Ni nini hatima ya zanzibar huru?

mama alikuwa muislam, ndugu zangu wote wa upande wa mama ni waislam, na hata jina langu la kwanza ni la kiislam hadi kupelekea watu kuhisi mimi nili'kigwangala jina la shule coz jina langu haliendani na dini yangu, mimi ni msambaa na tunaishi mbeya na kujenga mbeya, dada yangu kaolewa na mnyamwezi, kaka yangu kaoa mngoni, ukabila na udni kwenye familia yetu kwishney!

Mkuu mara nyingi humu kuna watu ambao wanapojadili masuala ya Zanzibar na "muungano" huu, huzungumza kwa kejeli na dharau kama kwamba, kuikalia Zanzibar ni jambo la fahari kwao na kwamba sisi hatuna haki ya kujiamulia mustakbali wetu kama nchi.

Hawaoni kwamba "muungano" huu haukutusaidia sana sisi Zanzibar wala Tanganyika.

Ukisoma thread moja humu JF, utaona wale wale wanapinga Zanzibar kurudisha Utaifa wake, wanasema tuvunje ndoa na Wakenya kwa sababu ya EAC. Wanasahau kua sababu zile zille zile ndo sababu zetu.

Ahsante sana Mkuu, nimekuelewa.
 
mkuu nina hakika hujui falsafa tuliyojengewa wa bara na mwl. nyerere, keep this in your mind, hata siku moja makabila ya tanganyika hayawezi kuja kupigana, mimi ni msambaa na tunaishi mbeya, tumejenga mbeya na dadazangu wameolewa na wanyamwezi wa tabora, kaka zangu wameoa wangoni wa songea, kwa hili Nyerere alifanikiwa, ondoa kabisa hiyo ndoto ya ukabila au udini kwa watanganyika, udini unaaoonekana sasa unasababishwa na huu muungano na nyinyi wazenji.

Nilipo RED.

Hakika achana kabisa na Nyerere kwani huyo ndio aliyopandikiza yote hayo kwa Tanganyika, Kama wataka kujua hilo soma kitabu cha " Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania Bara 1953 -1985 " kimebainisha wazi njama alizokuwa anafanya mzee huyo na matokeo yake ndio sasa yanaonekana.

Nje ya Muungano na Zanzibar, wabara hamponi hata kidogo lazima yale ya Sudan yatawakumba tu. Hili halina mjadala wala siasa ndanimwe kwani ukweli haufichiki. Msijidanganye
 
Kama hamuutaki muungano Wa Zenji si fuateni utaratibu muuvunje,
tumechoka na kelele zenu, utadhani mnatusaidia kwa lolote,
mtulipe hela zetu fasta, muondoke huku Tanganyika mkabanane Mchambawima
maana hamjui mnachokitaka ni kelele tu
kama mnaona mnatawaliwa na Tanganyika si fanyeni mapinduzi mengine mjiondoe pia
mmezidi sana, mnasaidiwa lakini wapi, nongwa tu
 
Nilipo RED.

Hakika achana kabisa na Nyerere kwani huyo ndio aliyopandikiza yote hayo kwa Tanganyika, Kama wataka kujua hilo soma kitabu cha " Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania Bara 1953 -1985 " kimebainisha wazi njama alizokuwa anafanya mzee huyo na matokeo yake ndio sasa yanaonekana.

Nje ya Muungano na Zanzibar, wabara hamponi hata kidogo lazima yale ya Sudan yatawakumba tu. Hili halina mjadala wala siasa ndanimwe kwani ukweli haufichiki. Msijidanganye

hivi mkuu unaishi hapa nchini au? kwanza sidhani km unafikiri kwa kutumia ubongo, au la ubongo wako umechanganikana na damu, udini ndo tatizo lako kuu.
 
hivi mkuu unaishi hapa nchini au? kwanza sidhani km unafikiri kwa kutumia ubongo, au la ubongo wako umechanganikana na damu, udini ndo tatizo lako kuu.

Labda useme wewe utujuze.

Je ni kwanini Sudan ya kusini imejitenga kutoka nchi ya Sudan? Na kwanini Sudan ya kusini ni wakristo wakti sudan kaskazini ni waislam?

Je umeshasoma kijitabu cha kanisa katoliki na siasa za Tanzania bara 1953- 1985? Je umeelewa nini humo.

Je unaweza itofautishaje Sudan na tanganyika ( kwa maana tanzania nje ya muungano) hususan ukipitia matukio, mihadhara, magazeti ya dini zote na manunguniko ya wananchi na fikra potofu za wengi kuwa dini moja wasomi zaidi na wengine wasio wasomi .

jribu kufikiria hayo kwa makini kwa kutumia ubongo wako kisha weka taswira ya mnavyhobebwa na muungano katika ku share keki ya uhuru wenu.
 
basi mkuu, nakubali yaishe, sio kusudio langu kuanzisha thread hii kuelekea kwenye mlengo wa kidini zaidi, naona tunakoelekea tunajadili udini kuliko utaifa. pia naomba mods waifute thread hii. km nimekukwaza yaishe tu.
 
