Ni uhaini - as simple as that!

Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.

Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.

Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".

Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:



Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):


na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?

Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?


Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:

(

Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!



I couldn't be more blunt than that.

Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):

Ooh how prophetic!!!

I'm standing on guard, by CHOICE!
Pole Mzee Mwanakijiji,
Rasimu ya mabadiliko hayo, niliyaona kwenye kikao fulani cha nchi wafadhili, nikiamini yangewekwa hadharani ili yajadiliwe na Wanzazibari kabla ya kufikishwa Barazani.

Maana ni kuwa Bara iko very much aware kila kinachoendelea Zanzibar, kwanza waliomba bendera, halafu wakaomba wimbo wa taifa, sasa hawajaomba mipaka, bali wametangaza mipaka ili Zanzibar iwe nchi in terms of defined teritory ila usiwe na shaka, hiyo ni mipaka jina tuu, kama ulivyo wimbo wao wa taifa ni wimbo tuu, na bendera yao nayo ni bendera tuu.

Kama wewe nyumbani kwako unaitwa Baba, mwanao akalipenda sana jina la baba, ukakubali naye aitwe baba, akiitwa baba anafurahi, hivi wewe sasa ndio hautakuwa baba?. Wewe utabaki baba wa ukweli na yeye baba jina.

Hivi ndivyo ilivyo status ya Zanzibar, ni nchi jina tuu ila sio dola kwa sababu bado haina vyombo vya ulinzi, vyombo vya dola, Jeshi, Polisi, TISS etc, unless KMKM ndio polisi wao na JKU ndio jeshi lao, them huu utakuwa uhaini 100%.
 
May God help us and our brothers in Zanzibar and Pemba to fulfill this responsibilities.!

I always say huu muungano wetu ni Hoax-not documented. Read on the red. there is SISI, Wazanzibari na Wapemba.

Who is us-sisi according to nyerere????
Bora mchakato wa kuirejesha Tanganyika uanze. wazanzibari hawabebeki ijapokuwa wao ndio wanaofaidika na muungano socially, economically and politically-maana tanganyika ndiyo hutuliza jazba zao za kisiasa.
 
Unadhani iwapo jeshi linavamia Zanzibar, wazanzibar tutafunga mikono tukutazameni mnfavyofanya uhuni wenu...kama mlivyowafanyia Uganda...unajidanganya? au unadhani hilo jeshi lenyewe litabaki kama lilivyo baada ya kitendo hicho...kumbuka vijana wetu wazalendo, wapenda na wenye uchungu wa nchi yao ya Zanzibar pia wamo humo humo JWTZ, so unazungumzia CIVIL WAR THEN not military intervention any more...?


Hakika mimi si shabiki wa vita and I believe in dialogue, Lakini kwamba Jamhuri ya Watu wa Zanzibar inaweza kupigana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania NAONA NI KICHEKESHO CHA MWAKA. MAHALI PAKE NI ZE COMEDY!
 
Kwa mtazamo wangu mdogo kwa mimi ambaye nimezaliwa ndani ya muungano - Naona kama kuna mpungufu tokea mwanzo wa makubaliano kati ya Nyerere na Karume ( There are something behind the scene ). Na hapo ndio kuna shida kubwa sana. Nakumbuka nilishawahi kwenda ZNZ at young age with ma mum holding a passoport just to enter the same country !!! Likini hilo swala likaja kuondolewa... Nadhani kuna mapungufu makubwa sana katika muungano wetu.

Swala la muungano ni wakati wake kulizungumzia mezani na wala si kulificha au vile " Fikra na m/kiti zidumu"
 
Tatizo viongozi wetu wame liachia hili swala mpaka lime kua a controversial issue. Itafika kipindi kudiscuss Muungano ita kuwa kama kudiscuss dini. Mkuu Mwanakijiji maybe this is a wake up call that something should be done now. Tuta fika kipindi tuta kuwa kwenye point of no return. But mambo mengi nalaumu mfumo ulio wekwa kuendesha Muungano na nita rudi baadae kuelezea kwa nini (kwa maoni yangu).

Nadhani ni wakati muafaka sasa kutolifanya liwe nyeti tena na lizungumzwe kwa uwazi. Kama kweli dhamira ni kujitoa ndani ya Muungano, ni vema hilo likaelezwa wazi ili lishughuklikiwe kwa namna ambayo itatuacha tukiwa salama baada ya Muungano kuvunjwa. Kama tukiendelea kulifanya kinyemela, tutaumia huko mbele ya safari
 
Zanzibar mna imaaaaaaaindi siyo hamjiwezi...eti jamhuri yetu..ipi?
 
Lakini Watanzania bara hatujafanya lolote kuonesha kuwa haturidhiki na Muungano. Hatujadai Tanganyika kwa namna yoyote ile. Kwa hiyo hili ni suala la Zanzibar tu.

Mkuu, hao waliodai na wanaoendelea kudai serikali ya Tanganyika wali/ wametoka wapi? Hata hao wazanzibari wanaodai kuwa kuna kero katika Muungano hawasemi wazi kuwa hawataki Muungano. Kwa vile Muungano ni wa pande mbili ni lazima wote waulizwe. Kama watu wa bara wanautaka Muungano wapewe nafasi kusema wazi ili asitokee mtu hapo mbeleni na kusema hawakuulizwa.


NI asilimia ngapi ya kura za pande mbili zitahesabika kuwa watu wanataka? simple majority au absolute majority?

Simple majority. Wasiopiga kura hawatahesabiwa.

Ingekuwa rahisi kutengana kila watu wanapotaka Quebec ingekuwa imeshatengana na US ingekuwa imeshatengana. Ninachoona ni woga na kutotaka kugonganisha vichwa watanzania kutetea misingi ya taifa lao. Kuna aibu fulani hivi inawakumba watu kusikia wanatetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Urusi ilitengana lakini unadhani ndio ulikuwa mwisho wa matatizo kati yao? remember masuala ya Chechyniya na Georgia, au kuvunjika kwa Yugoslavia na mambo ya Montenegro, Sebria, Slovakia na Macedonia, Albania na Kosovo. Kutengana si mwisho wa matatizo ya mahusiano.

Quebec waliulizwa na walipata kigugumizi walipojua Rest of Canada wako tayari kuwaachia. Hakuna State Marekani yenye nia ya kujitenga ( kuanzia Texas, Alaska, California n.k.). Hii haina maana hakuna movements zinzodai kujitenga (Alaska ni mfano mmoja). Puerto Rico mpaka sasa na yenyewe wanapata kigugumizi inapofikia hatua ya uhuru kamili. Wote hawa wanajua siagi iko upande gani wa mkate! Sijasema kuwa kujitenga kunatatua matatizo yote. Ninachosema cha msingi ni namna ya kujitenga. Yugoslavia walikataa kabisa kuruhusu Slovenia, na wengine kijitenga na walikuwa tayari kumwaga damu kulinda umoja wa Yugoslavia. Tumeona yaliyotokea. USSR ingawa iligawanyika lakini ndani ya Russia bado kuna vijisehemu ambavyo vililazimishwa kubaki na vingi vyao ni vya huko Caucasus. Federation karibu zote za kulazimisha zina umwagaji wa damu ( India, Spain, China, Russia n.k). Zile ambazo zinatoa uwezekano wa kujitoa ni salama zaidi kama Marekani, Canada, Belgium n.k.

Hadi hivi sasa sijaona hoja hasa za "upande mmoja haziutaki" ni viongozi wahuni tu wa CCM na CUF ndio wanafanya hivi. kama waliweza kuwauliza Wazanzibari kuhusu mfumo wa serikali yao kwa kura ya maoni kwanini wasiwaulize kama wanataka au hawataki. Na uamuzi watakaochukua sisi Bara tutauheshimu.

Dhana hii ndiyo inatuponza. Kwa sababu watu wako kimya hakuna maana kuwa hawana msimamo kuhusu Muungano. Hao unaowaita viongozi wahuni ni lazima wana watu nyuma yao. Na hii ya kutufanya Bara mazezeta kuwa hatustahili kuulizwa ndiyo nashindwa kuelewa. Kama mna imani kuwa Bara wote wanautaka Muungano, mnaogopa nini kuwauliza?

Belgium inatawalika; na Yugoslavia ndio kama nilivyosema hapo juu. Lakini miungano hiyo si sawa na Watanzania. Sisi hatukuunganishwa kwa nguvu. Muungano wetu unafanana sana na wa US kuliko sehemu nyingine.

