Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Kwani huyo CAG naye si Fisadi tu, mahesabu kibao ya serikali yanapotea na hatoi taarifa, huyo naye Fisadi tu

Mimi nadhani Zitto katoa mwanga .So yule mtoa mada tena alikuwa na posts kama 2 ama tatu .Inawezekana kaja na kazi maalumu .Pokeeni ushauri na tuone akija atasema nini .Ama kama yupo anasoma ajitokeze ajibu hoja za Zitto .
 
Hivi hii mada imeshikiliwa na watu wangapi? Muwekaji anabadilika kila mara halafu mada yenyewe sioni kama ina nguvu sana inaonekana kama inaweweseka kabisa.

Lakini wenye data zaidi ya hizi wekeni na pia imenifundisha kuwa Sitta SIYO FISADI wa kuhatarisha maisha ya Watanzania.
 
Mkuu Zitto heshima mbele lakini naomba kutofautiana na wewe katika masuala yafuatayo:

Maadili! maadili! maadili!.
Viongozi ni kioo cha jamii,wao kwa matendo yao wanapaswa kuwa mfano mzuri kwa wale wanaowaongoza. Kiongozi asiyeheshimu ndoa yake ataweza kweli kuheshimu ndoa ya mwenzake?, kiongozi wa namna hii anajenga misingi ya familia bora na taifa au anabomoa?

Katika challenge tunazokutana nazo katika nchi yetu, na balaa hili la Ukimwi hivi unaweza kusema Ngono nje ya ndoa siyo ishu kweli?, yaani kwamba maadam kiongozi hajaliibia Taifa lakini hata kama mwenendo wake unatishia mustakbali wa taifa kwa kulea tabia zinazokwaza mapambano dhidi ya ukimwi hiyo siyo ishu kweli?.

Tutakuwa tunajidanganya tukidhani tutaweza kuiweka jamii yetu katika msitari ulionyooka kama tunadhani tunaweza kupambana na matatizo tuliyonayo kinjenje tu bila ya kuangalia mtatizo ya kindnindani ambayo kila mmoja wetu anayo.Ishu ya kujiheshimu,kuheshimu mume/mke kuheshimu familia yako ni jambo la msingi sana.

Kwa nchi kama marekani ikidhibitika kwamba unakwenda nje ya ndoa hata kama wewe ni raisi huo ni msala mnene tena unaweza kuondoka hivihivi na kiti unakiacha hivi hivi.

Lazima tufikie hatua iwepo aibu ya yale tunayoyatenda, Kiongozi/au mtu kwenda nje ya ndoa ni jambo la aibu, na kwa kiongozi anayetakiwa kubeba mwenge wa kumulika njia ya wananchi kisiasa na kijamii inabidi aonyeshe njia bora.

Hivi tutapambana vipi na Balaa la ukimwi iwapo tunaona yale yanayokuza ukimwi siyo ishu?
 
Hivi hii mada imeshikiliwa na watu wangapi? Muwekaji anabadilika kila mara halafu mada yenyewe sioni kama ina nguvu sana inaonekana kama inaweweseka kabisa.

Lakini wenye data zaidi ya hizi wekeni na pia imenifundisha kuwa Sitta SIYO FISADI wa kuhatarisha maisha ya Watanzania.

Kuna jamaa aliileta hapa hii mada ikawa inafutwa na ndiyo maana nimeomba ibakie ili kuondoa hisia mbaya .Si umeona sasa Zitto kaja kasadia kuweka sawa mambo ? Kuna jamaa ana posts kama 2 tatu ndiye source wa hii habari .Mods wanajua vyema the name wanaweza kutusaidia .
 
Hii mada ni nzito na kanuni zangu nilizotumia na kuzisema wakati wa sakata la Amina na Zitto bado zinaukweli kama tukiamua kuzifuata.

a. Kama kiongozi yeyote anahusika na uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote ambaye si kinyume cha sheria kuwa nayo, basi jambo hilo ni la binafsi.

b. Kama kiongozi huyo katika mahusiano hayo anaenda nje ya ndoa yake basi suala hilo ni la yeye na mwenzi wake, wachungaji/mashehe, na wanafamilia. Sisi watu wa nje, mwiko kuligusia.

c. Kama kiongozi anahusika na suala la mapenzi ambalo ni kinyume na sheria kama kubaka, mapenzi na watoto wa shule, au kujihusisha na makosa ya Sheria ya Kujamiiana (vipengele maalum) ya 1998 na sheria ya nyingine zihusianazo na makosa ya kujamiiana basi mtu huyo siyo tu anajadilika bali hastahili kushikilia uongozi.

d. Kama kiongozi wa umma (mwanasiasa au vinginevyo) anahusika na mahusiano ya mapenzi ambayo yanahusisha ofisi yake, cheo chake, jina, na hadhi yake, basi mtu huyo siyo tu anajadilika bali anastahili kujiuzulu kulinda heshima ya ofisi hiyo.

Kanuni hizo nne, kwangu zinaniongoza ninapoangalia hoja zilizotolewa hapo juu.

Nitumie mfano halisi ambao bado uko mawazoni mwa watu. Gavana wa New York Bw. Spitzer amejiuzulu wadhifa huo kwa kosa la kujihusisha na huduma ya malaya na kulipia karibu shilingi milioni 90! Licha ya kuwa alikuwa ni makini katika kuwafunga wengine (akiwa Mwanasheria Mkuu wa NY) kwa makosa kama hayo, lakini kibano kilipogeuzwa alijikuta hana ujanja.

Hata hivyo, Gavana mpya naye alipoingia jambo la kwanza kukiri ni kuwa yeye na mke wake walikwenda nje za ndoa yao baada ya kuwa katika mchakato wa talaka miaka kadhaa huko nyuma, na aliamua kuwa mkweli kuwa wakati huo hawakutarajia kurudiana, lakini waliporudiana walisameheeana na wako pamoja leo hii.

Sasa turudi kwenye suala la Spika Sitta.

Kama madai dhidi yake kuwa amehusisha ofisi yake na fedha za Watanzania katika kuhudumia his sexual trysts siyo tu amedhalilisha ofisi ya spika bali anastahili kuwa impeached.

Kama madai ya kutumia ofisi, fedha, na mali za serikali ni ya kweli (na huyu aliyeleta hii taarifa ameniweka kwenye hali ya "nusura nimuamini") basi Spika Sitta kama vile Mbowe anastahili kuambiwa arudishe fedha hizo, aombe msamaha, na kusafisha nyumba yake.

Kwanini basi mada hii inazungumzika hapa JF?

Kwa sababu, linapokuja suala la ngono na mambo ya mapenzi:

- Tumemzungumza Kikwete hapa
- Tumemzungumza Mengi hapa
- Tumemzungumza Manji hapa
- Tumemzungumza Amina hapa
- Tumemzungumza Zitto hapa
- Tumemzungumza Slaa hapa
na wengine wengi...

Sasa kwanini Sitta asiwe sehemu ya mazungumzo hayo? Kama madai haya ni ya uongo, ni ya kupuuza tu kwani hata mtu akitaka kutafuta ushahidi hawezi kuupata kama vile yule jamaa aliyekuja na madai kuwa Mbowe kabaka watoto wa shule na anakesi kibao mahakamani tangia miaka ya tisini, lakini alipoulizwa ataje mahakama na kesi hizo akakimbia! huyu aliyeleta suala la Sitta tukimuuliza hata majina sitashangaa.

NB:

Pamoja na maneno yangu mengi hapo juu nitoe angalizi moja. Niliripoti karibu mwezi mmoja uliopita kuhusu Agenda 21. Ninaamini (na ninazo sababu za kuamini) kuwa aliyeleta mada hii awali ni mtu wa agenda hiyo, na lengo ni kuhakikisha wanajibu mashambulizi hasa baada ya Spika Sitta kumzidi ujanja Lowassa (imeelezewa jinsi gani kwenye klhnews taarifa ya "Jinsi Lowassa alivyozidiwa kete".

Hivyo, sehemu hii ni sehemu ya mapambano yale yale na kwa vile JF imekuwa kama msumeno, tunaposhabikia wengine kuwakuta tusije shtuka siku moja na sisi tuko upande wake wa makali!

M. M.
 
.

b. Kama kiongozi huyo katika mahusiano hayo anaenda nje ya ndoa yake basi suala hilo ni la yeye na mwenzi wake, wachungaji/mashehe, na wanafamilia. Sisi watu wa nje, mwiko kuligusia.

japo sijui ni vigezo gani umetumia
kuweka standard hizi!

pia kutuhimiza kuwa ni mwiko kuligusia sijui unaupata wapi ujasiri wa namna hii.

let me put it like this:
Matendo kama haya ya kutembea na wake/waume za watu ni tishio kwa ustawi wa jamii,ni matendo yanayojenga chuki na kubomoa misingi ya ngazi ya awali ya Taifa ya familia kwa hiyo ni haki sisi kama jamii kuyakemea na kumkemea yeyote yule ambaye yupo within our reach.

Ni matendo yanayotishia jamii kutokana na kuwa kichocheo cha ukimwi!,hapa huwezi kuiambia jamii ikae hivi hivi,wakati unaona wale makamanda wanaoongoza mapambano wanaanza kuact kinyume!

Ndiyo sote tuna udhaifu, lakini udhaifu wetu usiwe sababu hata ya kutokemea yale yanayokwenda kinyume cha maadili ambayo kimsingi inabidi tuyafuate
 
.



japo sijui ni vigezo gani umetumia
kuweka standard hizi!

pia kutuhimiza kuwa ni mwiko kuligusia sijui unaupata wapi ujasiri wa namna hii.

Ni mwiko kwa sababu, hakuna mtu mwenye haki ya kumuambia mtu aliyeoa au kuolewa kuwa "tunakutaka ulale na mkeo/mumeo tu"! Ni wao waliokuwa kiapo cha ndoa na ni wao wataishi na matokeo ya kukivunja kiapo hicho. Sasa jukumu la jamii ni kuwasaidia kuishi katika ndoa hiyo vizuri, ndipo suala la wachungaji, n.k linapokuja.

Na linapokuja suala la watoto na mambo ya Ukimwi, hali halisi inaonesha kuwa si wote wenye ukimwi ni watu wa ndoa!
 
Ni mwiko kwa sababu, hakuna mtu mwenye haki ya kumuambia mtu aliyeoa au kuolewa kuwa "tunakutaka ulale na mkeo/mumeo tu"! Ni wao waliokuwa kiapo cha ndoa na ni wao wataishi na matokeo ya kukivunja kiapo hicho. Sasa jukumu la jamii ni kuwasaidia kuishi katika ndoa hiyo vizuri, ndipo suala la wachungaji, n.k linapokuja.
hakuna mtu mwenye haki ya kumwambia mtu alale au asilale na Mke/mme wake mwenyewe , lakini mtu mwenye kuibiwa mke/mme ana haki ya kumwambia mwenye kuiba aache kusarandia vya wenzie,hapo ndipo jukumu la jamii linapokuja, kukemea tendo zima linalosababisha huzuni kubwa na ukosefu wa harmony katika jamii na pengine kuweza kupeleka hat uvunjivu wa familia yenyewe.
Na linapokuja suala la watoto na mambo ya Ukimwi, hali halisi inaonesha kuwa si wote wenye ukimwi ni watu wa ndoa!
ni kweli siyo wote wenye ukimwi ni watu wa ndoa, lakini je hiyo pekee yafaa kutufanya tukae kimya hata kama ni dhahiri tendo linalotendwa linachochea ustawi wa tatizo?.tena tendo lenyewe liwe linafanywa na mtu ambaye kwa cheo chake ingebidi afahamu urefu wa kina cha tatizo na hivyo kuwa mfano wa namna ya kupambana na tatizo?.

Hii ni issue kubwa siyo ndogo hata kidogo.
bila values katika family hakuwezi kuwa na values katika taifa.
 
hakuna mtu mwenye haki ya kumwambia mtu alale au asilale na Mke/mme wake mwenyewe , lakini mtu mwenye kuibiwa mke/mme ana haki ya kumwambia mwenye kuiba aache kusarandia

Yaani mtu anamuiba mtu mwingine na unakuita huko kusarandia? Mtu akimtongoza mume/mke wa mtu na mtu huyo akaingia laini, huwezi kuita kuiba! Mtu ambaye anajua amefunga ndoa, na ana familia anapokubali vishawishi vya nje, na akaacha ndoa yake, mtu huyo ana sababu zake. Hakuibwa. Ila kama kuna mtu kweli anaingia kwenye nyumba ya mtu na kumuiba mke/mume wa mtu huyo mtu anastahili kutiwa pingu kwani anachofanya ni kile nilichokielezea kwenye mojawapo ya vifungu vya kanuni zangu.

vya wenzie,hapo ndipo jukumu la jamii linapokuja, kukemea tendo zima linalosababisha huzuni kubwa na ukosefu wa harmony katika jamii na pengine kuweza kupeleka hat uvunjivu wa familia yenyewe.

Hilo nakubaliana na wewe kabisa, lakini wenye jukumu la kwanza la kutunza na kulinda ndoa zao siyo jamii ni wana ndoa wenyewe! sisi wengine hata tupige matarumbeta mtu akiamua "kupata" nje ataruka ukuta (no pun intended)


ni kweli siyo wote wenye ukimwi ni watu wa ndoa, lakini je hiyo pekee yafaa kutufanya tukae kimya hata kama ni dhahiri tendo linalotendwa linachochea ustawi wa tatizo?.tena tendo lenyewe liwe linafanywa na mtu ambaye kwa cheo chake ingebidi afahamu urefu wa kina cha tatizo na hivyo kuwa mfano wa namna ya kupambana na tatizo?.

Matatizo ya ndoa hayaishi kwa kukemewa (historia inaoonesha hivyo) yanatokana na maadili mazuri ambayo msingi wake ni kumcha Mungu, maadili ambayo hupandikizwa tangu utoto na humwagiliwa kama miche katika maisha ya watu. Hata hivyo mwanadamu ni kiumbe huru na licha ya hayo yote akiamua kwenda nje ya ndoa au kufanya kitu kinyume na maadili ya ndoa ni yeye anawajibika kwa hilo.


Hii ni issue kubwa siyo ndogo hata kidogo.
bila values katika family hakuwezi kuwa na values katika taifa.

Sipingi hilo, na tuko mstari mmoja. Ninachosema, huwezi kuwalazimisha watu wazima na akili zao kuwa na maadili katika familia kama wameamua kutokuwa nayo utawafunga!?
 
Mzee Mwanakijiji,

Sawa hatuwezi kukufuatilia na maamuzi yako kama umemchoka mkeo na unataka visura wengine and what not--technically we can, na tutachonga tu kama kawaida yetu...

Lakini wananchi tuna-exclusive right to question matendo ya kiongozi! Ukiwa kama kiongozi, tuna right ya ku-question your ethical standards, na hilo la ndoa kwa mzee Sitta fits this scenario like a glove. Tutakuwaje na imani nawe kama unaweza kuiweka ndoa yako rehani? kama hawawezi kuacha uroda, waache kuwania uongozi!
 
Mzee Mwanakijiji,

Sawa hatuwezi kukufuatilia na maamuzi yako kama umemchoka mkeo na unataka visura wengine and what not--technically we can, na tutachonga tu kama kawaida yetu...

mnakaribishwa, niko kwenye basikweli yangu nani atanitaka! miye mrs anaitwa bi. "L.A. Ptop"..

Lakini wananchi tuna-exclusive right to question matendo ya kiongozi! Ukiwa kama kiongozi, tuna right ya ku-question your ethical standards,
Ethics yes tuko pamoja, wala sina ubishi! morality.. the line is very shady!

na hilo la ndoa kwa mzee Sitta fits this scenario like a glove.

Yes, to the extent that it involves his office, public money, and public office... ndio maana nimesema linazungumzika dada.

Tutakuwaje na imani nawe kama unaweza kuiweka ndoa yako rehani? kama hawawezi kuacha uroda, waache kuwania uongozi!

Don't worry about me, sina mpango na uongozi wa siasa.. ila nikiwa interested, nitayaweka yote hewani kama orodha ya mafisadi! Sina tatizo la kuficha ukweli..

aliyeacha uroda anyoshe kidole juu!
 
Mwanakijiji, nilipoandika
Sawa hatuwezi kukufuatilia na maamuzi yako kama umemchoka mkeo na unataka visura wengine and what not--technically we can, na tutachonga tu kama kawaida yetu...

...was not necessarily directed to you; but all people who have something on the side. Ndio maana nasema kama mtu anataka uroda aendelee tu, ila akiukwaa uongozi, tuta-question matendo yako. Lugha inaleta tabu at times.
 
Binafsi hoja alilolitoa huyu Mzee Busara inatupa mwangaza wa dealings za watu tunaowaita viongozi wetu. Kama kiongozi wenu ni mwizi, wafuasi mtaachaje kuwa wezi?

Sula la yeye kutoa risiti za uwongo mbona hilo ndilo linalofanyika katika kila ofisi la umma, ila tunahitaji kiongozi mmoja tumfanye scapegoat tumwaadhibishe mbele ya umma ili tabia hii ikome mara moja. Kama ni Sitta, so be it! Hili ni suala la kushikiliwa bango. Linauma sana pale ninapokatwa mshahara wangu 35% for PAYE alafu mpumbavu mmoja hashikilii community committments na anatumia hizo fedha kumfurahisha kimada wake, this is not fair. Wakati mimi nalazimika kwenda kukopa kwenye banking institutions ili kufidia the gap na kuweza kumudu maisha. This is not fair at all.

Zitto, kijana wangu, umekosea step kuja kumtetea spika na Mbowe. Were you there with them all along kujua kuwa ni watu wasafi?? Come on even I have skeletons in my closet ila skeletons zangu bahati nzuri hazimfikii huyo sitta wala mbowe maana ni personal skeletons!! Hii tabia ya viongozi kutaka wanaowatuhumu kutoa ushahidi badala ya wao kuachia ngazi ili upelelezi ufanyike inabidi hii tabia ikome.

Nimeshuhudia kimada wa kiongozi mkubwa serikalini akijengewa nyumba sinza karibu kabisa na Lion Hotel in one and half months ikakamilika na miukuta mirefu na geti kubwa. Nikashuhudia kimada huyohuyo akinunuliwa samani nyingi za bei kubwa sana kutoka nje na kwa wakati huo alikuwa na mimba, basi ToysRus ilihamia bongo. Lifestyle yake ilikuwa ya hali ya juu mno. Alijaribu kuwa msiri ila haikusaidia kitu because people asked questions na akajikuta she has to go to neighbors funerals and the sort hatimaye ukweli ukajulikana. Tatizo pia ni kwamba ni fedha za umma zilizotumika kujenga ile nyumba usiku na mchana for a month, generators ziliwaka pale hakuna mfano. Kwa nini nasema fedha za umma, yule binti hana elimu whatsoever na hana kazi ila magari ya serikali hayaishi kupeleka maji, kumpelekea chakula, akiumwa basilinakuja gari kumpeleka hospitalini. Akitaka kwenda safari ya mkoani basi linakuja gari kumpeleka kusalimia wazee wake huko na yote ni STJ vehichles.
Nasikia huyo kiongozi baada ya kumaliza muda wake na hakupewa shavu in the following cabinet. Hali ilianza kuwa mbaya pale na nyumba ni ghetto sasa.
Kumbuka there are children of poor people who would have used that money to go to school, pay for medical supplies at a neighbouring local dispensary. But no that money went to toysRus!

