Ni Nani Huyu- ENJI BIN UNUUTI?? TUSAIDIENI !!!

Sidhani kwamba ni kweli jua kabisa siku zote lisemwalo lipo!! unakumbuka kisa cha wayaudi weusi wabantu wa zimbabwe wale jamaa walikuwa wanaadithiwa hivi hivi na babu zao kuwa sisi asili yetu hasa ni wayaudi,watu wakawa wanawadharau na kuwacheka juzi mzungu kaenda kasikiliza stori akaona ngoja ajiridhishe akawapima DNA, shangaa!!
jamaa kumbe ni wayaudi kabisa tena damu yao ni ya kiyaudi kushinda hata wale wayaudi wazungu wa israel na marekani!!! hivi vitu vinaukweli hawawezi watu pwani yote wakatunga stori inayofanana.

Una maana ya Ethiopia au Zimbabwe? nakumbuka hii story ya Queen of Sheba kwa Wakushi wa kule Ethiopia.

Hii mbona iko wazi na inaingia akilini. Hiyo ya kuchukua samaki na kubanika kwenye jua km mil.90 haiingii akilini unless una elimu ya majini.
 
Moja ya story zake niliambiwa anaweza muopoa papa baharini alive na ana mchoma kwenye jua kwa kunyoosha tu mkono wenye papa juu (I mean by sun rays)
 
Una maana ya Ethiopia au Zimbabwe? nakumbuka hii story ya Queen of Sheba kwa Wakushi wa kule Ethiopia.

Hii mbona iko wazi na inaingia akilini. Hiyo ya kuchukua samaki na kubanika kwenye jua km mil.90 haiingii akilini unless una elimu ya majini.

sio ethiopia nasema ni zimbabwe na hilo kabila wanalosema la kiyaudi la ethippia linaitwa Falasha tribe la ethiopia hawa walichukuliwa mwaka 1984 kupelekwa israel,lakini baada ya DNA test kuchukuliwa juzi serikali ya israel inajuta maana ressults zinaonyesha kuwa sio wayaudi yaani walikuwa ni converted jews tu na sio wa damu.

lakini hili la zimbabwe ni kabila la kiyaudi ingawa ni weusi na dna test inaonyesha ni wayaudi pure kuliko wale wazungu walioko israeli mana hawa sheria ya kabila lao walikuwa hawaoani na watu ambao si wa kabila lao hivyo dna iko intact.
 
Unju bin Unuq

Kwa wale wakazi wa kilwa na maeneo ya karibu yake nadhani mtakuwa mnalijua au mmeshakulisikia jina hili la Enji Bin Nuuti inasemekana kwamba jamaa alikuwa ni mtu wa kale sana aliyetokea kaskazini na sifa yake kubwa ni kwamba alikuwa ni mrefu sana,inasemekana kwamba jamaa aliletwa ili apime kina cha bahari ya mwambao wote wa pwani yetu mbaka arabuni basi hata maji yawe na kina kiasi gani yalikuwa yanamfikia magotini tu.!!

Inasemekana kuwa huyu jamaa alikuwa anakwenda baharini anakamata samaki anayemtaka halafu ananyoosha mkono juu hafu samaki anakauka kwa jua mara moja ndio anamla.Wapemndwa tusishangae sana mana kizazi hiki itakuwa kilikuwepo tu duniani si mnakumbuka kwa wale wasomaji wa biblia kuwa kulikuwa na kizazi cha majitu kilichotokana kati ya bin adam na malaika? Au kwa waliosoma kitabu cha Enoki anawaelezea hawa watu ni wa namna gani vizuri zaidi !!!

Iinavyoonekana huyu bwana alikuwa wa mwisho wa kizazi chake cha majitu.Kisa kingine ni kwamba jamaa aliletwa kupima kina cha bahari na hawa wageni labda waarabu au waajemi na alipofika pwani ya kilwa inasemekana kuna sehemu alikuta kina kirefu sana maji yalimfikia kiunoni akaweka alama hadi leo nasikia alama alizoweka zipo.