Belgium hawana serikali stable kwa muda mrefu sasa. Flanders na Wallonia hazipikiki chungu kimoja. Si States zote za Marekani zilijiunga kwa 'hiari'. Mifano ni New Mexico na Texas ambapo dhulma, uhuni, ubaguzi wa rangi ulitumika katika kuungana kwao na Marekani. Ni wahamiaji kutoka Marekani ndiyo waliopelekea Texas ijitenge na Mexixo halafu iungane na Marekani. Muungano wetu haufanani na Marekani kwa vile hakuna nchi ya Bara ndani yake. Marekani State zote ziko sawa na zinatofautishwa na Federal Government ( ukiondoa eneo la District of Columbia). Muungano wetu unafanana zaidi na Finland inayojumisha kisiwa cha Aland.

Thats my point. Mimi sina hofu, lakini pia simuumini wa urahisi rahisi wa kuvunjika kwa jamhuri ati kwa sababu sehemu fulani ya jamhuri "hawataki". Ni kitu gani kitazuia watu wa Kilimanjaro kujitenga wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanatetea maslahi yao ambayo wanaona hayapatikani ndani ya Muungano? Hapo si tutaweza kutumia mfano wa Sudan na Sudani ya Kusini?

Context ya Sudan ni tofauti kabisa na ya kwetu. Sudan Kusini ni mkusanyiko wa makabila yenye asili ya weusi ambayo yamekuwa systematically marginalised katika Sudan ya sasa. Hawa wanaji identify kwa rangi na dini. Watu wa Kilimanjaro au Mtwara wakiweza kujenga hoja kuwa wao ni taifa na wamekuwa wakionewa ndani ya nchi yao kutokana na asili yao ( kuzuiwa kuabudu miungu yao, kutumia lugha zao n.k.) basi watakuwa na haki ya kudai uhuru zaidi wa kutawala mambo yao. Hata hivyo, kwenye hilo historia haiko upande wao. Sijasikia wakazi wa huko wakijihesabu kama watu wa taifa fulani la Kilimanjaro au Mtwara. Wote wanajihesabu ni wa kabila fulani ndani ya uraia wa Tanzania. Hii ni tofauti na wazanzibari. Nimewasikia wengi tu hasa ughaibuni wakijitambulisha kama wazanzibari na kufunika kabisa utanzania wao.

Amandla.......
 
kwa hiyo baada ya kuundwa kwa hii nchi ya Zanzibar kutakuwa na raia wa Zanzibar vile vile au watakuwa bado ni raia wa Tanzania? Hii nchi nyingine ndani ya nchi nyingine itaweza kutoa pasi za kusafiria au kama wakitaka kuna sababu ya wa kuwakatalia kuwa hawawezi?

Tukijitengana, Zanzibar itakuwa sovereign state yenye raia wake, jeshi lake n.k. Tanzania aidha itabki kuwa ni Bara na visiwa vyake vya Mafia n.k. Au jina la Tanzania litakufa na Tanganyika kufufuliwa. Watu wa bara hawatakuwa na haki ya kuwawekea mipaka nchi ya Zanzibar baada ya kutengana. Kama nchi huru, fate yao iachiwe mikononi mwao. Hakuna cha nchi nyingine ndani ya nyingine. Ni haki ya nchi yeyote kamili kutoa pasi za kusafiria kwa raia wake. Kuwazuia kufanya hivyo kutakuwa kulazimisha Muungano kwa njia ya uani!

Amandla.....
 
Hakika mimi si shabiki wa vita and I believe in dialogue, Lakini kwamba Jamhuri ya Watu wa Zanzibar inaweza kupigana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania NAONA NI KICHEKESHO CHA MWAKA. MAHALI PAKE NI ZE COMEDY!

Kuna kitu kinachoitwa kufanya nchi isitawalike. Mfano niAfghanistan. Bara haiwezi kuitawala Zanzibar kimabavu kama sehemu kubwa hawataki hivyo.

Amandla.....
 
Karume Mzee alileta Muungano. Amani Karume kaanzisha MCHAKATO wa kuuvunja! Nadhani Karume mtoto anajua baba hakuuacha Muungano huu uliopo sasa. Vunja Karume vunja!
 
from the layman point of view naomba kuuliza, ivi siku zooote izi kumbe Zanzibar sio nchi? mbona ina bunge (wao waita baraza la wawakilishi), ina raisi, ina serikali yake just like any other state, au sifa ya kuwa nchi ni ipi? sasa wakitangaza mipaka yao kuna shida gani

honestly sioni tatizo hapo, ila shida ninayoiona muungano huu setup yake imekaa kishkaji sana, ni wa kishkaji tu sio kitu ambacho kipo arranged seriously. nchi mbili haziwezi kuungana halafu zikatokea serikali mbili, sasa ndo mmefanya nini....yani kabla hamjaungana serikali zipo mbili...na mkishaungana zinaendelea kua mbili...aaahh hii imekaa kishkaji....nadhani maana halisi ya kuungana ni aidha muunde nchi moja yenye serikali moja na kila mtu aukane uraia wake wa awali na kuupokea uraia wa nchi mpya...au muunde serikali tatu huku kila nchi ikimaintain sovereinity yake...lakini huu muungano wetu fekiiiiiiiiiiiiiiii
 
Haya yote yanatokea kutokana na mapungufu makubwa ya viongozi wetu wa sasa na chama kinachotawala sasa! kwao suala la uzalendo na kutetea nchi yao si suala la kipaumbele bali wanaendekeza kutetea matumbo yao na ustawi wa chama chao. Tuna watu jasiri wachache waliobaki kama mmkj ambao wanaweza kukubali kuhesabiwa wakitetea utaratibu uliowekwa.
Viongozi wa serikali ya muungano hawana jeuri ya kutetea serikali wanayoongozwa hata kama wanaona mwelekeo tata wa waznzb.
Mungu ibariki Tanzania,
waacheni wanzibar waende zao, watuachie nchi yetu. Lakini walete hoja ya kutoka bila ya kujificha, nasi tutawaunga mkono lakini si kuimomonyoa nchi yetu tukiona!
 
CCM, waendelee tu kufanya usanii wa kisiasa. Kwenye mambo muhimu ya mustakabali wa taifa, waendelee tu, na usanii wa kuairisha tatizo badala ya kutafuta tiba. Kuna siku watajikuta, hawana taifa la kutawala! Huwezi ukawa na nchi ndani ya nchi nyingine. Wajitahidi kutofautisha eneo na nchi. Sovereignity is very very different from territoriality!
 
Bwana wanataka nchi
kula tano ndugu yangu.mkjj namkubali kwa mambo mengi lkn kwa hili sipo pamoja naye hata kidogo. baba aliingia kwenye ndoa akajuta lkn alikwisha chelewa.kumbuka alimpa likizo ya ghafla mwanasheria wake na akaazima mwanasheria toka naijeria ili amuandalie raasimu ya muungano chapu chapu akijua kabisa mwanasheria wake asingekubaliana naye. sasa mwana anavunja ndoa kuna dhambi gani??je dunia haijapata kushuhudia uwepo wa ussr???? je leo hii iko wapi?????
 
Hii nchi ni yetu sote na ni lazima sote tuulizwe. Tunaweza kushangaa hapo watakapokuta kuwa machogo nasi hatuutaki Muungano! Huku kutingisha kiberiti lazima kuwe na mwisho wake. Hii imani ya kuwa tuko tayari kuulinda Muungano kwa gharama yeyote ndiyo inayowapa kiburi. Watapojua kuwa hatuko tayari kumwaga damu kwa kitu ambacho ni figment ya imagination pengine watasita kabla ya kufanya upuuzi huu. Wasitugeuze Spain na Catalanya!

Amandla.......

Kadri ninavyojaribu kutafakari faida za muungano kwa Mtanganyika wa kawaida ndipo ninavyozidi kukosa sababu, naona kama Zanzibar kama nchi na watu wake wana faida zaidi kuwa kwenye muungano kuliko Tanganyika na Watanganyika.

Ni mtazamo tu.
 
Waandishi wa habari mlioko humu mfateni AG wetu awape ufafanuzi wa haya yanayoendelea kule Zanzibar.
 
Tatizo kubwa ni katiba, Period!!

Watu wako excited na hata wale ambao tunajua wana uhuru na upeo mzuri wa uchambuzi wa mambo kama Mkjj wamekua mstari wa mbele kutaka damu imwagike na uhaini kwa yeyote atakae thubutu kuongelea au hata kudadisi tu kuhusu maswala nyeti ya muungano. Hii inasikitisha, sababu katika jamii huru yeyote nasi kama ambavyo wote humu tunajaribu kujenga katika nchi yetu, ni vyema watu wote waruhusiwe kutoa mawazo yao hata kama hatukubaliani nayo au kuyapinga, hususan maswala nyeti kama muungano, katiba na madaraka ya rais wetu.