Kwa hiyo bwana acha watu tusikie uchungu maana amepewa dhamana na wananchi kuwatumikia basi na watumikie. Kama Mzee busara wa lying and has given us hazy details about Sitta, there are many more we can name for sure in this forum.

I remain.
 
Nadhani huu ni wakati murua wa JF kuwa na kamati itakayokuwa na wataalamu angalau 5 ambao wote humu ndani tutawachagua kutokana na hekima walizozionyesha ili watusaidie katika hiki kipindi kigumu nchini kwetu.

Ili kundi kubwa la mafisadi limegundua kuwa limegundulika na liko mbioni kumalizwa na hata kufungwa. In my humble opinion I believe they are trying to throw darts and smoke screen to everybody else with a clear intention of confusing wananchi who is a FISADI.

I do not condone the so called behavior allegations above against Hon. Speaker but come on when we are trying to deal with massive losses in billion dollar ranges, who really cares about the small time imprest problems??? Mr. Mbowe ameletewa maneno mengi kisa deni la 15 million Tshs!! Are we serious??

So jamani tuangalie uwezekano wa kuwa na tume ya kuchuja mambo tukianza kupata mashambulizi haya ya watu wenye post 1!!

I repeat sisemi tucensor vitu no way<< Nasema tuangalie tu uwezekano wa kugrade au kuflag issue kama hii maybe iletwe huku kwenye vibweka, mpaka mwelekeo uwe mzuri ndio tudwell in.


EL, Rostam and their croonies have more things in the pipeline against them like EPA, BOT, Vodacom, utalii, majengo ya NHC nk so I think tuwe tu careful smoke screen zikija kwa nguvu ili heshima ya JF ibaki palepale na tuweze kudeal zaidi na maswala ambayo yatasaidia nchi na watu wake wote.

My 2 cents
 
Yaani mtu anamuiba mtu mwingine na unakuita huko kusarandia? Mtu akimtongoza mume/mke wa mtu na mtu huyo akaingia laini, huwezi kuita kuiba! Mtu ambaye anajua amefunga ndoa, na ana familia anapokubali vishawishi vya nje, na akaacha ndoa yake, mtu huyo ana sababu zake. Hakuibwa. Ila kama kuna mtu kweli anaingia kwenye nyumba ya mtu na kumuiba mke/mume wa mtu huyo mtu anastahili kutiwa pingu kwani anachofanya ni kile nilichokielezea kwenye mojawapo ya vifungu vya kanuni zangu.
Hapa si kwamba kwa kuwa umetongoza na mkakubaliana basi hiyo eti iwe imekwisha!,bali hapa suala ni kwamba umemtongoza nani na umemkubali nani, kama ni kutongoza kuna watu wanawatongoza dada zao au hata kaka zao na wanakubaliana, je kwa mtizamo wako unataka kutuambia kwamba kama inatokea hivyo jamii ikae kimya eti kwa sababu ni makubaliano a watu wawili?.
kuna values jamii haiwezi kuzicompromise na kuacha hali iendelee bila kukemea,

ugoni haujawahi kuwa sahihi hata siku moja kwa kisingizio cha kukubaliana katika kutongozana.


Hilo nakubaliana na wewe kabisa, lakini wenye jukumu la kwanza la kutunza na kulinda ndoa zao siyo jamii ni wana ndoa wenyewe! sisi wengine hata tupige matarumbeta mtu akiamua "kupata" nje ataruka ukuta (no pun intended)
Ni kweli jukumu la kwanza la kutunza ndoa ni la wanandoa wenyewe lakini ni jukumu la jamii kusisitiza kwa nguvu zote umuhimu wa kuheshimu taasisi hii ya ndoa, na inapotokea kwamba mtu asiyeiheshimu taasisi hii ya ndoa ni kiongozi hii inakuwa serious zaidi kutokana na nafasi yake katika jamii ambayo yeye alitakiwa aonyeshe mfano bora.



Matatizo ya ndoa hayaishi kwa kukemewa (historia inaoonesha hivyo) yanatokana na maadili mazuri ambayo msingi wake ni kumcha Mungu, maadili ambayo hupandikizwa tangu utoto na humwagiliwa kama miche katika maisha ya watu. Hata hivyo mwanadamu ni kiumbe huru na licha ya hayo yote akiamua kwenda nje ya ndoa au kufanya kitu kinyume na maadili ya ndoa ni yeye anawajibika kwa hilo.
Ukweli wa Lengo la juhudi zote za kupambana na matitizo ya maadili katika jamii huwa siyo kumaliza tatizo, lengo huwa ni kupunguza tatizo, mfano kuweka sheria kali dhidi ya rushwa lengo ni kuipunguza si kuimaliza , lengo la kuweka sheria kali dhidi ya ubakaji utapunguza wabakaji lakini hutawamaliza,na hivyo hivyo hii tabia kwenda nje ya ndoa haitisha kwa kukemea lakini itapungua



Sipingi hilo, na tuko mstari mmoja. Ninachosema, huwezi kuwalazimisha watu wazima na akili zao kuwa na maadili katika familia kama wameamua kutokuwa nayo utawafunga!?

Nakubaliana na wewe kuwa huwezi kuwalazimisha watu wazima kuwa na maadili katika familia lakini naamini kwamba kwa kuweka scrunity katika matendo wanayoyafanya itasaidia kupunguza tatizo. chukulia mfano kwa kiongozi, iwapo kiongozi atafahamu kwamba kwa matendo yake anahatarisha nafasi yake basi huenda akaacha kujihusisha na matendo ya namna hiyo, na kwa kufikia hapo tutakuwa tumepunguza tatizo la infidelity katika jamii.
 
- Tumemzungumza Kikwete hapa
- Tumemzungumza Mengi hapa
- Tumemzungumza Manji hapa
- Tumemzungumza Amina hapa
- Tumemzungumza Zitto hapa
- Tumemzungumza Slaa hapa
na wengine wengi...

Issue sio ngoma au uaminifu katika ndoa tu. Hili jambo lilishaongelewa hapa JF tena na tena, Sitta na hao wengine wangekua walalahoi, who will give a damn! Ukishakua Public figure things change...mfano Bill Clinton and few US senators that had to resign because of sex scandals
 
Gamba, kama unaangalia viongozi wa siasa kuwa ni mfano wa jamii, you picked the wrong group! usimwangilie mtu mwingine yoyote kuwa mfano wa jinsi ya kuishi kwani watu wana disappoint sana.. believe me.. jiangalie wewe mwenyewe na uwe mfano kwa watoto wako.
 
Mungu ibariki Tanzania, Wabariki viongozi wake...

Kama watanzania wote tutamuomba Mungu (kutoka ndani ya mioyo yetu) wakati tuki-imba wimbo wetu wataifa basi janga la kupata viongozi na vitendo vyao kama kina Lowasa halitotukuta!

Kwasasa hivi viongozi tulionawo hauwezi ukapata hata mmoja ambaye atakua hana kasoro na msafi wa mambo haya ambayo aliyo andikiwa Mhs. Sitta.

Hii imeasiri jamii nzima; kwatulikuwepo Tanzania, ukiwa ndio umemaliza chuo na Umeajiriwa serikalini - mshahara pekeyake ni hautoshi kuendesha maisha yako, hivyo utaanza kutengeneza tabia ya kudokoa huku na kule.

Kama una Mke - nyumbani mapema hakurudiki - kwakuwa lazima utakumbana na msururo wa matatizo yanayohitaji fedha kutatuliwa.

Dawa ni kutafuta kimada nje - ambacho unajua wazi siku za mwanzo invoice haiwi kubwa - siku invoice itakapo ongezeka hapo huonekani (Hungera kwa Mhs Sitta anaweza kumudu zaidi ya Watatu - mambo ya kiislamu hayo - Ruhsa hadi wa-nne!).

Nini hasa ninachotaka kusema, kunahaja ya kuibadilisha jamii nzima - ili tuondokane na production ya viongozi kama hawa ambao tunaowapata hivi sasa. Na hili ni sijambo lasiku mbili!

Hivyo kama jamii itaweka mkakati - kwa mfano - kwanza tushughulikie mambo kama Richmond, EPA na kadhalika; tutakapo fanikisha haya ndiyo tuingie katika hatua nyengine ya udokozi, pamoja na tabiya ya viongozi wetu. Hapa tutaweza kuokoa mamilioni na kupelekwa kwenye jamii.

Kwahiyo nakubaliana na Mhs. Zito kuwa hili suala la Mhs. Sitta ni dogo sana kwa muda huu kulijadili.
 
Pamoja na mada hii kuwa tamu, hebu tujikumbushe hii habari ya Mwanakijiji hapa na kama JF nayo ni sehemu ya mkakati husika.

http://www.klhnews.com/index.php/headlines/agenda-21-yaundwa.php

Agenda 21 yaundwa kumsafisha Lowassa

1 2 3 4 5 (4 votes) Written by Mwanakijiji
Saturday, 23 February 2008
Mtandao mpya wa wale waliojikuta wametupwa nje ya serikali na ambao wanajiandaa kujibu mapigo umeundwa. Habari za kuaminika toka kwenye kuta na madirisha mbalimbali ya wahusika zinasema kuwa mtandao huo una lengo moja kubwa ambalo ni kulipiza kisasi kwa yale yaliyotokea Dodoma wiki karibu mbili zilizopita. Haijulikani maana ya "Ajenda 21" nini.
Inadaiwa kuwa ni baadhi ya watu hawa hawa ndio waliohusika kwa namna moja katika jaribio lao lililoshindwa la kuifuta Jambo Forum hewani. Vyanzo vya karibu na mitaa ya Magogoni Jijini Dar vinasema kuwa suala la Jambo Forums lilileta mgawanyiko wa wazi na ililazimu "Ikulu" kuingilia kati na kuamuru mtandao huo uachiliwe kwani "unaisaidia serikali na umekuwa ukiandika habari kwa usahihi zaidi kuliko vyombo vingi vya habari" kwa mujibu wa Ofisa mmoja mfagizi katika jengo la Ikulu.