Nafikiri unahitaji muda zaidi na kutafakari kabla kuleta hoja. Kwani hata kwa mantiki ndogo tu, hatma ya zanzibar imesha jidhihirisha ya kuweka Serikali ya umoja wa kitaifa ambayo ipo i place. Hilo limeondoa tofauti za jadi baina ya CCM na CUF kwa maana ya waunguja na wapemba.

Sasa ukitazama upande wa pili wa Shilingi yaani upande wa Bara. hapa kuna mtihani mzito sana ambao kwa mtazamo wangu na kwa evidence nilizokupa na kupitia masuala niliokuuliza unaona wazi mambo ya Sudan lazima yatokee nje ya Muungano kwani kwa sasa yanatulizwa na Zanzibar.

Tarbia moja kuu au dhana potofu walionayo watu wengi hapa Tanganyika ni kuwa kuna dini moja ni wasomi zaidi kuliko dini nyingine na wanashindwa kufahamu kuwa Keki ya uhuru wenu ni lazima iliwe na wote na kwa wasaa.

matukia yanayatokea ni dalili wazi kuwa sasa mpo kwenye mkondo ila Znz inawakinga na shari hiyo.
 
Watu wanapokuwa wamechoka na umoja waliokuwa nao huanzisha chokochoko hata ambazo hazina mikono wala miguu. Hili sio kwa nchi, Mikoa, Wilaya, na Vijiji; bali hata kwenye familia; utamuona baba mtu anatengana na mama mtu pamoja na kwamba wamekaa miaka kadhaa na watoto wamesomesha. Watu wanaungana, sisi tunashabikia kutengana.

Mimi binafsi sina wasiwasi wala tatizo Muungano ukiwepo au usiwepo; lakini kwa utashi, hadhi, heshima na uongozi wa siasa ya mfano; naona ni vyema Muunganoi uendelee.

Haya maneno ya Ukoloni, Unyonyaji, na mengine kama hayo ambayo hayana maana katika jamii ndio yanaturudisha nyuma. La msingi ifanywe kazi kuuweka Muungano wetu sawa; watoto, wajukuu na vitukuu waukute na waheshimu dhamira zetu za kuwa wamoja
 
sawa sawa mkuu... kwahiyo tupewe uhuru wa kuchagua ni muungano gani tunautaka? iswe mtu mmoja au kikundi cha watu fulani kiwaamulie wa tz wote... Kuwepo na uwazi juu ya suala la muungano... cha msingi kuwepo na kura ya maoni ya wa tz... tumechoka na zile hadithi eti baba wa taifa , eti karume ,eti kawawa uliusia muungano usiguswe... hawa watu hawapo, na kama lazima tuwe na muungano ,basi uendane na wakati huu...
 
Kwangu mimi naamini kuwa baada ya taifa la sudan ya kusini kuwa taifa huru la 194,naamini zanzibar ndio itakayo fwata na kuwa ya 195,incase wakiamua kujitenga wao kwa wao,sawa-maana huo utakiwa ni uamuzi wao wenyewe,
kwa hio tutegemee taifa lingine changa muda si mrefu-LIKIWA NA CHANGAMOTO ZAIDI YA SUDAN YA KUSINI
 
na baada ya znz kuwa ya 195 kupata uhuru itakayofuata na kuwa ya 196 ni pemba, na km hilo tunaliruhusu ujue hata tanganyika mnataka igawanyike vipande vipande kitu ambacho kwa tanganyika hakitatokea, eg. nchi ya arusha, mbeya, ruvuma nk. wkt sisi wenzetu wanaunganisha nguvu yao ulaya sisi tunashindana kutengana kwa sababu tu ya uchu wa madaraka, muungano uliopo una manung'uniko mengi sana, siungi mkono kuvunjika bali nashauri ufumuliwe na uundwe upya.
 
Hawa jamaa wanapenda sana kuwa ktk nafasi kubwa za uongozi Nahii ndiyo inayo wafanya waone muungano hauna maana kwani kila mara utawasikia; ktk ma IGP wote hakuna Mzenji hata mmoja, mara ktk wafanyakazi wa Bunge ni MMOJA tu toka Z'bar tatizo ni uongozi hawajui ktk uongozi sifa ndizo zina mata na si ilimradi mtu toka Z'bar MUUNGANO UFUMULIWE UANZE UPYA KAMA TUTAKAVYO FANYA KATIBA note ............. "" RUNNING FROM THE PROBLEM IS NOT A SOLUTION OF SOLVING IT ""
 
hawa jamaa wanapenda sana kuwa ktk nafasi kubwa za uongozi nahii ndiyo inayo wafanya waone muungano hauna maana kwani kila mara utawasikia; ktk ma igp wote hakuna mzenji hata mmoja, mara ktk wafanyakazi wa bunge ni mmoja tu toka z'bar tatizo ni uongozi hawajui ktk uongozi sifa ndizo zina mata na si ilimradi mtu toka z'bar muungano ufumuliwe uanze upya kama tutakavyo fanya katiba note ............. "" running from the problem is not a solution of solving it ""

mkuu hapa umeshamaliza kila kitu...ha ha ha ha ha ha ha! Ubwabwa ndo unaogombaniwa si kingine.
 
Back
Top Bottom