Hadithi hii mimi nilihadithiwa na babu yangu aliyekuwa na umri wa miaka yapata 107 sasa ni marehem (rip) na alinihakikishia kuwa stori hii ni kweli na akaniambia kuwa hapo kilwa hadi leo kaburi lake lipo!!! ila alisema lipo pembezoni karibu na bahari.
Na yeye history hii alihadithiwa na mzee wake.hivyo basi wana JF tunawaomba kama kuna mtu alishawahi kusikia habari yeyote kuhusu sahaba huyu naomba atujuze maana hili ni jambo la kihistoria kwetu na nchi yetu kwa ujumla na ni utalii tosha.
 
Huu uzi niwa muda kidogo,vipi hii story kuna anae fahamu zaidi.??
 
Mwenye uelewa na hii story atuweke wazi wakuu, nipo interested nayo ila naona haijajitosheleza sana
 
Me niliambiwa aliitwa Hunzi bin hunuzi (Unzi bin unuz) na babu fulani kitambo... Aliniambia hatua ya Hunzi ilikuwa ni mkoa to mkoa and then bonge la nyanyo na vyua ikinyesha hilo eneo huwa bwawa
 
Unju bin Unuq (pia: Unju bin
Unuku , Unzi Bin Ununuk ) ni jina la
jitu katika masimulizi ya wakazi wa
pwani ya Tanzania . Hadithi zake
zasimuliwa kuanzia Bagamoyo hadi
Kilwa .
Historia yake inapatikana katika
makumbusho ya Kaole huko
Bagamoyo.
Moja ya mambo ya ajabu ya mtu
huyu ni urefu wake yaani kimo,
inasadikiwa alikuwa na urefu
mkubwa ulioweza kumfanya
atembee baharini na miguu yake
kugusa chini.
Pia alikuwa akitembea kutoka nchi
hadi nchi kutokana na urefu wake.
Inasimuliwa kuwa moja kati ya
nyayo zake inapatikana kwenye jiwe
alilokanyaga huko Tabora ,
Tanzania, wayo wa mguu wa
kushoto wakati wayo wa mguu wa
kulia ulionekana kwenye jiwe
alilokanyaga huko Kongo.
Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa
akichukua samaki baharini kwa
mkono na kuchoma katika jua kisha
anakula.
Kuhusu maisha yake inasimuliwa
kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala
kuolewa kutokana na umbo lake.
Sehemu nyingine ya hadithi yake ni
alipokufa Unju bin Unuq,
aligawanyika vipandevipande
kutokana na urefu wake na
inasemekana kidole chake chenye
urefu wa kilometa moja kasoro
ndicho kilichopatikana na kuzikwa
pale Bagamoyo, lakini hakuna
simulizi mwili wake uliobaki
uliangukia wapi.
Unju bin Unuq alimuwa na ndugu
yake aliyejulikana kama Geofrey bin
Unuk, huyu alipatikana maeneo ya
Dodoma.
Au kwamba Unuq baada ya
kupotea kwa muda wa miaka mingi
alama zake zimeonekana katika mji
wa Dodoma na inaaminika bado
yupo hai.
 
Bagamoyo kwenye makumbusho nimefika ila sijaona hizo kumbukumbu... Next time nitatafuta
 
Natoa amri kaburi lake lifukuliwe na tuoke kama lina vinasaba vya hilo jitu pia nataka pembe yake (jokes)... Duh ndo kwanza nasikia hii
 
Unjuu ibn Unuq kama simulizi zinavyo sema!Mtu mrefu kuliko kiumbe chochote duniani,akipita nchi husika anafunika jua lote
Samaki aina ya Papa au Nyangumi ndiyo kilikuwa chakula chake anawakamata baharini anawapasha kwenye jua
Sidhani kama habari zake zinawezekana kisayansi
 
Unjuu ibn Unuq kama simulizi zinavyo sema!Mtu mrefu kuliko kiumbe chochote duniani,akipita nchi husika anafunika jua lote
Samaki aina ya Papa au Nyangumi ndiyo kilikuwa chakula chake anawakamata baharini anawapasha kwenye jua
Sidhani kama habari zake zinawezekana kisayansi
alizaliwa na nan huyu mtu na ana unao wake upo mpka leo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom