiimani imani inarudishwa halafu mnaonekana kama wahaini...nadhani unanipata...ni sawa na mtu kuhoji ujio wa Muhamad au Yesu, ni kama unataka kuzua balaa ivi..
Nchi mbili zinaunganaje halafu bado zitoke nchi mbili tena zenye full kila feature ya nchi? katiba, bunge, serikali????????&&&kuna walakini hapa...watu wakitaka kurekebisha hizi kasoro basi inaonekana kama wanataka kuuvunja?tunaweza kuvunja ndio huu wa nchi mbili na serikali mbili halafu tukaunda wa nchi moja na serikali moja which is much better, na kwenye hilo mkuu Mkandara nakubishia kabisa kuwa eti Zanzibari itamezwa na Bara, imezwe vipi?ikiwa nchi moja both Tanganyika na Zanzibar zitamezwa na Tanzania, thats what I understand? si kila mmoja amekubali kuolewa, akubali kulala fululu!!!!
Huu muungano feki huu, utazamwe!!!!
Mimi ni Mmang'ati wa hanang so sina interest yeyote binafsi!
wazanzibar wakitaka kwenda zao waachieni kama wameamua kwa utashi wao. muungano haulazimishwi. huenda sababu zilizopelekea muungano hazipo tena. sasa kuwalazimisha wazanzibar kama hawataki muungano ni kuwapa hisia kuwa bara ndo wanafaidika kuliko wao ndo maana wanaung'ang'ania.
thats exactly the point.. kila mtanzania au kundi la watanzania watakaoona kuwa Muungano hauwapi manufaa wanayotaka wajitenge. Hivi watu wa Kigoma (na wameshawahi kusema hili) wakisema Muungano hauwanufaishi au Tanzania Bara haiwanufaishi tutawabishia? Vipi kuhusu watu wa Mtwara na Lindi (nao wameshawahi kusema hili) wakisema kuwa Muungano hauwanufaishi na wangependa kuwa sehemu ya Msumbiji au kutangaja kijamhuri chao tutawaambia wanasema uongo au tutawakubalia ati kwa sababu muungano hauna manufaaa "kwa pande zote"? Hivi watu wa Chunya wananufaika vipi na Muungano? Watu wa Nansio, Mkongo na Duga wananufaika vipi na Muungano?
Hivi Wamarekani wote wananufaika na muungano wa US? Na wote wanafuraha?
Ndio maana nilisema wabongo tunapenda mambo mepesi mepesi!
@Mkandara, nimependa take yako.. thats whatsup!
yaani hata hii kauli ya kipuuzi iliyotolewa na Kikwete mwanzoni (na niliipinga wakati ule vile vile) watu hawafikirii wanachosema: "NDANI YA TANZANIA ZANZIBAR NI NCHI". Really?
It is our considered opinion that on the basis of this principle of duality and the established fact of exclusive jurisdiction of the Revolutionary Government of Zanzibar over all non-Union Matters in Zanzibar, the only logical conclusion is that sovereignty is divisible within the United Republic.
Balaza la wawakilishi lipo kisheria kama ilivyo kwa bunge la jamuhuri. Labda cha kujiuliza hapa ni je, baraza la wawakilishi linayo mamlaka ya kufanya mabadiliko iliyoyafanya katika katiba ya Zanzibar? Kama jibu ni ndiyo, then sioni uhaini unatokea wapi. Ndani ya mipaka ya jamuhuri, zanzibar ni nchi (lakini kimataifa hakuna nchi inayoitwa Zanzibar!)