Kila muungano hapa duniani una kundi la watu ambao wanataka kutoka au kuuvunja, sehemu nyingine ni minority(e.g quebec, alaska, texas, wales) kwengine ni wengi (e.g catalonia, scotland, south sudan, wallonia n.k) sehemu zote hizi watu hao wapo kwenye democracies (ukitoa sudan) na hatujasikia maneno ya uhaini punde sehemu hizo zilipopewa maamuzi zaidi ya utawala wa ndani (i.e kutumia bendera, wimbo wa taifa au lugha zao) yamkini maamuzi mengi ya kuruhusu kuwaongezea maamuzi ya ndani imezidisha hamu zao au tuseme raia wao kuonyesha hamu ya kubaki kwenye muungano na sio kutoka.

Wakazi wengi wa pande zote mbili bara na visiwani wanataka muungano udumu maana tunategemeana sana. Kuna watu humu wamesema wao hawaoni faida ya kuwa na znz, mi nadhani hao wanaishi bara (mikoani) maana kama unaishi tanga au dar basi si ajabu ukuwa na ndugu, jirani au jamaa ambae ametoka zenj au pemba. Muungano wetu ni wa kindugu, waunguja wengi wana ndugu zao bara, kuna wapemba wengi wanafanya biashara huku ilhali zanzibar pia kuna wabara wengi hata vijana wa kimorani wapo nungwi, sasa nani kweli hataki huu muungano?

cha msingi tuendelee kujadili mapunguvu yetu na kuyafanyia merekebisho kwenye katiba yetu, natumai serikali mpya itatilia mkazo hilo la katiba na hata ikibidi tupige kura ya maoni nchi nzima kuhusu muungano na katiba mpya, mi na imani muungano camp tutashinda kwa kishindo!!
 
Mwanakijiji;


Issue ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni suala la Kisera zaidi kuliko kiutendaji.

Kama kumbukumbu yangu iko sahihi ni kuwa NEC ya CCM iliyokaa Butiama iliazimia kuwa katika kumaliza mpasuko wa Kisiasa Zanzibar na kuleta Muafaka, ipigwe kura ya maoni.

Kwa maoni yangu hili lilianzia katika Chama na simple logic inataka kuwa matokeo ya kura ya maoni yangerudishwa katika chama ili yafanyiwe kazi. Kama lingekubalika kichama basi ilikuwa budi liwekwe katika Sera za CCM ili kulinadi na hatimaye kulitekeleza. Ikumbukwe kuwa Muungano ni Sera ya CCM.


Itakumbukwa kuwa akina Njelu Kisaka walikuwa na hoja ya G55 ya kuirudisha Tanganyika ambayo nusura Bunge liipitishe. Ilikuwa ni Mwalimu aliyefunga safari toka Butiama kuja DSM aliyelipigia kelele kuwa halikuwa sahihi kiutaratibu kwani kurudisha Tanganyika haikuwa sera ya CCM. Aliwashauri kama walitaka hivyo ilibidi lianzie kwenye Chama na liingizwe katika sera kwa kuwa sera za CCM ni kuulinda Muungano na wala si kuuvunja.


Suala la Muungano pia lipo katika Katiba. Muungano ni Ndoa. Hata kama Zanzibar kwa kuwa nchi haitaathiri utendaji wa serikali hizi mbili, bado wabara watakuwa na mengi ya kujiuliza kwa mambo yasiyoridhisha, mojawapo likiwa je unaweza kuwa na Nchi ndani ya Nchi?


Kama mke wangu wakati namuoa nilimpendea uzuri na tabia zake na akaendelea kudumu na tabia hizo na uzuri wake, bila ya shaka ndoa itadumu. Lakini pale atakapoanza kubadilika tabia na kubadili mwili wake wa njia mbalimbali, kujichubua, makalio ya kichina vyote bila ridhaa yangu nk, basi ndoa hii itakuwa katika hatihati. Hakika mambo ya Zanzibar yalianzia kwenye wimbo, then bendera, mafuta na sijui yatafika wapi nk.

Ni vema hata kama hoja inakubalika, lakini ifuate utaratibu uliowekwa. Sijui kama kamati ya Muungano ilishirikishwa . . . .

Inanikumbusha saana hadithi ya Ngamia . . . . .
 
Wakati umefika wa kuwaambia raia wa nchi hii namna gani wanavyofaidika na Muungano. Bara na Zanzibar kote kuwa na mjadala wa wazi wa faida na hasara za Muungano kwa kila pande. Tusiendelee kuweka plasta kwa kutaka kujadili kero badala ya kuangalia swali la msingi ambalo ni, Muungano una maslahi gani kwa wananchi wake".

Amandla.......
 
Back
Top Bottom