Mchunguzi wa KLH News aliyeko Arusha anaripoti kuwa mtandao huo ambao siyo tu una lengo la kujibu mapigo lakini pia umedhamiria kurejesha na kuinua tena wasifu wa aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa. Mtandao huo ambao mkoani Arusha unasadikiwa kuhusisha baadhi ya wafanya biashara inadaiwa umeandaa mapokezi makubwa kwa Bw. Lowassa ambaye anatarajiwa kuelekea jimboni kwake siku ya Jumamosi kuzungumza na wananchi wake.

"Ni kweli watu kadhaa wanashirikiana kuandaa mapokezi hayo, lakini ni nani hasa siwezi kukuambia" alisema mjumbe mmoja wa mtandao huo. Pamoja na ajenda yao hiyo mtandao huo una nguvu kubwa ya kiuchumi ambayo hailingani na mtandao mwingine wowote na baadhi ya mashabiki wa JF na KLH wanaona kuwa wako njiani kuzidiwa nguvu mara milioni kadhaa.

Uchunguzi wa KLHN ambao umepenya kwenye kingo za nyumba na maofisi ya watu hao unaonesha kuwa mtandao huo unaundwa na wanasiasa wa chama tawala ambao wamejikuta hawamo tena serikalini, wafanyabiashara maarufu, vyombo kadhaa vya habari (ambavyo vingine vimeanza kuandika habari zinazotokana na "agenda" hiyo) na mashabiki wengine wakubwa wa aliyekuwa Waziri Mkuu. Mmoja wapo wa watu watakaoshiriki katika kuandaa mapokezi hayo ya Lowassa ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyewahi kutumikia kifungo kutokana na makosa ya ujambazi Bw. Justin Nyari. Bw. Nyari baadaye aliweza kushinda rufaa yake kwenye Mahakama Kuu.

Wakati habari hii inaandikwa tayari Kikwete, Dk. Slaa, Mengi na Zitto walikwisha kuguswa na kuchafuliwa, sasa kaja Mbowe na baadaye Sitta. Nakumbuka mtu mmoja alimwambia Mbowe, "nitakujibu kwa staili yangu" baada ya mtu huyo kuguswa na mapigo ya wabunge wa Chadema hasa siku ile ilipotolewa kwa mara ya kwanza orodha ya MAFISADI. Kwa wanaokumbuka orodha ile hata hapa JF ilitolewa ikiwa na majina manane (8) likiwamo jina la Kikwete lakini bila ya majina ya Lowassa, Karamagi na Rostam,katika kipindi ambacho BoT (EPA) na Richmond na TICS zilikua zimepamba moto. Majina hayo ambayo yaliongezwa baadaye, yaliwakera wahusika. Sina hakika kama hili lilikua BAHATI MBAYA katika maandalizi ya orodha kwani wananchi waliwajua hawa kuwa ndio vinara wa UFISADI. Ndipo mtu mmoja akawaambia watu, "atajibu kiaana" na kwamba hana haraka na hilo, kwani ni SUALA LA MUDA TU.

Kabla sijahoji USAHIHI wa TAARIFA na kwamba pamoja na kuwa HOJA ya SITTA ni sehemu ya mapambano yetu ya kuhakikisha nchi inakua SAFI, kuna maswali ya kujiuliza, maswali ambayo nilijiuliza alipoanza kushambuliwa Slaa, Zitto na hata Mengi.

-Nilitoa mfano wa polisi (SITTA,SLAA, ZITTO, KILANGO, MWAKYEMBE, MENGI,MBOWE) ambaye 'tunamtuhumu' kwamba hana maadili ambaye AMESHIKA SILAHA na mbele yetu tuna MAJAMBAZI (LOWASSA, ROSTAM, KARAMAGI, CHENGE) yenye silaha yanaua WATANZANIA WENZETU, sasa tutaanza kumshughulikia huyo POLISI kwanza!!? ama tutampa nafasi ayadhibiti majambazi?!!! Hapa lazima tuzingatia kipindi tulichonacho, kwamba sasa ndicho ambacho wanaibuka watu wanaojifanya wana uchungu na nchi, watu ambao awali hawakua wenzetu kabisa, sasa wametoka nje eti ndio wanaona maovu, kuzuia wasishughulikiwe ama kuwatisha POLISI wetu wasipambane nao. KWanza tujue kwamba polisi (WAZALENDO) tulionao ni wachache mno na hawana SILAHA (uwezo) na vyombo vya usafiri (MEDIA) vilivyopo ni vichache (JF, MWANAHALISI, RAIAMWEMA, THISDAY, KLHN) na tunapoanza kugeukana na kugeuza mashambulizi upande wetu, tunampa adui nafasi ya kushinda VITA tuliyoisimamia kwa urahisi mkubwa na baadaye, majambazi hayo yatarudi na kutushughulikia wenyewe (kama walivyowakamata MAC na Mike), watafungia magazeti na mitandao yote na ikibidi wataua watu na NAWAHAKIKISHIA hawatafanya makosa tena ya KUJIAMINI MNO na kutudharau tena (kusema kelele za chura) kama walivyofanya kwa RICHMOND na EPA, sasa wameshajua JF, Mwanahalisi, Thisday, RaiaMwema ni kiboko kwa hiyo wameingia kwa KASI, NGUVU, ARI na PESA 'mpya' na ndugu zangu HISTORIA ITATUHUKUMU, MUNGU ATATULAANI kwa kusema, "Muliniomba nafasi nikawapa, nikawachanganya, mukaichezea kwa kugombana wenyewe kwa wenyewe tena hadharani". Tumeingiliwa ndani ya nyumba, sasa tunagombana wenyewe na wezi WANAPETA. Tumebadili mwelekeo, sasa FISADI ni MBOWE NA SITTA na LOWASSA, KARAMAGI, ROSTAM ni MASHUJAA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI NA MAKUWADI WAO

uliza, hivi kwanza tunataka kufanikisha nini kwa hoja hii? Kwamba Sitta ang'oke? Ili tufanikishe kitu gani katika malengo yetu makuu?
 
ORODHA YA KWANZA YA LIST OF SHAME

________________________________________
ORODHA YA MAFISADI
(LIST OF SHAME)

KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania.

MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI

A. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali’ kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:
(a) Kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi….”;

(b) Kwamba “lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi”; na

(c) Kwamba “Serikali itawajibika kwa wananchi….”
(d) ….”

Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, “… Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
(a) …
(b) Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

(c) Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(d) Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) …
(f) …
(g) …
(h) Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

(i) Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;

(j) Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
(k) ….”

Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa “… Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii …” ya Katiba. Katiba pia imewapa viongozi wa umma “… wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.” Aidha, viongozi wa umma wamepewa “… wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi….” Vile vile viongozi wote wa umma “watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili katika utumishi wa umma ambazo:

(a) Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma;
(b) …

(c) Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa;

(d) Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
(a) kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;

(b) kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;

(c) kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma;

(d) kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;

(e) kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;

(f) kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;

(g) kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
(h) …
(i) Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;

(j) Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma.

VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO NA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KAMA IFUATAVYO:

A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI

Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Gavana Balali amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;

(ii) Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006. Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005 inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd. zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba makampuni mawili ya Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. – nayo yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84 Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London. Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50 tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd. badala ya kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine haujulikani;

(iii) Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba “… mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.” Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007 inatamka wazi kwamba “Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni.” Barua hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha “majina ya wanahisa wa kampuni na mgawanyo wa hisa.” Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea “Jamhuri ya Mauritius” na anwani yake iko Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005. nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;

(iv) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30 Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola 2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu yenyewe! Kwa maana rahisi ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hadi kufikia mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za Marekani 62,847.91. “Katika mazingira haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, “hatukuweza kujiridhisha kwamba deni la dola la Marekani 5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006 linaweza kulipika.” Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila kudaiwa riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA, Mwananchi Gold Co. Ltd. ni kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa 500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni binafsi tarehe 12 Desemba 2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J. Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB Holdings (1996) Ltd. na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa Tanzania nchini Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T) Ltd;

(v) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali anadaiwa kuidhinisha malipo ya shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. “Katika mazingira haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, “hatukuridhika na uhalali wa hasara ya shillingi bilioni 131.9 zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006….” Kwa mantiki hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha hasara ya shilingi 131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 27 Juni 2007 imetamka kwamba “Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti hiyo hadi uchunguzi huo utakapokamilika.” Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa kata kata kutoa taarifa hizi kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.

2. ANDREW J. CHENGE

Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa “mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria….” Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
(i) Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
(ii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
(iii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

3. BASIL P. MRAMBA

Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa “hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06”! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba “hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani.”
(ii) Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote kuthibitisha kwamba ‘Bwana Basil’ anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la ‘Basil’ ni Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu hayo.
(iii) Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela wa rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

4. GRAY S. MGONJA

Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.

5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA

Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma.

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.

Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates’ Remuneration and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.

Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme’ iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: “Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)

Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: “Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP.”

7. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.

8. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

C. SHERIA YA UDHIBITI WA MAKOSA YA KUHUJUMU UCHUMI, 1984
D. SHERIA YA KUZUIA RUSHWA, 1971 na/au SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, 2007
 
Back
Top Bottom