Ni Nani Huyu- ENJI BIN UNUUTI?? TUSAIDIENI !!!

Kwa wale wakazi wa kilwa na maeneo ya karibu yake nadhani mtakuwa mnalijua au mmeshakulisikia jina hili la Enji Bin Nuuti inasemekana kwamba jamaa alikuwa ni mtu wa kale sana aliyetokea kaskazini na sifa yake kubwa ni kwamba alikuwa ni mrefu sana,inasemekana kwamba jamaa aliletwa ili apime kina cha bahari ya mwambao wote wa pwani yetu mbaka arabuni basi hata maji yawe na kina kiasi gani yalikuwa yanamfikia magotini tu.!!

Inasemekana kuwa huyu jamaa alikuwa anakwenda baharini anakamata samaki anayemtaka halafu ananyoosha mkono juu hafu samaki anakauka kwa jua mara moja ndio anamla.Wapemndwa tusishangae sana mana kizazi hiki itakuwa kilikuwepo tu duniani si mnakumbuka kwa wale wasomaji wa biblia kuwa kulikuwa na kizazi cha majitu kilichotokana kati ya bin adam na malaika? Au kwa waliosoma kitabu cha Enoki anawaelezea hawa watu ni wa namna gani vizuri zaidi !!!

Iinavyoonekana huyu bwana alikuwa wa mwisho wa kizazi chake cha majitu.Kisa kingine ni kwamba jamaa aliletwa kupima kina cha bahari na hawa wageni labda waarabu au waajemi na alipofika pwani ya kilwa inasemekana kuna sehemu alikuta kina kirefu sana maji yalimfikia kiunoni akaweka alama hadi leo nasikia alama alizoweka zipo.

Hadithi hii mimi nilihadithiwa na babu yangu aliyekuwa na umri wa miaka yapata 107 sasa ni marehem (rip) na alinihakikishia kuwa stori hii ni kweli na akaniambia kuwa hapo kilwa hadi leo kaburi lake lipo!!! ila alisema lipo pembezoni karibu na bahari.
Na yeye history hii alihadithiwa na mzee wake.hivyo basi wana JF tunawaomba kama kuna mtu alishawahi kusikia habari yeyote kuhusu sahaba huyu naomba atujuze maana hili ni jambo la kihistoria kwetu na nchi yetu kwa ujumla na ni utalii tosha.
Anaitwa U'NJI bin U'NUKI, huyu mtu inasemekana alikua ni mrefu sana kiasi kwamba akiingia baharini (kina kirefu) maji yalikua yanamfikia magotini. Alikua anakamata samaki baharini na kumuoka juani na kumla.
 
Kwa wale wakazi wa kilwa na maeneo ya karibu yake nadhani mtakuwa mnalijua au mmeshakulisikia jina hili la Enji Bin Nuuti inasemekana kwamba jamaa alikuwa ni mtu wa kale sana aliyetokea kaskazini na sifa yake kubwa ni kwamba alikuwa ni mrefu sana,inasemekana kwamba jamaa aliletwa ili apime kina cha bahari ya mwambao wote wa pwani yetu mbaka arabuni basi hata maji yawe na kina kiasi gani yalikuwa yanamfikia magotini tu.!!

Inasemekana kuwa huyu jamaa alikuwa anakwenda baharini anakamata samaki anayemtaka halafu ananyoosha mkono juu hafu samaki anakauka kwa jua mara moja ndio anamla.Wapemndwa tusishangae sana mana kizazi hiki itakuwa kilikuwepo tu duniani si mnakumbuka kwa wale wasomaji wa biblia kuwa kulikuwa na kizazi cha majitu kilichotokana kati ya bin adam na malaika? Au kwa waliosoma kitabu cha Enoki anawaelezea hawa watu ni wa namna gani vizuri zaidi !!!

Iinavyoonekana huyu bwana alikuwa wa mwisho wa kizazi chake cha majitu.Kisa kingine ni kwamba jamaa aliletwa kupima kina cha bahari na hawa wageni labda waarabu au waajemi na alipofika pwani ya kilwa inasemekana kuna sehemu alikuta kina kirefu sana maji yalimfikia kiunoni akaweka alama hadi leo nasikia alama alizoweka zipo.

Hadithi hii mimi nilihadithiwa na babu yangu aliyekuwa na umri wa miaka yapata 107 sasa ni marehem (rip) na alinihakikishia kuwa stori hii ni kweli na akaniambia kuwa hapo kilwa hadi leo kaburi lake lipo!!! ila alisema lipo pembezoni karibu na bahari.
Na yeye history hii alihadithiwa na mzee wake.hivyo basi wana JF tunawaomba kama kuna mtu alishawahi kusikia habari yeyote kuhusu sahaba huyu naomba atujuze maana hili ni jambo la kihistoria kwetu na nchi yetu kwa ujumla na ni utalii tosha.
Nilianza kukuelezea kabla sijasoma maelezo yako , nilisoma heading ya thread tu nikaanza kutype comment. Maelezo hayatofautiani
 
Sidhani kwamba ni kweli jua kabisa siku zote lisemwalo lipo!! unakumbuka kisa cha wayaudi weusi wabantu wa zimbabwe wale jamaa walikuwa wanaadithiwa hivi hivi na babu zao kuwa sisi asili yetu hasa ni wayaudi,watu wakawa wanawadharau na kuwacheka juzi mzungu kaenda kasikiliza stori akaona ngoja ajiridhishe akawapima DNA, shangaa!!
jamaa kumbe ni wayaudi kabisa tena damu yao ni ya kiyaudi kushinda hata wale wayaudi wazungu wa israel na marekani!!! hivi vitu vinaukweli hawawezi watu pwani yote wakatunga stori inayofanana.
mkuu ilikuwa wapi na mwaka gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom