Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 26,184
- 68,521
Habari wakuu, maisha yana mjumuiko wa matukio mengi sana.
Kuna matukio ambayo wengi wetu tunapenda kuyasikia sana na hayatupi shida yeyote, haya ni matukio mazuri au habari njema mfano, kupata mtoto, mavuno mazuri n.k
Kuna matukio tusiyopenda kuyasikia ni mwiba mkali maishani mwetu kwa wakati husika, haya ni matukio mabaya au habari mbaya. Kwa mfano fumanizi, ugomvi wa familia, ajali n.k
Haya matukio ni kawaida sana kutokea kwenye jamii na maisha yetu. Kuna muda upo mbali na linatokea tukio ambalo unahisi ungekuwepo karibu ungeweza kufanya kitu. Kwa wakati huo zinakujia hisia unatamani hata ungekuwa na mbawa upae ufike eneo la tukio ufanye chochote kizuri au kibaya(ukizingatia matukio yanatofautiana). Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana ni hisia tu kutokana na kinachoendelea mbali na ulipo.
Tukio la kwanza. Nakumbuka hali hii ilinitokea nilipopewa taarifa za kuumwa kwa bibi yangu na alikataa katu kwenda hospital, ni miongoni mwa watu niliokuwa nawapenda sana, nilitamani sana ningekuwepo alipo nimuone na niongee nae maana kipindi cha nyuma nilikuwa naongea nae mpaka anakubali kwenda, haikupita masaa mawili nikapokea taarifa za kifo chake. Huenda ningekuwa karibu ningekuwa msaada kwa namna moja. Niliumia sana may her soul R I P.
Tukio la pili. Long distance relationship, hakika fimbo ya mbali haiui nyoka. Mtu ananiambia yupo na wenzie hostel hajui kama mwanaume alienae kashaiba namba zangu kwenye simu yake na anawasiliana na mimi na picha kanitumia wakiwa wote. Nilitamani nipae nimuibukie alipo maana ile hasira na maumivu hayakuwa ya kawaida. Niliamua kumuacha kimya kimya ila nilikoma.
Habari nyingine nikizisikia natamani niwe eneo husika ni taarifa za kuuguliwa na wazazi wangu, huwa simu zinaita sana mpaka hali iwe shwari.
Matukio yapo mengi share lako zuri au baya.
Siku njema wadau.